XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu
5. Matokeo ya mtu anayemwamini Mungu katika dini na ambaye hupitia mchafuko na udhibiti wa Mafarisayo na wapinga Kristo ni yapi? Mtu anaweza kuokolewa na Mungu kama anamwamini Mungu kwa njia hii?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Kwa kuwa viongozi wa watu hawa wanawafanya wapotoke; nao wanaoongozwa na hao watu wameangamizwa” (Isaya 9:16).
Maneno Husika ya Mungu:
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale ambao hawajapitia hukumu
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
5. Matokeo ya mtu anayemwamini Mungu katika dini na ambaye hupitia mchafuko na udhibiti wa Mafarisayo na wapinga Kristo ni yapi? Mtu anaweza kuokolewa na Mungu kama anamwamini Mungu kwa njia hii?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Wao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwelekeza kipofu, wote wawili wataanguka ndani ya shimo”
(Mathayo 15:14).“Kwa kuwa viongozi wa watu hawa wanawafanya wapotoke; nao wanaoongozwa na hao watu wameangamizwa” (Isaya 9:16).
“Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa…. Walivyokuwa wakizidishwa, ndivyo walivyokuwa wakitenda dhambi dhidi Yangu: kwa hiyo nitabadili utukufu wao uwe aibu. Wanakula dhambi ya watu Wangu, nao hupendezwa na udhalimu wao. Na itakuwa, jinsi watu walivyo, ndivyo jinsi kuhani alivyo: na mimi nitawaadhibu kwa sababu ya njia zao, na kuwalipiza kwa sababu ya vitendo vyao”
(Hosea 4:6-9).Maneno Husika ya Mungu:
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua fikira zao, sembuse kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokionyesha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambao hauambatani na uhalisi na hauwezi kabisa kuwapa watu uzima.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale ambao hawajapitia hukumu
hawaonyeshi chochote isipokuwa mawazo ya kibinadamu, yakiwa yamechanganyika na ufahamu wa kibinadamu na talanta za ndani. Sio maonyesho sahihi wa mwanadamu wa kazi ya Mungu. Watu wanaowafuata wanaletwa mbele yao kwa tabia yao ya ndani. Kwa sababu wanaonyesha vitu vingi vya kuona na uzoefu wa mwanadamu, ambavyo takribani havina muungano na maana ya asili ya Mungu, na hutofautiana sana nayo, kazi ya mtu wa aina hii haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, lakini wataletwa kwake. … kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna watu wengi kanisani ambao hawana ufahamu, na jambo la uongo linapotendeka wanasimama tu upande wa Shetani. Wanapoitwa vibaraka wa Shetani wanahisi kuwa wamekosewa sana. Wanasemekana kuwa hawana ufahamu, lakini daima wanasimama upande usiokuwa na ukweli. Hakujakuwa na wakati muhimu ambapo wamesimama upande wa ukweli, hakuna wakati mmoja ambapo wamesimama na kutetea mjadala juu ya ukweli, kwa hivyo je, hawana ufahamu? Kwa nini daima wanasimama upande wa Shetani? Kwa nini hawasemi neno lolote la haki ama lenye mantiki kwa ukweli? Je, hali hii kweli imetokana na kuchanganyikiwa kwao kwa ghafla? Kadri mtu anapokuwa na ufahamu mdogo, ndivyo anavyozidi kushindwa kusimama upande wa ukweli. Je, hili linaonyesha nini? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu wanapenda uovu? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu ni watoto waaminifu wa Shetani? Je, ni kwa nini daima wanaweza kusimama upande wa Shetani na kuzungumza lugha moja naye? Kila neno na tendo lao, na maonyesho yao yanathibitisha vya kutosha kuwa wao sio wapenzi wa ukweli kwa namna yoyote, lakini badala yake wao ni watu wanaochukia ukweli. Kwamba wanaweza kusimama upande wa Shetani kunadhihirisha kuwa hakika Shetani anawapenda ibilisi hawa wadogo wanaopigana kwa ajili ya Shetani katika maisha yao yote. Je, taarifa hizi za kweli si wazi sana? Ikiwa hakika wewe ni mtu unayependa ukweli, basi kwa nini huwezi kuwaheshimu wale wanaotenda ukweli, na mbona unawafuata mara moja wale wasiotenda ukweli punde tu wanapokuwa na mabadiliko ya sura? Je, hili ni tatizo la aina gani? Sijali iwapo una ufahamu au la, sijali kwamba umelipa gharama kuu kiasi gani, sijali kuwa nguvu zako ni kuu kiasi gani na sijali ikiwa wewe ni nyoka mwovu wa ndani ama kiongozi anayepeperusha bendera. Ikiwa nguvu zako ni kuu basi ni kwa ajili tu ya usaidizi wa nguvu za Shetani; ikiwa hadhi yako iko juu, basi ni kwa sababu kuna wengi waliokuzunguka wasiotenda ukweli; ikiwa hujafukuzwa basi ni kwa kuwa sasa sio wakati wa kazi ya kufukuza, bali ni wakati wa kazi ya kuondoa. Hakuna haraka ya kukufukuza sasa. Ninahitaji tu kusubiri siku ifike ambayo utakuwa umeshaondolewa ili Nikuadhibu. Yeyote asiyetenda ukweli ataondolewa!
kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye dharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.
Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuipinga na kuikataa kazi ya Kristo. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa ulilazimishwa. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.
Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni makafiri na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo.
kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli? …
Katika imani ya watu katika Mungu, wawe walikuwa na mazoea ya kuwafuata watu wengine au hawakuridhisha mapenzi ya Mungu, lazima hatimaye waje mbele ya Mungu wakati wa hatua hii ya kazi ya siku za mwisho. Ikiwa una msingi wa kupitia hatua hii ya kazi, lakini bado unaendelea kuwafuata wengine, basi utakuwa wa kutosamehewa, na utaishia tu kama Paulo.
kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ingekuwa vyema kwa wale watu wanaosema kuwa wanamfuata Mungu kufungua macho yao watazame vizuri waone ni nani wanayemwamini hasa: Je, ni Mungu unayemwamini hakika, ama Shetani? Ikiwa unajua kuwa unayemwamini si Mungu ila sanamu zako mwenyewe, basi ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Ikiwa hakika hujui unayemwamini ni nani, basi, pia, ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Kusema hivi kutakuwa kukufuru! Hakuna anayekushurutisha umwamini Mungu. Msiseme kuwa mnaniamini Mimi, kwa kuwa Niliyasikia maneno hayo hapo kale wala Sitamani kuyasikia tena, kwa kuwa mnachoamini ni sanamu zilizo katika mioyo yenu na nyoka waovu wa ndani walio miongoni mwenu. Wale wanaotikisa vichwa vyao wanaposikia ukweli, wanaotabasamu sana wanaposikia mazungumzo ya kifo ni watoto wa Shetani, na wote ni vyombo vya kuondolewa.
kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Iwapo kuna waonevu kadhaa waovu ndani ya kanisa, na vilevile “nzi” wadogo wanaowafuata wale wasio na ufahamu kabisa, ikiwa wale wa kanisa bado hawawezi kutoa vifungu na ushawishi wa nyoka hawa baada ya wao kuona ukweli, basi hawa wajinga wataondolewa mwishoni. Ingawa nzi hawa wadogo wanaweza kuwa hawajafanya lolote baya, wao ni wenye hila hata zaidi, wadanganyifu hata zaidi na wenye kukwepa hata zaidi na kila mtu aliye namna hii ataondolewa. Hakuna yeyote atakayeachwa! Wale walio wa Shetani watarudishwa kwa Shetani, ilhali wale walio wa Mungu hakika watakwenda kutafuta ukweli; hili linaamuliwa na asili zao. Acheni wale wote wanaomfuata Shetani waangamie! Hakuna huruma watakayoonyeshwa watu hawa. Acheni wale wanaofuata ukweli wapate utoaji na muwakubalie kufurahia neno la Mungu hadi mioyo yao itosheke. Mungu ni mwenye haki; Yeye hawatendei watu kwa udhalimu. Ikiwa wewe ni ibilisi basi hutakuwa na uwezo wa kuutenda ukweli. Ikiwa wewe ni mtu anayetafuta ukweli basi ni wazi kuwa hutatekwa nyara na Shetani—hili halina tashwishi yoyote.
kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasiotenda ukweli lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaotenda ukweli mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasiotenda ukweli mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaotenda ukweli na wale wasioutenda.
kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.
kutoka katika “Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni