Umeme wa Mashariki | Christian movie Video Swahili | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China" Trailer
Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.
Miaka ya hivi karibuni pia imeona sera za serikali ya CCP zikianzishwa kwa kiwango kikubwa kwa lengo la "Usimilishaji " wa Ukristo. Maelfu ya misalaba ya makanisa yamevunjwa, majengo mengi ya kanisa yambomolewa, na idadi kubwa ya Wakristo katika makanisa ya nyumbani wamekamatwa na kuteswa. Makanisa ya Kikristo nchini China hupitia mateso ya ukatili na ya umwagikaji wa damu ...
Filamu hii kwa uaminifu na bila upendeleo inanakili uzoefu halisi wa mateso waliyoyapitia Wakristo wa China katika mikono ya serikali ya CCP. Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu. Walitembea njia sahihi ya uzima, lakini kwa wayowayo walishikwa na serikali ya CCP. Baadhi yao walifungwa, wengine wakateswa kwa namna yoyote, wengine wanaishi maisha ya wakimbizi kama wametengwa na waume au wake zao na watoto wao, na wengine hata walilemazwa au kuuawa kutokana na kutendewa vibaya. Filamu hii iliyopigwa vizuri sana inajaribu kusanifu upya kilichotokea kweli wakati huo, na hutoa tafakuri ya kina ya kuingiliwa bila haya kwa imani za kidini na haki za kibinadamu za Wakristo wa China. Ni nafasi ya kuelewa maisha ya kweli ya Wakristo wa China na familia za Kikristo, pamoja na tafakuri—inayoonekana mara chache katika miaka ya hivi karibuni—ya uzoefu na hisia za Wakristo wa China ambao wameteswa kwa sababu ya imani yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni