Jumatatu, 10 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo. Siku hiyo itakapofika, ndoto yenu ya kubarikiwa kwa imani yenu katika Mungu na kupata kuingia mbinguni, yote itakatizwa.

Jumapili, 9 Desemba 2018

Tamko la Arubaini na Nne

Tamko la Arubaini na Nne

Mwenyezi Mungu alisema, Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu! Nitafichua mara moja aliye wa kweli na aliye wa uongo. Hakuna haja ya kuwa na hofu, vitu vyote hufanya kazi kwa wakati Wangu. Ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati, ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati—Nitawaambia. Kuleni tu vizuri, kunyweni vizuri, njoo mbele Yangu na Nikaribieni nami Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe.

Jumamosi, 8 Desemba 2018

Tamko la Arubaini na Sita


Tamko la Arubaini na Sita

Yeyote anayejitumia na kujitolea kwa uaminifu kwa ajili Yangu, hakika Nitakukinga mpaka mwisho kabisa; mkono Wangu hakika utakushikilia ili kwamba daima una amani na mwenye furaha daima na kila siku una mwanga Wangu na ufunuo. Hakika Nitakupa baraka Zangu mara dufu, ili uwe na kile Nilicho nacho na umiliki kile Nilicho. Kile unachopewa ndani yako ni maisha yako, na hakuna mtu anayeweza kukichukua kutoka kwako. Usijiletee taabu au kufadhaika; ndani Yangu kuna amani na furaha tu.

Ijumaa, 7 Desemba 2018

Matamshi ya Mungu | "Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni"

Matamshi ya Mungu | "Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni"

Mwenyezi Mungu anasema, "Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.

Alhamisi, 6 Desemba 2018

Tamko la Arubaini na Saba

Tamko la Arubaini na Saba

Mwenyezi Mungu mwenye haki—Mwenyezi! Ndani Yako hakuna chochote kabisa kilichofichwa. Kila fumbo tangu zamani hadi milele, ambalo binadamu hawajawahi kufichua, ndani Yako linadhihirika na kwa jumla kuwa wazi. Hatuhitaji tena kutafuta na kupapasa, kwa maana leo nafsi Yako inadhihirika wazi kwetu, Wewe ndilo fumbo ambalo limefichuliwa, na Wewe ni Mungu aliye hai Mwenyewe, na kwa leo Umekuja uso kwa uso na sisi, na kwa sisi kuona nafsi Yako ni kuona kila fumbo la ulimwengu wa kiroho.

Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"

Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi.

Jumatano, 5 Desemba 2018

Tamko la Sabini na Tatu

Tamko la Sabini na Tatu

Maneno Yangu yanatimizwa mara tu yanaposemwa; hayabadiliki kamwe na ni sahihi kabisa. Kumbuka hili! Kila neno na kirai kutoka katika kinywa Changu lazima yafikiriwe kwa uangalifu. Kuwa makini zaidi, usije ukapitia upotezaji na kupokea hukumu Yangu, ghadhabu Yangu na moto Wangu pekee. Kazi Yangu sasa inasonga kwa haraka sana, lakini ni safi na ni ya kutaka uangalifu mkubwa hadi kwa kiasi fulani—karibu haionekani kwa jicho tupu na haiwezi kuguswa na mikono ya mwanadamu.