Alhamisi, 13 Desemba 2018

Tamko la Arubaini

Tamko la Arubaini

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa nini ninyi ni wa mwendo wa polepole? Kwa nini hamsikii? Makumbusho kadhaa hayajawazindua; hili linanihuzunisha. Kwa kweli Sipendi kuwaona wanangu namna hii. Moyo Wangu unawezaje kustahimili hili? Ah! Lazima Niwafundishe kwa mkono Wangu mwenyewe. Mwendo Wangu unaendelea kuwa wa kasi. Wanangu! Inukeni haraka na mshirikiane na Mimi. Nani wanajitumia kwa dhati kwa ajili Yangu sasa? Ni nani anayeweza kujitolea kikamilifu bila malalamiko hata kidogo?

Jumatano, 12 Desemba 2018

Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man

Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man

Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu
wanaomwabudu na kumtii Yeye.
Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena.
Wanajua ubaya wa Shetani, hivyo wanamkataa.

Jumanne, 11 Desemba 2018

Tamko la Arubaini na Mbili

Tamko la Arubaini na Mbili

Jinsi gani matendo ya Mwenyezi Mungu yalivyo makuu! Jinsi ilivyo ya ajabu! Jinsi ilivyo ya kushangaza! Tarumbeta saba zinatoa sauti, ngurumo saba zinatolewa, bakuli saba zinamwangwa—hii itadhihirika wazi mara moja na hakuwezi kuwa na shaka. Upendo wa Mungu huja juu yetu kila siku na ni Mwenyezi Mungu pekee Anayeweza kutuokoa; kama tunakabiliwa na bahati mbaya au kupokea baraka ni kwa sababu Yake kabisa, na sisi wanadamu hatuna njia ya kuamua hili. 

Jumatatu, 10 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo. Siku hiyo itakapofika, ndoto yenu ya kubarikiwa kwa imani yenu katika Mungu na kupata kuingia mbinguni, yote itakatizwa.

Jumapili, 9 Desemba 2018

Tamko la Arubaini na Nne

Tamko la Arubaini na Nne

Mwenyezi Mungu alisema, Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu! Nitafichua mara moja aliye wa kweli na aliye wa uongo. Hakuna haja ya kuwa na hofu, vitu vyote hufanya kazi kwa wakati Wangu. Ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati, ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati—Nitawaambia. Kuleni tu vizuri, kunyweni vizuri, njoo mbele Yangu na Nikaribieni nami Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe.

Jumamosi, 8 Desemba 2018

Tamko la Arubaini na Sita


Tamko la Arubaini na Sita

Yeyote anayejitumia na kujitolea kwa uaminifu kwa ajili Yangu, hakika Nitakukinga mpaka mwisho kabisa; mkono Wangu hakika utakushikilia ili kwamba daima una amani na mwenye furaha daima na kila siku una mwanga Wangu na ufunuo. Hakika Nitakupa baraka Zangu mara dufu, ili uwe na kile Nilicho nacho na umiliki kile Nilicho. Kile unachopewa ndani yako ni maisha yako, na hakuna mtu anayeweza kukichukua kutoka kwako. Usijiletee taabu au kufadhaika; ndani Yangu kuna amani na furaha tu.

Ijumaa, 7 Desemba 2018

Matamshi ya Mungu | "Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni"

Matamshi ya Mungu | "Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni"

Mwenyezi Mungu anasema, "Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.