Swali la 1: Tunaamini kwamba kurudi kwa Bwana kutamaanisha kwamba waumini wanainuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni, kwa maana imeandikwa katika Biblia: “Baada ya hayo sisi ambao tuko hai na kusalia tutachukuliwa pamoja na wao mawinguni, kwa ajili ya kukutana na Bwana katika hewa: na hivyo tutakuwa naye Bwana daima” (1Wathesalonike 4:17). Unashuhudia kuwa Bwana Yesu amerejea, hivyo ni kwa nini sisi sasa tuko duniani na bado hatujanyakuliwa?
Jibu:
Tunapaswa kutarajia kurudi kwa Bwana kulingana na unabii ambao Yeye Mwenyewe aliuzungumza. Hiyo ndiyo njia ya kawaida kabisa ya kusubiri kurudi kwa Bwana. Unamnukuu nani, kwa hakika? Je, unanukuu maneno ya Bwana au maneno ya wanadamu? “Kisha sisi tulio hai na tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani,” ni nani aliyasema hayo? Je, hayo ni maneno ya Bwana Yesu? Bwana Yesu hajawahi kamwe kusema kitu chochote kama hicho. Roho Mtakatifu hakuwahi kamwe kusema hilo, pia. Maneno unayoamini na unayonukuu ni maneno ya Paulo. Je, maneno ya Paulo yanawakilisha maneno ya Bwana Yesu?