XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu
2. Kwa nini inasemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote wanaitembea njia ya Mafarisayo? Ni nini asili yao?
Aya za Biblia za Kurejelea:
2. Kwa nini inasemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote wanaitembea njia ya Mafarisayo? Ni nini asili yao?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Naye akaanza kuzungumza nao kwa kutumia mifano. Mtu fulani alipanda shamba la mizabibu, naye akalizingira kwa ugo, naye akachimba mahala pa shinikizo ya zabibu, naye akaunda mnara, naye akalipanga kwa wakulima, na kuenda katika nchi ya mbali. Na kwa majira yake akamtuma mtumishi kwa wakulima wale, ili aweze kupata matunda ya shamba hilo la mizabibu kutoka kwa wakulima. Nao wakamkamata, na kumpiga, na kumtoa humo bila chochote. Na tena akamtuma mtumishi mwingine; nao wakamtupia mawe, na kumjeruhi kichwani, na kumwondoa humo kwa aibu. Na tena akamtuma mwingine; nao wakamwua, na wengine wengi; wakiwapiga wengine, na kuwaua wengine. Kwa sababu alikuwa na mwana mmoja, aliyempenda sana, alimtuma pia kwao mwisho, akisema, Watamheshimu mwanangu. Lakini wakulima hao waliambiana, Huyu ndiye mrithi; njooni, acha tumwue, na urithi wake utakuwa wetu. Nao wakamchukua, na kumwua, na kumtupa nje ya shamba la mizabibu. Bwana wa shamba hilo la mizabibu atafanyaje basi? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, naye atawapa wengine lile shamba la mizabibu” (Marka 12:1-9).