Alhamisi, 13 Juni 2019

2. Ni ushuhuda wa kweli wa imani katika Mungu kama mtu hufurahia neema ya Mungu tu?

XVIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kilicho Kufuata Mapenzi ya Mungu na Kilicho Ushahidi wa Kweli wa Imani katika Mungu
2. Ni ushuhuda wa kweli wa imani katika Mungu kama mtu hufurahia neema ya Mungu tu?
Maneno Husika ya Mungu:

Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haijafaulu. Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.

kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu. Baadhi wanaweza kutoshelezwa na amani na furaha ya mwili, maisha yenye furaha bila ya dhiki au msiba, huku wakiishi kwa amani na familia zao bila ya mapigano au ugomvi. Wanaweza hata kuamini kwamba hii ni baraka ya Mungu, lakini kwa kweli, ni neema ya Mungu tu. Hamwezi kutosheka tu kwa kufurahia neema ya Mungu. Kufikiria kwa aina hii ni kuchafu mno. Hata ukisoma neno la Mungu kila siku, uombe kila siku, na roho yako ihisi furaha na amani halisi, ilhali mwishowe huwezi kuzungumzia maarifa yoyote ya Mungu na kazi Yake au hujapata uzoefu wa mambo kama hayo, na haijalishi ni kiasi gani cha neno la Mungu ambacho umekula na kunywa, ukihisi tu amani na furaha katika roho yako na kwamba neno la Mungu ni tamu mno kiasi kwamba haliwezi kulinganishwa na kingine chochote, kana kwamba huwezi kulifurahia ukatosheka, lakini huna uzoefu halisi na huna hakika yoyote na neno la Mungu, basi ni nini unachoweza kupokea kutoka kwa aina hii ya imani katika Mungu? Kama huwezi kuishi kwa kudhihirisha kiini cha neno la Mungu, kula na kunywa kwako kwa maneno ya Mungu na maombi vyote vinahusu dini. Basi binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa na hawezi kupatwa na Mungu.

kutoka katika “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu ambao hawafanyi kitu zaidi ya kufurahia neema za Mungu hawawezi kukamilishwa, au kubadilishwa, na utii wao, uchaji Mungu, na upendo na ustahimilivu vyote hivyo ni vya juujuu tu. Wale ambao wanafurahia tu neema za Mungu hawawezi kumfahamu Mungu kweli, na hata pale wanapomjua Mungu, maarifa yao ni ya juujuu, na wanasema mambo kama vile Mungu anampenda mwanadamu, au Mungu ni mwenye huruma kwa mwanadamu. Hii haiwakilishi maisha ya mwanadamu, na haionyeshi kwamba kweli watu wanamjua Mungu. Ikiwa, maneno ya Mungu yatakapowasafisha, au majaribu yake yatakapowajia, watu hawataweza kumtii Mungu—ikiwa, badala yake, watakuwa watu wa mashaka na kuanguka chini—basi hawana utii hata kidogo.

kutoka katika “Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu huona tu kupata neema na furaha ya amani kama ishara ya imani katika Mungu, na kutafuta baraka kama msingi wa imani katika Mungu. Watu wachache sana wanatafuta kumjua Mungu au kutafuta mabadiliko katika tabia zao. Imani ya watu katika Mungu hutafuta kumfanya Mungu kuwapa hatima inayofaa, kuwapa neema yote chini ya jua, kumfanya Mungu mtumishi wao, kumfanya Mungu adumishe uhusiano wa amani, wa kirafiki pamoja nao, na ili kusiwe na mgogoro wowote kati yao. Yaani, imani yao kwa Mungu inahitaji Mungu kutoa ahadi ya kutimiza mahitaji yao yote, kuwapa chochote wanachoomba, kama ambavyo inasema katika Biblia “Nitazisikiliza sala zenu zote.” Wanahitaji Mungu kutomhukumu mtu yeyote au kushughulika na mtu yeyote, kwa kuwa Mungu daima ni Mwokozi Yesu mkarimu, ambaye huwa na uhusiano mzuri na watu wakati wote na mahali pote. Wanavyoamini ni hivi: Wao daima humwomba Mungu vitu bila haya, na Mungu huwapa kila kitu kwa upofu, kama wao ni waasi au watiifu. Watu daima wanataka “malipo” kutoka kwa Mungu na Mungu lazima Alipe bila upinzani wowote, na kulipa mara dufu, kama Mungu amepata chochote kutoka kwao au la. Anaweza tu kuwa chini yao; Hawezi kuwapanga watu kiholela, sembuse Hawezi kuwafunulia watu hekima Yake ya kale ya siri na tabia ya haki kama Anavyotaka, bila ruhusa yao. Wao huungama tu dhambi zao kwa Mungu na Mungu huwasamehe tu, na Hawezi kuchoshwa na hilo, na hii inaendelea milele. Wanamwamuru Mungu tu na Yeye anatii tu, kama ilivyonakiliwa katika Biblia ikisema “Kuja kwa Mungu si kumfanya mtu amsubiri, bali ili Yeye amsubiri mwanadamu. Amekuja kumtumikia mwanadamu.” Je, si siku zote mmeamini kwa njia hii? Wakati ambapo hamuwezi kupata chochote kutoka kwa Mungu basi mnataka kukimbia. Na wakati ambapo hamuelewi kitu mnapata hasira, na hata kwenda mbali ili kutoa aina zote za matusi. Hamuwezi tu kumruhusu Mungu Mwenyewe kuonyesha kikamilifu hekima na shani Yake, lakini badala yake unataka tu kufurahia urahisi wa muda na faraja. Hadi sasa, mtazamo wenu katika imani yenu kwa Mungu umekuwa sawa na maoni ya zamani. Mungu akiwaonyesha utukufu mdogo tu mnakosa furaha; je, mnaona sasa jinsi kimo chenu kilivyo? Msifikiri kuwa ninyi nyote ni waaminifu kwa Mungu wakati kwa kweli maoni yenu ya zamani hayajabadilika. Wakati ambapo hakuna chochote kibaya kinachokuangukia, unafikiri kwamba kila kitu kinaelekea kwa urahisi na unampenda Mungu kwa vilele vya juu zaidi. Lakini kitu kidogo kinapokukumba, unakushuka kuzimuni. Je, hii ni wewe kuwa mwaminifu kwa Mungu?

kutoka katika “Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wengi huamini katika Mungu kwa ajili ya amani na manufaa mengine. Isipokuwa kwa manufaa yako, wewe huamini katika Mungu, na ikiwa huwezi kupokea neema za Mungu, wewe huanza kununa. Hiki kingekuwaje kimo chako halisi? Inapofikia matukio ya familia yasiyoepukika (watoto kuwa wagonjwa, mume kwenda hospitalini, mazao mabaya ya mimea, kuteswa kwa watu wa familia, na kadhalika), huwezi hata kufaulu katika mambo haya ambayo hufanyika mara kwa mara katika maisha ya kila siku. Wakati ambapo mambo hayo hufanyika, wewe huingia katika hofu kubwa, hujui la kufanya—na wakati mwingi, wewe hulalamika kuhusu Mungu. Wewe hulalamika kwamba maneno ya Mungu yalikudanganya, kwamba kazi ya Mungu imekuvuruga wewe. Je, hamna mawazo kama haya? Unadhani mambo kama haya hufanyika miongoni mwenu mara chache tu? Mnatumia kila siku kuishi katikati ya matukio kama haya. Hamfikirii hata kidogo sana kuhusu mafanikio ya imani yenu katika Mungu, na namna ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Kimo chenu halisi ni kidogo sana, hata kidogo zaidi kuliko cha kifaranga mdogo. Wakati ambapo biashara ya waume zenu hupoteza pesa ninyi hulalamika kuhusu Mungu, wakati ambapo ninyi hujikuta katika mazingira yasiyo na ulinzi wa Mungu ninyi bado hulalamika kuhusu Mungu, ninyi hulalamika hata wakati ambapo mmoja wa vifaranga wenu hufa au ng’ombe mzee ndani ya zizi anapougua, ninyi hulalamika kama ni wakati wa wana wenu kuanzisha familia lakini familia yenu haina pesa za kutosha, na wakati ambapo wafanyakazi wa kanisa hula milo kadhaa nyumbani kwako lakini kanisa halikulipi au hakuna anayekutumia mboga zozote, wewe hulalamika pia. Tumbo lako limeshindiliwa pomoni na malalamiko, na wakati mwingine wewe huendi katika mikutano au kula na kunywa maneno ya Mungu kwa sababu ya hili, wewe huelekea kuwa mbaya kwa muda mrefu sana. Hakuna chochote kinachokufanyikia leo hii kilicho na uhusiano wowote na matazamio au majaliwa yako; mambo haya yangefanyika pia ikiwa hungeamini katika Mungu, ilhali leo hii unampitishia Mungu wajibu wa haya mambo, na kusisitiza kusema kwamba Mungu amekuondosha wewe. Na kuhusu imani yako katika Mungu, je, umeyatoa maisha yako kwa kweli? Mngepitia majaribio sawa na yale ya Ayubu, hakuna hata mmoja miongoni mwenu anayemfuata Mungu leo hii angeweza kusimama imara, nyote mngeanguka chini. Na kunayo, kawaida kabisa, tofauti kubwa kati ya ninyi na Petro. Leo, kama nusu ya mali yenu ingetwaliwa mngethubutu kukana kuwepo kwa Mungu; kama mtoto wenu wa kiume au wa kike angechukuliwa kutoka kwenu, mngekimbia barabarani mkilalamika vikali; kama maisha yako yangegonga mwamba, ungejaribu kuanza kujadiliana mada hiyo na Mungu, ukiuliza kwa nini Nilisema maneno mengi sana hapo mwanzo kukutisha wewe. Hakuna kitu chochote ambacho hamngethubutu kufanya katika nyakati kama hizi. Hili linaonyesha kwamba hamjaona kwa kweli, na hamna kimo cha kweli.

kutoka katika “Utendaji (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Umetosheka kuishi katika ushawishi wa Shetani, kwa amani na furaha, na raha kidogo ya kimwili? Je, wewe si mtu wa chini zaidi kati ya watu wote? Hakuna aliye mpumbavu kuliko wale ambao wameona wokovu lakini hawaufuati ili kuupata: Ni watu ambao wanalafua mwili na kufurahia Shetani. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote?

kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Leo mwanadamu huona kwamba na neema, upendo na rehema ya Mungu pekee, hana uwezo wa kujijua mwenyewe kweli, sembuse kuweza kujua kiini cha mwanadamu. Ni kupitia tu usafishaji na hukumu ya Mungu, ni wakati tu wa usafishaji kama huo ndiyo unaweza kujua kasoro zako, na kujua kwamba huna chochote. Hivyo, upendo wa mwanadamu kwa Mungu umejengwa juu ya msingi wa usafishaji na hukumu ya Mungu.

kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika uzoefu wako utaona kwamba wale ambao wanakabiliwa na usafishaji mkubwa na uchungu, na kushughulikiwa sana na kufundishwa nidhamu, wana upendo mkubwa kwa Mungu, na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wanaweza tu kusema: “Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye.” Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuyazungumza maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Kadiri inavyokosa kupenyeza kwako zaidi na kadiri isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda, kukupata, na kukufanya mkamilifu.

kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Je sasa mnaelewa imani kwa Mungu ni nini? Je kuamini Mungu ni kuona ishara na maajabu? Je ni kupanda mbinguni? Kuamini Mungu sio rahisi hata kidogo. Zile desturi za kidini lazima zitakaswe; kufuata uponyaji wa wagonjwa na kukemea mapepo, kusisitiza ishara na maajabu, kutamani zaidi neema, amani na furaha ya Mungu, kufuata mandhari na raha za mwili—haya ni matendo ya kidini, na matendo haya ya aina hii ya kidini ni aina ya imani isiyo dhahiri. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: Imani katika Mungu ni ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata.

kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni