Jumapili, 27 Januari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Mwenyezi Mungu anasema, "Nyie watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwakomboa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika vishawishi vya wanadamu? Na tena, ni mara ngapi mmejikuta katika ugomvi usio na kikomo kati yenu kwa kukosa kuziachilia nafsi zenu? Ni mara ngapi miili yenu imekuwa katika nyumba Yangu ila roho zenu zikiwa kusikojulikana? Licha ya hayo, ni mara ngapi Nimewanyooshea mkono Wangu wa ukombozi; ni mara ngapi Nimewaonea huruma; ni mara ngapi Nimekosa uvumilivu wa kuziona hali zenu za kuhuzunisha za mateso? Ni mara ngapi … hamfahamu?"

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni