Have You Been Rapturned? | "Kutamani Sana" | Swahili Christian Movie
Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu aliwaahidi wafuasi Wake: "Naenda kuwatayarishia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia" (Yohana 14:2-3). Kwa sababu ya hili, vizazi vya waumini vimeendelea kujawa na tumaini na kushikilia maombi kwa ajili ya kutimizwa kwa ahadi ya Bwana, na kutumaini na kuomba kwamba wanyakuliwe hadi kwenye mbingu ili kukutana na Bwana na kuingia katika ufalme wa mbinguni wakati Bwana atakapokuja.