Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sauti-ya-Mung. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sauti-ya-Mung. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 10 Oktoba 2019

5. Ni nini umuhimu na matokeo ya ulimwengu wa kidini kuikataa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho?

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

5. Ni nini umuhimu na matokeo ya ulimwengu wa kidini kuikataa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho?

Maneno Husika ya Mungu:

    Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu,

Ijumaa, 26 Julai 2019

5. Ni nini hasa imani ya kweli katika Mungu? Ni kwa jinsi gani mtu anafaa kumwamini Mungu ili kupata sifa Zake?

XI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Uhusiano kati ya Mungu na Biblia

5. Ni nini hasa imani ya kweli katika Mungu? Ni kwa jinsi gani mtu anafaa kumwamini Mungu ili kupata sifa Zake?
Maneno Husika ya Mungu:

   “Imani katika Mungu” inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu si sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni aina ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu.

Jumatatu, 15 Julai 2019

1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?

XII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Wanawali Wenye Busara Wakiisikia Sauti ya Mungu
1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?
Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata” (Yohana 10:27).

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

Ijumaa, 12 Julai 2019

2. Kuna tofauti ipi kati ya maneno ya watu wanaotumiwa na Mungu kote katika enzi zote ambayo yanakubaliana na ukweli na maneno ya Mungu?

XII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Wanawali Wenye Busara Wakiisikia Sauti ya Mungu
2. Kuna tofauti ipi kati ya maneno ya watu wanaotumiwa na Mungu kote katika enzi zote ambayo yanakubaliana na ukweli na maneno ya Mungu? Maneno Husika ya Mungu:

Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.

kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 27 Mei 2019

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video)

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video) 

Mungu awahimiza makabila yote, 
mataifa na nyanja zote: 
Sikizeni sauti Yake, muione kazi Yake; 
mzingatie hatima ya wanadamu; 
mfanye Mungu Mtakatifu na Mheshimiwa, 
Mkuu na wa pekee wakuabudiwa, 
ulimwengu wote, na wanadamu, 
waishi chini ya baraka Yake Mungu
kama vizazi vya Ibrahimu, 
walivyoishi na ahadi ya Yehova, 
kama viumbe vya Mungu, Adamu na Hawa, 
walivyoishi bustani Edeni. 

Alhamisi, 2 Mei 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Mwenyezi Mungu anasema, “Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka shtaka rasmi lililoandikwa; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika enzi zote, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga.