Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 23 Agosti 2019

3. Sura ya tatizo la mwanadamu kutokubali ukweli ulioonyeshwa na Kristo ni ipi? Matokeo ya mtu kutomchukua Kristo kama Mungu ni yapi?

IX. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kwamba Kristo ni Onyesho la Mungu Mwenyewe

3. Sura ya tatizo la mwanadamu kutokubali ukweli ulioonyeshwa na Kristo ni ipi? Matokeo ya mtu kutomchukua Kristo kama Mungu ni yapi?


Aya za Biblia za Kurejelea:


    “Yesu akawaambia, … Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake. Anaponena uwongo, anazungumza yaliyo yake mwenyewe: kwani yeye ni mwongo, na baba wa uwongo. Na kwa kuwa nawaambieni ukweli, hamniamini. … Yule ambaye ni wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu: nyinyi kwa hivyo hamyasikii, kwa kuwa nyinyi si wa Mungu” (Yohana 8:42-45, 47).

Jumanne, 18 Juni 2019

3. Kumuainisha Mungu mmoja wa kweli kama “Mungu wa utatu” ni kumkana na kumkufuru Mungu

XVI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kama Mungu Kweli ni Mungu wa Utatu au ni Mungu Mmoja wa Kweli

3. Kumuainisha Mungu mmoja wa kweli kama “Mungu wa utatu” ni kumkana na kumkufuru Mungu
Maneno Husika ya Mungu:

Hebu Niwaambie hilo, kwa hakika, Utatu Mtakatifu haupo popote katika dunia hii. Mungu hana Baba wala Mwana, vivyo hivyo hakuna dhana ya chombo kitumiwacho kwa pamoja na Baba na Mwana: Roho Mtakatifu.

Jumatano, 1 Mei 2019

Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili”

Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili”

1. Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu.

Jumapili, 21 Aprili 2019

maneno ya Mungu | Sura ya 9

maneno ya MunguSura ya 9

Mwenyezi Mungu alisema, Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu haneni lugha ya mwanadamu, wala mwanadamu hawezi kunena lugha ya Mungu, na kwa Mungu, madai ya mwanadamu Kwake ni rahisi, ilhali matakwa ya Mungu kwa mwanadamu hayafikiki na hayafikiriki kwa mwanadamu. Ukweli, hata hivyo, ni kinyume kabisa: Mungu anataka tu “asilimia 0.1” ya mwanadamu.

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”


Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo.