Alhamisi, 6 Desemba 2018

Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"

Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Mimi ndimi maisha, njia na ukweli, hakuna yeyote angejua uwepo Wangu au utambulisho Wangu. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba mbingu ndipo ambapo Baba Yangu anapoishi, hakuna aliyejua kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu, na tena Mungu Mwenyewe. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Nitaleta ukombozi kwa wanadamu wote na kulipia mwanadamu fidia, hakuna aliyejua Mimi ni Mkombozi wa mwanadamu; binadamu alinijua tu Mimi kama mtu mkarimu na mwenye huruma. Na mbali na Mimi Mwenyewe kuweza kufafanua kila kitu kuhusu Mimi, hakuna aliyeweza kunitambua Mimi, hakuna aliyeamini kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai. Binadamu pia anayo imani kama hii Kwangu Mimi, na ananidanganya Mimi kwa njia hii. Binadamu anawezaje kunitolea Mimi ushuhuda wakati anayo mitazamo kama hii kunihusu Mimi?"



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni