Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”
Mwenyezi Mungu anasema, “Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka shtaka rasmi lililoandikwa; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika enzi zote, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga.
Na wale wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu pekee watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao na kufurahia kuona hilo. Siku Yangu hatimaye imefika na siwezi kusubiri zaidi!”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni