Ijumaa, 2 Agosti 2019

3. Biblia ilikusanywa na mwanadamu, sio na Mungu; Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu

XI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Uhusiano kati ya Mungu na Biblia

3. Biblia ilikusanywa na mwanadamu, sio na Mungu; Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu

Aya za Biblia za Kurejelea:

    “Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai” (Yohana 5:39-40).

    “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6).


Maneno Husika ya Mungu:

    Biblia ni rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu katika Israeli, na inaandika utabiri mwingi wa manabii wa kale vilevile baadhi ya matamshi ya Yehova katika kazi Yake wakati huo. Hivyo, watu wote wanakitazama kitabu hiki kama kitakatifu (maana Mungu ni mtakatifu na mkuu). Kimsingi, hii yote ni matokeo ya uchaji wao kwa Yehova na vile walivyokuwa wanampenda Mungu. Watu wanarejelea kitabu hiki kwa namna hii kwa sababu tu viumbe wa Mungu wanamwabudu sana Muumba wao, na hata kuna wale ambao wanakiita kitabu hiki kitabu cha mbinguni. Kimsingi, ni rekodi tu za kibinadamu. Hakikupewa jina na Yehova Mwenyewe, wala Yehova Mwenyewe hakuongoza utengenezaji wake. Kwa maneno mengine, mwandishi wa kitabu hiki sio Mungu, bali ni wanadamu. Biblia Takatifu ni jina la heshima tu lililotolewa na mwanadamu. Jina hili halikuamuliwa na Yehova na Yesu baada ya kujadiliana; si chochote zaidi ya mawazo ya kibinadamu. Maana kitabu hiki hakikuandikwa na Yehova, wala kuandikwa na Yesu. Badala yake, ni maelezo ya manabii wengi wa kale, mitume na waonaji maono, ambayo baadaye yalipangiliwa na vizazi vilivyofuata na kuwa kitabu cha maandiko ya kale, ambayo kwa watu, yanaonekana kuwa matakatifu, kitabu ambacho wanaamini kimejumuisha siri nyingi ambazo hazieleweki na za kina ambazo zinasubiri kufunguliwa na vizazi vijavyo. Kwa namna hiyo, watu hata wanaamini kwamba kitabu hiki ni kitabu cha mbinguni. Ukijumlisha Injili Nne na Kitabu cha Ufunuo, mtazamo wa watu kuhusu kitabu hicho ni tofauti kabisa na vitabu vingine, na hivyo hakuna mtu anayethubutu kukichambua hiki kitabu cha mbinguni—kwa sababu ni kitakatifu sana.

kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

    Kabla ya hapo, watu wa Israeli walisoma tu Agano la Kale. Hiyo ni sawa na kusema, mwanzoni mwa Enzi ya Neema watu walisoma Agano la Kale. Agano Jipya lilionekana tu wakati wa Enzi ya Neema. Agano Jipya halikuwepo wakati wa kazi ya Yesu; watu waliandika kazi Yake baada ya kuwa amefufuka na kupaa mbinguni. Baada ya hapo kulikuwa na Injili Nne, katika nyongeza hiyo pia kulikuwa na nyaraka za Paulo na Petro, na vile vile kitabu cha Ufunuo. Zaidi ya miaka mia moja tu baada ya Yesu kupaa mbinguni, ambapo vizazi vilivyofuata vilipangilia rekodi zao, na kuzaliwa Agano Jipya. Ni baada tu ya kazi hii kukamilika ndipo kukapatikana Agano Jipya; halikuwepo hapo kabla. Mungu alikuwa amefanya kazi yote hiyo, mtume Paulo alifanya kazi yote hiyo, na baadaye nyaraka za Paulo na Petro ziliunganishwa, na njozi kuu zaidi iliyorekodiwa na Yohana katika kisiwa cha Patmo iliwekwa mwishoni, maana ilikuwa inatoa unabii wa kazi ya siku za mwisho. Hii yote ilikuwa ni mipango ya vizazi vilivyofuata…. Inaweza kusemwa kuwa, kile walichorekodi kilikuwa ni kulingana na kiwango chao cha elimu na tabia. Kile walichokirekodi kilikuwa ni uzoefu wa wanadamu, na kila mmoja alikuwa na namna yake ya kurekodi na kuelewa, na kila rekodi ilikuwa tofauti. Hivyo, ikiwa unaiabudu Biblia kama Mungu wewe ni mjinga na mpumbavu wa kutupwa!

    kutoka katika “Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

    Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Alivunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?

kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

    Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria? Kuleta mambo ya zamani leo kunayafanya yawe historia, haijalishi yana ukweli kiasi gani, bado ni historia—na historia haiwezi kushughulikia masuala ya leo. Maana Mungu haangalii historia! Na hivyo, kama unaelewa tu Biblia, na huelewi chochote kuhusu kazi ambayo Mungu anakusudia kufanya leo, na kama unamwamini Mungu, na hutafuti kazi ya Roho Mtakatifu, basi hujui inamaanisha nini kumtafuta Mungu. Ikiwa unasoma Biblia kwa lengo la kujifunza historia ya Israeli, kutafiti historia ya uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia, basi humwamini Mungu. Lakini leo, kwa kuwa unamwamini Mungu, na kutafuta uzima, kwa kuwa unatafuta maarifa juu ya Mungu, na hutafuti nyaraka na mafundisho mfu, au ufahamu wa historia, unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu ya leo, na unapaswa kutafuta uongozi wa kazi ya Roho Mtakatifu. Kama ungekuwa mwanaakiolojia ungeweza kusoma Biblia—lakini wewe sio mwanaakiolojia, wewe ni mmoja wa wale wanaomwamini Mungu, na utakuwa bora zaidi ukitafuta mapenzi ya Mungu ya leo.

    kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

    Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!

    kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

    Wale wanaojali tu kuhusu maneno ya Biblia, wasiojali kuhusu ukweli au kutafuta nyayo Zangu—wao wananipinga, kwa kuwa wao wananizuilia Mimi kulingana na Biblia, na kuniwekea vizuizi ndani ya na Biblia, na hivyo ni wa kukufuru pakubwa dhidi Yangu. Jinsi gani watu wa aina hii wanaweza kuja mbele Zangu? Wao hawatilii maanani matendo Yangu, au mapenzi Yangu, au ukweli, badala yake wanashikilia maneno, maneno yanayoua. Jinsi gani watu kama hao wanaweza kulingana na Mimi?

    kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

    Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu “vinavyofaa” hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu waliofuata maneno ya Maandiko kwa uimara; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

    Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. … Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?

    kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

   Ukweli Ninaoufafanua hapa ni huu: Kile Mungu alicho na anacho milele hakiishi wala hakina mipaka. Mungu ni chanzo cha uhai na vitu vyote. Mungu hawezi kueleweka na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Mwishowe, ni lazima bado Nimkumbushe kila mtu: Msimwekee Mungu mipaka katika vitabu, maneno, au tena katika matamshi Yake yaliyopita. Kuna neno moja tu kwa sifa ya kazi ya Mungu—mpya. Hapendi kuchukua njia za zamani au kurudia kazi Yake, na zaidi ya hayo Hapendi watu kumwabudu kwa kumwekea mipaka katika upeo fulani. Hii ndiyo tabia ya Mungu.

kutoka katika Hitimisho ya Neno Laonekana katika Mwili

    Maelezo ya Mungu ya asili, uundaji, na hitilafu za Biblia bila shaka sio kukataa kuwepo kwake, wala sio kuishutumu Biblia. Badala yake, ni kutoa ufafanuzi wa busara na wa kufaa, kurejesha sura ya asili ya Biblia, na kurekebisha kuelewa visivyo kwa watu kuhusu Biblia ili watu wote wawe na mtazamo sahihi kuihusu, wasiiabudu tena, na wasipotee tena—wao huchukulia kimakosa imani yao kwa Biblia isiyoweza kutambua kama kumwamini na kumwabudu Mungu, na hata hawathubutu kukabiliana na usuli wake wa kweli na upungufu wake. Baada ya kila mtu kuwa na ufahamu halisi wa Biblia ataweza kuiweka kando bila kusita na kuyakubali maneno mapya ya Mungu kwa ujasiri. Hili ni lengo la Mungu katika sura hizi kadhaa. Ukweli ambao Mungu anataka kuwaambia watu hapa ni kwamba hakuna nadharia au ukweli unaoweza kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu ya sasa au maneno, na hakuna kitu ambacho kinaweza kuchukua nafasi ya Mungu. Ikiwa watu hawawezi kuondoa wavu wa Biblia, hawataweza kuja mbele ya Mungu kamwe. Ikiwa wanataka kuja mbele ya Mungu, lazima kwanza watakase mioyo yao kutokana na chochote ambacho kinaweza kuchukua nafasi Yake—hivi Mungu ataridhika.

    kutoka katika Utangulizi ya Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Kipande cha gogo lililokufa: Nahau ya Kichina yenye maana “siyoweza kusaidiwa.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni