Jumapili, 27 Januari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Mwenyezi Mungu anasema, "Nyie watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwakomboa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani?

Ijumaa, 25 Januari 2019

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

 Umeme wa Mashariki | Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Mwenyezi Mungu alisema, Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. 

Alhamisi, 24 Januari 2019

Maonyesho ya Mungu | "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" (sehemu ya kwanza)

Maonyesho ya Mungu | "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" (sehemu ya kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Ukamilifu wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. … Hutekeleza kazi Yake kulingana na maendeleo ya nyakati, na Anatekeleza kazi Yake nyingi zaidi halisi kulingana na mabadiliko ya mambo. 

Jumatano, 23 Januari 2019

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (2) :Kurudi kwa Bwana katika Mwili Kunatimiza Unabii wa Biblia

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (2) :Kurudi kwa Bwana katika Mwili Kunatimiza Unabii wa Biblia

Kwa maana Bwana atarudi katika zile siku za mwisho, Bwana Yesu akasema, “Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja” (Luka 12:40)."Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17: 24-25).

Jumanne, 22 Januari 2019

Umeme wa Mashariki | Sura ya 20

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu aliwaumba wanadamu wote, na amewaongoza wanadamu wote mpaka leo. Hivyo, Mungu anajua yote yafanyikayo miongoni mwa wanadamu: Anajua uchungu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, Anaelewa utamu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, na kwa hiyo kila siku Yeye hufafanua hali za maisha za wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, hushughulikia udhaifu na upotovu wa wanadamu wote.

Jumatatu, 21 Januari 2019

Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days

Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days

Chen Peng alikuwa mchungaji katika kanisa la nyumba fulani. Alikuwa akimtumikia Bwana kwa bidii, na mara nyingi alifanya kazi kama mhubiri, akiwasaidia wafuasi wake, na kulibebea kanisa mizigo mizito. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kanisa lilizidi kuwa tupu zaidi na zaidi. Waumini walikuwa na roho dhaifu na wavivu, wakikosa mkutano baada ya mkutano. Na hivyo Mchungaji Chen aliona giza likiangukia nafsi yake, kana kwamba kisima cha roho yake kilikuwa kikavu, na hakuweza kuhisi uwepo wa Bwana.

Jumapili, 20 Januari 2019

Maonyesho ya Mungu | "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu"

Maonyesho ya Mungu | "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Kuamini katika Mungu na kutafuta maarifa ya Mungu si jambo rahisi. Hayawezi kupatikana kwa kukusanyika pamoja na kusikiliza mahubiri, na huwezi kukamilishwa kwa kupenda tu. Lazima upitie uzoefu, na ujue, na kuongozwa na kanuni katika matendo yako, na kupata kazi za Roho Mtakatifu. Utakapopitia katika uzoefu, utakuwa na uwezo wa kutofautisha mambo mengi—utakuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya jema na baya, kati ya haki na uovu, kati ya kile ambacho ni cha mwili na damu na kile ambacho ni cha kweli.