Jumanne, 12 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 6

Mwenyezi Mungu alisema, Binadamu wanapigwa bumbuazi kwa sababu ya matamshi ya Mungu wanapotambua kwamba Mungu amefanya kitendo kikubwa katika ulimwengu wa kiroho, kitu ambacho mwanadamu hawezi na ambacho Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anaweza kufanikisha. Kwa sababu hii, Mungu mara tena anawasilisha maneno ya huruma kwa wanadamu. Mioyo ya watu inapojaa ukinzani, ikishangaa: “Mungu ni Mungu asiye na huruma au upendo, lakini badala yake Mungu aliyejitolea kuwaangusha binadamu; kwa hiyo mbona Atuonyeshe huruma? Yawezekana kwamba Mungu kwa mara nyingine amehamia kwa utaratibu?” wakati ambapo fikira hii, wazo hili huumbika ndani ya akili zao, wao hung’ang’ana kulishinda kwa nguvu zao zote. Hata hivyo, baada ya kazi ya Mungu kuendelea mbele kwa kiasi kingine cha wakati, Roho Mtakatifu ameanza kazi kubwa katika kanisa, na kila mwanadamu ameanza kufanya kazi ili kutekeleza shughuli yake, kisha wakati huo binadamu wote wameingia katika utaratibu huu wa Mungu. Hili ni kwa sababu hakuna yeyote anayeweza kuona dosari yoyote ndani kile ambacho Mungu husema na kufanya, na kuhusu kile ambacho Mungu atafanya baada ya hapo kwa kweli, hakuna yeyote anayeweza kujua au hata kukikisia. Kama vile amesema Mungu kwa kinywa Chake Mwenyewe: “Kati ya watu wote wanaoishi chini ya mbingu, kuna yeyote ambaye hayuko ndani ya kiganja cha mkono Wangu? Kuna yeyote asiyetenda kufuatana na maagizo Yangu?” Lakini Nawapa ushauri kidogo: Katika masuala ambayo hamwelewi kabisa, yeyote kati yenu, asinene wala kutenda. Kile ambacho Nimesema sasa hivi sio ili kufyonza shauku yenu, bali kukuhimiza kufuata mwelekeo wa Mungu katika matendo yako. Kwa vyovyote vile, usife moyo au kuingia katika tashwishi, kwa sababu ya kile Nilichosema kuhusu “dosari”: Kusudi Langu ni hasa kukukumbusha utilie maanani maneno ya Mungu. Mungu asemapo: “Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, ili binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu,” kwa kusoma maneno haya, binadamu, kwa mara nyingine, hupigwa bumbuazi. Walichoona jana kilikuwa neno la kuonya, ulikuwa mfano wa huruma ya Mungu, lakini leo mazungumzo yamegeuka ghafula kuwa mambo ndani ya roho—hili linamaanisha nini hasa? Kwa nini Mungu huendelea kubadilisha njia Yake ya kunena? Na mbona haya yote yanapaswa kuchukuliwa kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika? Yawezekana kwamba maneno ya Mungu yanakosa uhalisi? Kwa kutafakari maneno haya, mtu hutambua hili: Wakati ambapo Roho wa Mungu na mwili vimetengana, basi mwili huo ni mwili wa maumbile ulio na sifa za mwili wa maumbile, kwa maneno mengine, kile ambacho watu huita maiti itembeayo. Mwili hutokana na Roho: Yeye ni kupata mwili kwa Roho, yaani, Neno lililopata mwili. Kwa maneno mengine, Mungu Mwenyewe huishi ndani ya mwili. Kutoka kwa hili mtu anaweza kuona mahali ambapo kuna kosa kubwa sana la kujaribu kutenganisha Roho na mwanadamu. Kwa sababu hii, ingawa Anaitwa “mwanadamu,” Yeye si wa jamii ya binadamu, na Hana sifa za binadamu: Huyu ni mtu ambaye Mungu hujivika, huyu ni mtu ambaye Mungu humthibitisha. Ndani ya maneno Roho wa Mungu amejumuishwa, na maneno ya Mungu yanafichuliwa moja kwa moja katika mwili. Hili linaeleza wazi zaidi kwamba Mungu huishi ndani ya mwili na ni Mungu wa vitendo zaidi, kutokana nalo inathibitishwa kwamba Mungu yupo, hivyo kumaliza enzi ya uasi wa binadamu dhidi ya Mungu. Kisha, baada ya kuufunza binadamu kuhusu njia inayoelekea kwa maarifa ya Mungu, Mungu anabadilisha mada tena, na kuchukua kipengele kingine cha tatizo.
“Nimetembea ulimwenguni kwa miguu Yangu, Nikinyoosha macho Yangu juu ya anga yake nzima, na Nimetembea miongoni mwa wanadamu wote, Nikionja ladha tamu, ya asidi, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu.” Kauli hii, ijapokuwa urahisi wake, siyo rahisi kufahamu. Ingawa mada imebadilika, kwa msingi inabaki ile ile: Bado inawawezesha binadamu kumjua katika mwili Wake. Kwa nini Mungu asema kwamba Ameonja ladha tamu, chachu, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu? Mbona Asema kwamba Ametembea miongoni mwa wanadamu wote? Mungu ni Roho, lakini pia Yeye ni mwanadamu mwenye mwili. Roho, asiyefungwa na mipaka ya mwanadamu, Anaweza kukanyaga juu ya ulimwengu wote, Akiuzingira ulimwengu kwa tazamo la jumla. Kutoka kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Roho wa Mungu hujaza eneo pana na wazi la ulimwengu na Hufunika dunia kutoka ncha hadi ncha; hakuna mahali ambapo hapajapangwa kwa mikono Yake, hakuna mahali pasipo na alama za nyayo Zake. Hata kama Roho, aliyepata mwili, anazaliwa kama mwanadamu, Yeye, kwa sababu ya kuweko Kwake kama Roho, Hakomi kuhitaji vitu vyote ambavyo wanadamu huhitaji, lakini kwa badala yake, kama mwanadamu wa kawaida, Hula chakula, Huvaa nguo, Hulala, na Huishi katika makazi, Akifanya kila kitu ambacho mwanadamu wa kawaida hufanya. Wakati huo huo, kiini cha ndani kikiwa tofauti, Yeye si sawa na kile ambacho mtu huzungumzia kwa kawaida kama mwanadamu. Ingawa Hustahimili mateso yote ya mwanadamu, Yeye kwa sababu hiyo Hatelekezi Roho; ingawa Hufurahia baraka, Yeye kwa sababu hiyo hasahau Roho. Roho na mwanadamu wameunganishwa kwa mapatano ya kimya; hao wawili Hawawezi kutenganishwa, na kamwe Hawajawahi kutenganishwa. Kwa kuwa mwanadamu ni kupata mwili kwa Roho, na hutoka kwa Roho, kutoka kwa Roho aliye na umbo, kwa hiyo Roho anayeishi ndani ya mwili si wa kupita uwezo wa binadamu, yaani, Hawezi kufanya mambo ya ajabu, ambalo ni kusema, Roho huyu hawezi kuondoka katika mwili wa maumbile, kwani Angefanya hivyo, kitendo cha Mungu cha kuwa mwili kingepoteza maana yake yote. Ni wakati ambapo Roho hudhihirishwa kwa ukamilifu ndani ya mwili wa maumbile tu ndipo binadamu wanaweza kusababishwa kumjua Mungu Mwenyewe wa vitendo, na wakati huo tu ndipo mapenzi ya Mungu hutimizwa. Ni baada tu ya Mungu kuwasilisha Roho na mwili mmoja mmoja kwa binadamu ndipo Huonyesha upofu na uasi wa mwanadamu: “lakini mwanadamu hakuwahi kweli kunitambua, wala hakuniona Nikitembea ng’ambo.” Kwa upande mmoja, Mungu asema kwamba, bila kujulikana kwa ulimwengu, Yeye hujificha ndani ya mwili, bila kufanya kamwe jambo lolote la miujiza kwa wanadamu kuona; kwa upande mwingine, Hulalamika dhidi ya binadamu kwa kukosa kumjua. Hakuna, hata hivyo, ukinzani ndani ya hili. Kwa kweli, ikitazamwa katika utondoti wake, si vigumu kuona kwamba kuna pande mbili kwa njia ambayo kwayo Mungu hutimiza malengo Yake. Sasa, kama Mungu angetekeleza ishara na maajabu ya miujiza, basi, bila kulazimika kuanza kazi yoyote kubwa, Angemlaani tu mtu kufa kwa kinywa Chake Mwenyewe, mtu huyo angekufa papo hapo, na kwa njia hii kila mwanadamu angeridhishwa; lakini hili halingetimiza lengo la Mungu katika kuwa mwili. Kama Mungu angefanya hili kweli, binadamu hawangeweza kamwe, kwa akili zao za kufahamu, kuamini kuweko Kwake, haungeweza kamwe kuamini kweli, na zaidi ya hayo ungedhania kwamba shetani ni Mungu. Hata la muhimu zaidi, binadamu hawangeijua tabia ya Mungu kamwe: Je, hiki si kipengele kimoja cha maana ya Mungu kuwa ndani ya mwili? Kama binadamu hawawezi kumjua Mungu, basi daima itakuwa Mungu asiye dhahiri, Mungu wa miujiza, ambaye Ana utawala mkubwa katika ufalme wa binadamu: Hili halingekuwa suala la fikira za mwanadamu kummiliki mwanadamu? Au, kulitamka hili tena kwa dhahiri zaidi, Shetani, ibilisi, hangekuwa ana utawala mkubwa? “Kwa nini Nasema Narejesha mamlaka Yangu? Kwa nini Nasema kwamba kupata mwili kuna maana nyingi sana?” Wakati ambapo Mungu hupata mwili, huo ndio wakati ambapo Hurejesha mamlaka Yake; pia ni wakati ambapo uungu Wake hujitokeza moja kwa moja kufanya kazi Yake. Hatua kwa hatua, kila mwanadamu huja kumjua Mungu wa vitendo, na kwa ajili ya hili nafasi inayoshikiliwa na Shetani ndani ya moyo wa mwanadamu hukandamizwa kabisa huku nafasi ya Mungu ikikuzwa. Awali, Mungu aliyekuwapo katika akili za watu alitambulika kama picha ya shetani, Mungu ambaye alikuwa hashikiki, Haonekani, na hata hivyo mtu aliamini Mungu huyu sio tu kuweko bali pia kuweza kutekeleza kila aina ya ishara na maajabu ya miujiza na kufichua kila aina ya mafumbo, kama vile kutisha kwa waliopagawa na pepo. Hili latosha kuthibitisha kwamba Mungu aliye ndani ya akili za watu si picha ya Mungu lakini badala yake ni picha ya kiumbe kando na Mungu. Mungu asema kwamba Anataka kuchukua nafasi inayomiliki asilimia 0.1 ya moyo wa mwanadamu, na kwamba hiki ni kiwango cha juu sana Atakacho kwa binadamu. Hakuna tu upande wa juujuu kwa kauli hii; pia kuna upande wa kweli. Kama haingefafanuliwa kwa njia hii, watu wangefikiria matakwa ambayo Mungu huhitaji kutoka kwao kuwa duni sana, kana kwamba Mungu alielewa kidogo sana kuwahusu. Je, hii siyo saikolojia ya binadamu?
Kama mtu atachukua yaliyo hapo juu na kuweka pamoja na mfano wa Petro ulio hapa chini, watapata kwamba Petro alikuwa kweli mtu aliyemjua Mungu bora zaidi, kwa sababu aliweza kuachana na Mungu asiye dhahiri na kufuatilia ufahamu wa Mungu wa vitendo. Kwa nini Mungu alitaja hoja maalum ya kufahamu kwamba wazazi wake walikuwa pepo waliompinga Mungu? Kutokana na hili inathibitishwa kwamba Petro hakuwa akimfuatilia Mungu aliye ndani ya moyo wake mwenyewe, na kwamba wazazi wake wanawakilisha Mungu asiye dhahiri: Hili ni kusudi la Mungu katika kuleta mfano wa wazazi wa Petro. Wengi sana wa watu huwa hawazingatii hasa ukweli huu, wakimakinikia uangalifu wao badala yake kwa maombi ya Petro, kwa kiwango ambacho wengine hata huweka maombi ya Petro daima ndani ya midomo yao na akilini mwao, lakini bila kamwe kufikiria kutofautisha Mungu asiye dhahiri na ufahamu wa Petro. Kwa nini Petro alienda kinyume cha wazazi wake na kutafuta kumjua Mungu? Kwa nini alichanganya mafunzo aliyokuwa amejifunza kutoka kwa wale waliokuwa wameshindwa zamani ili kujichochea kwa juhudi kuu zaidi? Kwa nini alisimilisha imani na upendo wa wale wote waliokuwa wamempenda Mungu kotekote katika enzi? Petro alielewa kwamba kila kitu chema hutokana na Mungu—huja moja kwa moja kutoka kwa Mungu bila kupitia utengenezaji wowote na Shetani. Kutoka kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Yule aliyemjua alikuwa Mungu wa vitendo na si Mungu wa miujiza. Kwa nini Mungu asema kwamba Petro alitilia maanani kwa njia maalum kusimilisha imani na upendo wa wale wote waliompenda Mungu kotekote katika enzi? Kutoka kwa hili mtu anaweza kuona kwamba sababu kuu mbona watu wameshindwa kotekote katika enzi ni kwamba walikuwa tu na imani na upendo lakini hawakumjua Mungu wa vitendo, na kwa hiyo imani yao iliendelea kuwa isiyo dhahiri. Kwa nini Mungu hutaja tu imani ya Ayubu mara nyingi bila kusema hata mara moja kwamba alimjua Mungu, na zaidi ya hayo kumwita wa chini kwa Petro? Kutoka kwa maneno ya Ayubu, “Nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio: lakini sasa jicho langu linakuona,” mtu anaweza kuona kwamba Ayubu alikuwa tu na imani lakini bila ufahamu. Kwa kusoma kauli, “Na mfano usiofaa wa wazazi wake kuwa kama foili[a], hii ilimwezesha kwa urahisi kutambua upendo na huruma Yangu,” watu wengi watachochewa kuleta maswali mengi: Ni kwa nini Petro anamjua Mungu tu anapowekwa dhidi ya mfano wa kinyume, lakini sio moja kwa moja? Ni kwa nini anajua tu huruma na upendo, lakini mambo mengine hayatajwi? Ni wakati tu ambapo mtu hutambua kutokuwa kweli kwa Mungu asiye dhahiri ndipo mtu hugeuka kuweza kufuatilia ufahamu wa Mungu wa vitendo. Lengo la tamko hili ni kuwaongoza watu kung’oa Mungu asiye dhahiri kutoka mioyoni mwao. Kama binadamu wangekuwa daima wamejua sura ya kweli ya Mungu, tangu mwanzoni mwa uumbaji kufikia siku ya leo, basi hawangekuwa wanaojua sana njia za Shetani, kama inavyojulikana kutoka kwa methali, “Mtu huwa hajali ardhi tambarare mpaka avuke mlima,” ambayo inaeleza wazi kwa utoshelevu maana ya Mungu katika kunena maneno haya. Kwa vile Angependa kuwaongoza watu kufahamu kwa kina zaidi ukweli wa mfano ambao Ametoa, Mungu anatia mkazo wa kusudi kwa huruma na upendo, Akithibitisha kwamba enzi ambayo Petro aliishi ndani ilikuwa Enzi ya Neema. Ikitazamwa kwa mtazamo mwingine, hii inafichua zaidi waziwazi sura ya kutisha ya shetani, ambaye hunasa mtegoni na kuwapotosha tu binadamu, na hivyo huanzisha, hata kwa utofauti mkavu zaidi, upendo na huruma ya Mungu.
Mungu pia anaeleza kwa muhtasari ukweli kuhusu majaribio ya Petro na zaidi ya hayo Anaeleza hali zao halisi, ili watu waweze kutambua bora yafuatayo: kwamba Mungu hana huruma na upendo tu, lakini pia Ana uadhama na ghadhabu, na kwamba wanaoishi kwa amani sio lazima kwamba wanaishi katikati ya baraka za Mungu. Zaidi ya hayo, kuwaambia watu kuhusu uzoefu wa Petro baada ya majaribio yake kunaonyesha hata kwa dhahiri zaidi ukweli wa maneno haya ya Ayubu: “Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Hii inatosha kuonyesha kwamba Petro alikuwa amefikia ufahamu usio na kifani wa Mungu, kitu ambacho hakuna yeyote katika enzi yoyote iliyotangulia alikuwa amewahi kufikia: Hiki ndicho Petro alipata wakati aliposimilisha imani na upendo wa wale wote ambao walikuwa wamempenda Mungu kotekote katika enzi na kuchanganya mafunzo ya kushindwa kwa zamani ili kujihimiza. Kwa sababu hii, yeyote ambaye hufikia ufahamu halisi wa Mungu huitwa “tunda,” na Petro ni mmoja miongoni mwa hawa. Katika maombi ya Petro kwa Mungu mtu anaweza kuona maarifa halisi ya Mungu ambayo alipata kupitia majaribio yake, lakini dosari moja ndogo ni kwamba hakuweza kufahamu kwa ukamilifu mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo maana, kwa kujenga juu ya msingi wa maarifa ya Mungu ambayo Petro alipata, Mungu ameanzisha matakwa ya “kumiliki asilimia 0.1 pekee ya moyo wa mwanadamu.” Kwa kuzingatia ukweli kwamba hata Petro, mtu aliyemjua Mungu bora zaidi, hakuweza kuelewa mapenzi ya Mungu sawasawa, inaweza tu kuhitimishwa kwamba binadamu hawajaandaliwa hasa na chombo cha kumjua Mungu, kwa vile Shetani tayari amempotosha mwanadamu kwa kiasi hicho, na hili linawaongoza watu wote kujua kiini cha binadamu. Haya masharti ya mwanzo mawili—kwamba binadamu wanakosa chombo cha kumjua Mungu na zaidi ya hayo umepenywa na Shetani kabisa—yanatoa mandhari ya kuonyesha nguvu kuu za Mungu, kwa kuwa Mungu, kupitia tu utumiaji wa maneno na bila hata kulazimika kuanza aina yoyote ya kazi, amechukua nafasi fulani katika moyo wa mwanadamu. Kwa nini kufikia asilimia 0.1 kuna maana ya kufikia utimizaji wa mapenzi ya Mungu? Kulieleza hili kwa kuzingatia ukweli kwamba Mungu hakumpa mwanadamu chombo kinachozungumziwa: Ikiwa, wakati chombo hiki hakipo, binadamu wangefikia asilimia mia moja ya maarifa, basi kila hatua na kitendo cha Mungu vingekuwa kitabu kilicho wazi kwa mwanadamu, na, kwa ajili ya tabia ya asili ya mwanadamu, angemuasi Mungu mara moja, akiinuka kumpinga hadharani (hivi ndivyo alivyoanguka Shetani). Na kwa hiyo Mungu huwa hamdunishi mwanadamu kamwe. Hili ni kwa sababu tayari Amemchambua mwanadamu kabisa, kiasi kwamba Anajua kila kitu kwa ubayana ulio dhahiri kabisa hata mpaka kwa kiasi gani cha maji kimechanganywa na damu yake: Je, sembuse kuelewa kwa dhahiri zaidi asili ya mwanadamu ya kuonekana? Mungu hafanyi makosa kamwe, na zaidi ya hayo, katika kutoa matamshi Yake, Huchagua maneno Yake kwa usahihi mkubwa. Kwa sababu hii, ukweli kwamba Petro hakuwa sahihi katika kuelewa mapenzi ya Mungu haikanushi ukweli kwamba yeye pia ni mtu aliyemjua Mungu bora zaidi, na kilicho zaidi vitu hivi viwili havihusiani kabisa. Mungu hakuleta mfano wa Petro ili kulenga uangalifu wa watu kwake. Kwa nini Petro aweze kufikia maarifa ya Mungu ikiwa hata mtu kama Ayubu hangeweza? Kwa nini angesema kwamba mtu anaweza kuyafikia na bado pia aseme kwamba ni kwa ajili ya nguvu kuu za Mungu? Je, ni kweli kwamba kipaji cha asili cha binadamu ni kizuri? Watu hawaoni ni rahisi kuelewa hoja hii—hakuna yeyote ambaye angejua maana yake ya ndani isipokuwa kama Ningeieleza. Lengo la maneno haya ni kuwawezesha wanadamu kufikia aina fulani ya mtazamo, ambayo kwayo watapata ujasiri kushirikiana na Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo Mungu, kwa kusaidiwa na juhudi za mwanadamu kushirikiana na Yeye, Anaweza kuchukua hatua: Hii ndiyo hali halisi katika ulimwengu wa kiroho, kitu ambacho binadamu hawawezi kabisa kuelewa. Ili kutangua nafasi ambayo Shetani anamiliki ndani ya moyo wa mwanadamu na tokea hapo kumwezesha Mungu kumiliki, hili linaitwa kukataa ushambulizi wa Shetani; ni wakati ambapo hili limefanyika tu ndipo inaweza kusemekana kwamba Kristo ameshuka duniani, na ni wakati huo tu ndipo inaweza kusemekana kwamba falme za ulimwengu zimekuwa ufalme wa Kristo.
Inatajwa hapa kwamba Petro amekuwa sampuli na mwenye kuonyesha mtindo kwa wanadamu kwa maelfu ya miaka. Hili silo tu kwa ajili ya kufafanua ukweli kwamba yeye ni sampuli na kielelezo: Maneno haya ni mfano wa onyesho halisi la vita katika ulimwengu wa kiroho. Wakati huu wote Shetani amekuwa akimfinyanga mwanadamu, akiwa na matumaini yasiyofaa ya kuwameza binadamu na kisha kusababisha Mungu kuuharibu ulimwengu na kupoteza ushahidi Wake. Lakini Mungu alisema: “Kwanza Nitaumba mfano ili Niweze kuchukua nafasi ndogo kabisa ndani ya moyo wa mwanadamu. Katika hatua hii, binadamu hawanifurahishi wala kunijua kwa ukamilifu; hata hivyo, kwa kutegemea nguvu Zangu kuu, mwanadamu ataweza kunitii Mimi kabisa na kukoma kuniasi, na Nitatumia mfano huu kumtiisha Shetani, huku ni kusema, Nitatumia nafasi Yangu iliyo na asilimia 0.1 kuzuia nguvu zote ambazo Shetani amekuwa akitumia kumtawala mwanadamu.” Na kwa hiyo, leo, Mungu ametoa mfano wa Petro ili aweze kutumika kwa wanadamu wote kama sampuli ya kufuata. Kuyaweka haya pamoja na maneno ya mwanzo, mtu anaweza kuona ukweli wa kile alichosema Mungu kuhusu hali halisi katika ulimwengu wa kiroho: “Mambo hayako sasa kama yalivyokuwa wakati mmoja: Naenda kufanya mambo ambayo, tangu mwanzo wa uumbaji, dunia haijawahi kuyaona, Naenda kusema Maneno ambayo, kupitia enzi nyingi, wanadamu hawajawahi kuyasikia, kwa sababu Nauliza kwamba binadamu wote waje wanijue katika mwili.” Kutokana na hili mtu anaweza kuona, kile alichonena Mungu kukihusu Amekianza leo. Wanadamu wanaweza tu kuyaona mambo yanavyoonekana nje na sio hali halisi ndani ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, Mungu alisema kwa njia ya moja kwa moja na waziwazi: “Hizi ndizo hatua kwa usimamizi Wangu, ambazo binadamu hawazijui hata kidogo. Hata Ninapozizungumzia wazi, mwanadamu bado amechanganyikiwa sana kwa akili yake mpaka haiwezekani kumwelezea kila kitu kuzihusu. Kutoka hapa kuna unyenyekevu dhalili wa mwanadamu, sivyo?” Kuna maneno yasiyosemeka ndani ya maneno haya, yakieleza kwamba vita vimefanyika katika ulimwengu wa kiroho, kama ilivyodokezwa hapo juu.
Kueleza kwa muhtasari hadithi ya Petro bado hakukufikia mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu, kwa hiyo Mungu alitoa matakwa yafuatayo kuhusiana na matukio katika maisha ya Petro: “Ulimwenguni mwote na maeneo yasiyo na kikomo ya anga, mambo lukuki ya uumbaji, mambo lukuki duniani, na mambo lukuki mbinguni yote yanatakasa nguvu yao yote kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kazi Yangu. Hakika hamtamani kubakia watazamaji walio kando, kuendeshwa hapa na pale na nguvu za Shetani?” Kushuhudia maarifa ya Petro kulikuwa kupata nuru kwa maana sana kwa binadamu, na kwa hiyo, ili kutimiza hata mafanikio bora zaidi, Mungu huwaruhusu binadamu waone matokeo ya kutozuiliwa kwa utukutu na kutomjua Yeye, na zaidi ya hayo Anawaambia binadamu—mara nyingine tena na kwa usahihi mkuu zaidi—kuhusu hali halisi za vita katika ulimwengu wa kiroho. Ni kwa njia hii pekee ndio wanadamu wanaweza kuwa na tahadhari zaidi katika kujilinda dhidi ya kukamatwa na Shetani; zaidi ya hayo, inaeleza wazi kwamba, wakati huu, wakianguka, hawatapokea wokovu kutoka kwa Mungu tena kama walivyofanya wakati huu. Yakichukuliwa pamoja, maonyo haya kadhaa, katika kuzidisha fikira za binadamu kuhusu maneno ya Mungu, yamewasababisha watu kutunza huruma Yake kwa upendo zaidi na kushikilia kwa makini zaidi maneno Yake ya kuonya, hivyo kufikia kweli lengo la Mungu la kuwaokoa wanadamu.
Tanbihi:
a. Foili—Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni