Jumatano, 28 Novemba 2018

Tamko la Hamsini na Nne

Tamko la Hamsini na Nne

Ninalielewa kila kanisa kama kiganja cha mkono Wangu. Usifikiri kwamba Siko wazi au sielewi. Ninawaelewa na kuwajua watu wote mbalimbali wa kila kanisa hata zaidi. Ninahisi hisia ya umuhimu kwamba ni lazima Nikufundishe. Nataka nikufanye ukue hadi utu uzima haraka zaidi ili kwamba siku ambayo unaweza kuwa wa msaada Kwangu itakuja haraka zaidi. Nataka vitendo vyenu viwe vimejaa hekima Yangu ili muweze kumdhihirisha Mungu kila pahali. Kwa njia hii lengo Langu kuu litafanikishwa. Wanangu! Unapaswa kuwa mwenye kufikiria nia Zangu, msifanye Nishikilie mkono wako Ninapokufundisha. Lazima mjifunze kuhisi nia Zangu, mjifunze kuona hadi kwenye kina cha mambo, kuwawezesha kushughulikia kila jambo linalowajia kwa urahisi na bila ugumu. Pengine katika mafundisho yenu, mara ya kwanza hamtaelewa, kisha mara ya pili, mara ya tatu.... Hatimaye mtaelewa nia Zangu.
Maneno yenu kila mara huwa na sifa isiyopenyeka, mfikiri wenyewe kuwa hii ni hekima, sivyo? Mara mkiwa wasiotii, na mara nyingine mkiwa wenye utani, wakati mwingine na mawazo au wivu wa mwanadamu.... Kwa jumla, mnazungumza bila uthabiti, msijue jinsi ya kuruzuku maisha kwa wengine au jinsi ya kuhisi hali zao, na kushiriki katika mawasiliano ya kibwege. Fikira zenu haziko wazi, hamjui hekima ni nini, ujanja ni nini, ninyi mmechanganyikiwa sana. Mnachukulia ujanja na udanganyifu kama hekima, je, hili haliliaibishi jina Langu? Je, hili halinikufuru? Je, hili halileti mashtaka ya uwongo dhidi Yangu? Hivyo lengo mnalotafuta ni lipi? Je, mmefikiria kuhusu hilo? Je, mmejitahidi kufanya hili? Nakuambia, nia Zangu ni mwelekeo na lengo ambalo mnatafuta, vinginevyo, yote yatakuwa bure. Wale ambao hawajui nia Zangu ni wale wasiojua jinsi ya kutafuta, na wataachwa, wataondolewa! Ni dhahiri, kugundua nia Zangu ni somo la kwanza ambalo lazima mjifunze. Ni kazi ya dharura zaidi, na hairuhusu kuchelewa! Msisubiri Mimi nionyeshe dosari zenu[a] mtu baada ya mwingine! Ninyi daima ni watu wapumbavu na mliochanganyikiwa. Ni jambo la kuchekesha! Siwezi kuamini ninyi ni wapumbavu hivi! Hamjali kuhusu nia Zangu! Jiulizeni, ni mara ngapi ninyi huelewa nia Zangu kabla ya kutenda? Mnapaswa kuwa ndio mnaojifunza wenyewe! Mnataka Niwashughulikie mmoja mmoja, hiyo haiwezekani! Mnapaswa kujifunza kupitia mnapotenda, mkikua katika maarifa na hekima. Maneno yanayotoka vinywani mwenu ni mazuri, lakini hali halisi ni ipi? Mnapokumbana na uhalisi hamtaweza kufanya chochote. Mnachosema hakilingani na uhalisi. Kwa kweli Siwezi kuvumilia kile ambacho ninyi mnafanya; Natazama na Siwezi kujizuia kuwa na huzuni. Kumbukeni hili! Katika siku zijazo jifunzeni kutambua nia Zangu!
Tanbihi:
a. Nakala asili inaacha "dosari zenu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili 

Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni