Jibu:
Ndugu, ikija kwa kungoja kushuka kwa Bwana na mawingu, lazima tusitegemee mawazo ya mwanadamu na fikira! Mafarisayo walifanya kosa kubwa kwa kungoja kufika kwa Masiha. Walitumia kabisa mawazo na fikira ya mwanadamu kumtathmini Bwana Yesu ambaye alisharudi tayari. Mwishowe, walimsulubisha Bwana Yesu msalabani. Je, huu sio ukweli? Je, kungoja kufika kwa Bwana ni rahisi kama tufikiriavyo? Ikiwa Bwana atarudi na kufanya kazi kati ya binadamu kama jinsi Bwana Yesu kwa mwili Alikuwa Amefanya, na hatumtambui Yeye, basi pia sisi tutamhukumu na kumshutumu Yeye kama vile Mafarisayo walivyofanya na kumsulubisha Yeye mara nyingine? Je, hu ni uwezekano? Bwana Yesu alitabiri kuwa Atarudi na Akasema maneno mengi kuihusu, lakini nyinyi mnashikilia tu unabii kuwa Bwana atashuka na mawingu na hamtafuti na kuchunguza nabii zingine muhimu zilizoongelewa na Bwana. Hii inafanya kutembea katika njia mbaya kuwa rahisi na kuachwa na Bwana! Kweli sio tu unabii wa "kushuka na mawingu" ndiyo upo katika Biblia. Kuna unabii mwingi kama huo kuwa Bwana atakuja kama mwizi na kushuka kwa siri. Kwa mfano, Ufunuo 16:15, "Tazama, Mimi nakuja kama mwizi." Mathayo 25:6, "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha." Na Ufunuo 3:20, "Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi." Unabii huu wote unarejelea Mungu kuwa mwili kama Mwana wa Adamu na kushuka kwa siri. "Kama mwizi" kunamaanisha kuja kwa upole, kwa siri. Watu hawatajua kuwa Yeye ni Mungu hata kama watamwona au kumsikia, kama tu ilivyokuwa awali wakati Bwana Yesu alitokea na kufanya kazi Yake. Kutoka nje, Bwana Yesu alikuwa tu Mwana wa Adamu wa kawaida na hakuna yeyote alijua Yeye ni Mungu, ndiyo sababu Bwana Yesu alitumia "kama mwizi" kama analojia ya kutokea na kazi ya Mwana wa Adamu. Hii ni inastahili sana! Wale ambao hawapendi ukweli, bila kujali jinsi Mungu katika mwili anavyoongea au kufanya kazi, au ukweli ngapi Anaoonyesha, hawakubali. Badala yake, wanamchukulia Mungu mwenye mwili kama mtu wa kawaida na kumshutumu na kumwacha Yeye. Hiyo ndiyo sababu Bwana Yesu alitabiri kuwa Atarudi: "Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki" (LK. 17:24-25). Kulingana na unabii wa Bwana, kurudi Kwake kutakuwa "kuja kwake Mwana wa Adamu." "Mwana wa Adamu" inarejelea Mungu katika mwili, sio mwili wa kiroho uliofufuka wa Bwana Yesu ukishuka na mawingu kuonekana wazi mbele ya watu wote. Mbona hali ni hii? Hebu tuzungumze kuihusu. Ikiwa ungekuwa mwili wa kiroho uliofufuka wa Bwana Yesu ambao ungekuwa unashuka kwa watu wote na mawingu, ingekuwa nguvu ya ajabu na ya kushtua ulimwengu. Kila mtu angeanguka chini na hakuna yeyote atathubutu kukataa. Kwa hali hiyo, je, Bwana Yesu aliyerudi bado Atastahimili mateso mengi na kukataliwa na kizazi hiki? Hiyo ndiyo sababu Bwana Yesu alitabiri kuwa kurudi Kwake kutakuwa "kuja kwake Mwana wa Adamu" na "kama mwizi." Kwa kweli, inarejelea Mungu mwenye mwili kama Mwana wa Adamu kufika kwa siri.