Momo Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui
Kabla ya kumwamini Mungu, bila kujali chochote nilichokuwa nikifanya, sikuwahi kutaka kubaki nyuma. Nilikuwa tayari kukubali shida yoyote ili mradi ingemaanisha ningeinuka juu ya kila mtu mwingine zaidi. Baada ya kumkubali Mungu, mtazamo wangu uliendelea kuwa sawa, kwa sababu niliamini kikamilifu msemo, "Hakuna maumivu, hakuna faida,"
na kuona mtazamo wangu kama ushahidi wa msukumo wangu. Wakati Mungu alinifichulia ukweli, hatimaye niligundua kuwa nilikuwa nikiishi chini ya jozi la Shetani, nikiishi chini ya miliki yake.
Sio muda mrefu sana uliopita, kanisa lilifanya mipango ya kumtuma dada niliyeshiriki naye ili aweze kuhudumu katika nafasi ya uongozi. Niliposikia habari hizo, nilisononeka. Sisi sote tulikuwa tunahudumu katika majukumu ya uongozi hadi tulipoteuliwa tena kama wahariri. Sasa dada yangu angerudia nafasi ya uongozi na kumtumikia Mungu akiwa na uwezekano usio na kikomo wa ukuaji, lakini bado ningebakia nikifanya kazi kwa dawati, nikitekeleza kazi yangu bilakuonekana. Kunaweza kuwa na mategemeo gani ya baadaye katika hayo? Kwa kubadili mawazo, nilikumbushwa msemo wa kale, "Kuna njia milioni tofauti za mafanikio." Ili mradi ningekamilisha kazi yangu vizuri, ningeweza pia kufanikiwa. Nilihitaji tu kuzidisha jitihada zangu katika kutafuatilia ukweli. Ikiwa ningelenga kuhariri mahubiri ili yawasilishe ukweli vizuri zaidi, labda siku moja viongozi wangeona kuwa nilielewa ukweli. Kisha wangenipandisha cheo na siku zangu za baadaye zingekuwa pia za kuchangamsha. Baada ya utambuzi huu, mawingu ya kijivu yalianza kurejea kwa ajili ya uamuzi mpya. Nilijitosa katika kazi yangu, na nikala na kunywa neno la Mungu wakati sikuwa na shughuli, bila kuthubutu kulegea hata kwa muda.
Siku moja, niliona kifungu kinachofuata katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha: "Kila kitu kinachokuzuia kumtafuta Mungu na kutafuta ukweli ni mojawapo ya pingu za Shetani. Ukiwa umefungwa na moja kati ya minyororo ya Shetani, unaishi maisha yako chini ya miliki yake." Baada ya kusikia haya, sikuweza kujizuia ila kuuliza, "Ni ipi kati ya jozi za shetanininayoishi chini yake? Ni ipi kati ya sumu zake inayozuia utafutiliaji wangu wa ukweli?" Nilipojaribu kutafakari swali hili kwa kimya, nilikumbushwa hali yangu ya hivi karibuni. Baada ya dada yangu kupelekwa kwenye daraja lake jipya, sikuwa wa kutoonyesha hisia. Kwa kweli, nilijitolea zaidi kula na kunywa neno la Mungu, kumwomba Mungu, na kutekeleza kikamilifu kazi yangu. Kijuujuu, nilionekana kuwa na bidii zaidi katika kutafuta ukweli kuliko hapo awali, lakini ukifunua pazia na kuichambua, uwezo wangu wa kukubali kubaki nyuma ni kwa sababu nilikuwa na matamanio ya kuendelea siku moja. Tamaa yangu ya kuchochea kuwa bora zaidi ilikuwa ndiyo sababu sikuwa wa kutoonyesha hisia na badala yake nilifuatilia ukweli zaidi mno, lakini kunakodhaniwa kuwa ufuatiliaji wangu wa ukweli kulikuwa tu njonzi, ufuatiliaji ulio mchafu. Nilikuwa nikishiriki ufuatiliaji wa muda wa ukweli ili kutimiza madhumuni yangu ya kibinafsi. Nikifikiri nyuma kwa miaka yangu iliyotumika kufuata Mungu, nilitambua kuwa dhabihu zangu zote zilikuwa zimelipwa na sumu ya Shetani "Hakuna maumivu, hakuna faida." Hivi ndivyo ilivyonifunga pingu isiyoonekana na kunitia kujitahidi kwa ubora. Nilipokuwa na cheo tayari, nilikuwa bado nikitafuta hata cha juu zaidi; Nilipopoteza cheo changu au niliposhindwa kujiendeleza, sikuwa wa kutoonyesha hisia; Mimi bado nilionekana kuwa na hiari ya kulipa bei ili kutafuta ukweli. Hata hivyo, hii haikuwa kwa sababu nilielewa ukweli na nilikuwa tayari kujitoa mhanga kwa ajili yake. Nilitaka tu kutumia kuonekana kwa kujitoa mhanga kwa jitihada za kufanikiwa. Hapo ndipo nilipobaini hatimaye kuwa msimamo wangu wa "Hakuna maumivu, hakuna faida," ulikuwa kweli mojawapo wa sumu za Shetani zilizokuwa zikitiririka kupitia mishipa yangu. Nilikuwa nimetanganywa; sumu ilikuwa imeninyonya ubinadamu wangu wote. Nilikuwa na kiburi na mwenye tamaa bila hisia yoyote ya taswira yoyote. Mambo hayo yote yalifanyika kabisa chini ya pua langu. Kwa kweli nilifikiri kuwa matamanio yangu yalikuwa ushuhuda wa matarajio yangu. Nilidhani kuwa hali yangu ya kiburi ya kutotaka kubaki nyuma ilikuwa ishara ya motisha yangu. Niliabudu uongo wa Shetani kama ukweli na kuuona kama beji ya heshima badala ya alama ya fedheha. Nilikuwa mjinga kiasi kipi hadi kudanganyika na Shetani kiasi kile, kutojua kutofautisha kati mema na uovu? Hatimaye niliona jinsi nilivyokuwa ovyo. Nilijifunza pia jinsi Shetani ni mwenye kudhuru kwa siri na mwenye kuleta hizaya. Shetanihutumia udanganyifu spesheli kutudanganya na kutupotosha. Hutupotosha, na tunaapa uaminifu kwa mipango yake danganyifu. Hii yote hufanywa bila ujuzi wetu. Tunadhani tunatafuta ukweli na kujitolea kwa ajili ya kweli, lakini kwa kweli tunaishi katika kujidanganya. Sumu za Shetani zina nguvu kabisa! Ikiwa haingekuwa nuru yake Mungu, singewahi kamwe kuona ukweli kwamba nilikuwa nimepotoshwa na Shetani, na hakika singeweza kamwe kubaini mipango yake ya udanganyifu. Ikiwa haingekuwa nuru ya Mungu, ningeendelea kuishi chini ya jozi la Shetani, hadi wakati Shetani hatimaye anitumie mzima.
Wakati huo, nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu: “Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mtiifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu” (“Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinionyesha njia ya kutenda: Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, napaswa kumpenda na kumridhisha bila masharti na kutekeleza wajibu wangu kwa dhati. Hii ndiyo hisi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kumiliki. Huu ni ufuatiliaji ambao unaambatana na mapenzi Yake. Kuanzia siku ya leo kwenda mbele, nitafanya liwezekanalo kufuatilia ukweli. Nitategemea ukweli ili kupenya udanganyifu wa Shetani na kutupa jozi lake. Sitafuatilia tena kitu chochote cha mwili. Badala yake, nitafanya kazi kwa bidii kwa kutoonekana, kutimiza wajibu wangu kumkidhi Mungu. Hata nikiachwa bila kitu chochote mwishowe, nitaendelea kwa hiari bila majuto yoyote, kwa sababu mimi ni moja tu wa viumbe duni wa Mungu. Kumridhisha Muumba ni nia yangu moja ya kweli maishani.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni