Jumanne, 23 Julai 2019

4. Hakuna njia ya uzima wa milele ndani ya Biblia; mwanadamu akiishika Biblia na kuiabudu, basi hatapata uzima wa milele

XI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Uhusiano kati ya Mungu na Biblia

4. Hakuna njia ya uzima wa milele ndani ya Biblia; mwanadamu akiishika Biblia na kuiabudu, basi hatapata uzima wa milele


Aya za Biblia za Kurejelea:

  “Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai” (Yohana 5:39-40).

  “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6).

Maneno Husika ya Mungu:

   Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

  kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

   Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!

  kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

  Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria? Kuleta mambo ya zamani leo kunayafanya yawe historia, haijalishi yana ukweli kiasi gani, bado ni historia—na historia haiwezi kushughulikia masuala ya leo. Maana Mungu haangalii historia! Na hivyo, kama unaelewa tu Biblia, na huelewi chochote kuhusu kazi ambayo Mungu anakusudia kufanya leo, na kama unamwamini Mungu, na hutafuti kazi ya Roho Mtakatifu, basi hujui inamaanisha nini kumtafuta Mungu. Ikiwa unasoma Biblia kwa lengo la kujifunza historia ya Israeli, kutafiti historia ya uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia, basi humwamini Mungu. Lakini leo, kwa kuwa unamwamini Mungu, na kutafuta uzima, kwa kuwa unatafuta maarifa juu ya Mungu, na hutafuti nyaraka na mafundisho mfu, au ufahamu wa historia, unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu ya leo, na unapaswa kutafuta uongozi wa kazi ya Roho Mtakatifu. Kama ungekuwa mwanaakiolojia ungeweza kusoma Biblia—lakini wewe sio mwanaakiolojia, wewe ni mmoja wa wale wanaomwamini Mungu, na utakuwa bora zaidi ukitafuta mapenzi ya Mungu ya leo.
  
  kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

  Ingawa Biblia inaleta pamoja baadhi ya vitabu vya maneno ya uzima, kama vile nyaraka za Paulo na nyaraka za Petro, na ingawa watu wanaweza kusaidiwa na vitabu hivi, vitabu hivi bado vimepitwa na wakati, bado ni vitabu vya enzi ya kale, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, vinafaa tu kwa ajili ya kipindi kimoja, na wala sio vya milele. Maana kazi ya Mungu siku zote inaendelea, na haiwezi kusimama tu katika kipindi cha Paulo na Petro, au siku zote ibaki katika Enzi ya Neema, enzi ambayo Yesu alisulubiwa. Na hivyo, vitabu hivi vinafaa tu katika Enzi ya Neema, na wala sio kwa ajili ya Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho. Vinaweza tu kuwa na manufaa kwa waumini wa Enzi ya Neema, na sio kwa watakatifu wa Enzi ya Ufalme, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, bado havifai kwa kipindi hiki. Ni sawa na kazi ya Yehova ya uumbaji au kazi Yake katika Israeli: Haijalishi kazi hii ilikuwa kubwa kiasi gani, bado imepitwa na wakati, na muda utaendelea kuja wakati umekwishapita. Kazi ya Mungu pia ni ile ile: Ni nzuri, lakini muda utafika ambapo itakoma; siku zote haitaendelea kubaki katikati ya kazi ya uumbaji, wala katikati ya kazi ile ya msalaba. Haijalishi kazi ya msalaba inashawishi kiasi gani, haijalishi ilikuwa ya ufanisi kiasi gani katika kumshinda Shetani, hata hivyo, kazi bado ni kazi, na enzi, hata hivyo bado ni enzi; kazi siku zote haiwezi kubaki katika msingi ule ule, wala nyakati haziwezi kukosa kubadilika, kwa sababu kulikuwa na uumbaji na lazima kuwepo na siku za mwisho. Hii haiepukiki! Hivyo, leo maneno ya uzima katika Agano Jipya—nyaraka za mitume, na Injili Nne—vimekuwa vitabu vya kihistoria, vimekuwa vitabu vya kale, na inawezekanaje vitabu vya kale kuwapeleka watu katika enzi mpya? Haijalishi ni kiasi gani vitabu hivi vinaweza kuwapatia watu uzima, haijalishi vina uwezo kiasi gani katika kuwaongoza watu kwenye msalaba, ndio kwamba havijapitwa na wakati? Havijaondokewa na thamani? Hivyo, Ninasema hupaswi kuviamini vitabu hivi bila kufikiri. Ni vya zamani sana, haviwezi kukupeleka katika kazi mpya, vinaweza kukulemea tu. Sio tu haviwezi kukuleta katika kazi mpya, na katika kuingia kupya, bali vinakupeleka katika makanisa ya dini ya kale na kama ni hivyo, havirudishi nyuma imani yako kwa Mungu?

  kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

  Ukipata maarifa kiasi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari dhidi Yake, hili silo tendo lisilohitajika? Unachopaswa kufanya ni kukubali, bila haja ya kuthibitisha zaidi kutoka kwa Biblia, kazi yoyote iwapo tu ni ya Roho Mtakatifu, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu.

  kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

  “Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho.” Mmeyasikia sasa maneno ya Roho Mtakatifu? Maneno ya Mungu yamekuja juu yenu. Mnayasikia? Mungu anafanya kazi ya neno katika siku za mwisho, na maneno haya ni yale ya Roho Mtakatifu, kwani Mungu ni Roho Mtakatifu na Anaweza pia kuwa mwili; kwa hivyo, maneno ya Roho Mtakatifu, yalivyosemwa zamani, ni maneno ya Mungu mwenye mwili wa leo. Kuna wanadamu wajinga wanaoamini kwamba maneno ya Roho Mtakatifu yanapaswa kuja chini kutoka mbinguni hadi kwa masikio ya mwanadamu. Yeyote anayefikiria hivi hajui kazi ya Mungu. Kwa kweli, matamshi yaliyosemwa na Roho Mtakatifu ni yale yaliyosemwa na Mungu aliyekuwa mwili. Roho Mtakatifu hawezi kuongea moja kwa moja na mwanadamu, na Yehova hakuongea moja kwa moja na watu, hata kwa Enzi ya Sheria. Si ungekuwa uwezekano wa chini zaidi kwamba Angefanya hivyo kwa enzi ya leo? Kwa Mungu kunena matamshi ili kutekeleza kazi, lazima Awe mwili, la sivyo kazi yake haiwezi kukamilisha malengo Yake. Wanaomkataa Mungu ni wale wasiojua Roho ama kanuni ambazo Mungu hufanya kazi. Wanaoamini kwamba sasa ni enzi ya Roho Mtakatifu lakini bado hawakubali kazi Yake mpya ni wale wanaoishi kwa imani isiyo dhahiri. Wanadamu kama hawa hawatapokea kamwe kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wanaotaka tu Roho Mtakatifu azungumze moja kwa moja na kutekeleza kazi Yake, lakini bado hawakubali maneno ama kazi ya Mungu mwenye mwili, kamwe hawataweza kuchukua hatua katika enzi mpya ama kupokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu!

  kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

  Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

  kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Kipande cha gogo lililokufa: Nahau ya Kichina yenye maana “siyoweza kusaidiwa.”


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni