Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Roho Mtakatifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Roho Mtakatifu. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 19 Juni 2019

2. Kwa nini inasemekana kwamba “Utatu” ni kauli ya upuuzi zaidi?

XVI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kama Mungu Kweli ni Mungu wa Utatu au ni Mungu Mmoja wa Kweli
2. Kwa nini inasemekana kwamba “Utatu” ni kauli ya upuuzi zaidi?
Maneno Husika ya Mungu:
Baada ya ukweli wa Yesu aliyepata mwili kutokea, mwanadamu aliamini hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili. Bila Baba Mtakatifu, Mungu asingekuwa mkamilifu. Vivyo hivyo, wala Mungu asingekuwa mkamilifu bila Mwana au Roho Mtakatifu. Katika mawazo yao, wanaamini kuwa Baba au Mwana pekee hawezi kuwa Mungu. Ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu tu kwa pamoja wanaoweza kuwa Mungu Mwenyewe. … Kwa karne nyingi, mwanadamu ameamini katika huu Utatu, ambao umebuniwa na mawazo katika akili za mwanadamu, ukatengenezwa na mwanadamu, na ambao haujawahi kuonekana na mwanadamu. Kwa miaka mingi, kumekuwa na watu maarufu wa kiroho ambao wameeleza “maana ya kweli” ya Utatu, ila maelezo hayo ya Utatu kama nafsi tatu dhahiri yamekuwa si yakini na hayapo wazi na watu wote wamepumbazwa na “ujenzi” wa Mungu. Hakuna mtu maarufu yeyote aliyewahi kutoa maelezo kamili; maelezo mengi yanafaa katika masuala ya mjadala na katika maandishi, ila hakuna hata mtu mmoja ambaye ana ufahamu kamili na wa wazi kuhusu maana ya Utatu. Hii ni kwa sababu huu Utatu huu mkuu ambao mwanadamu anashikilia moyoni kwa hakika haupo.

Jumatano, 12 Juni 2019

3. Ni nini hasa mtu anayefuata mapenzi ya Mungu? Na ushahidi wa kweli wa imani katika Mungu ni nini?

XVIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kilicho Kufuata Mapenzi ya Mungu na Kilicho Ushahidi wa Kweli wa Imani katika Mungu
3. Ni nini hasa mtu anayefuata mapenzi ya Mungu? Na ushahidi wa kweli wa imani katika Mungu ni nini?
Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu, Naye akasema, Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi; Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” (Ayubu 1:20-21).


Jumatatu, 10 Juni 2019

2. Kwa nini ulimwengu wa kidini daima umemkana Kristo, kumkataa na kumhukumu Yeye, na hivyo kupitia laana za Mungu?

XIX. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Ukweli wa ni Kwa Nini Njia ya Kweli Imepitia Usumbufu Tangu Nyakati za Kale
2. Kwa nini ulimwengu wa kidini daima umemkana Kristo, kumkataa na kumhukumu Yeye, na hivyo kupitia laana za Mungu?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Sikizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mwenye nyumba fulani, aliyepanda shamba la zabibu, na akalizingira kwa ua, na akachimba kishinikizo cha zabibu ndani yake, na akajenga mnara, na akalipangisha kwa wakulima, na akasafiri kwenda nchi ya mbali: Na wakati wa matunda ulipokaribia, aliwatuma watumwa wake kwa wakulima, ili waweze kupokea matunda yake. Na wakulima wakawachukua watumwa wake, wakampiga mmoja, na kumuua mwingine, na kumpiga mwingine kwa mawe. Tena, akawatuma watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza: na wakawafanyia vivyo hivyo. Lakini mwishowe kabisa alimtuma mwanawe kwao, akisema, Watamheshimu mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona mwana huyo, walisema miongoni mwao, Huyu ndiye mrithi; njooni, tumuue, na tutwae urithi wake. Na wakamshika, wakamtupa nje ya shamba la zabibu, na wakamchinja”
(Mathayo 21:33-39).

Jumanne, 4 Juni 2019

26. Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii kwa moyo wake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika.