Alhamisi, 27 Juni 2019

1. Kwa nini Bwana Yesu aliwalaani Mafarisayo? Ni nini hasa asili ya Mafarisayo?

XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu
1. Kwa nini Bwana Yesu aliwalaani Mafarisayo? Ni nini hasa asili ya Mafarisayo?
Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kwa nini nyinyi pia mnavunja amri ya Mungu kwa utamaduni wenu? Kwani Mungu aliamuru, Akisema, Mwonyeshe babako na mamako heshima: na, Yule anayemlaani baba au mama yake, na afe hicho kifo. Lakini mnasema, Yeyote ambaye atamwambia baba au mama yake, ni zawadi, chochote ambacho ungefaidi kupitia mimi;Na asimwonyeshe baba yake au mama yake heshima, atakuwa huru. Hivyo hamjaibatilisha amri ya Mungu kwa utamaduni wenu. Nyinyi wanafiki, Isaya alitabiri vyema kuwahusu, akisema, Watu hawa wananikaribia kwa vinywa vyao, na wananiheshimu kwa midomo yao; lakini moyo wao uko mbali nami. Lakini wananiabudu bure, wakifunza mafundisho ya dini ambayo ni amri za wanadamu” (Mathayo 15:3-9).


“Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi.

“Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko.

“Ole wenu ninyi, viongozi mlio vipofu, mnaosema, Yeyote atakayeapa kupitia kwa hekalu, haimaanishi chochote; lakini yeyote atakayeapa kupitia kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa kwa kiapo hicho. Ninyi mlio wapumbavu na vipofu: kwa kuwa kipi kilicho kikubwa zaidi, hiyo dhahabu, au hilo hekalu linaloitakasa dhahabu? Na, Yeyote atakayeapa kupitia kwa madhabahu, haimaanishi chochote; lakini yeyote atakayeapa kupitia kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu hiyo, amefungwa kwa kiapo hicho. Ninyi mlio wapumbavu na vipofu, kwa kuwa ni kipi kilicho kikubwa zaidi, hiyo sadaka, au hiyo madhabahu inayoitakasa sadaka? Basi yeyote anayeapa kupitia kwa madhabahu, huapa kupitia kwa madhabahu hiyo, na kila kitu kilicho juu yake. Na yeyote anayeapa kupitia kwa hekalu, huapa kupitia kwa hekalu hilo, na kupitia kwa yeye anayekaa hekaluni. Na yule anayeapa kupitia kwa mbingu, huapa kupitia kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kupitia kwa yule anayeketi juu yake.

“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, ninyi wanafiki! kwani mnatoa fungu la kumi la mnanaa na bizari na jira, na mmeacha mambo muhimu zaidi ya sheria, hukumu, fadhili, na imani: mlipaswa kuyafanya haya, na sio kutolifanya lingine. Nyinyi viongozi vipofu, mnaochunguza sana visubi, na kumeza ngamia.

“Ole wenu ninyi, waandishi na Mafarisayo, wazandiki! Kwa maana mnaosha nje ya kikombe na sahani, lakini ndani yake kumejaa kutoza kwa nguvu na kupenda zaidi ya kiasi. Ewe Farisayo aliye kipofu, osha kwanza kikombe na sahani kwa ndani, ili nje viwe safi pia.

“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, nyinyi wanafiki! Kwani nyinyi ni kama makaburi yaliyopakwa rangi nyeupe, ambayo kwa nje yanaonekana mazuri sana, lakini ndani yake mna mifupa ya wafu, na yenye uchafu wote. Hata hivyo ninyi pia mnaonekana wenye haki kwa wanadamu, lakini ndani yenu mmejaa unafiki na dhambi.

“Ole wenu, ninyi waandishi na Mafarisayo, wazandiki! kwa sababu mnajenga makaburi ya manabii, na kupamba makaburi ya wenye haki, Na kusema, iwapo tungelikuwa katika siku za baba zetu, hatungelishiriki na wao kuwaua manabii. Kwa nini mnakuwa mashahidi kwenu wenyewe, kuwa ninyi ni wana wa hao ambao waliwaua manabii. Basi kijazeni kiwango cha baba zenu. Ninyi nyoka, nyinyi kizazi cha nyoka, mnawezaje kuepuka laana ya jahanamu? Hivyo, tazama, natuma kwenu manabii, na wanadamu wenye busara, na waandishi: na mtauwa na kusulubisha baadhi yao; na mtawacharaza baadhi yao katika masinagogi yenu, na kuwatesa kutoka mji mmoja hadi mji mwingine: Ili damu yote yenye haki iliyomwagika duniani iweze kuwa juu yenu, kuanzia damu ya Habili aliyekuwa mwenye haki hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia, ambaye mlimwua katikati ya hekalu na madhabahu. Kweli nawaambieni, Mambo haya yote yatakifuata kizazi hiki” (Mathayo 23:13-36).

“Lakini makuhani wakuu na wazee waliushawishi umati kwamba iliwapasa kumwuliza Baraba, na wamwangamize Yesu. Liwali akawajibu na kunena, Ninyi mnataka nimwachilie nani kati ya hawa wawili? Wakasema, Baraba. Pilato akawaambia, Nifanye nini basi na Yesu anayeitwa Kristo? Wote wakamwambia, Acha asulubiwe. Naye liwali akasema, Mbona, amefanya maovu gani? Lakini walipaza sauti zaidi, wakisema, Acha asulubiwe. Pilato alipoona kwamba hangewashawishi, ila badala yake mafadhaiko yalifanywa, alichukua maji, na kunawa mikono yake mbele ya umati, akisema, Mimi sina kosa la damu ya mtu huyu aliye na haki: ninyi fanyeni hili wenyewe. Kisha watu wote wakajibu, na kusema, Damu yake iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu. Kisha akamwachilia Baraba kwao: na baada ya kumpiga Yesu mjeledi, akamtoa kwa minajili ya kusulubiwa” (Mathayo 27:20-26).

“Yesu akasema kwao, Iwapo Mungu angekuwa Baba yenu, ninyi mngenipenda Mimi: kwani nilitoka kwa Mungu na kuja hapa; sikuja kwa njia Yangu Mwenyewe, bali Yeye alinituma. Kwa nini hamwelewi nisemacho? hata kwa sababu hamwezi kusikia neno langu. Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake. Anaponena uwongo, anazungumza yaliyo yake mwenyewe: kwani yeye ni mwongo, na baba wa uwongo. Na kwa kuwa nawaambieni ukweli, hamniamini. Ni nani kati yenu ambaye anadhibitisha kwamba Mimi nina dhambi? Na nikisema ukweli, mbona hamnisadiki? Yule ambaye ni wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu: nyinyi kwa hivyo hamyasikii, kwa kuwa nyinyi si wa Mungu” (Yohana 8:42-47).

“Ee ninyi kizazi cha nyoka, mkiwa waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? kwani, kinywa cha mtu husema kutoka kwa mengi yaliyo moyoni mwake” (Mathayo 12:34).

Maneno Husika ya Mungu:

10. Hukumu ya Mafarisayo kwa Bwana Yesu

Marko 3:21-22 Na wakati marafiki zake walisikia kuhusu hilo, walitoka kumshika: kwani walisema, Yeye si wa akili sawa. Nao waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo.

11. Mafarisayo Kukemewa na Bwana Yesu

Mat 12:31-32 Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.

Mat 23:13-15 Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko.

Kunazo dondoo mbili tofauti hapo juu—hebu kwanza tuangalie dondoo ya kwanza: Hukumu ya Mafarisayo kwa Bwana Yesu.

Katika Biblia, tathmini ya Mafarisayo kwa Bwana Yesu Mwenyewe na mambo alioyafanya ilikuwa: “walisema, Yeye si wa akili sawa. … Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo” (Marko 3:21-22). Hukumu ya waandishi na Mafarisayo kwa Bwana Yesu haikuwa ikiiga mambo au ikifikiria tu kutoka popote—ilikuwa hitimisho yao kuhusu Bwana Yesu kutokana na yale walioyaona na kuyasikia kuhusu vitendo Vyake. Ingawa hitimisho yao ilitolewa kwa njia isiyo ya kweli au ya uongo kwa jina la haki, na kuonekana mbele ya watu ni kana kwamba ilikuwa imeshughulikiwa vyema, kiburi ambacho walitumia kumhukumu Bwana Yesu kilikuwa kigumu hata kwa wao wenyewe kuvumilia. Nguvu zao mchafukoge za chuki yao kwa Bwana Yesu ziliweza kufichua maono yao binafsi yasiyo na mipaka na sura zao za kishetani na uovu, pamoja na maumbile yao yenye nia mbaya ya kumpinga Mungu. Mambo haya waliyoyasema katika hukumu yao kwa Bwana Yesu yaliendeshwa na maono yao yasiyo na misingi, ya wivu, na hali ya ubovu na ubaya na ukatili wao dhidi ya Mungu na ukweli. Hawakuchunguza chanzo cha hatua za Bwana Yesu wala kuchunguza kiini cha kile Alichosema au kufanya. Badala yake, walimshambulia bila mpango, bila subira, kwa njia za kishenzi, na kwa makusudi ya kijicho pamoja na kutupilia mbali kile Alichokuwa Amefanya. Hii ilikuwa hadi kufikia kiwango cha kutupilia mbali Roho Wake bila kubagua, Yaani, Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu. Hivi ndivyo waliyomaanisha waliposema “Amerukwa na akili,” “Beelzebuli na mkuu wa pepo.” Hii ni kusema kwamba walisema Roho wa Mungu alikuwa Beelzebuli na pia mkuu wa pepo. Waliweza kupatia sifa ya kazi ambayo Roho wa Mungu mwenye mwili alikuwa amevalia kama kurukwa akili. Hawakukufuru tu Roho wa Mungu kama Beelzebuli na mkuu wa pepo, lakini waliishutumu kazi ya Mungu. Walimshutumu na kumkufuru Bwana Yesu Kristo. Kiini cha upingaji wao na kukufuru Mungu kilikuwa sawa kabisa na kiini cha Shetani na upingaji wa Shetani na kumkufuru Mungu. Wao hawakuwakilisha wanadamu waliopotoka tu, lakini hata zaidi walikuwa mfano halisi wa Shetani. Walikuwa ni njia ya Shetani kutumia miongoni mwa wanadamu, na walikuwa washiriki na wajumbe wa Shetani. Kiini cha kukufuru kwao na utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Yesu Kristo ndicho kilichokuwa mapambano yao na Mungu kwa ajili ya hadhi, mashindano yao na Mungu, na mapambano yao na Mungu yasiyoisha. Kiini cha upingaji wao kwa Mungu na mwelekeo wao wa ukatili kwake Yeye, pamoja na maneno yao na fikira zao moja kwa moja vilimkufuru na kumghadhabisha Roho wa Mungu. Hivyo basi, Mungu aliamua hukumu inayofaa ya na yale waliyoyasema na kufanya, na akaamua matendo yao kuwa dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi hii haiwezi kusameheka ulimwenguni humu na hata baadaye, kama vile tu maandiko yafuatayo yanasema: “… wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” na “… yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” …

… Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi mbili za maandiko? Baadhi ya watu husema wanaiona ghadhabu ya Mungu. Baadhi ya watu husema wanauona upande wa tabia ya Mungu ambao hauvumilii kosa la wanadamu, na kwamba watu wakifanya kitu ambacho kinamkufuru Mungu, hawatapata msamaha Wake. Licha ya ukweli kwamba watu wanaona na kutambua ghadhabu na kutovumilia makosa ya wanadamu kwa Mungu katika vifungu hivi viwili, bado hawaelewi kwa kweli mtazamo Wake. Dondoo hizi mbili zinao ufafanuzi wa mwelekeo na mtazamo wa kweli wa Mungu kwa wale wanaomkufuru na kumghadhabisha Yeye. Dondoo hii katika maandiko inashikilia maana halisi ya mwelekeo na mtazamo Wake: “yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Watu wanapomkufuru Mungu, wakati wanapomghadhabisha Yeye, Yeye hutoa hukumu, na hukumu hii ndiyo matokeo Yake ya mwisho. Hali hii inafafanuliwa hivi katika Biblia: “Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” (Mat 12:31), na “Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki!” (Mat 23:13).

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu waliofuata maneno ya Maandiko kwa uimara; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.

kutoka katika “Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote” katika Neno Laonekana katika Mwili

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki?

kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni