Jumatatu, 3 Juni 2019

Wakati wa Uzoefu Mmoja Niliona Ulinzi wa Mungu

Yongxin, Jiji la Yibin, Mkoa wa Sichuan
Hatukuwahi kumwamini Mungu kabla. Mnamo mwaka wa 2005, tukitiwa moyo na Mungu, mume wangu, baba mkwe wangu, mjomba wangu, na mimi wote tuliikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Baada ya muda mfupi, kanisa lilinipangia kufanya wajibu wa kuhifadhi vitabu. Baadaye, nyumba yetu ilishika moto, na wakati wa moto huu tulipokea ulinzi wa Mungu wa ajabu. Mungu kwa hakika ni mwenyezi!
Siku moja mwezi wa Machi ya mwaka wa 2006, baada ya chakula cha mchana takriban saa saba adhuhuri, kulikuwa kukinya theluji sana nje. Mume wangu, binti yangu na mimi tulikuwa ndani, tukijipasha joto kando ya moto na kubambua mahindi, wakati tuliposikia kwa ghafla sauti kutoka nje ikipiga yowe kwa sauti kubwa, “Nyumba yenu inachomeka! Haraka, tokeni nje na kuizima!” Kwa haraka tulikimbia nje, na kuona kwamba moto ulikuwa tayari umechoma paa la jikoni na banda la nguruwe. Wasioamini watatu walitusaidia kuuzima moto, na wakapaaza sauti, “Njooni msaidie kuzima moto!

Jumapili, 2 Juni 2019

Kupitia Utunzaji wa Uangalifu wa Mungu wa Wokovu wa Mwanadamu katika Maafa

Muling , Beijing
Agosti 16, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, Beijing ilipata mvua kubwa zaidi katika miaka sitini. Katika mvua hiyo kubwa niliona matendo ya Mungu na kuona jinsi Yeye huwaokoa mwanadamu.
Siku hiyo adhuhuri, dada zangu watatu na mimi tulikuwa tumekutana. Nje mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha. Saa kumi u nusu jioni mume wangu, ambaye hakuwa muumini, alirudi akitwambia kwamba kulikuwa na maji mengi kwa mzunguko kiasi kwamba watu hawakuweza kupitia. Hata hivyo, saa kumi na moja jioni aliondoka kwa haraka sana kwenda kwa zamu yake ya usiku kazini. Wakati huo sikuhisi kitu chochote kisicho cha kawaida, na nilienda kupika chakula cha jioni kama kawaida. Saa moja usiku, mpangaji wetu kwa ghafla alibisha mlango akiniita, na nilipotoka kuangalia, kile nilichoona kilinipa mshtuko mkubwa: Maji ya mvua yalikuwa tayari yamejaza ua na yalikuwa yakiingia kwa pembe za mashariki na magharibi za nyumba, wakati maji yaliyokuwa juu ya ardhi yaliendelea kuongezeka. Mwanangu wa kiume nami tulijaribu kuzuia mtiririko wa maji, lakini hatukufaulu.

Jumamosi, 1 Juni 2019

Sauti ya Mungu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili


Sauti ya Mungu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote. ... Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.”

Kuhusu Sisi:Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ijumaa, 31 Mei 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”



Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu.

Alhamisi, 30 Mei 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumatano, 29 Mei 2019

Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians



Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians

I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, ni jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo la Mungu. Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu, na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake. Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu, na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

Jumanne, 28 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili.