Ijumaa, 28 Septemba 2018

Tamko la Hamsini na Saba

Tamko la Hamsini na Saba

Je, umechunguza kila fikira na mawazo yako, na kila tendo lako? Uko wazi kuhusu gani kati ya haya yanalingana na mapenzi Yangu na gani hayalingani? Huna uwezo wa kutambua haya! Mbona hujaja mbele Yangu? Je, ni kwa sababu Sitakuambia, au ni kwa ajili ya sababu nyingine? Unapaswa kujua hili! Kujua kwamba wale walio wazembe hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu kabisa au kupokea mwangaza na ufunuo mkuu.

Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)

Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)

Zhang Hui alikuwa mzee katika kanisa la nyumbani la Kichina. Kila wakati alikuwa mtafutaji mwenye bidii, na alikuwa anangojea kuja kwa Bwana. Katika miaka ya hivi majuzi, alishuhudia kanisa likikumbwa na huzuni pole pole. Roho yake mwenyewe ilififia pia na hakuwa na chochote cha kuhubiri. Zaidi ya hayo, bibi yake alifariki kwa ghafla, jambo lililomuathiri sana. Alikutana na mashahidi wawili kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa sadfa tu. Kupitia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, roho yake yenye kiu ilipokea unyunyiziaji na chakula na aliweza kufurahia utamu wa kazi ya Roho Mtakatifu. Alihitimisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu na akakubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho.

Alhamisi, 27 Septemba 2018

Tamko la Hamsini na Tatu

Tamko la Hamsini na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Mimi ndiye mwanzo, na Mimi ndiye mwisho. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli aliyefufuka na kamili. Nasema maneno Yangu mbele yenu, na lazima muamini Ninachosema kwa thabiti. Mbingu na dunia zinaweza kupita lakini hakuna herufi moja au mstari mmoja wa kile Ninachosema kitawahi kupita. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Punde ambapo Nimesema, hakuna neno hata moja limewahi kurudishwa na kila neno litatimizwa. Sasa wakati umewadia na lazima muingie katika uhalisi kwa haraka.

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?

Filamu za Injili | Watu wengi katika ulimwengu wa kidini hufuata unabii unaosema kwamba Bwana atashuka akiwa juu ya wingu na wanamsubiria Yeye kuja kwa njia hiyo kisha kuwanyakua hadi kwenye ufalme wa mbinguni, lakini wanapuuza unabii mbalimbali wa Bwana kuhusu kuja kwa siri: "Tazama, mimi nakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (Mathayo 25:6). Hivyo unabii huu mbalimbali wa kurudi kwa Bwana unatimizwa vipi? Na tunafaa kuwa vipi wanawali wenye hekima ambao wanakaribisha kurudi kwa Bwana?




Jumatano, 26 Septemba 2018

Tamko la Arubaini na Moja

Tamko la Arubaini na Moja

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na uwe sauti Yangu.

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (2) - Tunawezaje Kuwa na Uhakika kuwa Bwana Yesu Tayari Amerudi?

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (2) - Tunawezaje Kuwa na Uhakika kuwa Bwana Yesu Tayari Amerudi?

Tangu makanisa yalipoanza kukumbwa na ukiwa, ndugu wengi katika Bwana wamehisi kwa uwazi ukosefu wa kazi ya Roho Mtakatifu na uwepo wa Bwana, na wote wanatamani kurudi kwa Bwana. Lakini wakati tunaposikia habari ya kwamba Bwana Yesu tayari amerudi, tunawezaje kuwa na uhakika wa hili?

Jumanne, 25 Septemba 2018

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (3) - Je, Hakuna Maneno au Kazi ya Mungu Nje ya Biblia?

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (3) - Je, Hakuna Maneno au Kazi ya Mungu Nje ya Biblia?

Watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanasadiki kwamba maneno yote ya Mungu yako ndani ya Biblia, na chochote kilicho nje ya Biblia hakina kazi Yake na maneno. Hawatafuti nje ya Biblia matamko Yake katika kurudi Kwake. Je, wataweza kukaribisha kurudi kwa Bwana kama wataendelea kushikilia wazo hili? Je, Mungu angeweza kuzuiliwa tu kwa kuongea maneno yaliyo ndani ya Biblia? Biblia inasema: "Na pia kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya, ambayo, yote yakiandikwa, ninafikiri kwamba hata dunia yenyewe haingetosha vitabu hivyo ambavyo vitaandikwa" (Yohana 21:25). Mungu anasema: "Yote yaliyoandikwa katika Biblia ni machache na hayawezi kuwakilisha kazi yote ya Mungu" (Neno Laonekana katika Mwili).