Jumamosi, 29 Desemba 2018

Wimbo za Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation

Wimbo za Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation

Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda,
uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme.
Maneno Yako yamenitakasa,
yakanifanya nianze kuishi maisha ya furaha.
Moyoni mwangu nahisi, kwa kweli, ni upendo Wako mkuu.
Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu!
Maneno Yako yote ni ukweli.

Ijumaa, 28 Desemba 2018

Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?" (Official Video)

Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?" (Official Video)

Mwenyezi Mungu anasema, "Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake.

Alhamisi, 27 Desemba 2018

Sura ya 24 na 25



Mwenyezi Mungu alisema, Bila kusoma kwa makini, haiwezekani kugundua kitu chochote katika matamko ya siku hizi mbili; kwa kweli, yangepaswa kunenwa kwa siku moja, lakini Mungu aliyagawanya kwa siku mbili. Hiyo ni kusema, matamko ya siku hizi mbili yanaunda moja kamili, lakini ili iwe rahisi kwa watu kuyakubali, Mungu aliyagawanya kwa siku mbili ili kuwapa watu nafasi ya kupumua. Hiyo ndiyo fikira ya Mungu kwa mwanadamu. Katika kazi yote ya Mungu, watu wote hutekeleza kazi zao na wajibu wao mahali pao wenyewe.

Jumatano, 26 Desemba 2018

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (6): Jinsi Wakristo Wanavyojibu "Chambo cha Familia" cha CCP

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (6): Jinsi Wakristo Wanavyojibu "Chambo cha Familia" cha CCP

Wakati ambapo CCP hakipati mafanikio katika jitihada zake za kuwalazimisha Wakristo kumtelekeza Mungukupitia mateso yao ya ukatili na kutia kasumba, wao kisha huzitumia familia zao kama chambo kuwajaribu. Wakiwa wamekabiliwa na mbinu hizi duni, Wakristo husimamaje imara na haki, wakizikanusha? Na wao hutoa onyo gani?

Jumanne, 25 Desemba 2018

Sura ya 8

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Sura ya 8

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa Roho, sauti Yake huelekezwa kwa wanadamu wote. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa mwanadamu, sauti Yake huelekezwa kwa wote wafuatao uongozi wa Roho Wake. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu (kile ambacho watu hutaja kama mtazamaji), Anaonyesha neno Lake moja kwa moja kwa watu ili watu wamwone kama mtoa maoni,

Jumatatu, 24 Desemba 2018

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (5): Upingaji wa Ajabu wa Mkristo wa Mawazo ya Mchungaji wa Utatu

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (5): Upingaji wa Ajabu wa Mkristo wa Mawazo ya Mchungaji wa Utatu

CCP kinamkaribisha mchungaji na Kanisa la Utatu kujaribu kumtia kasumba na kumbadilisha Mkristo mmoja. Huyu Mkristo na mchungaji wanafungua mjadala mzuri katika kukabiliana na dhana zilizotolewa na mchungaji wa Utatu. Je, Mkristo huyu atampingaje huyu mchungaji? Kwa nini jaribio hili la CCP katika kutia kasumba na ubadilishaji utaishia kushindwa?

Tufuate : Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Neno la Mwenyezi mungu

Jumapili, 23 Desemba 2018

Utangulizi



“Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima” ni sehemu ya pili ya matamshi yaliyoonyeshwa na Kristo. Ndani ya sehemu hii, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya sura arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na “Matamko ya Kristo Mwanzoni.” “Matamko ya Kristo Mwanzoni” inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho. Hatimaye, inaisha kwa “majaribu ya watendaji huduma.” Hata hivyo, “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima,” inaanza na hitimisho la utambulisho wa watu kama watendaji huduma na mwanzo wa maisha yao kama watu wa Mungu. Inaongoza watu ndani ya kipeo cha pili cha kazi ya Mungu, ambapo katika mkondo wake wanapitia majaribu ya jahanamu, majaribu ya kifo, na nyakati za kumpenda Mungu. Hatua hizi kadhaa zinafichua kikamilifu ubaya wa mwanadamu mbele ya Mungu na tabia yake ya kweli. Hatimaye, Mungu anamaliza na sura ambapo Anatengana na mwanadamu, hivyo kukamilisha hatua zote za kupata mwili huku kwa ushindi wa Mungu wa kikundi cha kwanza cha watu.

Katika “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima,” Mungu anaonyesha maneno Yake kutoka kwa mtazamo wa Roho. Namna ambavyo Anazungumza haiwezi kufikiwa na wanadamu walioumbwa. Aidha, msamiati na mtindo wa maneno Yake ni mzuri na wa kusisimua, na hakuna mtindo wowote wa maandishi ya binadamu ungechukua nafasi yake. Maneno ambayo Anatumia kumfichua mwanadamu ni sahihi, ni yasiokanushika na falsafa yoyote, nayo huwafanya watu wote kutii. Kama upanga wenye ncha kali, maneno Anayotumia kumhukumu mwanadamu hukata moja kwa moja hadi kwa kina cha nafsi za watu, hata kuwaacha bila mahali pa kujificha. Maneno Anayotumia kuwafariji watu yana huruma na wema wenye upendo, ni kunjufu kama kumbatio la mama mwenye upendo, na huwafanya watu wahisi salama kuliko walivyowahi hapo awali. Sifa moja kubwa zaidi ya matamshi haya ni kwamba, wakati wa hatua hii, Mungu hazungumzi kwa kutumia utambulisho wa Yehova au Yesu Kristo, wala wa Kristo wa siku za mwisho. Badala yake, kwa kutumia utambulisho Wake wa asili—Muumba—Anazungumza kwa na kuwafunza wote wanaomfuata Yeye na ambao bado hawajamfuata Yeye. Ni haki kusema kwamba hii ilikuwa mara ya kwanza tangu uumbaji kwa Mungu kuwahutubia wanadamu wote. Mungu hakuwa amewahi kuzungumza kwa wanadamu walioumbwa kinaganaga hivyo na kwa utaratibu sana. Bila shaka, hiyo pia ilikuwa mara ya kwanza Alipozungumza mengi hivyo, na kwa muda mrefu sana, kwa wanadamu wote. Ilikuwa ya kipekee kabisa. Na zaidi, matamshi haya yalikuwa maneno halisi ya kwanza yaliyoonyeshwa na Mungu miongoni mwa wanadamu ambapo Aliwafichua watu, akawaongoza, akawahukumu, na kuzungumza nao wazi wazi na kwa hiyo, pia, yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo kwayo Mungu aliwaruhusu watu wajue nyayo Zake, mahali Anapokaa, tabia ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, mawazo ya Mungu, na sikitiko Lake kwa wanadamu. Inaweza kusemwa kwamba haya yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo Mungu alikuwa amezungumza kwa wanadamu kutoka mbingu ya tatu tangu uumbaji, na mara ya kwanza ambapo Mungu alikuwa ametumia utambulisho Wake wa asili kuonekana na kuonyesha sauti Yake kwa wanadamu katikati ya maneno.
Matamshi haya ni ya kina na magumu sana; si rahisi kuyaelewa, wala haiwezekani kufahamu asili na makusudi ya maneno ya Mungu. Hivyo, Kristo ameongeza ufafanuzi baada ya kila sura, kwa kutumia lugha iliyo rahisi kwa mwanadamu kufahamu kuleta uwazi kwa sehemu kubwa zaidi ya matamshi hayo. Hili, likiunganishwa na matamshi yenyewe, linayafanya kuwa rahisi sana kwa kila mtu kuyaelewa na kuyajua maneno ya Mungu. Tumeyafanya maneno haya kiambatisho kwa “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima.” Ndani yake, Kristo anatoa ufafanuzi kwa kutumia maneno yaliyo rahisi sana kuelewa. Uunganishaji wa hayo mawili ni uoanishaji kamili wa uungu na Mungu katika ubinadamu. Ingawa Mungu anazungumza katika mtazamo wa nafsi ya tatu katika kiambatisho, hakuna anayeweza kukana kwamba maneno haya yalitamkwa na Mungu binafsi, kwani hakuna binadamu anayeweza kuyafafanua maneno ya Mungu kwa dhahiri; ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kufafanua asili na makusudi ya matamshi Yake. Hivyo, ingawa Mungu huzungumza kwa kutumia njia nyingi, makusudi ya kazi Yake hayabadiliki kamwe, wala lengo la mpango Wake haligeuki kamwe.
Ingawa “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima” inamalizika kwa sura ambayo ndani yake Mungu anatengana na mwanadamu, kwa kweli, huu ndio wakati ambapo kazi ya Mungu ya ushindi na wokovu miongoni mwa mwanadamu, na kazi Yake ya kuwafanya watu wakamilifu, ilionyeshwa kwa mara ya kwanza rasmi. Hivyo, inafaa zaidi kwetu kuchukulia “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima” kama unabii wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Kwani ni baada ya wakati huu tu ndipo Mwana wa Adamu aliyepata mwili alianza rasmi kufanya kazi na kuzungumza kwa kutumia utambulisho wa Kristo, akitembea miongoni mwa makanisa na kutoa uzima, na kunyunyizia na kuwachunga watu Wake wote—ambako kulisababisha matamshi mengi katika “Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani.”

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?