Jumapili, 17 Desemba 2017

Upendo wa Mungu na wokovu | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho


Upendo wa Mungu na wokovu | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho


Mwenyezi Mungu alisema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho.
Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake. Imani hii haiwezi kutambulika kufikia sasa kwa watu ambao hawana utambuzi. Hata hivyo, watu watu bado wanaitaka sana. Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kuchunguza, kuuchunguza moyo na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuamsha, ili usipate kiu na kupata njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote."

Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
                    Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni