Na Bong, Philippines
“Mwalimu mkuu, tafadhali mpe mwanangu fursa na kumruhusu afanye mtihani!” Macho ya mama yangu yalimsihi mwalimu mkuu alipokuwa akizungumza kwa sauti ya kutetemeka kidogo.
Bila kuonyesha hisia, mwalimu mkuu akasema, “Hapana, shule ina kanuni. Mtoto anaweza kufanya mtihani tu wakati ada ya mtihani imelipwa!”
Mama yangu alionekana mwenye kutayahari na kumsihi mwalimu mkuu, akisema, “Mwalimu mkuu, najua hili ni gumu sana kwako shuleni pia, lakini nina watoto wengi na sisi huweza kuishi kwa shida tu. Hatuwezi kwa kweli kumudu kulipa ada hii ya mtihani. Mbona nisiiandikie shule cheti cha ‘Naahidi Kulipa Deni’, umruhusu mwanangu afanye mtihani, nami nitajua jinsi ya kuwalipa haraka iwezekanavyo ….”