Tamko la Hamsini na Nane
Ukiielewa nia Yangu, utaweza kuufikiria mzigo Wangu na unaweza kupata mwanga na ufunuo, na kupata ufunguliwaji na uhuru, kuuridhisha moyo Wangu, kuyaruhusu mapenzi Yangu kwa ajili yako kutekelezwa, kuwaletea watakatifu wote ujenzi wa maadili, na kuufanya ufalme Wangu duniani kuwa imara na thabiti. Jambo la muhimu sasa ni kuelewa nia Yangu, hii ni njia mnayopaswa kuingia katika na hata zaidi ni wajibu wa kutimizwa na kila mtu.
Neno Langu ni dawa nzuri inayoponya kila aina ya maradhi. Alimradi uko tayari kuja mbele Yangu, Nitakuponya, na kukuruhusu kuona kuwepo kwa kudura Yangu, kuona matendo Yangu ya ajabu, kuona haki na uadhama Wangu na hata zaidi kuona upotovu wenu wenyewe na udhaifu wenu wenyewe. Naelewa kabisa kila hali ndani yako; daima unafanya vitu ndani ya moyo wako na hauonyeshi kwa nje. Niko wazi hata zaidi kuhusu kila kitu unachokifanya. Lakini unapaswa kujua ni vitu gani Ninavyovisifu, na ni vitu gani Nisivyovisifu; unapaswa kutofautisha kwa wazi hivi viwili na haupaswi kuchukulia hili kwa kawaida.
Unaunga mkono kwa maneno matupu tu haja ya kufikiria mzigo wa Mungu, lakini unapokabili ukweli, huufikiri vya kutosha ingawa unajua vizuri mzigo wa Mungu ni nini. Kweli umevurugwa kabisa, mjinga kwa kiwango fulani, na hata zaidi mshenzi kikamilifu. Hili linaeleza jinsi mwanadamu alivyo mgumu kushughulikia na yote anayofanya ni kuunga mkono kwa maneno matupu yanayosikika kuwa mazuri, akisema kitu kama “Siwezi kabisa kuielewa nia ya Mungu, lakini nikiielewa hakika ninatenda kulingana nayo.” Hii si hali yenu ya kweli? Ingawa nyote mnaijua nia ya Mungu, na mnajua chanzo cha ugonjwa wenu ni kipi, jambo la muhimu ni kwamba hamko tayari kutenda; huu ni ugumu mkubwa zaidi. Usipotatua hili mara moja, litakuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa maisha yako mwenyewe.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni