XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu
6. Katika ulimwengu wa kidini, ni ukweli na Mungu wanaoshikilia uwezo, au ni wapinga Kristo na Shetani wanaoshikilia uwezo?
Aya za Biblia za Kurejelea:
Maneno Husika ya Mungu:
6. Katika ulimwengu wa kidini, ni ukweli na Mungu wanaoshikilia uwezo, au ni wapinga Kristo na Shetani wanaoshikilia uwezo?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie”
(Mathayo 23:13).
“Na Yesu akaingia katika hekalu la Mungu, naye akawaondoa wote waliokuwa wakiuza na kununua katika hekalu, naye akaziangusha meza za wabadilishaji wa fedha, na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, Na akawaambia, imeandikwa, nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi; lakini mmeifanya pango la wezi” (Mathayo 21:12-13).
Maneno Husika ya Mungu:
Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?
kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Tumehubiri injili tena na tena kwa viongozi wengi katika jamii za dini, lakini bila kujali jinsi tunavyoshiriki ukweli na wao, wamekataa kuukubali. Kwa nini hivi? Ni kwa sababu majivuno yao yamekuwa tabia yao mbaya na Mungu hayuko tena mioyoni mwao! Watu wengine wanaweza kusema: “Watu walio chini ya uongozi wa baadhi ya wachungaji katika ulimwengu wa dini kweli wana msukumo mwingi. Inaonekana kwamba wana Mungu kati yao!” Haijalishi jinsi mahubiri ya wachungaji hao yanavyoweza kuwa makubwa, je, wanamjua Mungu? Kama kweli wangekuwa wanamcha Mungu mioyoni mwao, wangewafanya watu wawafuate na kuwatukuza? Je, wao wangewahodhi wengine? Je, wangethubutu kuwawekea vikwazo wengine wanaotafuta ukweli na kuchunguza njia ya kweli? Kama wanaamini kuwa kondoo wa Mungu kwa kweli ni wao na kwamba kondoo Wake wote wanapaswa wawasikilize, je, wao wenyewe hawatendi kama Mungu? Mtu wa aina hiyo ni mbaya hata zaidi kuliko Mafarisayo—yeye si mpinga Kristo? Kwa hiyo, asili yake ya majivuno inaweza kumdhibiti afanye mambo ambayo yanamsaliti Mungu.
>
kutoka katika “Asili yenye Majivuno ya Mwanadamu Ndiyo Chanzo cha Upinzani Wake kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu hawana uwepo wa Mungu na, zaidi, wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Maneno na matendo yao mengi yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini, si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kitu cha pekee kinachowaleta pamoja ni dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mkutano wa wale wote walio miongoni mwao unaweza tu kuitwa mkutano mkubwa wa watu wa dini, na bali hauwezi kuitwa kanisa. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa. Hawana kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wakifanyacho kinaonekana chenye kunuka dini, wanachoishi kwa kudhihirisha katika maisha yao kinaonekana kimejaa dini; hawana uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu, sembuse kustahiki kupokea nidhamu au nuru ya Roho Mtakatifu. Watu hawa wote ni miili isiyo na uhai, na funza wasio na mambo ya kiroho. Hawana ufahamu wa uasi na pingamizi wa mwanadamu, hawana ufahamu wa uovu wote wa mwanadamu, sembuse kujua kazi yote ya Mungu na mapenzi ya sasa ya Mungu. Wote ni watu wapumbavu, waovu, ni watu duni wasiostahili kuitwa waumini! Hakuna wafanyacho kinachohusiana na usimamizi wa Mungu, sembuse kuweza kuidhoofisha mipango ya Mungu. Maneno na matendo yao yanaudhi sana, yanasikitisha mno, na hayafai kutajwa kabisa. Hakuna chochote wakifanyacho walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu kinahusiana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu hata kidogo. Kwa sababu hii, haijalishi wanafanya nini, hawana nidhamu ya Roho Mtakatifu na zaidi, hawana nuru ya Roho Mtakatifu. Kwani wao ni watu wasiopenda ukweli, na wamechukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Wanaitwa watenda maovu kwani wanatembea katika mwili, na kufanya chochote kiwafurahishacho kwa kisingizio cha bango la Mungu. Mungu anapofanya kazi, wao wanakuwa maadui Kwake kwa makusudi, na kumkimbia Yeye. Kutoweza kushirikiana kwa mwanadamu na Mungu ni uasi wa hali ya juu, kwa hivyo wale watu wanaokimbia kinyume na Mungu makusudi si watapokea hakika malipo yao ya haki?
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?
kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni