Maoni Tofauti, Migongano Ya Siku Zote
Mimi ni mke wa kawaida, mke mzuri na mama mwenye upendo, mimi huwatunza vizuri mume wangu na watoto wangu, mimi hufanya kazi kwa bidii na mwekevu katika kuendesha nyumba yangu, na sijawahi kamwe kutumia fedha zangu bila hadhari. Lakini kitu kisichofikirika kilinifika. Mwanangu alimuoa msichana wa kisasa ambaye kwa kweli alipenda kujifurahisha na kuvaa na kufuata mitindo ya ulimwengu.
Alifuatilia na kununua chochote kilichopendwa ulimwenguni, alipoteza pesa nyingi mno, na kiasi cha pesa alichopata kila mwezi ndicho kiasi alichotumia. Kwa kuwa kulikuwa na tofauti kubwa sana katika njia zetu za kufikiria na kuishi, binti mkwe wangu na mimi daima tungegombana, tulikuwa na mabishano ya hasira, na matatizo yetu yaliendelea kuwa makali zaidi na zaidi.
Siku moja nilimwona binti mkwe wangu akiingia huku akibeba mkoba, kwa hiyo nikamwendea haraka kumuuliza ni nini alichokuwa amenunua, na ni pesa ngapi alizokuwa ametumia. Akafurahia na kusema: “Nilinunulia vazi, halikuwa la gharama kubwa, takriban yuan 400 tu.” Niliposikia hayo, nilikuwa na hasira mno: Angewezaje kuburudika jinsi hiyo, alikuwa akitenda kama mtu aliyekuwa na fedha nyingi mno. Ninaponunua vazi, ni chini ya yuan 100, na mimi huvaa kwa miaka kadhaa. Hata hivyo, mavazi ambayo alinunua yalikuwa ghali, na mara yalipopitwa na wakati angeacha kuyavaa, wakati kabati lake ya nguo lilikuwa limejaa nguo nyingi; jinsi nilivyozidi kufikiria hilo ndivyo nilivyozidi kukasirika, na lilianza kuchakaza uso wangu. Binti mkwe wangu alipoona kwamba sikuwa na furaha, hilo jambo lilifuta tabasamu usoni mwake, akageuka na kutembea hadi katika chumba chake cha kulala, na nikasikia sauti ya mlango ukifungwa kwa nguvu.
Ushauri Kutosikilizwa, Umbali Kupanuka
Baadaye, wakati wowote nilipomwona akirudi kutoka kwa ununuzi, ningemkaripia: “Lili, tazama familia yetu, sisi si matajiri sana, hivi karibuni mtoto wako atakua, na kisha kutakuwa na vitu vingi ambavyo tutahitaji kutumia fedha kwavyo, kwa hiyo hatuwezi kuendelea kutumia pesa hivyo bila kujali. Kama tuna nguo na viatu vinavyotosha, basi hilo litatosha; hatuwezi kuendelea kufuja fedha jinsi hii. Unahitaji kufikiria maisha yako ya baadaye.” Lakini binti mkwe wangu alijibu kwa kusema kuwa yeye na mwanangu walijua jinsi ya kuishi maisha yao na kusema kuwa sikufaa kuwa na wasiwasi sana kuhusu hilo. Kuona kwamba hakuelewa nililomaanisha kulinifanya kuhisi maudhi kwake, na mara nyingi tungetofautiana juu ya mambo haya. Baadaye, aliporudi kutoka kwa matembezi yake ya ununuzi, aliniepuka, akitumia kutozingatia kwangu kwa manufaa yake. Alikwenda kimya kimya ndani ya chumba chake na hakutoka nje hadi baada ya kuvificha vitu vyake. Nilipogundua jambo hili nilikuwa na hasira sana, lakini nilijua kuwa ingekuwa bure kulizungumzia, yote niliyoweza kufanya yalikuwa kulipuuza na kulivumilia. Lakini muda ulivyoendelea kweli sikuweza kulivumilia, na mara nyingi nilikuwa nikimnung’unikia mwanangu. Ilikuwa vigumu kwa mwanangu, ambaye alikuwa amebaniwa kati yetu, na siku moja aliniuliza bila kutarajiwa: “Mama, Lili anapoenda ununuzi huwa hakuulizi fedha, hivyo kwa nini unajali sana?” Kuona mwanangu pia alikuwa upande wake nilihisi kuumia hasa na kuhuzunika ndani. Nilikasirika sana kiasi kwamba niliwapuuza kwa siku kadhaa. Lakini baadaye binti mkwe wangu aliendelea kana kwamba hakuna chochote kilichokuwa kimetokea kamwe, jambo lililonifanya kuwa na hasira hata zaidi.
Neno la Mungu Likiongoza Njia, Nilipata Chanzo cha Tatizo
Siku Moja, mwanangu alipomwambia binti mkwe wangu kwamba wangekwenda nyumbani kwa mfanyakazi mwenzake kula, alikwenda kwa chumba chake ili kutumia vipodozi, na baada ya saa moja kupita alikuwa bado hajateremka chini. Baada ya kumwona jinsi hii, nilipanda juu na kumwambia hivi kwa hasira: “Kila wakati unapojipodoa kwa muda mrefu sana, kwa kweli ni kupoteza muda! Sikuwa nimewahi kutumia vipodozi kamwe katika maisha yangu yote, na nimeweza kwendelea kuishi, na sikai hunde zaidi ya watu wengine, mimi hukaa tu na sura yangu ya asili.” Binti mkwe wangu aliposikia nikisema hili alianza kugombana nami, na nilikasirika sana kiasi kwamba nilitaka kuondoka nyumbani mara moja na kuishi peke yangu, mbali naye. Nilijiwazia: “Kile nisichoweza kuona hakiwezi kunidhuru.” Lakini niliwaangalia mwanangu na mjukuu wangu na kujua kuwa singeweza kuwa mkatili jinsi hiyo, hivyo nililazimika kuuacha mpango huu. Lakini chuki niliyokuwa nayo katika moyo wangu kwa binti mkwe wangu ilikua zaidi na zaidi, na mara nyingi tungezozana juu ya mambo madogo. Hatukuwa tunadumisha nyumba ya amani.
Kuishi katika kaya aina hii ya ugomvi kulinifanya nihisi uchovu na uchungu sana, kwa hiyo nilifikiri kuwa kama muumini katika Mungu, nilikuwa nikiifichua tabia yangu potovu katika kugombana na binti mkwe wangu jinsi hii kutwa na kwamba haikupatana na mapenzi ya Mungu. Katika kuteseka kwangu yote niliyoweza kufanya yalikuwa ni kumwomba Mungu: “Ee Mungu! Ninajua kwamba sifai kubishana juu ya mambo yasiyo na maana na binti mkwe wangu, lakini siwezi kamwe kujizuia. Ee Mungu! Ninakuuliza unipatie nuru, tafadhali nifanye nielewe jinsi ya kumtendea binti mkwe wangu kwa namna inayopatana na mapenzi Yako; niko tayari kutenda ukweli ili kukuridhisha.” Baada ya kumwomba Mungu, nilifungua neno la Mungu, na kusoma mahali ambapo Mungu anasema: “Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Kwa mwanadamu ambaye si wa mwili na akili timamu, ambaye kamwe hajui ukweli, ambaye hawezi kusema tofauti kati ya vitu vyema na hasi, mienendo ya aina hii moja baada ya nyingine inawafanya wote wawe radhi kukubali mienendo hii, mtazamo wa maisha, filosofia za maisha na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani juu ya jinsi ya kukaribia maisha na jinsi ya kuishi ambayo Shetani ‘amewapa’. Hawana nguvu, wala hawana uwezo, wala ufahamu wa kupinga” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupitia ufunuo wa neno la Mungu, hatimaye nilielewa hili: Mwelekeo wa ulimwengu ni njia ya Shetani kumpotosha mwanadamu. Shetani hutumia mitindo ya kijamii kwa manufaa yake mwenyewe ili kutudhibiti na kutudanganya, hutufundisha kila aina ya maoni yasiyo sahihi kama vile, “Upendo wa uvutivu ni wa asili ya wanadamu,” “Nguo humkamilisha mwanadamu, tandiko humkamilisha farasi,” na “Tumia siku kwa ajili ya anasa, kwa maana maisha ni mafupi.” Mara tu maoni haya yenye makosa yanapoingia katika mawazo yetu, sisi huamini kwamba: maisha yetu yanapaswa kuwa juu ya kutafuatilia uzuri na kuzingatia jinsi tunavyovaa, na hili ni la asili na la kawaida. Jinsi unavyovaa ni ishara inayothibitisha hadhi na thamani yako; ukivaa vitu vya kupendeza na vya siku hizi na kuweka vipodozi ili upendeze, basi hutatengwa na jamii, halafu utathaminiwa na wengine; kama sivyo, utashushiwa hadhi na kuangaliwa kwa dharau na wengine. Kwa sababu ya mtazamo huu wenye makosa tunashawishika pasipo kujua na kuendelea katika mitindo miovu. Kuangalia jamii leo, bila kujali kama wewe ni kijana au mzee, kila mtu huendelea sambamba na mtindo wa hivi karibuni na hufuata mienendo ya sasa, kila mtu anataka kuvaa nguo badhirifu na hujipendeza na vipodozi, yeyote aliye kwa mstari wa mbele kwa wakati fulani ni yule anayekimbizwa na kila mtu, na hakuna mtu anayeamini kuwa hili ni jambo baya linalotoka kwa Shetani; kinyume chake, ana fikra kwamba kufuatilia vitu hivi ni jambo la busara na ni kama inavyofaa kuwa. Binti mkwe wangu hawamwamini Mungu, hauelewi ukweli, hana utambuzi, kwa hiyo anawezaje kukosa kuathiriwa kwa kuishi maisha yake chini ya aina hizi za hali? Ana upendo wa uzuri, anapenda kuvaa vizuri, na anapenda kupoteza fedha zake kwa sababu ameathiriwa, akiwa ameshawishiwa na kupotoshwa na mwenendo mbaya wa Shetani. Kuchochewa na aina hizi za mienendo mibaya humfanya ovyo hasa, yeye daima hujilinganisha na wengine, na huamini kuwa nguo na vipodozi anavyotumia ni kifaa chake cha manufaa ya kujithamini mwenyewe. Kwa kweli, binti mkwe wangu hana uhuru wa kutenda kwa kujitegemea. Kwa kuja kuelewa mambo haya nilikuja kupata chanzo cha tatizo, na nilihisi kuwa kila kitu kilikwisha kuwa wazi.
Baadaye, nilikuja mbele ya Mungu na kuomba: “Ee Mungu! Niko tayari kuacha chuki yangu isiyo na sababu kwa binti mkwe wangu. Tafadhali Uniongoze ili nipate kujiweka kando na kutenda na kutazama mambo kulingana na neno Lako.” Kuanzia wakati huo kwendelea, wakati wowote nilipoona binti mkwe wangu alitumia fedha bila hadhari kwa ununuzi na kunifanya nihisi vibaya, ningemwomba Mungu na kutafuta ulinzi wa Mungu ili moyo wangu uwe na amani mbele Yake. Polepole lakini kwa hakika, sikuwa na chuki nyingi sana katika moyo wangu kwa binti mkwe wangu, na kwa njia ya neno la Mungu nikajua: Sisi sote tu sehemu ya binadamu mpotovu, sisi sote tunaishi chini ya miliki ya Shetani na tunadanganywa na Shetani, bila kujua sisi sote tunaishi kwa msingi wa tabia zetu potovu. Binti mkwe wangu pia ni mwathiriwa wa mienendo hii miovu; sifai kumchukia, na bila shaka sifai kumtendea kwa misingi ya tabia potovu ya Shetani. Shetani ndiye mhalifu mkuu kwa vitu hivi vyote, Shetani ni mwenye karaha zaidi kuliko kitu kingine chochote.
Niliendelea kwa njia hii kwa kipindi cha muda, nikidhani kwamba nilikuwa tayari nimeweka kando chuki yangu isiyo na sababu kwa binti mkwe wangu, lakini kwa kuwa sikuwa na maarifa ya kweli kuhusu hali yangu potovu, kwa kuwa tabia yangu ya maisha haikuwa imebadilika, nilipokumbana na mambo ambayo hayakulingana na uchu wangu, tabia yangu potovu ilifichuliwa tena.
Neno la Mungu Liliniongoza Kujitambua Mwenyewe
Mwezi mmoja, baada ya binti mkwe wangu kutumia fedha zote alizokuwa nazo, hatukuwa hata na pesa za kulipia bima yetu ya kijamii. Baada ya kugundua jambo hili, nilijawa na ghadhabu nyingi sana kiasi kwamba nilitaka kumfukuza binti mkwe wangu mara moja. Nilipokuwa tu nikitaka kumkasirikia, ghafla niligundua kwamba nilikuwa tena nikiishi katika hali mbaya, kwa hiyo nilijituliza kwa haraka na nikamwomba Mungu, nikitafuta ulinzi Wake kwangu, ili niweze kutomtendea binti mkwe wangu kulingana na mwili wangu.
Nilipofungua kitabu cha neno la Mungu, nilisoma mahali panaposema: “Usiwe mwenye haki wa kibinafsi; … Ukiwaona wengine kuwa chini yako wewe basi ni mwenye haki binafsi, mwenye majivuno ya kibinafsi na huna manufaa kwa yeyote” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Hukumu na adabu za neno la Mungu zilinifanya kutambua kuwa siku zote nilimchukia binti mkwe wangu kwa sababu hakuna tendo lake lolote lililopatana na matarajio yangu, hakufikia kiwango cha kile nilichofikiri binti mkwe anafaa kuwa. Mimi ni msimamizi mwekevu wa nyumba, na nilimtaka binti mkwe wangu awe vivyo hivyo, kuwa mke mzuri na mama mwenye upendo. Nilipoona kwamba alikuwa sio tu mwenye bidii na mwekevu, lakini kwamba alitumia pesa zake bila hadhari, nilimdharau na kufikiria kwamba hakuelewa mambo na kuwa yeye alifuja pesa zake tu. Aidha, pia nilimtaka binti mkwe wangu kunitii katika chochote nilichomtaka afanye na kuishi kulingana na mtindo wangu wa maisha. Kila binti mkwe wangu alipokosa kufanya kile nilichomtaka afanye nilikasirika, nilimkosoa na kumtazama vibaya. Lakini katika wakati huu hatimaye niliona kwamba nilikuwa nimedhibitiwa kabisa na tabia ya shetani ya “kujiweka juu ya kila kitu kingine,” daima nikitaka kuuficha umma ukweli na kuwa wa kutoa kauli ya mwisho. Yote yaliyotoka kwangu yalikuwa tabia potovu ya kiburi na ya kujidai, na hayakuwa ya manufaa kwa yeyote. “Aidha, binti mkwe wangu na mimi tunatoka vizazi tofauti, hatuathiriwi na kushawishiwa na jamii kwa namna moja, lakini daima ninatumia viwango vyangu mwenyewe kumtaka afanye mambo; Si huku ni kuwa na kiburi na majivuno? Si mimi ninakuwa mtu mwenye kudhibiti? Nilifikiria jinsi Mungu alivyo mkuu, jinsi hata Alivyoonekana katika mwili kujificha kwa unyenyekevu na bila kuonekana kati yetu ili kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu, jinsi Mungu hajawahi kamwe kutumia mamlaka Yake kuwakandamiza wanadamu, na hajawalazimisha wanadamu kuweka neno Lake katika vitendo, jinsi wakati wote Ameonyesha tu ukweli kumruzuku mwanadamu, na kutumia upendo Wake kumhamasisha mwanadamu na kumfanya mwanadamu kutubu. Lakini wakati wowote tunapompinga na kumkataa Mungu, ingawa Yeye hutumia neno Lake kutufichua na kutuhukumu, wakati huo huo Yeye Anatuongoza kwa subira, kutuunga mkono na kuturuzuku, na kwa uvumilivu mkubwa na stahamala Yeye hutusubiri turudi Kwake. Mungu ni mnyenyekevu sana na mzuri sana! Hata hivyo, mimi, ambaye nimepotoshwa mno, hutenda kwa kiburi sana na bila sababu, daima namlazimisha binti mkwe wangu kunisikiliza katika mamlaka yangu kama mama mkwe, na yote ambayo ninaishi kwa kudhihirisha ni tabia potovu.” Nilivyozidi kufikira hili, ndivyo nilivyozidi kuhisi aibu. Niliona kwamba nilikuwa nimepotoshwa kwa kina sana na Shetani, kwamba wakati nilipokabiliwa na mambo sikuweza kuutuliza moyo wangu mbele ya Mungu. Uasili wangu ulikuwa na nguvu sana, na nilikuwa na matakwa mengi mno ya kibinafsi, na mara nyingi nilipoteza shahidi. Kwa kweli sikufaa kuishi mbele ya Mungu.
Baadaye, nilisoma pia katika neno la Mungu ambapo linasema: “Haikubaliki kwako kutojijua. Kwanza ponya ugonjwa wako mwenyewe, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako. Uache mwili na uasili. Daima yaruhusu maneno ya Mungu yawe na mamlaka ndani mwako. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwamba maisha yako hayabadiliki; utakuja polepole kuhisi kwamba tabia yako imebadilika kiasi kikubwa” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Neno la Mungu lilinionyesha njia za kutenda, na nikawa na habari kuwa kuna fundisho kwangu kujifunza juu ya binti mkwe wangu nami kutoweza kuishi kwa upatanifu, kwamba inanipasa kuingia katika ukweli husika, kwamba singemkodolea macho binti mkwe wangu mchana kutwa. “Ni lazima nizingatie kuiacha tabia yangu ya kiburi na ya kujidai ya kishetani. Siwezi kuendelea kumtaka binti mkwe wangu anisikilize kwa mujibu wa maoni yangu ya jadi na tabia zee ya asili, na siwezi kushikilia nafasi yangu kama mama mkwe ili kumkandamiza binti mkwe wangu. Ni lazima nijifunze jinsi ya kuweka kando hadhi yangu kama mzee, kuacha neno la Mungu liwe na mamlaka juu ya moyo wangu, kutumia ukweli kutatua masuala yangu mwenyewe na kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kwaida.” Baada ya kuyaelewa mapenzi ya Mungu nilimwomba Mungu nikimwambia Yeye kwamba nimeamua kujisaliti na kuweka neno la Mungu katika matendo.
Niliweka Ukweli Katika Matendo Na Kuanza Kuelewana na Binti Mkwe Wangu
Siku moja, wakati binti mkwe wangu aliporudi nyumbani kutoka kazini, nilikuwa katikati ya kazi zangu za nyumbani, na nikaona kwamba binti mkwe wangu alikuwa amebeba mifuko katika mikono yake miwili na mgongoni mwake, hivyo bila kufikiria nikamwuliza: “Unabeba vitu mikononi mwako na kwa mgongo wako, unafanya nini?” Binti mkwe wangu akasema: “Nilinunua jozi mbili za viatu vya ngozi na jozi moja ya ndara za ngozi.” Mara tu niliposikia kwamba alikuwa amenunua jozi tatu za viatu wakati mmoja nilikuwa karibu tu kuzungumza wakati ghafla nilitambua kwamba mara nyingine tena nilikuwa nikimtaka atende kwa mujibu wa tamaa zangu mwenyewe, na hapo hapo nikamwomba Mungu kimya kimya. Katika wakati huu nilifikiria jinsi neno la Mungu linavyosema: “Katika tabia za watu wa kawaida hakuna uhalifu au udanganyifu, watu wana uhusiano wa kawaida kati yao, hawafanyi mambo pekee yao, na maisha yao si duni wala ya kufifia. Kwa hiyo, vilevile, Mungu huinuliwa miongoni mwa wote, maneno Yake hupenya miongoni mwa wanadamu, watu huishi katika amani kati yao na chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, dunia imejaa upatanifu, bila kuingilia kwa Shetani, na utukufu wa Mungu huwa na umuhimu mkuu sana miongoni mwa wanadamu” (“Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Sita” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupata nuru kwa neno la Mungu kulinifanya niwe mtulivu kiasi kutoka kwa mtazamo wangu wa awali wa ghadhabu. Nilifikiri juu ya azimio nililomwambia Mungu ningefanya, na nikatambua kuwa leo Mungu alikuwa amepanga hali hizi ili kubadilisha tabia yangu potovu, ili nipate kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida na kuliweka neno la Mungu katika matendo. Hili lilihusisha mimi kuwa na ushuhuda, sifai siku zote kumkodolea macho yangu binti mkwe wangu, nilihitaji kwanza kujiweka kando na kisha kumtegemea Mungu na kuitupa tabia yangu ya kiburi na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu halisi. Binti mkwe wangu ana njia yake ya kuishi, siifai kuingilia, ni lazima nimheshimu, na kuacha mambo yaendelee kama kawaida yake. Alipoona kwamba sikuwa nikimwambia chochote, alitabasamu na kupeleka viatu vyake kwa chumba chake. Baada ya kuuangalia tukio hili nilimshukuru Mungu kimya kimya. Kama haikuwa kupata nuru na mwongozo wa neno la Mungu, basi leo haingeepukika kwa binti mkwe wangu na mimi kubadilishana maneno ya ugomvi.
Baada ya haya, haukujalisha kama binti mkwe wangu alinunua vipodozi au nguo, sikumuuliza kulihusu na sikuliwazia kamwe, nimemtendea tu vizuri kulingana na neno la Mungu, na bila ya kulijua nilikuwa tayari nimeacha chuki niliyokuwa nayo kwa binti mkwe wangu. Baada ya kuanza kuweka hili katika vitendo, haikuwa vigumu sana kupatana na binti mkwe wangu kama ilivyokuwa zamani. Jambo la ajabu ni kwamba, binti mkwe wangu alibadilika polepole na kuanza kunisaidia kufanya kazi kote nyumbani, na akaanza kuosha nguo za mwanangu na za mjukuu yeye mwenyewe. Yeye pia hakutumia fedha bila hadhari kama hapo awali, na hisia katika nyumba yetu ikawa ya kuridhisha zaidi na zaidi.
Siku moja, mwanangu akaniambia: “Mama, Lili anasema kwamba umebadilika, kwamba awali kila wakati ulipomwona akienda kwa ununuzi lilikufanya usiwe na furaha na ungemuuliza kulihusu, lakini sasa huko sawa kama awali.” Baada ya kusikia mwanangu akisema hivi, nilifurahi sana, na nikamjibu: “Yote ni kwa sababu ya neno la Mwenyezi Mungu kwamba nimebadilika. Awali, nilikuwa na kiburi na kujidai sana, daima nilimtaka Lili kufanya mambo kulingana na njia yangu ya kuishi, sikuwahi kamwe kuzingatia hisia zake, na sikujifikiria katika hali yake ili kuangalia mambo. Kama haikuwa kwa mwongozo wa neno la Mungu, basi singekuja kutambua tabia yangu mwenyewe potovu, na nisingeweza kujibadilisha, jambo ambalo lingelifanya kutoepukika kwa Lili na mimi kugombana sisi kwa sisi kila siku. Kuanzia sasa kwendelea sitajaribu kumfundisha funzo, Lili ni mtu mzima, ana njia yake ya kuishi, na mimi, kama mama mkwe, ninahitaji kumheshimu na kumpa uhuru. “Baada ya kusikia jibu langu, mwanangu aliniambia kwa furaha sana: “Mama, Mwenyezi Mungu unayemwamini kwa kweli ni mkuu!”
Kupitia uzoefu wangu, kwa kweli nilihisi furaha ambayo huja kutokana na kuliweka neno la Mungu katika vitendo. Maneno ya Mungu kwa kweli yanaweza kutubadilisha na kutuokoa, yakituwezesha kuishi maisha yenye furaha na yenye baraka. Sasa familia yangu inaweza kuishi pamoja kwa upatanifu, na kwa ajili ya hilo namshukuru Mungu kwa dhati kwa kuniokoa. Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu!
Chanzo: Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"
Sikiliza zaidi:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni