Alhamisi, 3 Oktoba 2019

2. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

2. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

Aya za Biblia za Kurejelea:

    “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

    “Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao. Nayo bahari ikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani yake; na kifo na kuzimu zikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani zao: na kila mtu alihukumiwa kulingana na vitendo vyake. Na kifo na kuzimu zikarushwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili. Na yeyote ambaye hakupatikana ameandikwa ndani ya kitabu cha uzima alirushwa katika ziwa la moto” (Ufunuo 20:11-15).

Jumatatu, 30 Septemba 2019

2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

Maneno Husika ya Mungu:

    Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Ijumaa, 27 Septemba 2019

10. Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

10. Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?


Aya za Biblia za Kurejelea:


    “Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

    “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu. Kama ninyi mngelinijua, pia mngelimjua Baba yangu: na kuanzia sasa mnamjua, na mmemwona” (Yohana 14:6-7).

   “Mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi” (Yohana 14:10).

    “Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30).

Jumanne, 24 Septemba 2019

9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Aya za Biblia za Kurejelea:

    “Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi: nao wata, nao watafua panga zao ili ziwe majembe, na mikuki yao ili iwe mundu: hakuna taifa litakaloinua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena. Enyi wa nyumba ya Yakobo, njooni, tutembee katika nuru ya Yehova” (Isaya 2:2-5).

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Neno la Mungu | “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” (Dondoo)


Neno la Mungu | “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” (Dondoo)

    Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu,

Jumatano, 18 Septemba 2019

"Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)" Sehemu ya Nne


Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)" Sehemu ya Nne

    Mwenyezi Mungu anasema, “Kwamba Mungu anakimu ulimwengu ina maana na matumizi mapana sana. Mungu hawakimu tu watu kwa kuwapatia mahitaji yao ya kila siku ya chakula na kinywaji, Anawapatia wanadamu kila kitu wanachohitaji, ikiwa ni pamoja na kila kitu ambacho watu wanakiona na vitu ambavyo haviwezi kuonekana. Mungu anatetea, anasimamia na anatawala mazingira ya kuishi ambayo binadamu anahitaji.

Jumapili, 15 Septemba 2019

Swali la 6: Mungu alimtumia Musa kufanya kazi ya Enzi ya Sheria, hivyo kwa nini Mungu hawatumii watu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lakini badala yake Analazimika kupata mwili ili kuifanya Mwenyewe?

Jibu:

    Ni kwa nini lazima Mungu apate mwili ili kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho? ni swali ambalo wengi walio na kiu ya ukweli na wanatafuta kuonekana kwa Mungu wanalijali sana. Pia ni swali linalohusiana na kama tunaweza kunyakuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuelewa kipengele hiki cha ukweli. Ni kwa nini lazima Mungu ajipatie mwili ili kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho badala ya kumtumia mwanadamu kuifanya kazi Yake? Hili linaamuliwa na hali ya kazi ya hukumu. Kwa sababu kazi ya hukumu ni onyesho la Mungu la ukweli na onyesho la tabia Yake yenye haki ili kuwashinda, kuwatakasa, na kuwaokoa wanadamu. Hebu tusome vifungu vichache kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu.