Jumanne, 14 Mei 2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,  Umeme wa Mashariki, ushuhuda wa injili
Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Katika siku chache zilizofuata, ingawa Jingru hakuwa ameanguka katika majaribu ya Shetani na alijua kwamba hangeweza kuwa mwenzi wa Wang Wei kamwe, mkutano wake na Wang Wei jioni hiyo na ungamo lake la kweli vilirudiwa akilini mwake tena na tena kama onyesho katika filamu …
Wang Wei alipompigia simu tena, moyo wa Jingru ulishtuka kidogo, naye akajiambia: “Sote wawili hatuwezi kuwa kitu kimoja, lakini bado tunaweza kuwa marafiki wa kawaida.

Jumatatu, 13 Mei 2019

Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"

Maoni Tofauti, Migongano Ya Siku Zote
Mimi ni mke wa kawaida, mke mzuri na mama mwenye upendo, mimi huwatunza vizuri mume wangu na watoto wangu, mimi hufanya kazi kwa bidii na mwekevu katika kuendesha nyumba yangu, na sijawahi kamwe kutumia fedha zangu bila hadhari. Lakini kitu kisichofikirika kilinifika. Mwanangu alimuoa msichana wa kisasa ambaye kwa kweli alipenda kujifurahisha na kuvaa na kufuata mitindo ya ulimwengu.

Jumapili, 12 Mei 2019

Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu

Na Ouyang Mo, Mkoa wa Hubei
Baada ya miongo miwili ya mema na mabaya ambayo yeye na mumewe walipitia pamoja, hakuwahi kamwe kufikiria kwamba mumewe angekuwa na uhusiano wa nje ya ndoa. Alishindwa kabisa kuvumilia wakati alipogundua hilo. Licha ya kujaribu kila kitu ili kumfanya mumewe ampende tena, yote ilikuwa kazi bure. Katikati ya maumivu yake na kutokuwa na tumaini, ni maneno ya Munguyaliyomwokoa, yakimsaidia kupata kiini cha maumivu yake, kuelewa maana ya maisha, na hatua kwa hatua kutoka kwenye fadhaa ya mateso yake.

Jumamosi, 11 Mei 2019

Ushuhuda wa Maisha | Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Umuhumi wa Maombi, Ushuhuda wa Maisha, Umeme wa Mashariki

Ushuhuda wa Maisha | Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Huanbao Mji wa Dalian, Mkoa wa Liaoning
Tangu kwanza nianze kumwamini Mwenyezi Mungu, daima nimewapenda wale ndugu wa kiume na wa kike ambao wanaweza kupokea huduma ya kibinafsi ya Kristo, ambao wanaweza kusikia mahubiri Yake kwa masikio yao wenyewe. Katika moyo wangu, nimewaza jinsi ingekuwa vizuri sana kama siku moja katika siku zijazo ninaweza kusikia mahubiri ya Kristo, bila shaka kumwona Yeye kungekuwa kwa ajabu hata zaidi. Lakini hivi karibuni, kwa njia ya kusikiliza ushirika Wake, nimekuja kuhisi kwa undani moyoni mwangu kwamba mimi sifai kumwona Kristo.
Ilikuwa wakati ambapo Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia kwa Maisha Juzuu ya1 hadi 3 zilipotolewa. 

Ijumaa, 10 Mei 2019

Maneno ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne

Maneno ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. ... Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa.

Alhamisi, 9 Mei 2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 1)



Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Jioni moja, Jingru alikuwa akinadhifisha kwake.
“Krr, krr.” Simu ilianza kulia. Aliijibu na sauti ngeni lakini bado inayojulikana ililia sikioni mwake: “Halo! Ni Wang Wei. Uko nyumbani!”
“Wang Wei?” Jingru kwa namna fulani alistaajabu: Kwa nini alikuwa akimpigia simu sasa baada ya miaka mingi sana?
“Ndiyo … niko nyumbani. Kuna nini?” aliuliza Jingru kwa mshangao.
“Hatujaonana kwa muda mrefu. Ningependa kukupeleka matembezini.

Jumatano, 8 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi.” Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.”