Jumamosi, 26 Agosti 2017

Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani

  • 🎼🎵Sikiliza nyimbo:https://sw.godfootsteps.org/the-happiness-in-the-good-land-of-canaan.html
  • I
  • Nimerudi kwa familia ya Mungu,
  • mchangamfu na mwenye furaha.
  • Mikono yangu imemshika mpendwa wangu,
  • moyo wangu ni miliki Yake.
  • Japo nimepitia Bonde la Machozi,
  • nimeyaona mapenzi ya Mungu.
  • Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku,
  • Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu.
  • Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu,
  • moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu.
  • Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha,
  • nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
  • Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu,
  • nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
  • Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha,
  • nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
  • II
  • Katika nchi hii iliyobarikiwa ya Kanaani,
  • yote ni mabichi, yote ni mapya,
  • yakifurika na nafsi ya uhai ya maisha.
  • Maji ya uzima hutiririka kutoka kwa Mungu wa vitendo,
  • hunifanya niruzukike na maisha.
  • Naweza kufurahia baraka kutoka mbinguni,
  • hakuna tena kutafuta, kuchakura, kuwa na uchu.
  • Nimewasili katika nchi iliyobarikiwa ya Kanaani,
  • furaha yangu haina kifani!
  • Upendo wangu kwa Mungu huniletea nguvu isiyoisha.
  • Sauti za kusifu hupaa juu mbinguni,
  • zikimwambia upendo wangu wa ndani.
  • Ni haiba ilioje mpendwa wangu aliyo nayo!
  • Uzuri Wake huiteka roho yangu.
  • Manukato ya mpendwa wangu
  • hunifanya nione ugumu wa kumwacha.
  • III
  • Nyota mbinguni zatabasamu kwangu,
  • jua lanikubali kutoka juu.
  • Pamoja na mwanga wa jua, na mvua na umande,
  • tunda la uzima hukua kwa uthabiti na ubivu.
  • Maneno ya Mungu, mengi na ya fahari,
  • hutuletea sikukuu tamu.
  • Riziki nzima na ya kutosha ya Mungu hutufanya tutosheke.
  • Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu;
  • upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.
  • Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu;
  • upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.
  • Harufu nzuri ya matunda hujaa hewani.
  • Ukikaa hapa kwa siku chache,
  • utapapenda kuliko chochote kingine.
  • Hakuna wakati utataka kuondoka.
  • IV
  • Mwezi wa fedha hunurisha mwanga wake.
  • Mzuri na mchangamfu, ni maisha yangu.
  • Uliye mpendwa moyoni mwangu,
  • uzuri Wako umepita maneno yote.
  • Moyo wangu u katika mapenzi matamu Nawe,
  • siwezi kujizuia kuruka kwa furaha.
  • Daima Uko moyoni mwangu,
  • nitakuwa nawe maisha yangu yote.
  • Moyo wangu hukutamani Wewe daima;
  • kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.
  • Ee mpenzi moyoni mwangu!
  • Nimekupa mapenzi yangu yote.
  • Moyo wangu hukutamani Wewe daima;
  • kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.
  • Ee mpenzi moyoni mwangu!
  • Nimekupa mapenzi yangu yote.
  •  
  • kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni