Wote wanaogopa wanaposikia neno Langu. Wote wamejawa na hofu. Mnaogopa nini? Sitawaua! Ni kwa sababu mnahisi hatia na mnaogopa kugunduliwa. Yale unayoyafanya nyuma Yangu ni ya upuuzi na yasiyo na maana kabisa. Hili limenifanya Nikuchukie sana hivi kwamba Ninatamani sana Ningekuwa nimewatupa wale ambao Sikuwa nimewajaalia wala kuwachagua katika shimo lisilokuwa na mwisho wavunjwe vipande vipande. Hata hivyo, Nina mpango Wangu, Nina malengo Yangu.
I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu
Kupata Mwili kwa Mungu
1. Bwana Yesu Mwenyewe alitabiri ya kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho na kuonekana kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi.
Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja" (LK. 12:40).