1. Kufuata mapenzi ya Mungu ni nini? Ni kufuata mapenzi ya Mungu kama mtu anatekeleza kazi ya misheni kwa ajili yaBwana?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda” (Mathayo 22:37-39).
“Kama mwanadamu ananipenda, atayazingatia maneno yangu…. Yeye asiyenipenda hayazingatii maneno yangu” (Yohana 14:23-24).
“Mkidumu katika neno langu, basi ninyi ni wanafunzi wangu kweli …” (Yohana 8:31).
“Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni. Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu” (Mathayo 7:21-23).
Maneno Husika ya Mungu:
Hivi sasa, njia ambayo Roho Mtakatifu
hutembea ni maneno halisi ya Mungu. Kwa hiyo, kwa mtu kuitembea, ni lazima atii, na kula na kunywa maneno halisi ya Mungu mwenye mwili. Anafanya kazi ya neno, na kila kitu kinaanza kutoka kwa neno Lake, na kila kitu kinaanzishwa juu ya neno Lake, neno Lake la sasa. Kama ni kuwa bila shaka yoyote kabisa kuhusu Mungu kuwa mwili au kumjua Yeye, mtu anapaswa kuweka bidii zaidi katika maneno Yake. Vinginevyo, hawezi kutimiza chochote kamwe, na ataachwa bila chochote. Ni kwa kuja kumjua Mungu tu na kumridhisha kwa msingi wa kula na kunywa maneno Yake ndipo mtu anaweza kuanzisha polepole uhusiano unaofaa na Yeye. Kula na kunywa maneno Yake na kuyaweka katika matendo ni ushirikiano bora zaidi na Mungu, na ni kitendo kinachotoa ushuhuda vizuri zaidi kama mmoja wa watu Wake. Mtu akielewa na aweze kutii kiini cha maneno halisi ya Mungu, anaishi katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu na ameingia katika njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu.
…………
Ikiwa unaweza kukubali kile Mungu anakuaminia wewe, kukubali ahadi Yake, na kufuata njia ya Roho Mtakatifu, hii ni kufanya mapenzi ya Mungu.
kutoka katika “Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kila enzi, Mungu huwapa binadamu baadhi ya maneno Anapofanya kazi ulimwenguni, huku akimwambia mwanadamu kuhusu baadhi ya ukweli. Ukweli huu unahudumu kama njia ambayo binadamu anafaa kuitii, njia ya kutembelewa na binadamu, njia ambayo humwezesha binadamu kumcha Mungu na kujiepusha na uovu, na njia ambayo watu wanafaa kuweka katika vitendo na kuitii katika maisha yao na kwenye mkondo wa safari zao za maisha. Ni kwa sababu hizi ambapo Mungu anampa binadamu maneno haya. Binadamu anafaa kuyatii maneno haya yanayotoka kwa Mungu, na kuyatii ni kupokea uzima. Kama mtu hataweza kuyatii, na hayatii kwenye matendo, na haishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu katika maisha yake, basi mtu huyo hautilii ukweli katika matendo. Na kama hawatilii ukweli katika matendo, basi hawamchi Mungu na hawaepuki uovu, wala hawawezi kumtosheleza Mungu. Kama mtu hawezi kumtosheleza Mungu, basi hawezi kupokea sifa ya Mungu; mtu wa aina hii hana matokeo.
kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kutembea katika njia ya Mungu hakuhusu kuangalia sheria juujuu. Badala yake, kunamaanisha kwamba unapokabiliwa na suala, kwanza kabisa, unaliangalia kama ni hali ambayo imepangwa na Mungu, wajibu uliopewa wewe na Yeye, au kitu ambacho Amekuaminia wewe, na kwamba unapokabiliana na suala hili, unapaswa kuliona kama jaribio kutoka kwa Mungu. Wakati unapokabiliwa na suala hili, lazima uwe na kiwango, lazima ufikirie kwamba suala hilo limetoka kwa Mungu. Lazima ufikirie ni vipi ambavyo utashughulikia suala hili kiasi cha kwamba unaweza kutimiza wajibu wako, na kuwa mwaminifu kwa Mungu; namna ya kulifanya bila ya kumghadhabisha Mungu; au kukosea tabia Yake.
kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Ingawa imani hii ni sahihi, ni ya kuegemea upande mmoja sana; kile ambacho Mungu anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu; ni huduma zaidi na kujitoa ndani ya roho. … Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu alio nao kwa Mungu na maarifa aliyo nayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu, na yote ambayo mwanadamu anapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupata uzoefu wa Mungu sio tu kuweza kula na kunywa neno Lake; na muhimu zaidi, mnapaswa kuweza kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia na kumkimu mwanadamu. Hii ni kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza. Kuna watu wengi ambao wanatilia mkazo tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu, lakini hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuza kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu.
kutoka katika “Kazi na Kuingia (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Fikiria kwamba wewe unaweza kumfanyia Mungu kazi, ilhali wewe humtii Mungu, na huna uwezo wa kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa njia hii, wewe hutakuwa tu umekosa kutimiza wajibu wa kiumbe cha Mungu, lakini pia utalaaniwa na Mungu, kwa kuwa wewe ni mtu ambaye hana ukweli, ambaye hana uwezo wa kumtii Mungu, na ambaye si mtiifu kwa Mungu. Wewe unajali tu kuhusu kumfanyia Mungu kazi, na hujali kuhusu kuweka ukweli katika vitendo, ama kujifahamu. Wewe humfahamu ama kumjua Muumba, na humtii ama kumpenda Muumba. Wewe ni mtu ambaye asilia si mtiifu kwa Mungu, na hivyo watu kama hawa hawapendwi na Muumba.
kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.
kutoka katika “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” katika Neno Laonekana katika Mwili
Baadhi ya watu husema, “Paulo alifanya kazi kubwa kiasi cha ajabu, na alibeba mizigo mikubwa ya makanisa na aliwachangia mno. Nyaraka kumi na tatu ya Paulo zilizingatia miaka 2,000 ya Enzi ya Neema, na ni za pili tu baada ya Injili Nne. Nani anaweza kulinganishwa naye? Hakuna ambaye anaweza kufumbua maandiko ya Ufunuo wa Yohana, ilhali nyaraka za Paulo zinatoa maisha, na kazi ambayo alifanya ilikuwa na manufaa kwa makanisa. Ni nani mwingine angeweza kutimiza mambo kama haya? Na kipi ambacho Petro alikifanya?” Mwanadamu anapowapima wengine, ni kwa mujibu wa michango yao. Mungu anapompima mwanadamu, ni kwa mujibu wa asili yake. Miongoni mwa wale ambao hutafuta uzima, Paulo alikuwa mtu ambaye hakujua kiini chake mwenyewe. Hakuwa kwa njia yoyote mnyenyekevu ama mtiifu, wala kujua kiini chake, ambacho kilikinzana na Mungu. Na kwa hivyo, alikuwa mtu ambaye hakuwa amepitia matukio ya kina, na alikuwa mtu ambaye hakuweka ukweli katika vitendo. Petro alikuwa tofauti. Yeye alijua kutokamilika kwake, udhaifu, na tabia yake potovu kama kiumbe wa Mungu, na hivyo alikuwa na njia ya vitendo ambayo angebadilishia tabia yake; hakuwa mmoja wa wale ambao walikuwa tu na mafundisho ya kidini lakini hawakuwa na uhalisi. Wale ambao hubadilika ni watu wapya ambao wameokolewa, ni wale ambao wana sifa zinazostahili katika kufuatilia ukweli. Watu ambao hawabadiliki ni wa wale ambao hawafai kwa sasa kiasili; ni wale ambao hawajaokolewa, yaani, ni wale ambao wamechukiwa na kukataliwa na Mungu. Hawatawekwa kwenye ukumbusho na Mungu bila kujali jinsi kazi zao ni kubwa. Wakati unapolinganisha haya na harakati yako mwenyewe, kama wewe hatimaye ni mtu wa aina sawa na Petro au Paulo inapaswa kuwa dhahiri kibinafsi. Kama bado hakuna ukweli kwa yale unayotafuta, na kama hata leo bado wewe ni mwenye kiburi na jeuri kama Paulo, na bado wewe ni mwepesi wa kusema bila kusema ukweli na mwenye kujitukuza kama yeye, basi bila shaka wewe ni aliyeharibika tabia na ambaye hushindwa. Kama wewe hutafuta jinsi sawa na Petro, kama unatafuta vitendo na mabadiliko ya kweli, na usiwe mwenye kiburi au mkaidi, bali utafute kutekeleza majukumu yako, basi utakuwa kiumbe wa Mungu ambaye anaweza kufikia ushindi.
kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ukiishi daima kulingana na mwili, daima kuridhisha tamaa zako mwenyewe za binafsi, basi mtu kama huyo hana uhalisi wa ukweli. Hii ni alama ya mtu ambaye anamwaibisha Mungu. Unasema, “Sijafanya chochote; nimemwaibisha Mungu vipi?” Katika mawazo na fikira zako, katika nia, malengo na sababu za matendo yako, na katika matokeo ya yale ambayo umeyafanya—katika kila njia unamridhisha Shetani, ukiwa kichekesho chake, na kumwacha ajue jambo litakalokuathiri. Huna ushuhuda unaopaswa kuwa nao kama Mkristo hata kidogo. Unafedhehesha jina la Mungu katika mambo yote na huna ushuhuda wa kweli. Je, Mungu atakumbuka mambo ambayo umeyafanya? Mwishowe, Mungu atakuwa na uamuzi upi kuhusu matendo yako na wajibu ambao umetimiza? Je, hakupaswi kuwa na matokeo ya hayo, aina fulani ya maelezo? Katika Biblia, Bwana Yesu anasema, “Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Kwa nini Bwana Yesu alisema hili? Kwa nini wale wanaowaponya wagonjwa na kuwatoa mapepo katika jina la Bwana, ambao wanasafiri kuhubiri katika jina la Bwana, wanageuka kuwa watenda maovu? Hawa watenda maovu ni nani? Je, ni wale wasiomwamini Mungu? Wote wanamwamini Mungu na kumfuata Mungu. Pia wanatelekeza vitu kwa ajili ya Mungu, kujitumia kwa ajili ya Mungu, na kutimiza wajibu wao. Hata hivyo, katika kutimiza wajibu wao wanakosa moyo na ushuhuda, kwa hiyo imekuwa kutenda maovu. Hii ndiyo maana Bwana Yesu alisema, “Tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.”
kutoka katika “Unaweza Kupata Ukweli Baada ya Kumkabidhi Mungu Moyo Wako Halisi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale kati yenu ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Kinyume cha hayo, Mimi Huwatendea wale ambao hawajatosheleza madai Yangu kwa adhabu, siyo zawadi, sembuse huruma yoyote. Labda mnawaza kwamba kwa kuwa wafuasi kwa miaka mingi mnaweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote hadi sasa mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na kutokuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na mwanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa bora zaidi Niigeuze miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa utupu, kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo.
kutoka katika “Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Baadhi ya watu wataishia kusema, “Mimi nimefanya kazi nyingi kwa ajili yako, na ingawa kuna uwezekano kuwa hazikuwa na mafanikio ya kusherehekewa, bado nimekuwa mwenye jitihada kwenye juhudi zangu. Huwezi tu kuniruhusu niingie mbinguni ili nile tunda la uzima?” Ni lazima ujue aina ya watu ambao Ninataka; wale walio najisi hawakubaliki kuingia katika ufalme, wale walio najisi hawakubaliki kuchafua nchi takatifu. Ingawa unaweza kuwa umefanya kazi nyingi, na umefanya kazi kwa miaka mingi, mwishowe kama bado wewe ni mwovu kupindukia—hakuvumiliki kwa sheria ya Mbinguni kwamba wewe unataka kuingia katika ufalme wangu! Tangu mwanzo wa dunia hadi leo, kamwe Sijatoa njia rahisi ya kuingilia ufalme Wangu kwa wale wenye neema Yangu. Hii ni sheria ya Mbinguni, na hakuna awezaye kuivunja. Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao hutafuta mabadiliko katika tabia yao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee watakaofanywa wakamilifu. Kama wewe tu unatazamia tuzo, na hutafuti kubadilisha tabia ya maisha yako mwenyewe, basi juhudi zako zote zitakuwa za bure—na huu ni ukweli usiobadilika!
kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu.
kutoka katika “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni