Jumapili, 12 Mei 2019

Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu

Na Ouyang Mo, Mkoa wa Hubei
Baada ya miongo miwili ya mema na mabaya ambayo yeye na mumewe walipitia pamoja, hakuwahi kamwe kufikiria kwamba mumewe angekuwa na uhusiano wa nje ya ndoa. Alishindwa kabisa kuvumilia wakati alipogundua hilo. Licha ya kujaribu kila kitu ili kumfanya mumewe ampende tena, yote ilikuwa kazi bure. Katikati ya maumivu yake na kutokuwa na tumaini, ni maneno ya Munguyaliyomwokoa, yakimsaidia kupata kiini cha maumivu yake, kuelewa maana ya maisha, na hatua kwa hatua kutoka kwenye fadhaa ya mateso yake.
Muda kweli huyoyoma. Hong’er alikua kutoka msichana mdogo mshamba na kuwa mwanamke mzuri kijana, na shauku yake katika upendo ikaamka. Yeye hakupendelea utajiri au hadhi, lakini alitaka tu uhusiano ambao, bila kujali shida wanazopitia, kuna urafiki wa karibu sana na upendo, wao husaidiana wakati wa haja, na kuzeeka pamoja. Alikuwa akisubiri kwa utulivu kuwasili kwa wakati fulani …
Mume aliingia ghafla ndani ya ulimwengu wa Hong’er, akiufanya moyo wake upapatishwe na uso wake mzuri na macho maangavu kabisa, na pia alikuwa na hisia kwa kweli kwa Hong’er. Kuanzia hapo, siku zake tulivu, shwari zilikuwa zimejaa kianga. Baada ya muda walikuja pamoja, na upole wake na busara yake vilitia msukumo upendo ndani ya Hong’er hata zaidi ya uzuri yake. Hong’er alijua kwamba yeye ndiye aliyetaka kumwaminia maisha yake na kuzeeka pamoja naye. Pia yule mume aliapa kumpa furaha ya maisha. Hata hivyo, wazazi wake walilalamika kwamba yule mume alitoka kwenye familia masikini na wakamtaka amwache. Hong’er hakujali kabisa kuhusu hilo, kwamba tu kwa kweli walipendana na wangeweza kubaki pamoja imara maisha yote. Licha ya vipingamizi vya wazazi wake, alihamia mbali pamoja naye.
Baada ya muda mfupi walikuwa na mtoto mvulana wa kupendeka, mnenemnene, na walifanya kazi kwa bidii kumpa maisha mazuri. Ingawa lilikuwa jambo gumu na la kuchosha kwa Hong’er, kufanya kazi kwa bidii pamoja na mpenzi wake kuilea nyumba yao pamoja ilikuwa furaha nzuri sana kwake. Hasa siku ya kuzaliwa kwake, mume alitumia mshahara wake wa nusu mwezi ili kuagiza wimbo wa mapenzi—Inyeshe Isinyeshe—uchezwe redioni kwa ajili yake. Mara tu ulipoanza aliguswa sana kiasi kwamba alilia; katika wimbo huo, alisikia sauti za mioyo yao zikiunganishwa. Ni kipi kinachoweza kuwa cha thamani zaidi kuliko watu wawili wanaopendana ambao wamegundishwa pamoja milele, walioahidiana kuwa pamoja? Hong’er hakuwa akitafuta utajiri mkubwa, ni aina hii ya upatanifu wa ndoa tu na mapenzi. Nyumba kama hiyo patanifu ilitosha kwake.
Miaka ilipita kama siku, na kufumba na kufumbua tayari ilikuwa miaka 20. Mwana wao alikuwa mtu mzima na walikuwa wanafanya kazi kwa bidii pamoja ili kuanzisha biashara kubwa ya familia. Lakini kwa wakati fulani alitambua kwamba mumewe alikuwa akija nyumbani mara chache zaidi na zaidi, na kutoa udhuru zaidi na zaidi kwamba ilimlazimu kuwaburudisha wengine. Nyumba iliyokuwa kwa wakati mmoja yenye upendo, na furaha ilianza kuonekana kutokuwa na urafiki zaidi na zaidi. Hong’er alikuwa na wasiwasi: Walipokuwa tu wakiandaa ujenzi wa kampuni hiyo kulikuwa na vitu vingi ambavyo mume alilazimika kuvishughulikia mwenyewe, na ingawa kweli alikuwa na shughuli nyingi wakati huo daima angekuja nyumbani haraka alivyoweza. Sasa vipengele vyote vya uendeshaji wa kampuni hiyo vilikuwa vinafuata mkondo na hakuwa na shughuli nyingi kama hapo awali, hivyo kwa nini angerudi nyumbani mara chache? Hong’er alijihisi mpweke. Alikuwa na uelewa wa asili wa mtindo wa wateja wao: Huduma ya mahali pamoja ya aina zote za burudani kama vile kusinga miguu, bafu za mvuke, karaoke, na klabu za usiku zilishakuwa kanuni zisizosemwa za sekta hiyo, na ulishakuwa mtindo kwa wanaume wengi kuzuru kila aina za maeneo ya burudani kuwa na ushirikiano wa ngono wa usiku mmoja au uhusiano wa nje ya ndoa. Mumewe akiwaburudisha wageni siku baada ya siku, akiingia na kutoka katika aina hizo za maeneo ya burudani ambazo zilijaa majaribu, inaweza kuwa kwamba …? Hapana, Isingewezekana! Yeye na mumewe walikuwa wametembea pamoja kupitia kila shida kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita, na kila kitu kidogo wakati huo kilikuwa ushahidi kwa mapenzi yao. Msingi wa nguvu jinsi hiyo wa upendo ungewezaje kuvunjika mbele ya majaribu kidogo? Alikuwa na uhakika kwamba upendo wao ungeweza kuhimili mtihani wowote. Hong’er alitumia hilo kujifariji, lakini akiwa amekabiliwa na uhalisi wake, bado hakuwa na utulivu kabisa.
Lakini uhalisi haukukubaliana na kujituliza kwa Hong’er kama ambavyo angependa. Mumewe alikuwa na gharama moja kubwa, isiyoelezwa baada ya nyingine, alishindwa kurudi nyumbani mara kwa mara zaidi, na alikuwa mjanja sana katika sababu zake. Mambo yote haya yalikuwa mapigo kwake; wasiwasi ndani ya moyo wake ulimsumbua hata zaidi. Ingawa alihisi, kwa kutegemeza kulingana na tabia isiyo ya kawaida ya mumewe, kwamba labda hakuwa mwaminifu kwake, hakuwa tayari kukubali au kukiri uhalisi huo. Hakuthubutu kuamini kwamba mtu ambaye alikuwa amemwahidi kumpa furaha ya maisha na ambaye alikuwa amepitia miongo miwili ya matatizo pamoja naye angeweza kumsaliti ghafla. Yaweza kuwa kiapo cha “mpaka kifo kitutenganishe” hakikuwa kitu ila uwongo rahisi?
Uhalisi haukumruhusu Hong’er kuendelea kujidanganya tena; akaanza kumfuata. Siku moja, alimfuata hadi kwenye jamii moja ya kitajiri sana na akagundua kulikuwa na nyumba pale aliyokuwa ameijenga na mwanamke mwingine. Wakati alipomwona huyo mwanamke amemshika mtoto mdogo mikononi mwake ulikuwa mshtuko kamili. Hakuthubutu kuyaamini macho yake mwenyewe. Lilikuwa limeingia mawazoni mwake mara nyingi kwamba iliwezekana mumewe alikuwa akiingia na kutoka kwenye hoteli na wanawake wengine, kwamba alikuwa na urafiki wa ndani nao, lakini hakuweza kufikiri kwamba angeanzisha familia nyingine na kuwa na mtoto na mwanamke mwingine. Wakati huo chembe ya mwisho ya faraja aliyokuwa nayo kwake mwenyewe ilivunjikavunjika, ikaanguka akiwa amekabiliwa na ukweli wa kuchukiza. Kufumba na kufumbua, viapo vyao, na kila sehemu ya zaidi ya miongo miwili ya kusaidiana kwa pamoja viliporomoka hadi chini, chini kabisa. Angewezaje kuwa katili hivyo? Angeweza kweli kuwa amesahau ahadi yake kumpa furaha ya maisha? Alikuwa amesahau hisia alizozionyesha kupitia wimbo “Inyeshe Isinyeshe”? Alikuwa amesahau kwamba alikuwa ameacha kila kitu kwa ajili yake, na kila kitu ambacho walipitia pamoja? Angewezaje kusahau? Angemfanyia hivyo kwa nini? Miaka ishirini ya upendo ingeshindwaje kuhimili majaribu ya mgeni? Wakati huo hasira na huzuni vilimghadhabisha Hong’er; moyo wake ulikuwa unatetemeka na machozi yalimtiririka usoni bila kupenda. Alimpigia mumewe kelele kwa sauti iliyopwelea, “Una hakika unataka kututupa mimi na mwanao kando na kumchagua mwanamke huyu?” Alitumaini kuona sura ya hatia kwenye uso wa mumewe, kumwambia kwamba alikuwa amekosea, kusema kwamba bado alikuwa ameichukua familia yao moyoni mwake, lakini mumewe alikuwa kimya kabisa licha ya machozi yake na kuhoji kwake. Kuona mtazamo wake, Hong’er alichanganyikiwa kabisa. Hakuwa na habari kabisa kwa nini angeweza kumsaliti kinyama hivyo. Akampiga kofi kwa nguvu, akishindwa kudhibiti chuki iliyokuwa ndani ya moyo wake.
Hong’er hakuwa na kumbukumbu ya kuondoka mahali hapo—ilionekana kama kila kitu kilikuwa kimefyonzwa kutoka ndani yake. Alisimama ufuoni kadiri utusitusi wa jioni ulivyoongezeka, bila mwenzi isipokuwa mwanga uliokuwa ukififia na alama za jua linalotua. Wimbi baada ya wimbi la maumivu lilichemka moyoni mwake. Onyesho baada ya onyesho la miongo yao pamoja lilitokea mbele ya macho yake moja baada ya jingine. Alikuwa amepuuza upinzani wa familia yake dhidi ya huyu mwanamume na alikuwa amehamia mbali sana kutoka nyumbani wakiwa naye. Alikuwa amefanya kazi kwa bidii pamoja naye na hakuna matatizo yao yoyote ya kifedha yaliyokuwa yamefifiza hisia zao hata kidogo. Walikuwa wamefika umbali huu pamoja wakipitia yote machungu na matamu, upepo na mvua. Walikuwa wametajirika na mtoto wao alikuwa amekua, lakini mumewe alikuwa na uwezo wa kuitupa familia yenye furaha ili kujenga kiota na mwanamke mwingine. Alichukia kukosa kwake msimamo, na kuuchukia ukatili wake. Lakini mara tu alipofikiria familia hii yenye furaha ambayo alikuwa ameifanyia kazi kwa bidii ikipotea tu, alihisi kuwa hawezi kuvumilia kutengana nayo na hivyo alitaka kufanya yote aliyoweza kuirudisha. Mradi angerudi angeweza kuyasamehe makosa yake ya zamani kwa sababu alikuwa amebahatishia furaha yake yote naye.
Baada ya kurudi nyumbani Hong’er alianza kufanya mipango ya kuiokoa ndoa yake. Rafiki mmoja akamwambia: “Mwanamume anapokwenda nje kufanya kazi ili kukimu maisha, yeye hupata matamshi mengi mno ya dharau huko nje. Anapokuja nyumbani yeye huhitaji upendo wa nyumbani; kwa njia hiyo atakuwa na furaha. Kama tu wanavyosema, ‘Mwanamume humpenda mkewe kwa kupikiwa chakula kitamu na mkewe.’” Hong’er alijua kwamba mumewe alipenda maandazi ya kinyunya, hivyo kila siku kwa utaratibu alitengeneza aina mbalimbali za maandazi ya kinyunya kwa mikono na kufikiria kila njia yoyote nyingine kuuliza juu yake kwa umakini. Alimtumia mtoto wao kutengeneza sababu za aina zote za kumfanya aje nyumbani, lakini bila kujali jinsi Hong’er alivyomshawishi daima alikuwa amevuvuwaa. Hong’er alifikiria labda hakupenda kwa sababu Hong’er alikuwa akizeeka na kupoteza urembo wake hivyo akaanza kutumia nguvu nyingi katika kujipamba ili kuonekana kijana. Alifikiria njia nyingi za kuurejesha moyo wa mumewe, lakini yote ilikuwa bure. Kipindi hicho kweli kilikuwa kigumu na cha kuchosha kwa Hong’er, na alihisi kweli kutojiweza. Kila siku, aliosha uso wake kwa machozi na hakuweza kulala vizuri usiku. Hakujua ni vitu vingapi alivyovijaribu kurekebisha nyumba yao iliyovunjika. Bila chaguo jingine lolote, angesubiri tu katika maumivu yake, na kusubiri mumewe kuja karibu.
Hong’er alisubiri hivyo kwa miaka mitatu, na katika siku hizo zote ndefu alijiuliza zaidi ya mara moja: “Hisia kutoka kwenye miaka zaidi ya ishirini zinawezaje kutoweka hivyo tu? Kwa nini nisingeweza kuirudisha familia yenye furaha, kamilifu kutokana na jitihada zangu zote?” Aliuliza tena na tena, lakini hakuna mtu aliyeweza kumpa jibu. Alisubiri siku baada ya siku, lakini hakuna kitu kilichokuja. Ilikuwa bila shaka “hukumu ya kifo” kwa ndoa yake na mumewe. Akiwa na huzuni nyingi, Hong’er hakuwa na nguvu tena ya kuhimili aina hiyo ya pigo. Alikuwa amefika mwisho na hakuwa tena na ujasiri au nguvu za kuendelea. Alimeza kwa funda moja tembe arobaini za dawa za kulegeza misuli…
Aliamka siku iliyofuata na kujikuta hospitalini na kuona kuwa mwanawe na mumewe walikuwa hapo. Machozi ya uchungu yalifurika bila kukoma usoni mwake—alilia hadi akapata kizunguzungu, moyo wake ukiwa umevunjika. Familia kuja pamoja katika hali hizi ilikuwa ni kejeli sana, lakini hakuna kitu angeweza kufanya juu ya jambo hilo. Aliangalia juu angani na kushusha pumzi: “Ni nani anayeweza kuniambia ni kwa nini mume na mke wanaweza kufaulu katika shida pamoja, lakini hawawezi kufaulu katika utajiri? Mapenzi ya zaidi ya miongo miwili yanawezaje kuwa dhaifu hivi?”

Muda mfupi baada ya hayo, mama mkwe wa mwanawe akashiriki injili ya Mungu ya siku za mwisho na Hong’er na kumwambia kuwa ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa na kushughulikia mateso yake yote. Hii ni kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu; hapo mwanzo, wanadamu waliishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu na waliishi kwa furaha sana, lakini wakawa mbali na Mungu kwa sababu walikuwa wamepotoshwa na Shetani. Walianza kukataa kuwepo kwa Mungu na kuishi ndani ya madhara ya Shetani; kukatishwa tamaa kwao na maumivu yao vilikua na kukua. Mungu mwenyewe akawa mwili ili kuonyesha ukweli na kumwokoa wanadamu ili kuwapokonya wanadamu kutoka kwenye mkamato wa Shetani. Mtu akija mbele ya Mungu, asome maneno Yake na kuelewa ukweli kupitia kwayo, ni wakati huo tu anapoweza kubaini kiini cha uovu katika jamii, kukaa mbali na madhara ya Shetani, na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu. Mama mkwe wa mwanawe akasoma kifungu cha maneno ya Mungu: “Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu yako itarejea: ukiwa na utambuzi wa ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, kwa namna fulani na mahala fulani ulipopotea kwa wakati mmoja, ukianguka barabarani ukiwa hujitambui, halafu pasipo kujua unakuwa na baba. Unatambua zaidi kuwa mwenye Uweza amekuwa akiangalia, akisubiri kurejea kwako muda huu wote” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Baada ya kusikiliza maneno haya ambayo hakuwahi kamwe kusikia kama hayo kabla, Hong’er aliguswa mno, kana kwamba mkondo wa vuguvugu ulikuwa ukifurika ndani ya moyo wake na kumtia joto, mwili na moyo. Kwa miaka hiyo michache iliyopita hakuna mtu aliyekuwa ameielewa huzuni kali ndani ya moyo wake, na hakuna mtu angeweza kushiriki mzigo wa maumivu yake. Hasa, hakuna mtu aliyeweza kumwelewa au kumfariji. Alikuwa amekaa siku nyingi usiku za upweke, kukosa usingizi, akilia kimya mpaka alfajiri akiwa peke yake. Hilo jeraha lilimfuata kama kivuli ambacho hakuweza kamwe kukisahau au kukiondoa. Alidhani hakuwa na chaguo ila kuendelea mbele jinsi hiyo, akiwa mpweke na mwenye maumivu, kwa miaka yake iliyobaki. Lakini siku hiyo, kifungu hicho kilibisha mlango wa moyo wake. Aligundua kwamba alipokuwa na maumivu, akivumilia mateso, na akilia, Mungu alijua na Alikuwa daima pembeni yake akisubiri ageuke. Aliposikia maneno ya Mungu ya kulea, Hong’er hakuweza kujizuia kujawa na machozi; alihisi kuwa Mungu alikuwa pamoja naye na kwa kweli hakuwa peke yake. Ingawa hakuwa amesikia kumhusu Mungu kabla na hakujua chochote juu Yake, alikuwa daima Akimwangalia akiwa kando yake. Hakumwokoa tu mapema na kuhifadhi maisha yake wakati aliamua kufa, lakini wakati alipopoteza kabisa matumaini katika maisha, Alimruhusu kusikia sauti Yake kupitia mkwe wa mwanawe. Alitumia maneno Yake kumgusa na kuupa moyo wake upendo, akileta matumaini na kuboresha maisha yake ya kukata tamaa na maumivu. Wakati huo, Hong’er aliona upendo na wokovu wa Mungu na moyo wake uliojeruhiwa ulifarijika. Alikuwa na kitu cha kutegemea.
Baada ya hayo Hong’er ilianza kuhudhuria Kanisa la Mwenyezi Mungu, kusoma maneno ya Mungu, kushiriki ukweli, na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu wakiwa na ndugu na dada zake. Aliona kwamba wote walikuwa wema na waliwatendea wengine kwa uaminifu. Waliweza kusema kwa uaminifu na kwa urahisi kuhusu upotovu walioufichua, kisha kuchangua upotovu huo kulingana na maneno ya Mungu na kutafuta kuwa watu waaminifu ambao Mungu huwapenda. Hakuna mtu aliyemdhihaki mtu mwingine yeyote, lakini walisaidiana na kupeana riziki. Kila uso ulikuwa unafurika tabasamu zenye furaha. Hong’er aliona hali ya kweli, yenye furaha ikiwa ya kuambukiza na alipata aina ya utulivu na uhuru ndani ya familia hiyo kubwa ambayo hakuwahi kuwa nayo kamwe kabla. Aligundua upya upendo ambao hakuwa ameuhisi kwa muda mrefu na hisia ya kuja nyumbani. Dhiki yake ilipungua siku baada ya siku, na polepole tabasamu zilionekana kwenye uso wake. Ndani ya maneno ya Mungu alipata majibu ya mambo ambayo kwa muda mrefu yalimchanganya na akajua kiini cha mateso yake mwenyewe. Aliona yafuatayo katika maneno ya Mungu: “Kwa kweli, kati ya vitu vingi katika uumbaji wa Mungu, mwanadamu ni wa kiwango cha chini sana. Ingawa ni mtawala wa vitu vyote, mwanadamu ni kiumbe pekee ambaye yupo chini ya hila za Shetani, ni kiumbe pekee ambaye anashikwa kwa namna nyingi katika uharibifu wake. Mwanadamu hajawahi kuwa na ukuu juu yake mwenyewe. Watu wengi wanaishi katika uovu wa Shetani, na kuumizwa na dhihaka zake; anawaudhi kwa njia hii hata hapo watakapokuwa wamelemewa kabisa, wakistahimili kila badiliko, kila ugumu katika ulimwengu wa kibinadamu. Baada ya kuwachezea, Shetani huimaliza hatima yao” (“Kazi na Kuingia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Moja baada ya nyingine, hii mienendo yote inabeba ushawishi mwovu unaoendelea kumpotosha mwanadamu, kumfanya kuendelea kupoteza dhamiri, ubinadamu na mantiki, na unaoshukisha maadili yao na ubora wao wa tabia zaidi na zaidi, hadi kwa kiwango ambamo tunaweza hata kusema wengi wa watu sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, wala hawana dhamiri yoyote, wala akili yoyote” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Nyote mnao uzoefu wa neno “usaliti” kwa sababu watu wengi wamefanya kitu kuwasaliti wengine awali, kama vile mume kumsaliti mke wake, mke kumsaliti mume wake, mwana kumsaliti baba yake, binti kumsaliti mama yake, mtumwa kumsaliti bwana wake, marafiki kusalitiana, jamaa kusalitiana, wauzaji kuwasaliti wanunuzi, na mengineyo. Mifano hii yote ina asili ya usaliti” (“Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Asili ya mtu ni maisha yake, ni kanuni ambayo anaitegemea ili kuendelea kuishi, na anashindwa kuibadilisha. Jinsi ilivyo hali ya usaliti—kama unaweza kufanya kitu ili kumsaliti ndugu au rafiki, hii inathibitisha kwamba ni sehemu ya maisha yako na hali ambayo ulizaliwa nayo. Hiki ni kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukikana” (“Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Kupitia maneno ya Mungu, Hong’er alielewa kuwa mateso yote ya binadamu hutokana na upotovu wa Shetani, na kwamba watu wote huishi ndani ya pipa kubwa, lililokolezwa kabisa uovu. Huwa tunashambuliwa na jumbe mbovu za Shetani kama vile: “Fanya nyumba yako kuwa imara, na uwe na burudani pembeni”; “Maisha ni mafupi. Yafurahiye wakati unapoweza”; “Chukua fursa kustarehe, kwa maana maisha ni mafupi”; “Wanaume tisa kati ya kumi huchezacheza, wa kumi ni mpumbavu tu.” Hizi hudai kwamba mwanamume kujihusisha na mwanamke mwingine, kuwa na hawara kunavumilika na ni ishara ya hadhi. Aidha, kumbi za burudani ambazo zimejaa majaribu tele ziko kila mahali, kutoka mitaa mikubwa hadi vichochoro vidogo, zikifanya iwe rahisi sana kwa watu kujiingiza katika raha za kimwili. Watu wengi hujishughulisha bila aibu na ushirikiano wa ngono wa usiku mmoja na uhusiano wa nje ya ndoa. Wao ni waovu na wapotovu sana, wameharibiwa sana kiasi kwamba hawana mfano wa binadamu. Watu wanapokosa kuuelewa ukweli hawana utambuzi wowote kati ya mema na maovu, uzuri na ubaya, au uwezo wowote wa kutofautisha kati ya mambo hasi na mambo chanya. Mitazamo yao juu ya mambo imepotoka na huchukua mambo maovu kama ya haki na ya heshima. Wao hukataa ahadi zao na kuzisaliti ndoa zao ili tu kuziridhisha tamaa zao za kimwili, wakipoteza mshiko wa ubinadamu, mantiki, maadili, na heshima ambazo wanadamu wanapaswa kuwa nazo. Wao huishi chini ya miliki ya Shetani na hujifurahisha kikamilifu katika mwili, hufuatilia starehe, na kuziridhisha tamaa zao zisizofaa. Hong’er akaiwazia jamii hii mbovu. Waume kuwasaliti wake na wake kuwasaliti waume ni matukio ya kawaida; chini ya uharibifu wa mitindo miovu, watu ambao hawana ukweli hawana upinzani kwa mambo haya. Wana uelekeo wa kupatwa na athari za mawazo haya maovu japo hawatarajii hilo, na wao hupuuza majukumu, maadili na haki, na dhamiri zao ili tu kuiridhisha tamaa ya muda mfupi ya kimwili. Huwatupa pembeni wake au waume zao, wakisababisha madhara yasiyoaminika kwa familia zao, labda hata mateso ya maisha. Aliona kwamba mumewe pia alikuwa mwathirika wa mitindo hii miovu ya Shetani. Hong’er alikumbuka jinsi mumewe alivyozoea kumtunza na kumpenda sana, na kwamba hawakujitafutia utajiri wa mali—ni upendo wa wote wawili na huba tu, na furaha na upatanifu. Lakini mara tu walipotajirika alianza kuwaburudisha wateja mara nyingi na kuruka kutoka eneo moja la burudani hadi jingine. Hakuweza kukataa mvuto wa mitindo hiyo miovu na alianza kuishi maisha ya uasherati. Alikuwa na uhusiano wa nje ya ndoa na alikuwa akiishi kwa tamaa zake zisizofaa, akifikiria tu juu ya kuiridhisha tamaa yake ya kimwili. Hakufikiria kamwe hisia za mkewe, sembuse familia yao. Hili lilisababisha kuvunjika kwa nyumba yao na kutengana kwao. Upendo waliokuwa nao kwa zaidi ya miaka ishirini ulionekana kuwa dhaifu sana mbele ya hiyo mitindo miovu; haungeweza kuhimili pigo dogo kabisa. Si hayo yote yalisababishwa na Shetani kumpotosha mwanadamu?
Hong’er alitambua kwamba alikuwa amedhuriwa sana na Shetani, daima akitafuta upendo wa upatanifu wa ndoa, kuzeeka pamoja, na “hadi kifo kitutenganishe.” Alidhani kwamba kuwa na ndoa ya aina hiyo kulikuwa ndiyo furaha ya pekee katika maisha. Baada ya mumewe kupotea alijaribu kila kitu ili kuokoa upendo wao ulioharibiwa, na wakati matamanio yake yalipokuwa hayakutimizwa aliishi katika fadhaa ya maumivu na hakuweza kujinasua, hata kujaribu kupata faraja katika kifo. Si hayo yote yalikuwa ni mawazo na mitazamo isiyo sahihi tu ambayo Shetani amewajaza wanadamu nayo katika kumchezea na kumdhuru Hong’er? Ni kwa kusoma maneno ya Mungu tu ndipo Hong’er alielewa kwamba wanadamu wote ni wenye ubinafsi na hufanya vitu vyote kwa manufaa yao wenyewe na kulingana na kanuni zao wenyewe. Hakuna upendo wa kweli kati ya watu wawili; upendo wa kimapenzi haupo kabisa. Lakini Shetani hutumia dhana za aina zote za upuuzi kuwapotosha na kuwashawishi watu ili wauheshimu uovu na kufuatilia upendo wa kimapenzi zaidi ya yote, wakiishi kabisa ndani ya uongo wake. Wanakuwa wapotovu na waliokengeuka zaidi na zaidi, na kuwa mbali na Mungu zaidi na zaidi. Ilikuwa ni wakati huo ambapo Hong’er kweli aliona kwamba bila ya ukweli, watu hawana utambuzi kati ya mema na maovu, uzuri na ubaya, na hakuna utambuzi kwa mambo chanya. Watachezewa na kudhuriwa tu na Shetani, na hatimaye kumezwa wazima na Shetani. Kwa sababu ya wokovu wa Mungu, Hong’er aliona ukweli wa upotoshwaji wa wanadamu na Shetani na kugundua kiini cha mateso. Maneno ya Mungu yaliuchangamsha moyo wake sana; alihisi starehe zaidi.
Halafu Hong’er akasoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu kina uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Hong’er alielewa kutoka kwenye maneno ya Mungu kwamba ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye upotovu wa Shetani, na watu wanaweza tu kupata utambuzi juu ya mbinu na utaratibu wa kuwapotosha wanadamu wa Shetani kwa kuuelewa ukweli kupitia maneno ya Mungu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kupata ufahamu kuhusu ulaghai wa Shetani, kuepuka madhara yake, na kuishi kwa uhuru. Alishusha pumzi, akisikitika kwamba kwa miaka mingi sana alikuwa ametawaliwa na mawazo yasiyo sahihi na kwamba kutafuta furaha kwa kupitia ndoa ilikuwa njozi tu. Alifikiria ukweli kwamba mumewe pia alikuwa mtu aliyepotoshwa na Shetani, na yote aliyoyatafuta yalikuwa mambo hasi, maovu. Kwa hivyo angeweza tu kumletea mateso na uharibifu; hangeweza kumletea furaha yoyote. Ni upendo wa Mungu kwa watu tu usio wa ubinafsi, na ni Mungu tu anayetaka kwa dhati kuwaokoa watu kutoka kwenye utawala wa Shetani. Mungu ameonyesha kila aina ya ukweli na hupanga kila aina ya mazingira ili kuwatakasa na kuwabadili wanadamu, na yote ni kuwaongoza watu kuepuka madhara ya Shetani na kuwaletea maisha ya furaha. Lakini kwa wanadamu wapotovu, mara tu kitu kinapogusa maslahi yao wenyewe binafsi watasaliti; ni Mungu pekee anayeweza kuwa upande wa watu wakati wote, mahali pote, na kuwasaidia kukabiliana na shida zote. Ni Mungu pekee anayeweza kutegemewa kwa hakika, na nyumba ya Mungu ni bandari halisi pekee kwa roho ya mtu. Wakati wa zamani, Hong’er hakuwa na ufahamu wa mitindo miovu ambayo huibuka kutoka kwa Shetani na alikuwa ameishi tu kwa kumchukia mumewe bila furaha yoyote au nderemo. Aliishi kila siku katika mateso, kama amefungwa na kudhuriwa na Shetani—maumivu hayakusemeka. Sasa kwa vile alikuwa amepata kiini cha mateso yake hakumchukia mumewe tena. Ilikuwa ni kama uzito mkubwa ukiondolewa kutoka kwenye mabega yake, na alihisi aina fulani ya amani, utulivu, na uhuru katika roho yake ambavyo hakuwahi kuwa navyo awali kamwe! Kwa kweli alipata uzoefu wa kuwa na ufahamu kuhusu kila aina ya watu, matukio, na mambo kupitia kuufahamu ukweli na hatimaye alikuwa huru kutoka kwenye maumivu makali ya mateso na madhara kutoka kwa Shetani.

Sasa kwa vile alikuwa na nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu, Hong’er hakusononeka tena hivyo kama awali. Pia alimwachilia kabisa mumewe na kuwa na amani na usaliti wake wa ndoa yao. Hatimaye aliziaga hizo siku za fadhaa zilizomtisha na kila mtu aliyemjua alisema kuwa alikuwa amebadilika kama mtu, kwamba alikuwa amekuwa mwenye kufikiri vizuri zaidi na asiye na mawazo. Alijaa shukrani kwa Mungu kwa sababu mabadiliko haya yote yalifanikishwa ndani yake kupitia maneno ya Mungu.
Miaka kadhaa imepita. Hong’er husoma maneno ya Mungu mara nyingi, huishi maisha ya kanisa, ana ushirika juu ya maneno ya Mungu na ndugu zake na dada zake, na huweka kila kitu katika kutimiza wajibu wa mmoja wa viumbe. Siku zake zinatosheleza sana. Ameuelewa ukweli fulani na ameona kwa dhahiri kwamba maisha ya mtu duniani hayaishwi tu kwa ajili ya mume au mke wa mtu au watoto, lakini ni kutimiza wajibu sahihi wa kiumbe, na kwamba ni kwa kuishi kwa njia hiyo tu mtu anaweza kuleta furaha kwa Mungu. Hatimaye amepata njia sahihi katika maisha, ambayo ni kumfuata Mungu, kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, kupitia kazi ya Mungu, na kutafuta kuelewa na kupata ukweli. Ni kumwogopa Mungu na kuepukana na uovu, na kuwa mtu ambaye humtii na kumwabudu Mungu. Haya yote tu ndiyo aina ya maisha yenye maana na yenye furaha zaidi. Nia ya Hong’er ni kuichukua njia ya aina hii katika maisha chini ya mwongozo na uongozi wa Mungu, kupata ukweli na uzima, kujiweka huru kabisa na madhara ya Shetani, na kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana—kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli na kuleta utukufu kwa Mungu!

Chanzo: Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni