Jibu:
Imani yenu katika Bwana Yesu kama kupata mwili kwa Mungu si uwongo. Lakini mbona mnamwamini Bwana Yesu? Je, kweli mnamfikiria Bwana Yesu kuwa ni Mungu? Mnamwamini Bwana Yesu kwa sababu ya kile kilichorekodiwa katika Biblia na kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini haijalishi mnachosema, ikiwa hamjamwona Bwana Yesu uso kwa uso, je, mwaweza kuthubutu kusema kwamba mnamjua Bwana Yesu? Katika imani yenu kwa Bwana, mnarudia tu maneno ya Petro, aliyesema kwamba Bwana Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu aishiye, lakini je, mnaamini kwamba Bwana Yesu ni dhihirisho la Mungu,
ni Mungu Mwenyewe? Mnathubutu kusema kwamba mnatambua kiini kitakatifu cha Bwana Yesu? Mnathubutu kuahidi kwamba kama Bwana Yesu angekuja tena akionyesha ukweli, mngetambua sauti Yake? Imani yenu kwa Bwana Yesu si chochote ila imani katika maneno haya mawili “Bwana Yesu.” Mnaamini katika jina Lake pekee. Hamwelewi kiini kitakatifu cha Bwana Yesu. Ikiwa mnaelewa, basi mbona hamwezi kubainisha sauti ya Roho wa Mungu? Mbona msikubali kwamba ukweli ambao Mwenyezi Mungu anaonyesha unatoka kwa Mungu na ni sauti na neno la Roho Mtakatifu? Kutokana na kile ambacho nimeona leo, jinsi mnavyoikataa sauti ya Mungu na kukana ukweli ambao Mungu anaonyesha, nina hakika kwamba hammjui Mungu aliyepata mwili! Kama mngezaliwa miaka elfu mbili iliyopita, katika enzi ambamo Bwana Yesu alikuwa akihubiri na kufanya kazi Yake, bila shaka mngejiunga na makuhani wakuu, waandishi, Mafarisayo wa Kiyahudi kumshutumu Bwana Yesu. Je, hii si kweli? Makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo walikuwa wamemwamini Mungu mmoja na wa pekee kwa miaka mingi, lakini ni kwa nini hawakumtambua Bwana Yesu? Kwa nini walimpigilia misumari msalabani? Tatizo lilikuwa gani? Ni kwa nini wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini katika siku za mwisho wanakosa kusikia sauti ya Roho Mtakatifu? Kwa nini bado wanashutumu kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho? Hebu niwaulize nyote: Je, si mtu anayemwamini Mungu lakini akakataa kukubali kupata mwili kwa Mungu ni mpinga Kristo? Viongozi wa Kiyahudi walimpinga na kumshutumu Bwana Yesu, Mungu mwenye mwili. Wote walikuwa wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu. Kuhusu wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini katika siku za mwisho ambao wanapinga na kushutumu Mwenyezi Mungu aliyepata mwili, wao si wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu? Sote twaweza kuona waziwazi kwamba wengi wa wachungaji na wazee wa kanisa katika ulimwengu wa dini wote wanapinga na kushutumu kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho; wanaiangalia kazi ya Mwenyezi Mungu bila kuona kweli, wanayasikia maneno Yake bila kuyasikiliza kweli. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli wote kutakasa na kuwaokoa wanadamu. Ameshinda, Ameokoa, na Amekifanya kikundi cha washindi. Injili ya ufalme inaenea kotekote ulimwenguni, hili ni lisilobadilika wala kuzuilika Je, wachungaji na viongozi wa ulimwengu wa dini haikuwezekana wao kuona ukweli wa kazi ya Mungu? Wanawezaje kuendelea kusema jambo la dhihaka kama, “Kumwamini Mwenyezi Mungu ni kumwamini mwanadamu”? Tatizo ni lipi hapa? Hili linaonyesha tu kwamba kuna wengi wanaomwamini Mungu asiye yakini wa mbingu za juu, lakini kuna wachache ambao wana ufahamu wa Mungu aliyepata mwili. Je, sivyo? Ni kwa nini Bwana Yesu aliwashutumu wale Mafarisayo waliompinga? Kwa sababu waliamini tu katika Mungu asiye yakini wa mbingu za juu, lakini walimshutumu na kumpinga Mungu aliyepata mwili.
ni Mungu Mwenyewe? Mnathubutu kusema kwamba mnatambua kiini kitakatifu cha Bwana Yesu? Mnathubutu kuahidi kwamba kama Bwana Yesu angekuja tena akionyesha ukweli, mngetambua sauti Yake? Imani yenu kwa Bwana Yesu si chochote ila imani katika maneno haya mawili “Bwana Yesu.” Mnaamini katika jina Lake pekee. Hamwelewi kiini kitakatifu cha Bwana Yesu. Ikiwa mnaelewa, basi mbona hamwezi kubainisha sauti ya Roho wa Mungu? Mbona msikubali kwamba ukweli ambao Mwenyezi Mungu anaonyesha unatoka kwa Mungu na ni sauti na neno la Roho Mtakatifu? Kutokana na kile ambacho nimeona leo, jinsi mnavyoikataa sauti ya Mungu na kukana ukweli ambao Mungu anaonyesha, nina hakika kwamba hammjui Mungu aliyepata mwili! Kama mngezaliwa miaka elfu mbili iliyopita, katika enzi ambamo Bwana Yesu alikuwa akihubiri na kufanya kazi Yake, bila shaka mngejiunga na makuhani wakuu, waandishi, Mafarisayo wa Kiyahudi kumshutumu Bwana Yesu. Je, hii si kweli? Makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo walikuwa wamemwamini Mungu mmoja na wa pekee kwa miaka mingi, lakini ni kwa nini hawakumtambua Bwana Yesu? Kwa nini walimpigilia misumari msalabani? Tatizo lilikuwa gani? Ni kwa nini wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini katika siku za mwisho wanakosa kusikia sauti ya Roho Mtakatifu? Kwa nini bado wanashutumu kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho? Hebu niwaulize nyote: Je, si mtu anayemwamini Mungu lakini akakataa kukubali kupata mwili kwa Mungu ni mpinga Kristo? Viongozi wa Kiyahudi walimpinga na kumshutumu Bwana Yesu, Mungu mwenye mwili. Wote walikuwa wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu. Kuhusu wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini katika siku za mwisho ambao wanapinga na kushutumu Mwenyezi Mungu aliyepata mwili, wao si wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu? Sote twaweza kuona waziwazi kwamba wengi wa wachungaji na wazee wa kanisa katika ulimwengu wa dini wote wanapinga na kushutumu kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho; wanaiangalia kazi ya Mwenyezi Mungu bila kuona kweli, wanayasikia maneno Yake bila kuyasikiliza kweli. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli wote kutakasa na kuwaokoa wanadamu. Ameshinda, Ameokoa, na Amekifanya kikundi cha washindi. Injili ya ufalme inaenea kotekote ulimwenguni, hili ni lisilobadilika wala kuzuilika Je, wachungaji na viongozi wa ulimwengu wa dini haikuwezekana wao kuona ukweli wa kazi ya Mungu? Wanawezaje kuendelea kusema jambo la dhihaka kama, “Kumwamini Mwenyezi Mungu ni kumwamini mwanadamu”? Tatizo ni lipi hapa? Hili linaonyesha tu kwamba kuna wengi wanaomwamini Mungu asiye yakini wa mbingu za juu, lakini kuna wachache ambao wana ufahamu wa Mungu aliyepata mwili. Je, sivyo? Ni kwa nini Bwana Yesu aliwashutumu wale Mafarisayo waliompinga? Kwa sababu waliamini tu katika Mungu asiye yakini wa mbingu za juu, lakini walimshutumu na kumpinga Mungu aliyepata mwili.
Makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo waliona waziwazi mamlaka na nguvu za maneno na kazi ya Bwana Yesu. Kwa hiyo kwa nini bado waliweza kupinga, kushutumu, na kumkufuru Bwana Yesu bila haya? Walisema kwamba aliwafukuza pepo kwa njia ya Belzebubu, mkuu wa pepo, na alinuia kumdanganya mwanadamu, na hata wakampigilia misumari msalabani akiwa hai, hili linaonyesha nini? Je, haikuwa kwa sababu walimwona Bwana Yesu kuwa mwanadamu wa kawaida ndipo walifanya haya yote? Kama walivyosema tu, “Je, huyo si Mnazareti, mwana wa seremala?” Katika dhana ya Mafarisayo, mwili wa Mungu mwenye mwili unapaswa kuwa na sifa za ajabu. Anapaswa kuwa na kimo kikubwa na umbo la nguvu, na mwenendo wa kishujaa na uwepo mkuu. Maneno Yake yanapaswa kuwa na mlio wa ajabu na mkubwa, yanatakiwa kuweka woga ndani ya mioyo ya wanadamu, ili mtu yeyote asithubutu kumkaribia. La sivyo, Hangeweza kufikiriwa kuwa Mungu. Kwa kweli, hawakuwa na ufahamu hata kidogo wa kinachomaanishwa na kupata mwili na hawakutafuta ukweli katika neno na kazi ya Bwana Yesu, kupata tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu alicho na Anacho. Walimchukulia Bwana Yesu kuwa mwanadamu wa kawaida, wakimhukumu na kumkufuru kwa kutegemea njozi na dhana zao. Hili linathibitisha kwamba wakati walimwamini Mungu, hawakumjua na hata walimpinga. Sasa, wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini wanasema kwamba Yule tunayemwamini ni mwanadamu tu. Hii si tofauti na jinsi makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo waliwashutumu wafuasi wa Bwana Yesu. Kama mwonavyo, wengi wa wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini si tofauti na Mafarisayo wanafiki wa zamani, wote wanamwamini Mungu huku wakimpinga wakati huo huo. Wao ni waovu wanaomkubali tu Mungu asiye yakini wa mbingu za juu huku wakimkana Kristo Mwenyewe! Wana haki gani kuwashutumu wale wanaomkubali na kumtii Kristo?
kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Kuhusu swali la ni nini kupata mwili, na ni nini kiini cha Mungu mwenye mwili, mngesema, hii ni siri ya ukweli ambao hakuna muumini anayeelewa. Ingawa waumini kwa maelfu ya miaka wamejua kwamba Bwana Yesu ni kupata mwili kwa Mungu, hakuna anayeelewa kupata mwili na kiini halisi cha kupata mwili. Ni sasa tu ambapo Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho amekuja, ndipo kipengele hiki cha siri ya ukweli kimefichuliwa kwa mwanadamu. Hebu tusome vifungu vichache vya neno la Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu asema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu” (“Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe” (“Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Kristo mwenye ubinadamu wa kawaida ni mwili ambao kwao Roho Hupatikana, Akiwa na ubinadamu wa kawaida, ufahamu wa kawaida, na fikira za wanadamu. ‘Kupatikana’ kunamaanisha Mungu kuwa mwanadamu, Roho kuwa mwili; kuiweka wazi, ni wakati ambapo Mungu Mwenyewe Anaishi katika mwili wenye ubinadamu wa kawaida, na kupitia kwenye huo mwili, Anaonyesha kazi yake ya uungu—hii ndiyo maana ya kupatikana, au kupata mwili” (“Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Kwa sababu ni mwanadamu mwenye kiini cha Mungu, Yuko juu ya wanadamu wote walioumbwa, juu ya mwanadamu yeyote anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu. Kwa hivyo, miongoni mwa wale wote walio na umbo la binadamu kama Lake, miongoni mwa wale wote walio na ubinadamu, Yeye pekee ndiye Mungu mwenye mwili Mwenyewe—wengine wote ni wanadamu walioumbwa. Japokuwa wote wana ubinadamu, wanadamu walioumbwa si chochote zaidi ya wanadamu, ilhali Mungu mwenye mwili ni tofauti: katika mwili Wake, si tu kwamba ana ubinadamu ila pia muhimu zaidi Ana uungu. Ubinadamu Wake waweza kuonekana katika mwonekano wa nje wa Mwili Wake na katika maisha Yake ya kila siku; ila uungu Wake ni vigumu kuonekana. Kwa kuwa uungu Wake huonyeshwa pale tu Anapokuwa na ubinadamu, na si wa kimuujiza kama watu wanavyoukisia kuwa, ni vigumu sana kwa watu kuuona. … Kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, kiini Chake ni muungano wa ubinadamu na uungu. Muungano huu unaitwa Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe duniani” (“Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu tunaweza kuona kwamba kupata mwili ni Roho wa Mungu aliyevaa mwili, yaani, Roho wa Mungu anatokea katika mwili akiwa na ubinadamu wa kawaida na fikira za mwanadamu za kawaida, na hivyo anakuwa mtu wa kawaida Akifanya kazi na kuzungumza miongoni mwa wanadamu. Mwili huu una ubinadamu wa kawaida, lakini pia una uungu kamili. Ingawa kwa sura ya nje mwili Wake unaonekana ni wa kawaida, Anaweza kuifanya kazi ya Mungu, Anaweza kuonyesha sauti ya Mungu, kuwaongoza na kuwaokoa wanadamu. Hili ni kwa sababu ana uungu kamili. Uungu kamili unamaanisha kwamba chote ambacho Roho wa Mungu anamiliki—tabia ya asili ya Mungu, Kiini cha Mungu takatifu na cha haki, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu za Mungu—haya yote yametokea katika mwili. Mwili huu ni Kristo, ni Mungu wa vitendo ambaye Yuko hapa duniani kufanya kazi na kuwaokoa wanadamu. Kutokana na sura Yake ya nje, Kristo ni Mwana wa Adamu wa kawaida, lakini Yeye ni tofauti na mwanadamu yeyote aliyeumbwa kwa kweli. Mwanadamu aliyeumbwa ana ubinadamu pekee, hana hata dalili yoyote ya kiini cha uungu. Kristo, hata hivyo, hana ubinadamu wa kawaida pekee; la muhimu zaidi, Ana uungu kamili. Kwa hiyo, Ana kiini cha Mungu, Anaweza kumwakilisha Mungu kabisa, kuonyesha ukweli wote kama Mungu Mwenyewe, kuonyesha tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho, na kumjalia mwanadamu na ukweli, njia, na uzima. Hakuna mwanadamu aliyeumbwa anaweza kufanya matendo magumu kama hayo. Kristo anafanya kazi na kunena, Anaonyesha tabia ya Mungu, na chote ambacho Mungu anacho na Alicho katika mwili Wake. Haijalishi vile Anavyoonyesha neno la Mungu na kufanya kazi ya Mungu, Yeye hufanya hivyo daima katika ubinadamu wa kawaida. Ana mwili wa kawaida, hakuna chochote cha ajabu kumhusu. Hili linathibitisha kwamba Mungu amekuja katika mwili, Amekuwa mwanadamu wa kawaida tayari. Mwili huu wa kawaida umetimiza ukweli wa “Neno Laonekana katika Mwili.” Yeye ni Mungu mwenye mwili wa vitendo. Kwa kuwa Kristo ana uungu kamili, Anaweza kumwakilisha Mungu, kuonyesha ukweli, na kuwaokoa wanadamu. Kwa kuwa Kristo ana uungu kamili, Anaweza kuonyesha neno la Mungu moja kwa moja, sio tu kupeleka au kupitisha neno la Mungu. Anaweza kuonyesha ukweli wakati wowote na mahali popote, Akiruzuku, Akinyunyizia, na kumchunga mwanadamu, Akiwaongoza wanadamu wote. Ni kwa sababu tu Kristo ana uungu kamili, na Anamiliki utambulisho na kiini cha Mungu, ndio tunaweza kusema kwamba Yeye ni kupata mwili kwa Mungu, Mungu Mwenyewe wa vitendo.
Siri kubwa zaidi ya kupata mwili haina uhusiano na kama mwili wa Mungu ni mkubwa kwa kimo au kama ule wa mwanadamu wa kawaida. Badala yake inahusu ukweli kwamba uungu kamili umejificha ndani ya mwili huu wa kawaida. Hakuna mwanadamu anayeweza kugundua au kuuona uungu huu. Kama tu wakati ambapo Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, kama mtu yeyote hangekuwa amesikia sauti Yake na kupitia neno na kazi Yake, basi hakuna ambaye angetambua kwamba Bwana Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu. Kwa hiyo kupata mwili kwa Mungu ndiyo njia bora zaidi ya Yeye kushuka kisirisiri miongoni mwa wanadamu. Wakati Bwana Yesu alikuja, hakuna mtu angeweza kujua kutokana na sura Yake ya nje kwamba Alikuwa Kristo, Mungu mwenye mwili, na hakuna mtu angeweza kuona uungu uliofichwa ndani ya ubinadamu Wake. Ni baada tu ya Bwana Yesu kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya ukombozi wa wanadamu, ndipo mwanadamu aligundua kwamba neno Lake lina mamlaka na nguvu, na wakati huo tu ndipo wanadamu walianza kumfuata. Ni wakati ambao Bwana Yesu alionekana kwa watu baada ya kufufuka tu, ndipo walitambua kwamba Yeye ni Kristo mwenye mwili, kuonekana kwa Mungu. Kama hangekuwa ameonyesha ukweli na kufanya kazi Yake, hakuna mtu angemfuata. Kama hangeshuhudia ukweli kwamba Yeye ni Kristo, kuonekana kwa Mungu, hakuna mtu angemtambua. Kwa kuwa mwanadamu anaamini kwamba kama Yeye ni Mungu mwenye mwili kweli, mwili Wake unapaswa kuwa na sifa za miujiza, Anapaswa kupita uwezo wa binadamu, Awe mwenye kimo kipana, cha nguvu, na umbo refu, Hapaswi kuzungumza na mamlaka na nguvu tu, bali Anapaswa pia kufanya ishara na miujiza popote Aendapo—hivi ndivyo Mungu aliyepata mwili Anapaswa kufanana. Kama Yeye ni wa kawaida katika sura ya nje, kama mwanadamu mwingine yeyote wa kawaida, na ana ubinadamu wa kawaida, basi Yeye bila shaka si kupata mwili kwa Mungu. Hebu tukumbuke tena, wakati Bwana Yesu alipata mwili kunena na kufanya kazi, haijalishi vile Alivyoonyesha ukweli na sauti ya Mungu, hakuna aliyemtambua. Makuhani wakuu, waandishi, Mafarisayo wa Kiyahudi sana hawakumtambua. Wakati walimsikia mtu fulani akitoa ushuhuda kwa Bwana Yesu hata walisema: Huyu si mwana wa Yusufu? Je, huyu si Mnazareti? Kwa nini makuhani wakuu, waandishi, Mafarisayo wazungumze hivi kumhusu? Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa na ubinadamu wa kawaida katika sura ya nje. Alikuwa mtu wastani, wa kawaida, na Hakuwa na umbo refu, kwa hiyo hakuna aliyemkubali. Kwa kweli, hata ingawa Yeye ni Aliyepata mwili, Anapaswa kuwa na ubinadamu wa kawaida kwa hakika, Anapaswa kuwaonyesha watu kwamba mwili ambao Mungu anajivika ni mwili wa kawaida, Anaonekana kama mwanadamu wa kawaida. Kama Mungu angejivika mwili wa anayepita uwezo wa binadamu, usio wa mtu aliye na ubinadamu wa kawaida, basi maana yote ya kupata mwili ingepotea. Kwa hiyo, lazima Kristo awe na ubinadamu wa kawaida. Ni kwa njia hii pekee ndio inaweza kuthibitishwa kwamba Yeye ni Neno aliyepata mwili.
Hebu tusome kifungu kingine cha neno la Mwenyezi Mungu: “Umuhimu wa kupata mwili ni kwamba mtu wa kawaida Anatekeleza kazi ya Mungu Mwenyewe; yaani, kwamba Mungu Anatekeleza kazi Yake ya uungu katika ubinadamu na hivyo kumshinda Shetani. … Ikiwa, wakati wa kuja Kwake wa kwanza, Mungu Asingekuwa Amekuwa na ubinadamu wa kawaida kabla ya umri wa miaka ishirini na tisa—ikiwa mara tu Alipozaliwa Angeweza kufanya miujiza, ikiwa mara tu Alipojifunza kuongea Angeweza kuongea lugha ya mbinguni, ikiwa mara tu Alipokanyaga duniani Angeweza kuyaelewa mambo yote ya kidunia, kung’amua fikira za kila mtu na nia zao—mtu kama huyu asingeitwa mwanadamu wa kawaida, na mwili Wake usingeitwa mwili wa mwanadamu. Iwapo mambo yangekuwa hivi kwa Kristo, basi maana na kiini cha kuwa mwili kwa Mungu ingepotea. Kuwa Kwake na ubinadamu wa kawaida kunathibitisha kuwa Alikuwa Mungu Aliyejidhihirisha katika mwili; ukweli kwamba Alipitia ukuaji wa kawaida wa binadamu unaonyesha zaidi kuwa Alikuwa mwili wa kawaida; na zaidi, kazi Yake ni uthibitisho tosha kuwa Alikuwa Neno la Mungu, Roho wa Mungu, kuwa mwili. Mungu Anakuwa mwili kwa sababu ya mahitaji ya kazi; kwa maneno mengine, hii hatua ya kazi inapaswa kufanywa kwa mwili, kufanywa katika ubinadamu wa kawaida. Hili ndilo sharti la ‘Neno kuwa mwili,’ la ‘Neno kuonekana katika mwili,’ na ndio ukweli wa Mungu kupata mwili mara Mbili” (“Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Iwapo Mungu mwenye mwili Angeanza huduma Yake kwa dhati tangu kuzaliwa kwake, na kufanya ishara na maajabu ya mwujiza, basi Asingekuwa na kiini cha kimwili. Kwa hivyo, ubinadamu Wake upo kwa sababu ya kiini chake cha Kimwili; hakuwezi kuwepo na mwili bila ubinadamu, na mtu bila ubinadamu si mwanadamu. Kwa njia hii, ubinadamu wa mwili wa Mungu ni sifa ya ndani ya mwili wa Mungu. Kusema kwamba ‘Mungu Anapokuwa mwili Anakuwa na uungu kamili, kwa vyovyote vile si ubinadamu,’ ni kufuru, kwa sababu huu ni msimamo usioweza kuchukuliwa, msimamo unaokinzana na kanuni ya Yesu kuupata mwili. …
“… Ubinadamu wa Mungu kuwa mwili huwepo kudumisha kazi ya kawaida ya uungu katika mwili; fikira Zake za kawaida za binadamu zinadumisha ubinadamu Wake wa kawaida na shughuli Zake zote za kimwili. Mtu anaweza kusema kuwa fikira zake za kawaida za binadamu zipo ili kudumisha kazi yote ya Mungu katika mwili. Kama mwili huu usingekuwa na akili ya mwanadamu wa kawaida, basi Mungu Asingefanya kazi katika mwili, na Anachopaswa kufanya kimwili kisingetimilika. … Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili ni lazima Awe na akili za binadamu, ni lazima Awe na ubinadamu wa kawaida, kwa sababu ni lazima Atekeleze kazi Yake katika ubinadamu akiwa na akili za kawaida. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Mungu mwenye Mwili, kiini chenyewe cha Mungu mwenye mwili” (“Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu tunaona waziwazi kwamba Mungu mwenye mwili lazima awe na ubinadamu wa kawaida, la sivyo, Hangekuwa kupata mwili kwa Mungu. Katika umbo la nje, Anafanana na mtu wa kawaida, na hakuna chochote cha miujiza kuhusu ubinadamu Wake. Kwa hiyo, tukimpima Kristo tukitumia dhana na mawazo yetu, hatutawahi kumkiri au kumkubali Kristo. Kwa kiwango kikubwa zaidi tutakiri tu kwamba Yeye ni nabii Aliyetumwa na Mungu, au yule ambaye Mungu hutumia. Ikiwa tunataka kumjua Kristo kweli, lazima tuchunguze maneno yake na kazi kuona kama kile ambacho Anaonyesha ni sauti ya Mungu Mwenyewe, ikiwa maneno Anayoonyesha ni madhihirisho ya tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho, na kuona kama kazi Yake na ukweli Anaoonyesha unaweza kuwaokoa wanadamu. Wakati huo tu ndipo tunaweza kumjua, kumkubali na kumtii Kristo. Ikiwa hatutafuti ukweli, hatuchunguzi kazi ya Mungu, hata tukiyasikia maneno ya Mungu na kuiona kazi ya Kristo, bado hatutamjua Kristo. Hata kama tuko na Kristo tangu asubuhi mpaka usiku, bado tutamchukulia kama mwanadamu wa kawaida na hivyo tutampinga na kumshutumu Kristo. Kwa kweli, ili kumkiri na kumkubali Kristo, yote tunayohitaji kufanya ni kuitambua sauti ya Mungu na kukiri kwamba Anafanya kazi ya Mungu. Lakini kujua kiini cha uungu wa Kristo na hivyo kutimiza utiifu wa kweli kwa Kristo na kumpenda Mungu wa vitendo, lazima tugundue ukweli ndani ya maneno na kazi ya Kristo, tuone tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho, tuone kiini kitakatifu, uweza, na hekima ya Mungu, tuone kwamba Mungu ni mwenye upendo na tukubali makusudi Yake yenye ari. Ni kwa namna hii tu ndio mtu anaweza kumtii Kristo kweli na kumwabudu Mungu wa vitendo katika moyo wake.
Sisi waumini sote tunajua kwamba namna ambayo Bwana Yesu alihubiri, neno Aliloonyesha, siri za ufalme wa mbinguni ambazo Alifichua, na matakwa Aliyotoa kwa mwanadamu yote yalikuwa ukweli, yote yalikuwa sauti ya Mungu Mwenyewe, na yote yalikuwa madhihirisho ya tabia ya maisha ya Mungu na chote ambacho Anacho na Alicho. Miujiza aliyofanya—kuwaponya wagonjwa, kutoa pepo, kutuliza upepo na bahari, kuwalisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili, na kuwafufua wafu—yote yalikuwa madhihirisho ya mamlaka na nguvu za Mungu Mwenyewe, ambavyo hakuna mwanadamu aliyeumbwa aliye navyo au anayeweza kuwa navyo. Wale walioutafuta ukweli wakati huo, kama vile Petro, Yohana, Mathayo, na Nathanieli, walitambua kutoka kwa neno na kazi ya Bwana Yesu kwamba Yeye ni Masihi aliyeahidiwa, na hivyo wakamfuata na wakapokea wokovu Wake. Ilhali Mafarisayo wa Kiyahudi, licha ya kusikia mahubiri ya Bwana Yesu na kumwona Akifanya miujiza, bado walimwona kama mtu wa kawaida tu, Asiye na nguvu au kimo, Kwa hiyo walithubutu kumpinga na kumshutumu vikali bila woga hata kidogo. Mwishowe walitenda dhambi kubwa zaidi kwa kumpigilia misumari Bwana Yesu juu ya msalaba. Somo la Mafarisayo linahitaji tafakari ya kina! Hili linafichua waziwazi asili yao ya mpinga Kristo ya kuchukia ukweli na kumchukia Mungu, na inafichua upumbavu na ujinga wa wanadamu wapotovu. Wakati huu, Mwenyezi Mungu aliyepata mwili, kama tu Bwana Yesu, Anafanya kazi ya Mungu Mwenyewe ndani ya ubinadamu wa kawaida. Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote ambao wanadamu wapotovu wanahitaji ili kuokolewa, na Anatekeleza kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Yeye hahukumu na kufichua tu asili ya kishetani ya wanadamu wapotovu na ukweli wa upotovu wao, Amefichua pia siri zote za mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita wa kuwaokoa wanadamu, Amefafanua njia ambayo wanadamu wanaweza kuwekwa huru kutoka kwa dhambi, watakaswe na kuokolewa na Mungu, Amefichua tabia yenye haki ya asili ya Mungu, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, na nguvu na mamlaka ya Mungu ya pekee…. neno na kazi ya Mwenyezi Mungu ni dhihirisho kamili la utambulisho na kiini cha Mungu Mwenyewe. Siku hizi, wale wote wanaomfuata Mwenyezi Mungu wamesikia sauti ya Mungu katika neno na kazi ya Mwenyezi Mungu, wameona dhihirisho la neno la Mungu katika mwili na wamekuja mbele za kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, wakipokea utakaso na kukamilishwa kwa Mungu. Wale wa ulimwengu wa kidini ambao bado wanakana, wanapinga, na kushutumu Mwenyezi Mungu wamefanya kosa lile lile kama la Mafarisayo wa Kiyahudi, wakimtendea Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, kama mtu mwingine yeyote wa kawaida, bila kujali kutumia jitihada hata kidogo kutafuta na kuchunguza ukweli wote ambao Mwenyezi Mungu ameonyesha, hivyo wanampigilia Mungu misumari msalabani tena na kukasirisha tabia ya Mungu. Kama awezavyo kuona mtu, ikiwa mwanadamu anashikilia dhana na fikira zake, na hatafuti na kuchunguza ukweli ambao Kristo anaonyesha, hataweza kutambua sauti ya Mungu inayoonyeshwa na Kristo, hataweza kukubali na kutii kazi ya Kristo, na hatawahi kupokea wokovu wa Mungu katika siku za mwisho. Ikiwa mwanadamu haelewi ukweli wa kupata mwili, hataweza kukubali na kutii kazi ya Mungu, Atamshutumu Kristo na kumpinga Mungu, na kuna uwezekano pia wa yeye kupokea adhabu na laana za Mungu. Kwa hiyo, katika imani yetu, ili kuokolewa na Mungu, ni muhimu kabisa tutafute ukweli na kuelewa siri ya kupata mwili!
kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni