Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Siku-za- Mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Siku-za- Mwisho. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 3 Oktoba 2019

2. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

2. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

Aya za Biblia za Kurejelea:

    “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

    “Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao. Nayo bahari ikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani yake; na kifo na kuzimu zikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani zao: na kila mtu alihukumiwa kulingana na vitendo vyake. Na kifo na kuzimu zikarushwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili. Na yeyote ambaye hakupatikana ameandikwa ndani ya kitabu cha uzima alirushwa katika ziwa la moto” (Ufunuo 20:11-15).

Jumapili, 15 Septemba 2019

Swali la 6: Mungu alimtumia Musa kufanya kazi ya Enzi ya Sheria, hivyo kwa nini Mungu hawatumii watu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lakini badala yake Analazimika kupata mwili ili kuifanya Mwenyewe?

Jibu:

    Ni kwa nini lazima Mungu apate mwili ili kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho? ni swali ambalo wengi walio na kiu ya ukweli na wanatafuta kuonekana kwa Mungu wanalijali sana. Pia ni swali linalohusiana na kama tunaweza kunyakuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuelewa kipengele hiki cha ukweli. Ni kwa nini lazima Mungu ajipatie mwili ili kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho badala ya kumtumia mwanadamu kuifanya kazi Yake? Hili linaamuliwa na hali ya kazi ya hukumu. Kwa sababu kazi ya hukumu ni onyesho la Mungu la ukweli na onyesho la tabia Yake yenye haki ili kuwashinda, kuwatakasa, na kuwaokoa wanadamu. Hebu tusome vifungu vichache kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu.