Alhamisi, 31 Agosti 2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

 Umeme wa Mashariki | Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe.

Jumatano, 30 Agosti 2017

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Umeme wa Mashariki | Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele


Mwenyezi Mungu alisema, Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

Jumatatu, 28 Agosti 2017

Tafuteni Maana ya Maisha - "Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi" (Video Rasmi ya Muziki)


Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi


Haikuwa wazi ni kwa ajili ya nani mtu anapaswa kuishi. Sasa nina jibu kwa hilo.
Nilikuwa naishi tu kwa ajili yangu mwenyewe, kutafuta hadhi tu na umaarufu.
Maombi kwa Mungu yaliyojaa maneno mema, lakini nikishikilia njia zangu mwenyewe katika maisha halisi.

Jumapili, 27 Agosti 2017

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki"


Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale,
na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki.
Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga
ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga,
wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Jumamosi, 26 Agosti 2017

Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani

  • 🎼🎵Sikiliza nyimbo:https://sw.godfootsteps.org/the-happiness-in-the-good-land-of-canaan.html
  • I
  • Nimerudi kwa familia ya Mungu,
  • mchangamfu na mwenye furaha.
  • Mikono yangu imemshika mpendwa wangu,
  • moyo wangu ni miliki Yake.
  • Japo nimepitia Bonde la Machozi,
  • nimeyaona mapenzi ya Mungu.
  • Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku,
  • Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu.
  • Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu,
  • moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu.
  • Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha,
  • nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
  • Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu,
  • nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
  • Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha,
  • nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
  • II
  • Katika nchi hii iliyobarikiwa ya Kanaani,
  • yote ni mabichi, yote ni mapya,
  • yakifurika na nafsi ya uhai ya maisha.
  • Maji ya uzima hutiririka kutoka kwa Mungu wa vitendo,
  • hunifanya niruzukike na maisha.
  • Naweza kufurahia baraka kutoka mbinguni,
  • hakuna tena kutafuta, kuchakura, kuwa na uchu.
  • Nimewasili katika nchi iliyobarikiwa ya Kanaani,
  • furaha yangu haina kifani!
  • Upendo wangu kwa Mungu huniletea nguvu isiyoisha.
  • Sauti za kusifu hupaa juu mbinguni,
  • zikimwambia upendo wangu wa ndani.
  • Ni haiba ilioje mpendwa wangu aliyo nayo!
  • Uzuri Wake huiteka roho yangu.
  • Manukato ya mpendwa wangu
  • hunifanya nione ugumu wa kumwacha.
  • III
  • Nyota mbinguni zatabasamu kwangu,
  • jua lanikubali kutoka juu.
  • Pamoja na mwanga wa jua, na mvua na umande,
  • tunda la uzima hukua kwa uthabiti na ubivu.
  • Maneno ya Mungu, mengi na ya fahari,
  • hutuletea sikukuu tamu.
  • Riziki nzima na ya kutosha ya Mungu hutufanya tutosheke.
  • Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu;
  • upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.
  • Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu;
  • upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.
  • Harufu nzuri ya matunda hujaa hewani.
  • Ukikaa hapa kwa siku chache,
  • utapapenda kuliko chochote kingine.
  • Hakuna wakati utataka kuondoka.
  • IV
  • Mwezi wa fedha hunurisha mwanga wake.
  • Mzuri na mchangamfu, ni maisha yangu.
  • Uliye mpendwa moyoni mwangu,
  • uzuri Wako umepita maneno yote.
  • Moyo wangu u katika mapenzi matamu Nawe,
  • siwezi kujizuia kuruka kwa furaha.
  • Daima Uko moyoni mwangu,
  • nitakuwa nawe maisha yangu yote.
  • Moyo wangu hukutamani Wewe daima;
  • kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.
  • Ee mpenzi moyoni mwangu!
  • Nimekupa mapenzi yangu yote.
  • Moyo wangu hukutamani Wewe daima;
  • kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.
  • Ee mpenzi moyoni mwangu!
  • Nimekupa mapenzi yangu yote.
  •  
  • kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Ijumaa, 25 Agosti 2017

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake



Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?


Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushirikiane kuhusu mada ya kumfuata Mungu.