Jumamosi, 18 Mei 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika. Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu.”

Sikiliza zaidi: Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians

Ijumaa, 17 Mei 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili. Kama kusingekuwa na udhibiti na ukuu wa Mungu, hakuna mwanadamu ambaye angeweza kudumisha na kuweka wiano katika mazingira, hata kama yaliumbwa na Mungu kwanza.”

Alhamisi, 16 Mei 2019

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)

Xiaoxue, Malesia
Siku moja baada ya mlo mkuu wa siku, nilimfundisha mwanangu mvulana mkubwa jinsi ya kusoma Kichina—maneno rahisi tu, “Mbinguni, dunia, watu, na, dunia, baba, mama….” Nilimfundisha mara chache hasa, lakini bado hakuweza kuandika. Angeandika neno la kwanza na kisha kusahau lililofuata. Hasira ndani yangu ilipanda, na kunyakua rula iliyokuwa juu ya meza na kumgonga mara kadhaa.

Jumatano, 15 Mei 2019

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kuwafundisha Wanangu (I)


Xiaoxue, Malesia

Nina wana wawili wa kiume na wameachana na mwaka mmoja. Ili kuwalea kuwa watu waliostaarabika, wenye tabia nzuri, watu wema ambao wataweza watajijengea jina katika jamii na kufanikiwa, walipokuwa na umri wa miaka miwili, nilijadiliana na mume wangu juu ya kuwatafutia shule nzuri ya chekechea.

Jumanne, 14 Mei 2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,  Umeme wa Mashariki, ushuhuda wa injili
Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Katika siku chache zilizofuata, ingawa Jingru hakuwa ameanguka katika majaribu ya Shetani na alijua kwamba hangeweza kuwa mwenzi wa Wang Wei kamwe, mkutano wake na Wang Wei jioni hiyo na ungamo lake la kweli vilirudiwa akilini mwake tena na tena kama onyesho katika filamu …
Wang Wei alipompigia simu tena, moyo wa Jingru ulishtuka kidogo, naye akajiambia: “Sote wawili hatuwezi kuwa kitu kimoja, lakini bado tunaweza kuwa marafiki wa kawaida.

Jumatatu, 13 Mei 2019

Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"

Maoni Tofauti, Migongano Ya Siku Zote
Mimi ni mke wa kawaida, mke mzuri na mama mwenye upendo, mimi huwatunza vizuri mume wangu na watoto wangu, mimi hufanya kazi kwa bidii na mwekevu katika kuendesha nyumba yangu, na sijawahi kamwe kutumia fedha zangu bila hadhari. Lakini kitu kisichofikirika kilinifika. Mwanangu alimuoa msichana wa kisasa ambaye kwa kweli alipenda kujifurahisha na kuvaa na kufuata mitindo ya ulimwengu.

Jumapili, 12 Mei 2019

Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu

Na Ouyang Mo, Mkoa wa Hubei
Baada ya miongo miwili ya mema na mabaya ambayo yeye na mumewe walipitia pamoja, hakuwahi kamwe kufikiria kwamba mumewe angekuwa na uhusiano wa nje ya ndoa. Alishindwa kabisa kuvumilia wakati alipogundua hilo. Licha ya kujaribu kila kitu ili kumfanya mumewe ampende tena, yote ilikuwa kazi bure. Katikati ya maumivu yake na kutokuwa na tumaini, ni maneno ya Munguyaliyomwokoa, yakimsaidia kupata kiini cha maumivu yake, kuelewa maana ya maisha, na hatua kwa hatua kutoka kwenye fadhaa ya mateso yake.