Mapambano ya Kufa na Kupona
Chang Moyang Mjini Zhengzhou, Mkoani Henan
"Unapoutelekeza mwili, bila shaka kutakuwa na mapambano ndani. Shetani anataka ufuate dhana za mwili, kulinda maslahi ya mwili. Hata hivyo, neno la Mungu bado linakupa nuru na kukuangaza ndani, linakupa msukumo kwa ndani na kufanya kazi kutoka ndani. Katika hatua hii, ni juu yako kama unamfuata Mungu, au Shetani. Kila wakati ambapo ukweli unatendwa na kila wakati ambapo watu wanapofanya mazoezi ya kumpenda Mungu, kuna pambano kubwa. Unapotenda ukweli, ndani kabisa kuna pambano la kufa na kupona. Ushindi utaamuliwa tu baada ya mapigano makali. Ni machozi mangapi ya huzuni yamemwagwa" (“Kila Unapoutelekeza Mwili Kuna Pambano la Kufa na Kupona” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).