Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo wokovu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo wokovu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 14 Desemba 2018

2018 Gospel Music "Usimamizi wa Mungu Daima Ukiendelea Mbele" (Swahili Subtitles)

2018 Gospel Music "Usimamizi wa Mungu Daima Ukiendelea Mbele" (Swahili Subtitles)

Mababu wa wanadamu, Adamu na Hawa, walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza usimamizi Wake wa wokovu wa wanadamu. Tangu wakati huo, Amefanya kazi bila ya kukoma: Mungu alitangaza sheria kuwaongoza wanadamu, na Yeye binafsi alikuja miongoni mwa wanadamu kusulubiwa na kuwakomboa wanadamu, na katika siku za mwisho, Mungu anaendelea na kazi Yake, akitimiza unabii wa Biblia: "Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali" (Yohana 14:2). "Naja upesi; 

Alhamisi, 6 Desemba 2018

Tamko la Arubaini na Saba

Tamko la Arubaini na Saba

Mwenyezi Mungu mwenye haki—Mwenyezi! Ndani Yako hakuna chochote kabisa kilichofichwa. Kila fumbo tangu zamani hadi milele, ambalo binadamu hawajawahi kufichua, ndani Yako linadhihirika na kwa jumla kuwa wazi. Hatuhitaji tena kutafuta na kupapasa, kwa maana leo nafsi Yako inadhihirika wazi kwetu, Wewe ndilo fumbo ambalo limefichuliwa, na Wewe ni Mungu aliye hai Mwenyewe, na kwa leo Umekuja uso kwa uso na sisi, na kwa sisi kuona nafsi Yako ni kuona kila fumbo la ulimwengu wa kiroho.

Jumanne, 4 Desemba 2018

Neno la Mungu | "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" (Sehemu ya Kwanza)

Neno la Mungu | "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" (Sehemu ya Kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu;

Jumapili, 2 Desemba 2018

Tamko la Themanini na Sita

Tamko la Themanini na Sita

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia.

Jumamosi, 1 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Umekuwa Hai Tena?"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Umekuwa Hai Tena?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa.

Jumamosi, 17 Novemba 2018

4. Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

4. Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Usimamizi mzima wa Mungu umegawika kwa hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayopatana yanatokana na mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu huongezeka hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na hivyo mahitaji ya mwanadamu huongezeka hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huongezeka hata zaidi. …

Ijumaa, 16 Novemba 2018

3. Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

3. Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja.

Alhamisi, 15 Novemba 2018

1. Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu.

II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

1. Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu.

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi);

Jumatano, 7 Novemba 2018

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana" (YN. 5:22).
"Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu" (YN. 5:27).

Jumamosi, 27 Oktoba 2018

Tamko la Themanini na Saba

Tamko la Themanini na Saba

Lazima uharakishe hatua na ufanye kile Nataka kufanya. Hii ni kusudi Langu lenye hamu kwenu. Inawezekana kuwa kwa wakati huu bado hamjaelewa maana ya maneno Yangu? Inawezekana kuwa bado hamjui kusudi Langu? Nimezungumza wazi zaidi na zaidi, na kusema mengi zaidi, lakini, je, ninyi hamjajitahidi kujaribu kuelewa maana ya maneno Yangu? Shetani, usifikiri kwamba unaweza kuharibu mpango Wangu! Wale wanaomtumikia Shetani, yaani, uzao wa Shetani (hii inahusu wale ambao wanamilikiwa na Shetani.

Ijumaa, 26 Oktoba 2018

Tamko la Themanini na Nne

Tamko la Themanini na Nne

Kwa sababu ya ukosefu wao wa ujuzi kunihusu Mimi, mwanadamu amekatiza usimamizi Wangu na kudhoofisha mipango Yangu mara zisizo na idadi, lakini hawajawahi kuweza kuzuia hatua Zangu zinazoendelea mbele. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu wa hekima. Pamoja na Mimi kuna hekima isiyo na mipaka; pamoja na Mimi kuna siri isiyo na mipaka na isiyoweza kueleweka. Mwanadamu hajawahi kuweza kuielewa na kuifahamu kabisa tangu zamani za kale hadi milele. Je, hilo haliko hivyo?

Jumatatu, 22 Oktoba 2018

Tamko La Thelathini Na Tano

Tamko La Thelathini Na Tano

Ngurumo saba zinatoka kwenye kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinageuza mbingu na ardhi, na zinavuma angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha. Nuru ya ghafla ya umeme na sauti ya radi zinatumwa mbele, zikiiangusha chini mbingu na ardhi papo hapo, na watu wamekaribia kufa. Kisha, dhoruba ya mvua kali inafagia ulimwengu wote kwa kasi ya umeme, ikianguka kutoka angani!

Ijumaa, 19 Oktoba 2018

Tamko la Hamsini na Sita

Tamko la Hamsini na Sita

Nimeanza kuchukua hatua kuadhibu wale ambao hufanya uovu, wale ambao hushika madaraka, na wale ambao hutesa wana wa Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, yeyote anayenipinga katika moyo wake, mkono wa amri Zangu za utawala utakuwa daima juu yake. Fahamu hili! Huu ndio mwanzo wa hukumu Yangu na hakutakuwa na huruma itakayoonyeshwa kwa yeyote na hakuna atakayesamehewa kwani Mimi ni Mungu asiye na hisia ambaye hutenda haki; ingekuwa vyema kwenu kutambua hili.

Jumanne, 16 Oktoba 2018

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu

Chama cha Kikomunisti cha China ni serikali ya kishetani ambayo huchukia ukweli na Mungu. Kinajua kwamba Mwenyezi Mungu peke Yake katika ulimwengu ndiye Anayeweza kuonyesha ukweli. Mwenyezi Mungu yuko katika mchakato wa kufanya kazi ya wokovu wa siku za mwisho. Neno la Mwenyezi Mungu likienezwa kati ya watu, wale wote wanaopenda ukweli watarejea kwa Mwenyezi Mungu. Uso wa kishetani wa Chama cha Kikomunisti cha China, uso wake wa kweli, ambao huchukia ukweli na kumpinga Mungu utafunuliwa.

Alhamisi, 4 Oktoba 2018

"Kaa Mbali na Shughuli Zangu" (3) - Tunaweza Kunyakuliwa Hadi kwenye Ufalme wa Mbinguni Baada ya Kukubali Ukombozi Kutoka kwa Bwana Yesu?

"Kaa Mbali na Shughuli Zangu" (3) - Tunaweza Kunyakuliwa Hadi kwenye Ufalme wa Mbinguni Baada ya Kukubali Ukombozi Kutoka kwa Bwana Yesu?

Kwa msingi wa maneno ya Bwana Yesu akiwa msalabani "Imekwisha," wachungaji na wazee wa kanisa wa jamii ya dini kwa kawaida huhitimisha kwamba kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu ilikuwa basi imekamilika. Bwana aliporudi, waumini wangepokelewa kwenye ufalme wa mbinguni, bila ya haja ya kazi yoyote ya utakaso na uokoaji wa watu. Je, mtazamo huu wa wachungaji na wazee wa kanisa unalingana na maneno ya Mungu? Bwana Yesu alikuwa akirejelea nini hatimaye, Aliposema "Imekwisha" akiwa msalabani? Kwa nini Mungu atake kuuonyesha ukweli wakati wa siku za mwisho, akiifanya kazi ya kuhukumu na kuwatakasa watu?

Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumanne, 2 Oktoba 2018

Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God

Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God

Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu, na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.

Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake.
Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho.
Nguvu ya Shetani haiwezi kumfikia Mungu, kwani Yeye amejawa na utukufu, haki, na hukumu.

Jumatatu, 1 Oktoba 2018

Tamko la Sitini na Mbili

Tamko la Sitini na Mbili

Kuyaelewa mapenzi Yangu hakufanywi ili tu kwamba uweze kujua, ila pia kwamba uweze kutenda kulingana na nia Yangu. Watu hawauelewi moyo Wangu. Ninaposema huku ni mashariki, wanalazimika kuenda na kutafakari, wakijiuliza, “Kweli ni mashariki? Pengine sio. Siwezi kuamini kwa urahisi hivyo. Nahitaji kujionea mwenyewe.” Ninyi watu ni wagumu sana kushughulikia, na hamjui utii wa kweli ni nini. Mnapoijua nia Yangu kisha mwende kuitenda kwa kusita—hakuna haja ya kuifikiria!

Jumatatu, 24 Septemba 2018

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (5) - Je, Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho ni Adhabu au Wokovu?

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (5) - Je, Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho ni Adhabu au Wokovu?

Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu? Maneno ya Mungu yanasema: "Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu." "Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi" (Neno Laonekana katika Mwili). Ni njia gani nzuri ya kufahamu kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho?

Jumapili, 16 Septemba 2018

Swahili Christian Music Video "Hadithi ya Xiaozhen" (3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu

Swahili Christian Music Video "Hadithi ya Xiaozhen" (3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu

    Katika ulimwengu huu wa mioyo mibaya ambapo pesa ni mfalme, ni machaguo yapi ambayo Xiaozhen aliye safi na mzuri aliyafanya, ya maisha na ya kuendelea kuishi …

Jumamosi, 15 Septemba 2018

Swahili Christian Musical Trailer "Hadithi ya Xiaozhen" | Praise God for His Great Love

Swahili Christian Musical Trailer "Hadithi ya Xiaozhen" | Praise God for His Great Love

    Xiaozhen alikuwa Mkristo mwenye moyo safi, ulio na huruma, ambaye kila wakati alikuwa akiwashughulikia wenzake kwa uaminifu. Hata hivyo, ilipokuwa ni kwa manufaa yao, marafiki wake wa awali waligeuka na kuwa maadui wake. Baada ya kuteseka kutokana na msiba huu, Xiaozhen alilazimika kuuacha moyo wake wa kweli na kanuni zake za awali.