Jumapili, 11 Machi 2018

Kuamini Uvumi ni Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho

Kuamini Uvumi ni Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho


Wakati wowote wanaposikia mtu akizungumza juu ya injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ndugu wengi wa kiume na wa kike kanisani wanashindwa kusikiliza na hawathubutu kukubali kile kinachosemwa kwa kuwa wameshtushwa na uvumi wa mihemko.  Wanaweza kusikia mtu akisema: "Wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu ni watu muhimu kweli, utadanganywa ukiwasiliana nao. Kuna waumini wengi wa kweli katika kila dhehebu la kidini na wana sifa nzuri za ndani, wao ni wanakondoo wanaopenda ukweli lakini wanaibwa na wanaomwamini Mwenyezi Mungu ..." Au mtu fulani amesema: "Waumini wa Mwenyezi Mungu kwa kweli wana shauku kubwa juu ya kueneza Injili. Wakimbadilisha muumini wao hupata tuzo ya RMB 2,000 (takribani dola 300), wakimbadilisha kiongozi wa kanisa wanaweza kupata RMB 10,000 hadi 20,000(takribani dola 1,500 hadi 3,000) ..." Na bado wengine wamesema: "Hawana mipaka mizuri sana kati ya wanaume na wanawake na wote ni wazinzi sana ..." Na bado wengine wamesema: "Umeme wa Mashariki ni shirika la jinai. Ukijihusisha nao hutaweza kuponyoka kamwe. Ukiponyoka, watayang'oa macho yako na kukata masikio yako, au wataivunja miguu yako ..." nk. nk. Ni uvumi kama huu ambao huwafanya baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike ambao hawana habari dhahiri juu ya ukweli kuchelewa au hata kukataa wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Sijui kama ndugu wowote wa kiume au wa kike ndani ya kanisa kwa ari wamefikiria au kuchunguza kama mambo haya ambayo yanasemwa yanaambatana na ukweli au hapana; kuna msingi wowote wenye ukweli? Je, umewahi kuwaza kuhusu ni aina gani ya madhara makubwa yatakayokuwepo ukiamini uvumi wote unaousikia na kuendelea kufanya mambo kwa njia isiyo sahihi? Kwa sasa, hatuhitaji kujadili ni nani chanzo cha uvumi huu au ni kwa nini angebuni kwa makusudi mambo haya. Badala yake, kwanza tutafanya ushirika rahisi kuhusu uvumi huu ili tuweze kuwawezesha ndugu wetu wa kiume na wa kike kuona wazi kiini cha uvumi huu.
Uvumi huenda hivi: "Wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu ni watu muhimu kweli, utadanganywa ukiwasiliana nao. Kuna waumini wengi wa kweli miongoni mwa kila dhehebu la kidini na wana sifa nzuri za ndani, wao ni wanakondoo wanaopenda ukweli lakini wanaibwa na wanaomwamini Mwenyezi Mungu ..." Leo hii, wengi wa wanaomwamini Mwenyezi Mungu kwa kweli hutoka kwa madhehebu mengi ya kidini na miongoni mwao, wengi sana ni watu waliojitolea sana, lakini kusema kuwa wote wamedanganywa ni kashfa yenye nia mbaya, ndivyo ilivyo. Hebu lifikirie: Watu wengi sana wenye kumcha Mungu wakitoka kwa makundi mengi tofauti ya kidini kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho wote wanaweza kudanganywa? Inaleta maana yoyote kwamba wangekuwa waumini kwa miaka mingi sana bila kuwa na ufahamu fulani? Hata kama kuna udanganyifu kiasi, inaweza tu kuwa ni wale ambao si watafutaji na ambao wamevurugika katika imani yao wanaodanganywa. Inawezekanaje kuwa hata watu wengi sana wanaotafuta na wengi sana wenye imani ya kweli katika Mungu wanaweza kudanganywa? Kama kila mtu anavyojua, imani yetu iko katika Mwenyezi Mungu–Roho Mtakatifu ambaye ni Roho aliyezidishwa nguvu mara saba–na ni kazi ya Roho Mtakatifu tu inayoweza kuwahimiza watafutaji na waumini wa kweli kurudi kwa Mungu. Leo, kuna watafutaji wengi wa kweli kutoka kwa madhehebu mbalimbali ya kidini ambao wameisoma na kusoma tena Biblia na ambao sasa wamekuja kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kwa hiyo hilo linaonyesha nini? Ndugu wote wa kiume na wa kike wenye welekevu wa kiroho wanajua jibu, ambalo ni hili: Kanisa la Mwenyezi Mungu lina kazi ya Roho Mtakatifu na lina ukweli! Kama haikuwa kazi ya Mungu Mwenyewe, basi ni nani ambaye angewaleta ndugu hawa wa kiume na wa kike kutoka kwa makundi mengi tofauti ya kidini pamoja? Je, muujiza mkubwa kama huo ungekuwa ni kazi ya mwanadamu? Mwenyezi Mungu kweli ni kurudi kwa Bwana Yesu; Yeye ni kuonekana kwa Mungu mmoja wa kweli! Yeye atavuna na kupembua katika siku za mwisho na kufanya kazi ambapo madhehebu yote ya kidini yanarudi kuwa moja na Atawaleta waumini wote wa kweli katika ufalme Wake. Kwa hiyo, ndugu wa kiume na wa kike ambao ni waumini wa kweli kutoka kwa madhehebu yote ya kidini wamerudi mmoja mmoja kusimama mbele ya kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu baada ya kuisikia sauti ya Mungu. Mwenyezi Mungu ameleta ukweli, njia, na uzima na Yeye hufichua mafumbo ya mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu. Yeye hutuambia mafumbo yote ya Biblia ambayo hatukuyafahamu na wakati watafutaji wa kweli wa Mungu wanaposikia ukweli huu na kuona kuonekana kwa Mungu, wangewezaje kutokubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho? Nani ambaye hangetaka kufuata nyayo za Mwanakondoo? Hii ndiyo sababu watafutaji wengi kutoka madhehebu tofauti ya kidini wameikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Wazo kwamba watu ambao wameikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho wanadanganywa ni wazi kuwa ni uongo papo hapo, ni uharibifu wa jina, na ni kukufuru kwa Mungu.
Watu wengine wamesema: "Wanaomwamini Mwenyezi Mungu ni wenye shauku sana juu ya kueneza injili. Wakimbadilisha muumini wao hupata tuzo ya RMB 2,000 (takribani dola 300), wakimbadilisha kiongozi wa kanisa wanaweza kupata RMB 10,000 hadi 20,000(takribani dola 1,500 hadi 3,000) ..." Ndani ya uwongo huu, imetajwa kuwa wanaomwamini Mwenyezi Mungu wana shauku sana juu ya kueneza Injili ya Mwenyezi Mungu. Wakati sehemu hii kweli ni sahihi, mengine kuhusu wanaomwamini Mwenyezi Mungu kuhongwa kwa fedha ili kueneza injili Yake ni upuuzi mtupu uliobuniwa na uvumi wa kashifa. Ukweli ni kwamba, wanaomwamini Mwenyezi Mungu ambao hueneza injili Yake hawapokei tuzo ya aina yoyote. Badala yake, wao hutumia akiba zao kufanya hivyo, na wakati mwingine yote waliyo nayo. Sababu yao kuwa na shauku sana si kwa sababu wamehongwa na fedha, bali, ni kwa sababu kweli wameona kuonekana kwa Mungu, wamesikia neno la Mungu, kupokea wokovu Wake mkuu, na wamepitia upendo wa Mungu. Kwa hiyo, wanapenda kutumia yote waliyo nayo na kuvumilia shida yoyote au fedheha ili kueneza injili ya ufalme wa Mungu. Wao ni kama tu wanafunzi wa asili wa Bwana Yesu Kristo; wameona kuonekana kwa Mungu na wamepata upendo wa Mungu. Wameacha nyumba zao na kazi zao ili kumshuhudia Mungu; ni kweli! Labda baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike wameona binafsi jinsi wanaomwamini Mwenyezi Mungu wanavyotendewa wakati wanapoeneza injili: Wengine wanaaibishwa, wengine hupigwa kwa rungu, wengine hufukuzwa, wengine wamefukuzwa, na wengine hata wamehukumiwa na kufungwa jela mikononi mwa watu walio utawalani; wao hupata kila aina za mateso. ... Ninamhimiza kila mtu awazie hili: Ni nani ambaye yuko tayari kujitoa apate laana, kupigwa, na kuaibishwa ili kuieneza injili ya Mungu ya siku za mwisho kama haingekuwa ni kwa sababu ya upendo mkubwa wa Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu? Ni nani angejasiri hatari ya gerezani kueneza injili ya wokovu wa Mungu katika siku za mwisho kama hangekuwa ameona kuonekana kwa Mungu? Kama ingekuwa kweli ni kuhusu fedha, si ingekuwa rahisi kwenda nje ulimwenguni na kuifanyia kazi? Kwa nini kustahimili fedheha na mateso jinsi hiyo ili kueneza Injili? Kama tukichukua mtazamo mwingine kwa ndugu wa kiume na wa kike ambao hueneza injili ya siku za mwisho, ni wangapi wao ambao wanavaa au kutumia bidhaa maarufu au bidhaa ghali sana? Kama uvumi huu ungekuwa kweli kwamba kuleta muumini wao hupata RMB 2,000 na kuleta kiongozi wa kanisa wao hupata RMB 10,000 hadi 20,000, si kungekuwa na umma mkubwa wa ndugu wa kiume na wa kike katika China ambao wanatajirika kila siku kwa kueneza injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho? Hakuna madhara katika kufanya utafiti wa haraka: Hebu tuone hasa ni nani miongoni mwa ndugu wa kike na wa kiume katika Kanisa la Mwenyezi Mungu aliyepata utajiri kutokana na uenezaji wa injili. Hivyo "kumbadilisha muumini anapata tuzo ya RMB 2,000, na kumbadilisha kiongozi wa kanisa anapata 10,000 hadi 20,000 RMB" ni uwongo dhahiri na ni kashifa.
Bado kuna wengine ambao wamesema: "Hawana mipaka mizuri sana kati ya wanaume na wanawake na wote ni wazinzi sana ..." Kuhusu jambo hili, hebu tuangalie maneno ya Mwenyezi Mungu: "Mimi ni Mungu Mtakatifu Mwenyewe, Siwezi kuvunjiwa hadhi, na siwezi kuwa na hekalu lililo najisi" (Neno Laonekana Katika Mwili). Na kanuni hiyo ni wazi sana katika "Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme": "Mwanadamu anayo tabia ya upotovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atatupiliwa mbali, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili." Tunaweza kuona kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu kuwa Yeye ni mtakatifu na haishi katika hekalu lisilo safi. Tabia Yake ya haki haivumilii kosa lolote kutoka kwa wanadamu na mtu yeyote ambaye ni mfuasi wa Mwenyezi Mungu lazima afuate kwa akali amri za utawala wa Mungu au atafukuzwa kutoka kanisani; hakuna wa kupendelewa. Injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu imeenea kote katika China Bara na kuna wanaomwamini katika kila mahali. Huenda umewaona wewe mwenyewe na wanaomwamini Mwenyezi Mungu wote ni wenye hadhi na waadilifu, maneno yao na njia zao ni sahihi na nzuri, wao hujichukua kwa tabia yenye maadili, husema na hufanya kazi kirazini, wana ubinadamu, na maisha yao ya kudhihirisha yanastahili kupendeza. Wao ni bora miongoni mwa wanachama wengine wa jamii; ni ukweli! Tena, ndugu hawa wa kiume na wa kike ambao wanamwamini Mwenyezi Mungu wanavutwa hasa kutoka kwa watafutaji halisi kutoka kwa madhehebu mbalimbali ya kidini na wengi ni viongozi na wafanyakazi wenza kutoka madhehebu tofauti tofauti. Wamejua kutoka kwa Enzi ya Neema kwamba Mungu huchukia shughuli za uasherati na daima wameweka amri za Bwana Yesu, jambo ambalo kwa hakika watu wa kustahi sana wamefanya wakati uliopita. Mtu kama huyu angeweza kwa kudhamiria kukiuka amri za utawala za ufalme wa Mungu leo? Katika siku za nyuma, walisafiri pamoja kwa ajili ya Bwana, wakaacha kila kitu walichokuwa nacho, na kubeba msalaba na kuteseka kwa miaka mingi, inaleta maana kwamba hawaelewi sheria rahisi na ya msingi kama hiyo? Hivyo unaweza kuona, kiini cha uvumi huu ni cha upuuzi tu na kina maana ya kumpaka mtu matope tu.
Watu wengine wamesema kwamba "Umeme wa Mashariki ni shirika la jinai. Kama utajihusisha nao hutaweza kuponyoka kamwe. Ukiponyoka, watang'oa macho yako na kukata masikio yako, au watavunja miguu yako ..." Wanapotaja mashirika ya jinai, sisi sote tunajua kuwa hayo yanahusika na wauaji, wachomaji wa mali kwa makusudi, na watu wa kulipiza kisasi sana ambao hufanya mambo mengi ya uovu. Hakuna mtu anayetaka kuwachochea watu wa aina hii. Hata Chama Cha Kikomunisti cha China na polisi wake hawawezi kuthubutu kuvurugana nao, si hilo ni kweli? Basi hebu tuangalie ndugu wa kiume na wa kike ambao hueneza injili ya siku za mwisho. Wakati wanapoenda nje kuleta watu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, wao huvumilia kutupwa nje, kutukanwa, kupigwa, kushambuliwa na mbwa, kukamatwa, kufungwa, na kuteswa. Wao hupitia kila aina ya matendo ya kikatili. Kama ndugu hawa wa kiume na wa kike walikuwa wahalifu kweli, mtu yeyote kweli angethubutu kuwatendea kwa njia hiyo? Ni nani angewagonga? Nani angeachilia mbwa wao wawashambulie? Ni nani angethubutu kuwakamata? Hakuna mtu angefanya hivyo! Mhalifu angevumilia matusi bila kulipiza kisasi? Mhalifu angeweza kupigwa na asilipize kisasi? Unawajua wahalifu kama hao? Kama ndugu hawa wa kiume na wa kike walikuwa wahalifu kweli, kwa nini wangekuwa wakijaribu hasa kuwabadilisha waumini wa kweli wa Mungu ambao ni watafutaji waliojitolea kiasi? Aidha, kuna ndugu wengi wa kiume na wa kike kutoka madhehebu mbalimbali ya kidini ambao wamesikia injili ya Mungu ya siku ya mwisho. Ikiwa waliikubali injili na kisha wakaondoka kanisani au kama hawakuikubali kamwe hasa, ni nani kati yao aliyeng'olewa macho, masikio kukatwa, au miguu kuvunjwa? Je, kuna misingi yoyote ya kweli kwa lolote ambalo hawa waeneza uvumi wamesema? Pia hakuna msingi wa kweli wanaposema mambo kama: "Kama ukijihusisha na kumwamini Mwenyezi Mungu hutaweza kuponyoka kamwe." Kwa kweli, waumini wote wa kweli na wale ambao wana hakika kwa dhati juu ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho ambao wanaamua kamwe kutoondoka, hufanya hivyo kwa sababu hawataki kuondoka. Hili ni kwa nini? Mwenyezi Mungu anasema, “Hali ya Mungu kupata mwili imesababisha mawimbi mazito katika vikundi na madhehebu yote, 'imeparaganya' mpangilio wao wa awali, na imetikisa mioyo ya wale wanaotamani sana kujitokeza kwa Mungu. Ni nani asiyeabudu? Nani hatamani kumwona Mungu? Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi sana, lakini mwanadamu kamwe hajawahi kutambua. Leo, Mungu Mwenyewe amejitokeza, na Ameonyesha utambulisho Wake kwa watu—inawezekanaje hii isiupatie moyo wa mwanadamu furaha?” (“Kazi na Kuingia (10)” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. … Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uhai” (“Dibaji” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupata mwili kwa Mungu katika siku za mwisho hasa kumetuma wimbi la kishindo kupitia makundi mbalimbali ya ulimwengu wa kidini na kumeitikisa mioyo ya wale walio na kiu ya kuonekana kwa Mungu. Sababu ya ndugu wa kiume na wa kike kutoka madhehebu mbalimbali wamerejea kusimama mbele ya Mungu ni kwa sababu wameona kuonekana kwa Mungu, kusikia neno lake, kuelewa Kristo wa siku za mwisho ni ukweli, njia, na uzima, na kwamba ni imani tu katika Mwenyezi Mungu itawawezesha kufanikisha wokovu na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ni nani angependa kuondoka baada ya kupokea wokovu kama huu? Kwa hiyo, ni rahisi kuona kwamba uvumi kuhusu watu kutotaka kuondoka kutokana na hofu kuwa macho yao yatang'olewa, masikio kukatwa, au miguu kuvunjwa unatungwa tu na watu wenye nia iliyofichika.
Kutokana na kile tulichofanya ushirika kuhusu hapo juu, tunaweza kuona kwamba maoni ya kashfa kuhusu kazi ya Mungu katika siku za mwisho si kitu ila uongo ambao ni uzushi kamili na hauna msingi katika ukweli. Kuwa muumini ambaye hutunga uongo na kutoa ushahidi wa uongo ni tabia ambayo Mungu huchukia sana na huchukuliwa kama tabia ya dhambi na Mungu, kama vile tu Biblia inavyosema hapa: "Yeye ambaye hutamka maneno ya kweli huonyesha haki: lakini muongo huonyesha udanganyifu" (Mithali 12: 17). "Midomo idanganyayo ni chukizo kwa BWANA: lakini wafanyao yaliyo ya kweli ni furaha yake" (Mithali 12: 22). Bwana Yesu alisema: "Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake. Anaponena uwongo, anazungumza yaliyo yake mwenyewe: kwani yeye ni mwongo, na baba wa uwongo” (Yohana 8:44). Kwa kuzingatia kwamba hiki ni kitu ambacho Mungu hakipendi, kwa nini wanaendelea kufanya hivyo? Katika Yohana sura ya 11 mistari ya 47-48 inasema: "Kisha makuhani wakuu na Mafarisayo walikonga baraza, wakasema, Tufanye nini? Kwani mtu huyu anatenda miujiza mingi. Tukimwacha hivi peke yake, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja na kuichukua nafasi yetu na taifa letu." Mathayo sura ya 28 inasema ukweli huu: Baada ya kufufuka kwa Bwana Yesu, makuhani wakuu na wazee waliogopa kwamba kila mtu angeenda kumwamini Bwana Yesu na kwa hiyo wangepoteza hadhi zao na mapato. Basi walikula njama kuuficha ukweli kwamba Bwana Yesu alifufuliwa. Waliwahonga askari kwa fedha na wakabuni uongo ili kuwashawishi watu kwamba Bwana Yesu hakufufuka kamwe, wakisema kuwa wanafunzi waliuchukua mwili wa Kristo wakati askari walikuwa wamelala. Tunaona kutokana na hili kwamba watu wanaweza kubuni uongo na kashfa na kumkufuru Mungu, ambayo inaonyesha tabia yao mbovu, kwamba wao huchukia ukweli na kwamba ni maadui wa Mungu. Wao hufanya hivi ili kulinda sifa zao wenyewe, hadhi, faida, na raha za kimwili. Ni kama tu ilivyo leo. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amepanua kazi Yake ya siku za mwisho nchini China Bara, makundi makubwa ya waumini kutoka madhehebu mbalimbali ya kidini yamekuja kukubali kazi mpya ya Mungu. Wakati baadhi ya viongozi wa madhehebu haya wanaona watu zaidi na zaidi wakiikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho wakati makanisa yao yanapungua, wao hubuni kila aina za uongo na kashfa kuishutumu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ili waweze kulinda hadhi na mapato yao wenyewe. Hivi ndivyo wanavyowadanganya na kuwaogofya ndugu wa kiume na wa kike ili kuwafanya waogope kukubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho; kusudi lao ni kuitega na kuidhibiti mikusanyiko yao ya waumini. Watu hawa humtendea Mwenyezi Mungu kwa njia ile ile ambayo Mafarisayo walimtendea Bwana Yesu; wao ni Mafarisayo wa kisasa! Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba watu kwa kudhamiria na kwa makusudi hueneza uongo.
Kama tunashindwa kutambua uongo huu na kuufuata kwa upofu, basi tunasimama upande wa wale wanaoikashifu, kuipinga, na kuivuruga kazi ya Mungu. Hili halimsababishi mtu kupoteza wokovu wa Mungu katika siku za mwisho tu, pia humgeuza mtu kuwa lengo la chuki la Mungu na kukataliwa na adhabu. Hii ni kama tu kazi ya Bwana Yesu miongoni mwa watu wa Kiyahudi, ambapo Mafarisayo walibuni uongo wa aina zote na kashfa dhidi Yake, kama vile kusema kuwa uwezo wa Bwana Yesu wa kuwatoa pepo ulikuwa tu kwa sababu Alikuwa akifanya mizungu na mkuu wa pepo, Beelzebuli, pamoja na mambo mengine ya kukufuru. Kwa hiyo, watu wengi wa Kiyahudi walichukua njia mbovu ya kumpinga Mungu wakati walipokubali kwa upofu uongo wa Mafarisayo kwa sababu ya kukosa utambuzi na kukosa kuchunguza kwa uangalifu yale waliyoyaona na kwa hiyo wakawafuata Mafarisayo ili kumtelekeza na kumwua Bwana Yesu. Mafarisayo walieneza uongo na kashfa kuhusu Mungu, na sote tunajua ni mwisho upi waliokutana nao, lakini je wale Wayahudi waliouchukua uongo huo na kashfa kuwa ukweli, si mwisho wao ulikuwa tu wa kuhuzunisha vile vile? Taifa la Wayahudi liliangamizwa na watu wa Kiyahudi wakatawanywa pande zote. Walikuwa hawana nyumbani kwa kurudi kwa miaka 2,000 na waliadhibiwa na Mungu kama vile Mafarisayo walivyoadhibiwa. Si haya ni matokeo ya kuuchukua uongo wa Mafarisayo kuwa ukweli na kumpinga Mungu? Tunaweza kuona basi, kwamba wale wanaomwamini Mungu bila moyo wa kustahi na ambao hawatafuti kuchunguza kazi mpya ya Mungu na wale wanaoamini uongo kwa urahisi huwa ni washirika wa Shetani na huja kuwa watenda maovu ambao humpinga Mungu. Mwishwe, wataupoteza wokovu wa Mungu. Ni sawa leo kama ilivyokuwa wakati huo wa nyuma. Kama waumini na wafuasi wa Mungu, tunapokabiliana na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, tunapaswa kuitafuta na kuisoma kwa mioyo ya kustahi. Hii ndiyo njia ya pekee ya kusogelea jambo hili ikiwa tunataka kwenda sambamba na kazi ya Mungu na kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Vinginevyo tutakuwa kama Wayahudi katika siku za nyuma ambao walikuwa vyombo vilivyonyonywa na Shetani, waliompinga Mungu, na ambao walikuwa maadui wachungu wa Mungu na hivyo wakawa chini ya adhabu ya Mungu.
Tunapaswa kujua kwamba uvumi ni mojawapo ya mbinu za Shetani na kwamba uvumi ni moja ya mbinu zake za kuipinga kazi ya Mungu. Hata hivyo, hekima ya Mungu daima iko hatua moja mbele ya mbinu za Shetani. Shetani hawezi tu kutoivuruga kazi ya Mungu, lakini badala yake hufanya kazi ya Mungu kuwa na ufanisi zaidi. Kama vile waandishi wa Kiyahudi na Mafarisayo walivyojitahidi sana kuipinga na kuihukumu kazi ya Bwana Yesu; walishirikiana na Roma ili kumfanya Bwana Yesu asulubiwe, lakini hawakuwa na njia ya kujua umuhimu wa kweli wa wakati Bwana Yesu aliposema: "Limekwisha." Hili linatuonyesha kwamba Mungu alitumia hila ya Shetani ili kufanikisha mpango Wake mwenyewe na kuukamilisha ukombozi Wake wa wanadamu. Leo si tofauti. Ingawa kuna viongozi na wafanyakazi wenza katika madhehebu mbalimbali ya kidini ambao hutumia mbinu zao za makusudi na kutwezwa kubuni uongo na uvumi wa kuipinga kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku ya mwisho, hata hivyo, hakuna hata moja ya mbinu hizi ina uwezo wa kuathiri kazi ya Mungu. Badala yake, zina manufaa kwa kufanikiwa kwa kazi ya Mungu ya siku za mwisho ili kuainisha wanadamu kulingana na aina yao na kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Ingawa uongo wao umewadanganya baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike, watu wanaotaka kuonekana kwa Mungu kwa kweli hatimaye wamekuja kusimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Uongo unaweza kuunganisha "vigugu mwitu" kwa nguvu, lakini uongo huu haufanyi vivyo hivyo kwa "nafaka za ngano." Upepo hupeperusha makapi kwenda nje, papo hapo mbegu nene zitakusanywa kwenye ghala hatimaye. Kuliweka kwa njia nyingine, uongo utawafichua na kuwaondosha wale ambao si wa Mungu, ambao hawana uchaji kwa Mungu, na wafuata kanuni. Lakini kwa wale watafuta ukweli wa kweli ambao wana kiu ya kuonekana kwa Mungu, watachukuliwa na Mungu kwelekea kwa hatima nzuri. Kwa namna hii, mbinu za Shetani huishia tu kusaidia kukamilisha kazi ya Mungu katika siku za mwisho ya kuainisha wanadamu kulingana na aina yao, na pia kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu, si huu ni mfano mkubwa wa uweza wa Mungu na hekima?
Tutamalizia ushirika wetu hapa. Naamini kuwa nyote mnapokabiliwa na uvumi mtaelewa chanzo chake, kiini chake, na madhara yake! Na sasa, kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho imefikia upeo mpya usio na kifani na unajongelea mwisho wake mtukufu na Mwenyezi Mungu atajifichua Mwenyewe kwa mataifa yote na watu wote kuona. Kwa wakati muhimu kama huo, uko radhi kupoteza maisha yako na kutelekeza wokovu wa Mungu wa siku za mwisho ili tu kuamini uvumi fulani? Ninajua kwamba utafanya chaguo la hekima.
Kuondoa Ukungu ili kuona Mwanga wa Kweli


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni