Alhamisi, 9 Mei 2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 1)



Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Jioni moja, Jingru alikuwa akinadhifisha kwake.
“Krr, krr.” Simu ilianza kulia. Aliijibu na sauti ngeni lakini bado inayojulikana ililia sikioni mwake: “Halo! Ni Wang Wei. Uko nyumbani!”
“Wang Wei?” Jingru kwa namna fulani alistaajabu: Kwa nini alikuwa akimpigia simu sasa baada ya miaka mingi sana?
“Ndiyo … niko nyumbani. Kuna nini?” aliuliza Jingru kwa mshangao.
“Hatujaonana kwa muda mrefu. Ningependa kukupeleka matembezini. Niko njiani kuja kwako na nitawasili hivi punde. Nisubiri nje ya mlango wako!” Wang Wei akasema.
Baada ya kukata simu, moyo wa Jingru ulianza kupigapiga, na mawazo yake mara moja yakarudia siku zile za shuleni…

Jingru alikuwa hajakuwa wa kupendeza tu, lakini pia alipata alama nzuri, na wavulana wengi shuleni, ikiwa ni pamoja na Wang Wei, walimwandama. Ili kujiingiza katika ulimwengu wa Jingru, Wang Wei alitumia njia za aina zote ili kuwa karibu naye, kama kupitisha jumbe, kuandika barua na kumpa zawadi ili kuelezea hisia zake kwake. Lakini Jingru alikuwa msichana mtiifu, mwenye busara, na hakutaka masomo yake yaathirike au kuvunja matarajio ya wazazi wake kwake kwa sababu ya kushughulishwa na mhemko fulani, na hivyo daima alichukua mtazamo wa kutojali alipokabiliwa na ufuatiliaji wa kung’ang’ania wa Wang Wei. Lakini Wang Wei hakukata tamaa kwa sababu tu Jingru alimpuuza, na miaka kadhaa baadaye Wang Wei alikuwa bado anamfuatilia kama vile alivyofanya daima. Ung’ang’anivu wake ulianza kuugusa kidogo sana moyo wa Jingru, lakini aliguswa kidogo tu. Baadaye, wanafunzi wenza wachache wa kike walianza kuonekana karibu na Wang Wei, na wangemfuata pote mchana kutwa. Moyo mtulivu wa Jingru ulianza kukurupuka na hisia, na alifikiri angeweza kutumia hali hii kumpima Wang Wei kwa muhula mmoja; kama angekosa kuathiriwa na hisi juu ya hawa wasichana na kwendelea kumfuatilia, basi angepunguza ukali kwa ufuatiliaji wake …
“Bip bip!” Honi ya gari ilisitisha njozi ya Jingru. Wang Wei tayari alikuwa nje akisubiri.
Jingru aliingia ndani ya gari lake, na akiwa amekabiliwa na mkutano huu ambao haukuwepo kwa muda mrefu, usiotarajia, wote wawili walikaa kimya.

Walitembea pote kwa gari bila lengo, na hali ikawa ya kufedhehesha kiasi.
Baada ya muda mrefu, Wang Wei alivunja ukimya. “Hivyo … umekuwaje?”
“Vyema, asante. Yote mazuri,” Jingru akajibu kwa upole.
“Umekuwa wapi miaka yote hii? Sikuweza kukupata. Ilikuwa kama ulikuwa umeaga dunia. Ni wakati niliona nambari yako kwenye simu ya rafiki tu ndipo nilipokupigia simu, vinginevyo ni nani anayejua wakati ningekuona tena!” akasema Wang Wei, akiendesha gari na kumwangalia Jingru kila wakati alipokuwa akizungumza.
“Sijakuwa popote. Ni kuwa tu kwamba kazi zimekuwa nyingi sana, hivyo sijakuwa nikiwasiliana na yeyote kati yenu,” alisema Jingru kwa sauti ya uangalifu.
Wang Wei akaegesha gari kando ya barabara. Kisha akamwambia Jingru yaliyokuwa ndani ya moyo wake, na katika sauti yake nzito kulikuwa na huzuni na majuto: “Nilikuwa siku zote nikikufuatilia tulipokuwa shuleni. Kwa miaka mitano nilikuandama! Lakini daima ulikuwa unanipuuza sana, sijui nilipitiaje miaka yote hiyo. Baada ya wewe kuondoka shuleni, nilijiandikisha katika shule ya kijeshi, lakini bado nilikuwaza wakati wote. Baada ya kuhitimu, nilikutafuta kila mahali, lakini sikukupata. Hatimaye, nilioa kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa familia yangu, lakini bado ulikuwa moyoni mwangu, kabla, sasa na milele. Nilipoiona namba yako ya simu bila kutarajia, kulikuwa na neno moja tu katika mawazo yangu: Majuto. Nasikitika kwamba sikungoja kuoa, na kwamba sikukutana nawe mapema…”
Kumsikia Wang Wei akifanya ungamo hilo la kweli, Jingru alihisi huzuni kali. Kumwangalia Wang Wei sasa, ambaye uso wake daima ulikuwa mzuri sasa ulikuwa umekomaa zaidi na wenye hadhi, kwa mshangao wake, moyo wa Jingru ulimgeukia Wang Wei…
“Aa, kukuandama miaka yote hiyo na kutendewa kwa kupuuzwa sana nawe, nilikuwa katika giza, na nilichagua kusubiri jibu lako mwaka mmoja zaidi, lakini mwishowe … bado ulikuwa wewe, nami bado nilikuwa mimi. Niambie, kwa nini ulinipuuza daima shuleni? Ulifikiria nini juu yangu? Je, unaweza kuniambia?” Wang Wei aliyeonekana kusononeka akauliza.
Kusikia hili, Jingru pia alihisi kusononeka na kupata majuto—kusononeka kwa sababu alikuwa mkatili sana wakati huo na pia alikuwa amemuumiza Wang Wei, na majuto kwa sababu alikuwa amekosa nafasi ya kuwa pamoja na Wang Wei wakati huo kwa sababu ya kutojali kwake. Kumwangalia Wang Wei, Jingru alishusha pumzi kwamba baada ya miaka mingi Wang Wei kweli bado alimuweka katika mawazo yake. Alifikiria jinsi ambavyo hakuwa tena mdogo na jinsi ambavyo bado hakuwa na mpenzi wa kufaa, na jinsi ambavyo marafiki zake wote walikuwa wamefunga ndoa mmoja mmoja, wakimwacha yeye kama pekee aliyekuwa peke yake. Alitaka patna ambaye alimpenda pia, na mara nyingi alikuwa ameota picha ya kimapenzi ya yeye na mpenzi wakiwa wandani sana na walio karibu, na hata alikuwa ameota ndoto ya yeye na Wang Wei wakienda pamoja …. Pia alifikiria jinsi Wang Wei alivyokuwa amemwandama kwa ung’ang’anivu wakati wa nyuma, na alijuta kwamba hakuweza kuthamini jambo hilo. Sasa Wang Wei alikuwa bado akimwandama na kwa kweli alitaka kupunguza ukali kwake, na kuwa patna wake. Lakini akili yake ikamwambia: “Wang Wei ameoa tayari! Kama Mkristo, lazima uwe na ushuhuda wa Kikristo. Bila shaka ni lazima usiseme kwa msukumo hisia zako za kweli kwa Wang Wei. Ni kwa wewe kutenda tu kulingana na matakwa ya Mungu ambapo unaweza kupatana na mapenzi ya Mungu.” Lakini hisia za ndani ya moyo wake na akili yake vilimvuruga kwa njia tofauti, na alihisi kuhuzunishwa.
Jingru aliyaweka sawa mawazo yake yaliyotatizika, akijilazimisha kujifanya kuwa hakuna chochote kilichokuwa kibaya, na kumjibu Wang Wei: “Mwaka huo, nilitaka kukujaribu kwa muhula mmoja zaidi. Ikiwa hisia zako kwangu hazingebadilika, basi ningefikiria kuwa na urafiki nawe. Lakini baadaye nilifikiria matarajio ya wazazi wangu kwangu … nadhani ilikuwa kudura!”
Jingru alificha hisia zake aliposema hili, lakini alihisi maumivu makali. Kama angeweza kurudisha saa nyuma, bila shaka angekubali kuwa na urafiki na Wang Wei bila kusita hata kidogo, na labda hawangekuwa katika hali hii sasa. Lakini sasa, Jingru alikuwa anafanya yote anayoweza kuzizuia hisia zake, na machozi yakaanza kutiririka kimya kimya usoni mwake. Alihofia Wang Wei angeona, kwa hiyo akageuza uso wake kuelekea dirishani. Lakini Wang Wei alihisi kuwa Jingru alikuwa analia, na kwa haraka akatoa karatasi ya shashi kuyafuta macho yake.
Moyoni mwake, Jingru alimwita Mungu kimya kimya kumtunza, ili aweze kujikaza asianguke katika majaribu na kupoteza ushuhuda wa Mkristo. Aliichukua ile karatasi ya shashi na kusema, “Nitajifuta.” Baada ya kuyakausha machozi yake, Wang Wei kwa ghafla alichukua mkono wake na akaanza kuuleta juu kwa bega lake, na wakati huo huo, akiwa amefadhaika, Jingru kweli alihitaji bega kwa faraja. Kwa muda mfupi, Jingru alijihisi kuwa katika mpagao, na alitaka kuliegemea bega hilo, lakini maneno ya Mungu ambayo huwafundisha na kuwaonya watu yalitokea katika mawazo yake: “Na kuhusu watu wote watendao uovu (wale ambao huzini, au hujihusisha na fedha chafu, au wana mipaka isiyo wazi kati ya wanaume na wanawake, au ambao hukatiza au kuharibu usimamizi Wangu, au ambao roho zao zimezibwa, au waliopagawa na mapepo mabaya, na kadhalika—wote isipokuwa wateule Wangu), hakuna kati yao ataachiliwa, wala yeyote kusamehewa, lakini wote watatupwa chini Kuzimu na kufa milele!” (“Sura ya 94” katika Matamko ya Kristo Mwanzoni). Jingru alihisi kuwa maneno ya Mungu yalikuwa yakimhukumu na kumkaripia, na kwa muda mfupi alizinduka kutoka kwenye mpagao wake. Alijua kwa dhahiri kwamba Mungu ni mtakatifu, kwamba tabia ya Mungu ni ya haki na haiwezi kudhurika, na kwamba kile ambacho Mungu huchukia hasa ni watu wanaohusika na uasherati na ambao wana mipaka isiyo wazi kati ya wanaume na wanawake. Alijua kwamba kama angefanya kosa katika uhusiano wake na wanaume, basi angetiwa doa milele, na angehukumiwa, kuchukiwa na kulaaniwa na Mungu, angepoteza ushuhuda wa Mkristo na angepoteza wokovu wa Mungu. Jingru alijua kwamba wakati angechukua hatua moja kumwelekea Wang Wei, basi angekuwa amepotea kabisa. Akiwa amekabiliwa na hali hii, Jingru alihisi hofu na wasiwasi visivyokuwa na kifani. Alidhani kwamba hangekosa tu kufanya chochote ambacho kingeikosea tabia ya Mungu, lakini pia ni lazima angeiheshimu ndoa ya Wang Wei. Wang Wei hakuwa tena mvulana katika uga wa shule ambaye alikuwa amemwandama, lakini sasa alikuwa mwanamume mwenye familia, mke na watoto. Kama angechukua hatua mbaya sasa, angeiangamiza familia ya mtu mwingine, na kuwa yule mwanamke mwingine wa kuaibisha. Maneno ya hukumu ya Mungu yalisababisha moyo wa kumwogopa Mungu kuinuka ndani ya Jingru. Akitumia nguvu zake zote, aliutupa mkono wa Wang Wei, akasema kwa dharau, “Muda umeenda sana. Nipeleke nyumbani!”
“Baada ya miaka yote hii, kwa nini bado unanizuia? Siwezi hata kukufariji?” akasema Wang Wei bila furaha.
“Umeelewa visivyo. Sikuzuii. Ninakuheshimu, kwa sababu una familia. Ni lazima uwaafikirie,” akajibu Jingru kwa utulivu.
Lakini Wang Wei alimsisitizia Jingru, akisema, “Na kama nikitoa talaka? Unaweza kunipa fursa basi? Sisemi hivi tu kwa ghafula!”
Swali hili lilisababisha moyo wa Jingru kukurupuka na hisia tena, na hakujua cha kusema. Alisali tu kwa Mungu kimya kimya moyoni mwake: “Ee Mungu! Tafadhali ulinde moyo wangu na unizuie kufanya kitu chochote kinachoweza kuikosea tabia Yako.” Baada ya kuomba, alifikiria maneno haya ya Mungu ambayo yanasema: “Maneno yao hulisha moyo wako na kukupendeza mno ili ukanganywe na bila kulitambua, unavutwa ndani na uko radhi kuwa wa huduma kwao, uwe mlango wao na kadhalika mtumishi wao. Huna malalamiko kamwe lakini uko radhi kutumiwa nao—unadanganywa nao” (“Tabia Yako Ni Duni Sana!”). Maneno ya Mungu mara nyingine tena yalimzindua Jingru, na alijua kwamba kukurupuka na hisia kwa moyo wake kulikuwa ni kwa sababu alikuwa akianguka chini ya udhibiti wa tamaa mbovu; huyu alikuwa ni Shetani akiweka njama ya hila za kijanja katika kitendo ili kumshawishi, kumfanya aishi katika dhambi na kupoteza ushuhuda wa Mkristo, na kumfanya atumbukie katika tamaa ya kimwili na kuwa mtovu wa tabia na mpotovu zaidi na zaidi. Kwa hiyo, alijua kwamba ni lazima awe na utambuzi, na ni lazima abaini mpango wa hila wa Shetani. Wang Wei tayari alikuwa ameoa—huo ulikuwa ni ukweli—na Jingru alijua kwamba hangeweza kudanganywa hadi kupoteza mantiki yake kwa sababu ya maneno matamu ya mpito. Kama kwa kweli angechukua hatua mbaya na kusema mambo mabaya, basi angekuwa mjinga wa Shetani, angekuwa akitumika kama fursa ya Shetani ya kutolea hisia na angekuwa yule mwanamke mwingine anayetia aibu; matokeo yake yangekuwa familia iliyovunjika, maumivu ya kudumu kwa mke wa Wang Wei na watoto, na yeye mwenyewe angekuwa na mawaa yasiyorekebishika mbele ya Mungu—matokeo hayangefikirika.
Alipofikia utambuzi huu, Jingru aliimarisha hisia zake, na akajibu kwa utulivu: “Usiwe mjinga. Hata kama ukitoa talaka, tutakuwa marafiki tu. Nilichukulia ulichokisema kuwa utani. Nipeleke nyumbani.” Wang Wei aliona mtazamo thabiti wa Jingru, na hakusema tena zaidi.

Hatimaye, walirudi kwenye mlango wa Jingru, na Jingru alipokuwa tu akitaka kutoka nje ya gari, Wang Wei alikwenda kuushika mkono wake tena, lakini alitoka nje kwa haraka na kurudi kwenye mlango wake. Baada ya kufika ndani, akalala kitandani mwake. Hakuweza kutuliza moyo wake kwa muda mrefu, akifikiria kilichokuwa kimejiri tu hivi punde, na alijaa hisia za aina zote: Isingekuwa kwa ulinzi wa Mungu, kwa kweli hangeweza kujizuia akiwa amekabiliwa na ungamo hilo la kweli la Wang Wei, wema na faraja, na labda angeweza kufanya kitu kibaya ambacho kilikuwa kiovu na ambacho kingeangamiza familia ya mtu mwingine. Na hata zito zaidi ni kwamba angeanguka katika majaribu ya kihisia, kuikosea tabia ya Mungu, kupoteza ushuhuda wa Mkristo, na kuachwa na kosa lisilosamehewa ambalo angelijutia maisha yake yote. Kwa kweli Jingru alianza kutambua vyema jinsi maneno ya Mungu yalivyokuwa ya muhimu kwake, kwa sababu hayakumwezesha tu kupata ulinzi wa Mungu alipokabiliwa na majaribu, lakini pia yalimwezesha kubaki mtulivu na mwenye busara katika kusema na kutenda, na kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Uzoefu huu ulimletea Jingru hisia za amani na raha, na hakuweza kujizuia kumshukuru na kumtukuza Mungu kutoka moyoni mwake: Ulikuwa ni ulinzi wa Mungu ambao ulimruhusu kuyashinda majaribu ya Shetani na kuwa shahidi kama Mkristo. Na hivyo akaenda mbele ya Mungu kusema sala ya shukrani, na kisha akalala.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni