Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neema-ya-mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neema-ya-mungu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 17 Agosti 2019

2. Kristo ni Mwana wa Mungu au ni Mungu Mwenyewe?

IX. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kwamba Kristo ni Onyesho la Mungu Mwenyewe

2. Kristo ni Mwana wa Mungu au ni Mungu Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:

   “Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, na hiyo itatutosha. Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo. Niamini kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi, la sivyo niamini kwa ajili ya kazi hizo” (Yohana 14:8-11).

Alhamisi, 20 Juni 2019

1. Mungu wa kweli aliyeziumba mbingu na ardhi na vitu vyote ni mmoja au watatu?

XVI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kama Mungu Kweli ni Mungu wa Utatu au ni Mungu Mmoja wa Kweli
1. Mungu wa kweli aliyeziumba mbingu na ardhi na vitu vyote ni mmoja au watatu?
Aya za Biblia za Kurejelea:

“Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, na hiyo itatutosha. Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo” (Yohana 14:8-10).

Alhamisi, 13 Juni 2019

2. Ni ushuhuda wa kweli wa imani katika Mungu kama mtu hufurahia neema ya Mungu tu?

XVIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kilicho Kufuata Mapenzi ya Mungu na Kilicho Ushahidi wa Kweli wa Imani katika Mungu
2. Ni ushuhuda wa kweli wa imani katika Mungu kama mtu hufurahia neema ya Mungu tu?
Maneno Husika ya Mungu:

Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haijafaulu. Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Na Bong, Philippines
Nataka Kuwa Tajiri
“Mwalimu mkuu, tafadhali mpe mwanangu fursa na kumruhusu afanye mtihani!” Macho ya mama yangu yalimsihi mwalimu mkuu alipokuwa akizungumza kwa sauti ya kutetemeka kidogo.
Bila kuonyesha hisia, mwalimu mkuu akasema, “Hapana, shule ina kanuni. Mtoto anaweza kufanya mtihani tu wakati ada ya mtihani imelipwa!”
Mama yangu alionekana mwenye kutayahari na kumsihi mwalimu mkuu, akisema, “Mwalimu mkuu, najua hili ni gumu sana kwako shuleni pia, lakini nina watoto wengi na sisi huweza kuishi kwa shida tu. Hatuwezi kwa kweli kumudu kulipa ada hii ya mtihani. Mbona nisiiandikie shule cheti cha ‘Naahidi Kulipa Deni’, umruhusu mwanangu afanye mtihani, nami nitajua jinsi ya kuwalipa haraka iwezekanavyo ….”

Jumapili, 2 Juni 2019

Kupitia Utunzaji wa Uangalifu wa Mungu wa Wokovu wa Mwanadamu katika Maafa

Muling , Beijing
Agosti 16, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, Beijing ilipata mvua kubwa zaidi katika miaka sitini. Katika mvua hiyo kubwa niliona matendo ya Mungu na kuona jinsi Yeye huwaokoa mwanadamu.
Siku hiyo adhuhuri, dada zangu watatu na mimi tulikuwa tumekutana. Nje mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha. Saa kumi u nusu jioni mume wangu, ambaye hakuwa muumini, alirudi akitwambia kwamba kulikuwa na maji mengi kwa mzunguko kiasi kwamba watu hawakuweza kupitia. Hata hivyo, saa kumi na moja jioni aliondoka kwa haraka sana kwenda kwa zamu yake ya usiku kazini. Wakati huo sikuhisi kitu chochote kisicho cha kawaida, na nilienda kupika chakula cha jioni kama kawaida. Saa moja usiku, mpangaji wetu kwa ghafla alibisha mlango akiniita, na nilipotoka kuangalia, kile nilichoona kilinipa mshtuko mkubwa: Maji ya mvua yalikuwa tayari yamejaza ua na yalikuwa yakiingia kwa pembe za mashariki na magharibi za nyumba, wakati maji yaliyokuwa juu ya ardhi yaliendelea kuongezeka. Mwanangu wa kiume nami tulijaribu kuzuia mtiririko wa maji, lakini hatukufaulu.