Jumapili, 12 Novemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

 Mwenyezi Mungu,Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)

 Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.
Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu. Matendo haya yanayofanywa na Mungu hayakomei tu kwenye maandalizi Yake ya mazingira kwa ajili ya watu kuendelea kuishi na riziki zao za kila siku–yana mawanda mapana zaidi kuliko hayo. Licha ya aina mbili hizi za kazi, pia Anaandaa mazingira mengi na hali kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni lazima kwa ajili ya maisha ya mwanadamu. Hii ni mada nyingine ambayo tutaijadili leo, ambayo pia inahusiana na matendo ya Mungu. Vinginevyo, kuizungumzia hapa isingekuwa na maana. Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu lakini wana maana ya moja kwa moja na ya kimafundisho ya "Mungu," ya neno hilo, au ya vipengele vyote vya kile Mungu anacho na alicho, huo sio uelewa wa kweli. Sasa, njia kwa ajili ya maarifa ya Mungu ni ipi? Ni kumjua Yeye, kujua kila kipengele Chake kupitia matendo Yake. Kwa hiyo, kinachofuata tunapaswa kushiriki kuhusu matendo ya Mungu pale alipoumba vitu vyote.
Tangu Mungu alipoviumba, kulingana na sheria ambazo Aliziamua, vitu vyote vimekuwa vikitenda kazi na vimekuwa vikiendelea kukua kwa kawaida. Chini ya uangalizi Wake, chini ya kanuni Yake, vitu vyote vimekuwa vikiendelea kwa kawaida sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu. Hakuna kitu hata kimoja kinaweza kubadilisha sheria hizi, na hakuna hata kitu kimoja kinachoweza kuziharibu sheria hizi. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu ndipo viumbe vyote vinaweza kuongezeka, na kwa sababu ya kanuni na usimamizi Wake ndipo vitu vyote vinaweza kuendelea kuishi. Hii ni kusema kwamba chini ya kanuni ya Mungu, viumbe vyote vinakuwepo, vinastawi, vinatoweka, na kuzaliwa upya kwa namna ya mpangilio. Msimu wa machipuo unapowadia, mvua ya manyunyu huleta hisia hiyo ya machipuo na kuipatia nchi unyevunyevu. Ardhi huanza kuyeyuka, majani huota na kujipenyeza juu ya udongo na miti taratibu hubadilika kuwa ya kijani. Viumbe hai hivi vyote vinaleta uzima mpya katika dunia. Hii ndiyo picha ya viumbe vyote kuwepo na kustawi. Wanyama wa kila aina pia hutoka matunduni mwao ili kupata uvuguvugu wa msimu wa machipuo na kuanza mwaka mpya. Viumbe vyote vinaota jua kwenye joto wakati wa kiangazi na kufurahia uvuguvugu unaoletwa na msimu huu. Vinakua haraka; miti, nyasi, na aina zote za mimea inakua haraka sana, kisha inachanua na kuzaa matunda. Viumbe vyote vinakuwa vimetingwa sana wakati wa kiangazi, binadamu wakiwemo. Katika msimu wa majani kupukutika, mvua inaleta utulivu wa msimu wa majani kupukutika, na aina zote za viumbe hai vinaanza kupitia uzoefu wa msimu wa kiangazi. Viumbe vyote vinazaa matunda, na binadamu pia wanaanza kuvuna aina zote za vitu kwa sababu ya msimu wa majani kupukutika kuzalisha viumbe vyote hivi, ili kuandaa chakula kwa ajili ya msimu wa baridi. Katika msimu wa baridi viumbe vyote taratibu vinaanza kupumzika katika ubaridi, kuwa kimya, na watu pia wanachukua pumziko wakati wa msimu huu. Mabadiliko haya kutoka masimu wa machipuo kwenda msimu wa kiangazi kwenda msimu wa mapukutiko na kwenda msimu wa baridi--mabadiliko haya yote yanatokea kulingana na sheria zilizoanzishwa na Mungu. Anawaongoza viumbe na binadamu kwa kutumia sheria hizi na Ameanzisha maisha yenye utajiri na ya kupendeza kwa ajili ya mwanadamu, Akiandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo yana halijoto tofautitofauti na misimu tofautitofauti. Chini ya mazingira haya yaliyopangiliwa kwa ajili ya kuendelea kuishi, binadamu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka kwa namna ya mpangilio. Binadamu hawawezi kuzibadilisha sheria hizi, na hakuna mtu hata mmoja au kiumbe ambacho kinaweza kuzivunja. Haijalishi ni mabadiliko makubwa kiasi gani yanatokea duniani, sheria hizi zinaendelea kuwepo na zipo kwa sababu Mungu yupo. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Kwa aina hii ya mpangilio, mazingira makubwa, maisha ya watu yanaendelea ndani ya sheria na kanuni hizi. Sheria hizi ziliendeleza kizazi baada ya kizazi cha watu na kizazi baada ya kizazi cha watu wameendelea kuishi ndani ya sheria hizi. Watu wamefurahia viumbe na mazingira haya ya mpangilio kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoumbwa na Mungu kwa ajili ya kizazi baada ya kizazi cha binadamu. Ingawa watu wanahisi kwamba aina hii ya sheria ni za kiasili, ingawa wanazipuuza kabisa sheria hizo, na ingawa hawawezi kuhisi kuwa Mungu ndiye anaweka utaratibu wa sheria hizi, kwamba Mungu anatawala sheria hizi, haijalishi, Mungu siku zote anajihusisha katika kazi hii isiyobadilika. Kusudi lake katika kazi hii isiyobadilika ni kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na ili binadamu waweze kuendelea.

1. Mungu Anaweka Mipaka kwa ajili ya Vitu Vyote ili Kuwalea Binadamu Wote

Leo nitazungumza juu ya mada ya jinsi aina ya kanuni hizi ambazo Mungu anazileta kwa binadamu na viumbe vyote humlea binadamu. Kwa hiyo mada hii ni nini? Ni jinsi ambavyo aina hii ya sheria ambazo Mungu amezileta kwa viumbe vyote humlea binadamu. Hii ni mada kubwa, kwa hiyo tunaweza kuigawanya katika sehemu kadhaa na kuzijadili moja baada ya nyingine ili ziweze kufafanuliwa vizuri kwenu. Kwa njia hii itakuwa rahisi kwenu kupata maana na taratibu mnaweza kuielewa.
Kwanza, Mungu alipoviumba vitu vyote, Aliweka mipaka kwa ajili ya milima, tambarare, majangwa, vilima, mito, na maziwa. Duniani kuna milima, tambarare, majangwa, vilima, vilevile vyanzo mbalimbali vya maji–haya yote ni nini? Je, hayo si mandhari tofautitofauti? Mungu aliweka mipaka kati ya mandhari haya yote tofautitofauti. Tunapozungumza juu ya kuweka mipaka, je, hiyo inamaanisha nini? Ina maana kwamba milima ina mipaka yake, tambarare zina mipaka yake, majangwa yana mawanda fulani, na vilima vina eneo mahususi. Pia kuna kiwango mahususi cha vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Yaani, Mungu alipoumba vitu vyote aligawanya kila kitu vizuri kabisa. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha mlima ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha tambarare ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Alipokuwa anaumba viumbe vyote pia Aliamua mawanda ya jangwa, vilevile mawanda ya vilima na uwiano wao, na vile vilivyopakana navyo–pia Aliamua yote haya. Aliamua mawanda ya mito na maziwa Alipokuwa anaviumba–vyote vina mipaka yao. Kwa hiyo ina maana gani tunaposema "mipaka"? Tulizungumza tu kuhusu ambavyo utawala wa Mungu kwa vitu vyote unavyoanzisha sheria kwa viumbe vyote. Kwa mfano, mawanda na mipaka ya milima havitaongezeka au kupungua kwa sababu ya mzunguko wa dunia au muda kupita. Hii haibadiliki: Hii "isiyobadilika" ni kanuni ya Mungu. Kwamaeneo ya tambarare, mawanda yao, kile kilichopakana nayo, hii imewekwa na Mungu. Yana mipaka, na tuta haliwezi kutokea tu bila mpangilio, katikati ya tambarare. Tambarare haiwezi tu kubadilika na kuwa mlima–hii haitatokea. Sheria na mipaka tuliyoizungumzia inarejelea hili. Kwa jangwa, hatutataja wajibu wa jangwa au mandhari nyingineyo au eneo la kijiogarafia hapa, ni mipaka yake tu. Chini ya kanuni ya Mungu mawanda ya jangwa nayo pia hayatapanuka. Hii ni kwa sababu Mungu amelipatia sheria yake, mawanda yake. Eneo lake ni kubwa kiasi gani na wajibu wake ni upi, kile kilichopakana nalo, na lipo mahali gani–hii imeshawekwa na Mungu tayari. Halitazidisha mawanda yake, kuhamisha sehemu yake, na halitaongeza eneo lake kiholela tu. Ingawa mtiririko wa maji kama vile mito na maziwa yote yapo katika mpangilio na mwendelezo, hayajawahi kwenda nje ya mawanda yao au kwenda zaidi ya mipaka yao. Yote yanafuata mwelekeo mmoja kwa namna ya mpangilio, yakitiririka kuelekea mwelekeo yanaopaswa kwenda. Kwa hiyo chini ya sheria ya kanuni ya Mungu, hakuna mto au ziwa ambalo litakauka kiholela tu, au kubadilisha mwelekeo au kiwango cha kutiririka kwake kiholela tu kwa sababu ya mzunguko wa dunia au kupita kwa muda. Hii yote ipo ndani ya maarifa ya Mungu, ndani ya kanuni Yake. Hiyo ni sawa na kusema, viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu katikati ya binadamu vina sehemu zao, maeneo yao, na mawanda yao yasiyobadilika. Yaani, Mungu alipoviumba viumbe vyote, mipaka yao ilianzishwa na hii haiwezi kugeuzwa kiholela tu, kufanywa upya au kubadilishwa. "Kiholela" inamaanisha nini? Ina maana kwamba havitahama, kupanuka, au kubadilisha umbo lao asilia bila mpangilio kwa sababu ya hali ya hewa, halijoto, au kasi ya mzunguko wa dunia. Kwa mfano, mlima una kimo fulani, kitako chake ni cha eneo fulani, una mwinuko fulani, na una kiasi fulani cha uoto. Hii yote imepangwa na kukokotolewa na Mungu na kimo au eneo lake halitabadilika kiholela. Kwa tambarare, idadi kubwa ya binadamu wanaishi katika tambarare, na hakuna mabadiliko ya hali ya hewa yatakayoathiri maeneo yao au thamani ya uwepo wao. Sio hata kile ambacho kimejumuishwa katika mandhari haya na mazingira ya kijiografia ambayo yaliumbwa na Mungu yatabadilika kiholela. Kwa mfano, vipengele vya jangwa ni vipi, ni aina gani ya madini yaliyopo chini ya ardhi, yanajumuisha mchanga kiasi gani na rangi ya mchanga, upana wake–haya hayatabadilika kiholela. Kwa nini hayatabadilika kiholela? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Ndani ya mandhari haya yote tofautitofauti na mazingira ya kijiogorafia yaliyoumbwa na Mungu, Anasimamia kila kitu kwa njia iliyopangwa na kwa mpangilio. Kwa hiyo mazingira haya yote ya kijiografia bado yapo kwa miaka elfu kadhaa, makumi elfu ya miaka baada ya kuwa yameumbwa na Mungu. Bado yanatimiza kila wajibu wao. Ingawa wakati wa vipindi fulani volkano hulipuka, wakati wa vipindi fulani matetemeko ya ardhi hutokea, na kuna mabadiliko makubwa ya ardhi, hakika Mungu hataruhusu aina yoyote ya mandhari kupoteza kazi yake ya asili. Ni kwa sababu tu ya usimamizi huu unaofanywa na Mungu, utawala Wake na udhibiti wa sheria hizi, kwamba yote haya–yote haya yanayofurahiwa na binadamu na kuonwa na binadamu–yanaweza kuendelea kuishi duniani kwa njia ya mpangilio. Sasa kwa nini Mungu anasimamia mandhari yote haya yaliyopo duniani kwa njia hii? Kusudi ni ili viumbe hai vinavyoendelea kuishi katika mazingira mbalimbali ya kijiografia yote yatakuwa na mazingira imara, na kwamba wataweza kuendelea kuishi na kuongezeka katika mazingira hayo imara. Viumbe vyote hivi–vile vinavyotembea na vile ambavyo havitembei, vile ambavyo vinapumua kupitia pua zao na vile ambavyo havipumui—vinaunda mazingira ya tofauti kabisa kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ni aina hii tu ya mazingira ndiyo inaweza kulea kizazi baada ya kizazi cha binadamu, na ni aina hii tu ya mazingira inaweza kuruhusu binadamu kuendelea kuishi kwa amani, kizazi baada ya kizazi.
Mmeona nini kutokana na kile ambacho nimekizungumzia? Ni kwamba sheria za Mungu katika utawala wake wa vitu vyote ni muhimu sana–muhimu sana! Je, masharti ya awali ni yapi kwa viumbe vyote kukua ndani ya sheria hizi? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu. Ni kwa sababu ya kanuni Yake ndipo viumbe vyote vinafanya kazi zao ndani ya kanuni Yake. Kwa mfano, milima inalea misitu, halafu misitu inalea na kuwalinda ndege mbalimbali na wanyama wanaoishi ndani yake. Tambarare ni jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya binadamu kupanda mazao vilevile kwa ajili ya ndege na wanyama mbalimbali. Zinaruhusu idadi kubwa ya binadamu kuishi katika ardhi tambarare na kutoa hali isiyo na taabu katika maisha ya binadamu. Na tambarare pia zinajumuisha ukanda wa mbuga—malundo ya ukanda wa mbuga. Ukanda wa mbuga ni uoto wa nchi. Unalinda ardhi na kuwalea ng'ombe, kondoo na farasi wanaoishi katika ukanda wa mbuga. Jangwa pia linafanya kazi yake. Sio sehemu kwa ajili ya binadamu kuishi; jukumu lake ni kufanya hali ya hewa ya unyevunyevu kuwa kavu. Kutiririka kwa mito na maziwa kunaleta hali isiyo ya usumbufu kwa ajili ya watu kunywa maji na kwa mahitaji ya viumbe vyote. Vyovyote vile yanavyotiririka, watu watakuwa na maji kwa ajili ya kunywa. Hii ni mipaka iliyochorwa na Mungu kwa ajili ya mandhari mbalimbali. Kwa sababu ya mipaka hii ambayo Mungu ameichora, mandhari mbalimbali yamezalisha mazingira tofautitofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na mazingira haya kwa ajili ya kuendelea kuishi yamekuwa na hali isiyokuwa na usumbufu kwa ajili ya aina tofautitofauti ya ndege na wanyama na vilevile kuleta nafasi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kutokana na hili, mipaka kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa viumbe hai mbalimbali imeendelezwa. Hiki ndicho tutakachokwenda kuzungumzia baadaye.
Pili, ni aina gani ya mazingira ambamo ndege na wanyama na wadudu wanaishi? Licha ya kuanzisha mipaka kwa ajili ya mazingira mbalimbali ya kijiografia, pia Aliweka mipaka kwa ajili ya ndege na wanyama, samaki, wadudu mbalimbali, na mimea yote. Pia alianzisha sheria. Kwa sababu ya tofauti za mazingira mbalimbali ya kijiografia na kwa sababu ya uwepo wa mazingira tofauti ya kijiografia, aina tofautitofauti za ndege na wanyama, samaki, wadudu, na mimea vina mazingira tofauti kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ndege na wanyama na wadudu wanaishi miongoni mwa mimea, samaki wanaishi majini, na mimea inakua kwenye nchi kavu. Nchi kavu inajumuisha nini? Maeneo mbalimbali kama vile milima, tambarare, na vilima. Kwa hiyo, ndege na wanyama wana makazi yao yasiyobadilika na hawatazungukazunguka mahali popote tu. Makazi yao ni misitu na milima. Ikiwa, siku moja makazi yao yataharibiwa, mpangilio huu utakuwa machafuko. Mara tu mpangilio huo unapokuwa machafuko, madhara yake ni yapi? Wa kwanza kuumizwa ni akina nani? (Binadamu.) Ni binadamu! Ndani ya sheria na mipaka hii ambayo Mungu ameianzisha, je, mmewahi kuona tukio lolote la ajabu? Kwa mfano, tembo wakizungukazunguka tu jangwani kwa kawaida. Mmewahi kuona tukio hilo? Kama ingekuwa hivyo, lingekuwa ni tukio la ajabu sana. Hii ni kwa sababu mazingira ambamo tembo wanaishi ni msitu, na msitu ni mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliwaandalia. Ana mazingira yake kwa ajili ya kuendelea kuishi na ana makazi yake yasiyobadilika, sasa kwa nini atangetange? Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuona simba na duma wakizungukazunguka baharini? Makazi ya simba na duma ni msituni na kwenye milima. Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kumwona nyangumi au papa kutoka baharini wakitembea jangwani? Nyangumi na papa makazi yao ni baharini na hawawezi kuishi kwenye nchi kavu. Katika mazingira ya kuishi ya binadamu, je, kuna watu ambao wanaishi pamoja na dubu wa kahawia? Je, kuna watu ambao siku zote wamezungukwa na tausi au ndege wengineo, ndani au nje ya makazi yao? Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kumwona ng'ombe au kondoo msituni? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaona tai au bata bukini wa mwituni wakicheza na tumbili? Kama mlishawahi kuona, basi haya yatakuwa ni matukio ya pekee sana. Hii ndio sababu Ninazungumza juu ya vitu hivi ambavyo ni matukio ya pekee machoni mwenu. Ni kuwafanya muelewe kwamba vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu–haijalishi kama vimewekwa katika sehemu moja au vina pumzi na vinaweza kutembea–vyote vina sheria zao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Zamani kabla Mungu hajaumba viumbe hai hivi Alikuwa ameviandalia makazi yao, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai hivi vilikuwa na mazingira yao yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi, chakula chao, makazi yao yasiyobadilika, sehemu zao zisizobadilika zinazowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, maeneo yenye halijoto inayowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa njia hiyo wasingezungukazunguka au kuhafifisha hali ya mwanadamu kuendelea kuishi au kuathiri maisha yao. Hivi ndivyo Mungu anavyosimamia viumbe vyote. Ni kumwandalia binadamu mazingira mazuri kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai chini ya viumbe vyote kila kimoja kina chakula kinachokimu maisha ndani ya mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa chakula hicho, vinajifunga katika mazingira yao ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi; vimejifunga katika mazingira hayo. Katika aina hiyo ya mazingira bado vinaendelea kuishi, kuzaliana, na kuendelea kulingana na sheria za Mungu alizozianzisha kwa ajili yao. Kwa sababu ya aina hizi za sheria, kwa sababu ya majaaliwa ya Mungu, viumbe vyote vinaingiliana na binadamu kwa upatanifu, na binadamu na viumbe vyote vinategemeana.
Mungu aliviumba viumbe vyote na akaanzisha mipaka kwa ajili yao na miongoni mwao akalea aina zote za viumbe hai. Huku viumbe vyote vikiwa vinalea aina zote za viumbe hai, pia Aliandaa mbinu tofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, hivyo unaweza kuona kwamba binadamu hawana njia moja tu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Pia hawana aina moja tu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hapo kabla tulizungumza juu ya Mungu kuandaa aina mbalimbali za chakula na vyanzo vya maji kwa ajili ya binadamu, kitu ambacho ni muhimu sana kufanya uhai wa binadamu katika mwili kuendelea. Hata hivyo, miongoni mwa binadamu huyu, sio watu wote wanaishi kwa kula nafaka. Watu wana mbinu tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa sababu ya tofauti za mazingira ya kijiografia na mandhari. Mbinu hizi za kuendelea kuishi zote zimeandaliwa na Mungu. Hivyo si binadamu wote wanajihusisha na kilimo. Yaani, si watu wote wanapata chakula chao kwa kulima mazao. Hii ni hoja ya tatu ambayo tutakwenda kuizungumzia. Mipaka imetengenezwa kutokana na mitindo mbalimbali ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ni aina nyingine ipi ya mtindo wa maisha ambayo binadamu wanayo? Ni vyanzo gani vingine vya vyakula ambavyo binadamu wanavyo? Kuna aina za msingi kadhaa:
Ya kwanza ni mtindo wa maisha wa uwindaji. Kila mmoja anajua kuhusu hilo. Je, wowote kati yenu wanawinda kwa ajili ya kuishi? Nyinyi nyote ni watu wa kisasa—hamjui jinsi ya kuwinda, jinsi ya kushika bunduki. Vyanzo vyenu vya chakula vinatoka ardhini. Watu wanaoishi kwa kuwinda wanakula nini? (Windo.) Wanakula ndege na wanyama wa mwituni. "Windo" ni neno la kisasa. Wawindaji hawaoni kwamba ni mchezo, wanaona kama chakula, kama riziki yao ya kila siku. Kwa mfano, wangefurahi endapo wangepata paa. "Vizuri, paa huyu anatosha kwa chakula kwa ajili ya familia kwa siku kadhaa." Wanapopata paa huyu ni sawa tu na mkulima kupata mazao kutoka ardhini. Mkulima hupata mazao kutoka ardhini, na anapoona mazao yake anakuwa na furaha na anahisi amani. "Kwa sasa kuna kitu cha kula; hatuna haja ya kuogopa kuwa na njaa." Familia haitakuwa na njaa ya mazao ya kula. Moyo wake una amani na anahisi kuridhika. Na mwindaji pia anahisi amani na kuridhika akiangalia kile ambacho amekamata kwa sababu hana haja ya kuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula. Kuna kitu cha kula kwa ajili ya mlo unaofuata, hakuna haja ya kuwa na njaa. Huyu ni mtu ambaye anawinda kwa ajili ya kuishi. Ni mazingira ya aina gani ambayo mara nyingi watu wanaoishi kwa kutegemea uwindaji wanaishi? Wanaishi katika misitu ya milima. Kwa kiasi kikubwa hawalimi au kupanda mazao; wanaishi katika misitu ya milima. Je, kuna ardhi inayolimika katika misitu ya milima? Sio rahisi kupata ardhi inayolimika, kwa hiyo wanaishi kwa kutegemea viumbe hai mbalimbali, aina mbalimbali za mawindo. Hii ni aina ya kwanza ya mtindo wa maisha ambao ni tofauti na ule wa watu wa kawaida.
Aina ya pili ni mtindo wa maisha wa ufugaji. Wale ambao wanafuga kwa ajili ya kuishi hawalimi, sasa wanafanya nini? Wanafuga tu? Ikiwa yeyote miongoni mwenu hapa ni mtu wa Mongolia, mnaweza kuzungumza kidogo kuhusu mtindo wenu wa maisha ya kuhamahama. (Kwa sehemu kubwa, tunafuga ng'ombe na kondoo kwa ajili ya kuishi, hatulimi, na msimu wa baridi tunawachinja na kuwala mifugo wetu. Chakula chetu kikuu kinatokana na nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, tunakunywa chai ya maziwa, tunakula mchele uliokaushwa, na mbogamboga chache sana. Sasa aina zote za usafiri hazina usumbufu na tuna aina zote za mbogamboga na nafaka. Wamongolia hunywa chai ya maziwa, na Watibeti hunywa chai ya siagi. Ingawa wafugaji wanatingwa misimu yote minne, lakini wanakula vizuri. Hawapungukiwi na maziwa, bidhaa za maziwa, au nyama. Walikuwa wanaishi katika viduku lakini sasa wote wanajenga nyumba.) Chakula cha msingi cha watu wa Mongolia ni kula nyama ya ng’ome na nyama ya kondoo, kunywa maziwa, na kuendesha farasi kuenda kulisha wanyama wao. Huu ni mtindo wa maisha wa mfugaji. Mtindo wa maisha wa mfugaji sio mbaya–wanaendesha madume ya ng'ombe na farasi uwandani na upepo kwenye nywele zao, jua usoni pao, na hawana msongo wa mawazo juu ya maisha ya kisasa. Siku nzima wanaona tu upana wa wingu la bluu na tambarare za majani. Watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi wote wanaishi kwenye uwanda wa mbuga na wanaweza kuendelea na mtindo wao wa maisha ya kuhamahama kwa kizazi baada ya kizazi. Ingawa maisha katika uwanda wa mbuga ni ya upweke kidogo, pia ni maisha ya furaha. Si mtindo mbaya wa maisha!
Aina ya tatu ni mtindo wa maisha ya uvuvi. Kuna sehemu ndogo ya binadamu wanaoishi pembezoni mwa bahari au kwenye visiwa vidogo. Wamezungukwa na maji, wakikabiliana na bahari. Aina hii ya watu hufanya uvuvi kwa ajili ya kuishi. Watu hawa wanaofanya uvuvi kwa ajili ya kuishi hutegemea nini kwa ajili ya chakula? Chanzo cha chakula chao ni nini? Ni aina zote za samaki na vyakula vya baharini? Wakati Hong Kong ilikuwa ni kijiji kidogo tu cha uvuvi, watu ambao waliishi pale waliweza kuvua kwa ajili ya kuishi. Hawakulima–walikwenda kuvua kila siku. Chakula chao cha msingi kilikuwa ni aina mbalimbali za samaki, nyama, na vyakula vya baharini. Mara chache waliweza kuuza kiasi cha samaki kwa kubadilishana na mchele, unga, na mahitaji ya kila siku. Watu wanaoishi kwa kutegemea uvuvi wote wanaishi pembezoni mwa bahari, na baadhi wanaishi kwenye mashua. Huu ni mtindo tofauti wa maisha wa watu wanaoishi pembezoni mwa maji. Wale wanaoishi pembezoni mwa maji wanategemea uvuvi; ni chanzo cha riziki yao vilevile chanzo chao cha chakula.
Licha ya wale ambao hulima kwa ajili ya kuishi, kimsingi kuna aina tatu tofauti za mtindo wa maisha zilizotajwa hapo juu. Licha ya wale ambao wanaishi kwa kutegemea ufugaji, uvuvi, na kuwinda, idadi kubwa ya watu hulima kwa ajili ya chakula. Na watu wanaolima kwa ajili ya kuishi wanahitaji nini? Wanahitaji udongo. Wale ambao wanategemea kulima kwa ajili ya kupata riziki zao kimsingi wanapanda mazao kwa vizazi. Wanapata chakula chao kutoka ardhini. Ama wanapanda mbogamboga, matunda au nafaka, wote wanapata mahitaji yao ya kila siku kutoka ardhini.
Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Hii ni sawa na kusema, ikiwa wawindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, basi wasingekuwa tena na riziki yao. Hivyo ikiwa watu ambao wanategemea uwindaji wangepoteza milima ya misitu na wasiwe tena na ndege na wanyama, wasingekuwa tena na chanzo cha riziki yao. Aina ya mbari hiyo ingeelekea upande gani; aina ya watu hao wangeelekea wapi? Uwezo wa kuendelea kuishi au la ni kiwango kisichojulikana na wangeweza tu kutoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao–wanategemea uwanda wa mbuga. Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo wao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi–uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng'ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama wangekuwa na riziki gani? Wasingekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Mara tu tatizo linapotokea na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi–zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, matokeo yake yangekuwa nini? Wasingeweza kupanda vitu, wasingeweza kupata vyakula vyao kutoka katika mimea. Matokeo yake yangekuwa ni nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali ya kiikolojia. Ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira–ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.
Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingewea kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo. Kwa aina hiyo ya mazingira yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni ya kufaa na yapo katika mpangilio, aina zote za watu duniani, aina zote za jamii zinaweza kuishi ndani ya mawanda yao husika. Hakuna anayeweza kwenda zaidi ya mawanda haya au mipaka hii kwa sababu ni Mungu ambaye ameichora. Kwa nini Mungu aichore kwa namna hii? Hii ni muhimu sana kwa binadamu wote–ni muhimu sana! Mungu alichora mawanda ya kila aina ya kiumbe hai na aliweka mbinu ya kuendelea kuishi kwa kila aina ya binadamu. Pia aligawanya aina mbalimbali za watu na jamii mbalimbali duniani na akaweka mawanda yao. Hiki ndicho tunachotaka kujadili wakati ujao.
Nne, Mungu alichora mipaka kati ya jamii za rangi tofautitofauti. Duniani kuna watu weupe, watu weusi, watu wa kahawia na watu wa njano. Hawa ni aina tofuati za watu. Mungu pia aliweka mawanda kwa ajili ya maisha ya aina hizi tofauti za watu, na bila kutambua, watu wanaishi ndani ya mazingira yao stahiki kwa kuendelea kuishi chini ya usimamizi wa Mungu. Hakuna anayeweza kwenda nje ya hapa. Kwa mfano, jamii ya watu weupe–yaani, wazungu–ni maeneo gani ambayo wanaishi kwa kiasi kikubwa? Kwa kiasi kikubwa wanaishi Ulaya na nchi za Marekani. Watu weusi kimsingi wanaishi Afrika. Na watu wa rangi ya kahawia wanaishi ndani ya eneo gani? Kimsingi ni Asia ya Kusinimashariki kama vile Thailand, India, Myanmar, Vietnam na Laos. Yaani ukanda wa Asia ya Kusinimashariki. Watu wa njano kimsingi wanaishi Asia, yaani, China, Japan, Korea ya Kusini na nchi nyinginezo kama hizo. Mungu amegawanya aina hizi tofautitofauti za jamii kwa usawa kiasi kwamba jamii hizi tofautitofauti zimegawanywa katika sehemu tofautitofauti za dunia. Katika sehemu tofautitofauti hizi za dunia, Mungu aliandaa zamani sana mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yanayofaa kwa ajili ya kila jamii tofauti ya binadamu. Ndani ya aina hizi za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi, Mungu amewaandalia rangi na vijenzi vya udongo. Vijenzi katika miili ya watu weupe na miili ya watu weusi havifanani, na pia ni tofauti na vijenzi vya miili ya watu wa rangi nyinginezo. Mungu alipoumba viumbe vyote, tayari Alikuwa ameandaa mazingira ya namna hiyo kwa ajili ya kuendelea kuishi. Lengo Lake katika hili lilikuwa kwamba pale ambapo aina hiyo ya watu inaanza kuongezeka, watakapoanza kuongezeka kwa idadi, wangeweza kuwekwa ndani ya mawanda hayo. Kabla Mungu hajawaumba binadamu alikuwa amekwishatafakari yote–Angeweza kutoa eneo fulani kwa watu weupe na kuwaruhusu kuliendeleza na kuendelea kuishi. Kwa hiyo Mungu alipokuwa anatengeneza dunia tayari Alikuwa na mpango, alikuwa na nia na kusudi katika kile alichokuwa anakiweka katika kipande hicho cha ardhi, na kile ambacho kingelelewa katika kipande hicho cha ardhi. Kwa mfano, Mungu zamani sana aliandaa mlima upi, tambarare ngapi, vyanzo vya maji vingapi, ni aina gani ya ndege na wanyama, samaki gani, na mimea gani ingeweza kuwepo katika ardhi hiyo. Alipokuwa anaandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina ya binadamu, kwa ajili ya jamii, Mungu aliangalia vipengele vingi vya masuala: mazingira ya kijiografia, vijenzi vya udongo, aina ya ndege na wanyama, ukubwa wa aina tofautitofauti za samaki, vijenzi katika samaki, ubora tofauti wa maji, vilevile aina tofauti za mimea... Mungu alikuwa ameandaa yote hayo zamani sana. Aina hiyo ya mazingira ni mazingira ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaumba na kuyaandaa kwa ajili ya watu weupe.
Mnapaswa kuweza kuona kwamba Mungu alipoviumba viumbe vyote, Alitafakari sana. Alifanya vitu kwa mpango. Sasa mnaweza kuona hilo, sio? (Fikira za Mungu kwa aina mbalimbali za watu zilikuwa ni za uangalifu sana. Kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina tofautitofauti za binadamu, aliandaa aina za ndege na wanyama na aina za samaki, milima mingapi na tambarare ngapi zitakuwepo. Yote haya yalifikiriwa kwa uangalifu sana na kwa usahihi.) Kwa mfano, chakula wanachokula wazungu hasa ni kipi? (Kwa kiasi kikubwa ni vyakula vyenye kiwango cha juu cha protini–aina tofautitofauti za nyama, bidhaa za maziwa, na vyakula vinavyotokana na ngano.) Vyakula ambavyo watu weupe wanakula ni tofauti sana na vyakula ambavyo watu wa Asia wanakula. Vyakula vikuu ambavyo watu weupe wanakula hasa ni nyama, mayai, maziwa, na kuku. Nafaka kama vile mkate na mchele kwa ujumla sio chakula kikuu ambacho kinawekwa pembeni mwa sahani. Hata pale wanapokula kachumbari, ambayo imetengenezwa na mbogamboga, wanaweka kiasi cha nyama ya kukaanga au kuku ndani yake. Hata kama wanakula vyakula vinavyotokana na ngano, wanaongeza siagi, mayai, au nyama kwenye chakula hicho. Hiyo ni kusema, vyakula vyao vikuu havijumuishi hasa vyakula vinavyotokana na ngano au mchele; wanakula sana nyama na siagi. Mara nyingi wanakunywa maji ya barafu kwa sababu wanakula vyakula vyenye kalori ya juu sana. Wanapokula chakula, kabla chakula hakijawekwa mezani kila mtu anakunywa maji ya barafu kwanza, kwa hiyo watu weupe ni wenye afya kweli. Hivi ndivyo vyanzo vya maisha yao, mazingira yao kwa ajili ya kuishi yaliandaliwa na Mungu kwa ajili yao, yanawafanya wawe na aina hiyo ya mtindo wa maisha. Mtindo huo wa maisha ni tofuti na mitindo ya maisha ya watu wa rangi nyingine. Hakuna baya au zuri katika mtindo huu wa maisha–ni wa kuzaliwa, uliamuliwa kabla na Mungu na kwa sababu ya kanuni ya Mungu na mipangilio Yake. Aina hii ya mbari ina mtindo fulani wa maisha na vyanzo fulani vya riziki zao kitu ambacho ni kwa sababu ya mbari yao, vilevile ni kwa sababu ya mazingira kwa ajili ya kuendealea kuishi yaliyoandaliwa na Mungu kwa ajili yao. Mngeweza kusema kwamba mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili ya watu weupe na chakula cha kila siku wanachokipata kutoka katika mazingira hayo ni kingi na kimejaa tele.
Mungu pia aliandaa mazingira faafu kwa ajili ya mbari nyingine kuendelea kuishi. Pia kuna watu weusi–watu weusi wanapatikana wapi? Hasa wanapatikana katikati na kusini mwa Afrika. Mungu aliwaandalia nini kwa ajili ya kuishi katika aina hiyo ya mazingira? Misitu ya kitropiki, aina zote za ndege na wanyama, pia majangwa, na aina zote za mimea ambayo inaambatana nao. Wana vyanzo vya maji, riziki zao, na chakula. Mungu hakuwabagua. Bila kujali kile walichowahi kukifanya, kuendelea kuishi kwao hakujawahi kuwa tatizo. Pia wanachukua mahali fulani maalumu na eneo fulani katika sehemu ya dunia.
Sasa, hebu tuzungumze kidogo kuhusu watu wanjano. Watu wa njano hasa wanapatikana nchi za Mashariki. Kuna tofauti gani kati ya mazingira na sehemu za kijiografia za nchi za Mashariki na nchi za Magharibi? Katika nchi za Mashariki, eneo kubwa la ardhi ni la rutuba, na zina hazina kubwa ya vitu na madini. Yaani, aina zote za rasilimali za juu ya ardhi na za chini ya ardhi zimejaa tele. Na kwa kundi hili la watu, kwa mbari hii, Mungu pia aliandaa udongo, hali ya hewa inayofanana nao, na mazingira mbalimbali ya kijiografia ambayo yanawafaa. Ingwa kuna tofauti kubwa kati ya mazingira hayo ya kijiografia na mazingira ya nchi za Magharibi, chakula cha lazima cha watu, riziki, na vyanzo kwa ajili ya kuendelea kuishi viliandaliwa na Mungu. Ni mazingira tofauti tu kwa ajili ya kuishi kuliko yale ambayo watu weupe wanayo katika nchi za Magharibi. Lakini kitu kimoja ni kipi ambacho Ninahitaji kuvuta usikivu wenu, ambacho Ninahitaji kuwaambia? Idadi ya mbari ya Mashariki kiasi fulani ni kubwa, hivyo Mungu aliongeza vipengele vingi katika kipande hicho cha nchi ambavyo ni tofauti na vya Magharibi. Katika upande huo wa dunia, Aliongeza mandhari mengi mbalimbali na aina zote za vitu vingi. Huko rasilimali za asili ni tele; mandhari pia yanatofautiana na anuwai, yanatosha kwa ajili ya kulea idadi kubwa ya mbari ya Mashariki. Kitu fulani ambacho ni tofauti na Magharibi ni kwamba Mashariki–kutoka kusini kwenda kaskazini, kutoka mashariki kwenda magharibi–hali ya hewa ni nzuri kuliko ya Magharibi. Misimu minne imeoneshwa kinaganaga, hali ya joto ni nzuri, rasilimali za asili zipo tele, mazingira ya asili na aina za mandhari ni mazuri zaidi kuliko ya Magharibi. Kwa nini Mungu alifanya hivi? Mungu alitengeneza uwiano razini kabisa kati ya watu weupe na watu wa njano. Hii inamaanisha nini? Kila kipengele ambacho watu weupe wanaweza kukifurahia ni kizuri zaidi kuliko kile ambacho watu wa njano wanaweza kukifurahia. Chakula chao na vitu ambavyo wanatumia ni bora zaidi. Hata hivyo, Mungu habagui mbari yoyote. Mungu aliwapatia watu wa njano mazingira mazuri na bora zaidi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hii ni uwiano. Kwa hiyo sasa mnaelewa, sio?
Mungu ameamua kabla ni aina gani ya watu waishi katika sehemu ipi ya dunia na binadamu hawawezi kwenda nje ya mawanda haya. Hili ni jambo la ajabu! Hata kama kuna vita au uvamizi katika enzi mbalimbali au nyakati fulani, vita hivi, uvamizi huu, hakika hauwezi kuharibu mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaamua kabla kwa ajili ya kila mbari. Yaani, Mungu amewaweka aina fulani ya watu katika eneo fulani la dunia na hawawezi kwenda nje ya mawanda hayo. Hata kama watu wana lengo la kubadilisha au kuongeza eneo lao, bila ruhusa ya Mungu, hii itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Kwa mfano, watu weupe walitaka kuongeza maeneo yao na wakazitawala kwa mabavu baadhi ya nchi. Wajerumani walivamia baadhi ya nchi, Uingerza waliitwaa India. Matokeo yalikuwa ni nini? Mwishowe walishindwa. Tunaona nini kutokana na kushindwa huku? Kile ambacho Mungu amekiamua kabla hakiwezi kuharibiwa. Kwa hiyo, haijalishi ni nguvu kubwa kiasi gani ambayo umeweza kuiona katika upanuzi wa Uingereza, mwishowe matokeo ni kwamba bado walitakiwa kuondoka na ardhi hiyo bado ni ya India. Wale ambao wanaishi katika ardhi hiyo bado ni Wahindi, na si Waingereza. Hii ni kwa sababu ni kitu ambacho Mungu haruhusu. Baadhi ya wale ambao wanatafiti historia au siasa wametoa tasnifu juu ya hili. Wanatoa sababu kwa nini Uingereza ilishindwa, wanasema kwamba pengine ilikuwa ni kwa sababu mbari fulani isingeweza kushindwa, au pengine ni kwa sababu ya sababu nyinginezo za kibinadamu... Hizi sio sababu za kweli. Sababu ya kweli ni kwa sababu ya Mungu–Haruhusu hilo. Mungu anaamua mbari waishi katika nchi fulani na Anawaweka hapo, na kama Mungu hawaruhusu kuhama hawataweza kuhama kamwe. Ikiwa Mungu ataamua mawanda kwa ajili yao, wataishi ndani ya mawanda hayo. Binadamu hawezi kuvunja bure au kwenda nje ya mawanda haya. Hii ni hakika. Haijalishi nguvu za wavamizi ni kubwa kiasi gani, au jinsi gani wale wanaovamiwa ni dhaifu, mafanikio yao mwishowe yanamtegemea Mungu. Ameshaliamua hili tayari na hakuna anayeweza kulibadilisha. Hivi ndivyo Mungu alivyogawanya mbari mbalimbali. Ni kazi gani ambayo Mungu amefanya kuzigawanya mbari? Kwanza, aliandaa mazingira makubwa ya kijiografia, mazingira makubwa, akatoa maeneo tofautitofauti kwa ajili ya watu, kisha kizazi baada ya kizazi kuendelea kuishi pale. Hii imeamuliwa–mawanda ya kuendelea kuishi kwao yameamuliwa. Na milo yao, maisha yao, kile wanachokula, kile wanachokunywa, riziki zao–Mungu aliamua hayo yote zamani sana. Na Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, Alifanya maandalizi tofautitofauti kwa ajili ya aina tofauti za watu: Kuna vijenzi tofautitofauti vya udongo, hali ya hewa tofauti, mimea tofauti, na mazingira tofauti ya kijiografia. Maeneo tofautitofauti yana hata ndege na wanyama tofauti, maji tofauti yana aina tofauti za samaki na bidhaa za majini, na hata aina ya wadudu inaamuliwa na Mungu. Kwa mfano, kuna magipai (ndege wa jamii ya kunguru) Asia lakini pengine hawapatikani Marekani. Hii ni maalumu sana. Na shorewanda wa Marekani ni tofauti na shorewanda wa China Bara. Vitu ambavyo vinakua katika bara la Marekani vyote ni vikubwa sana, virefu sana na vyenye nguvu sana. Mizizi ya miti msituni yote haina kina kirefu kabisa, lakini inakua mirefu sana. Inaweza kurefuka hadi kufikia zaidi ya futi mia moja, lakini miti katika misitu ya Asia kwa kiasi kikubwa si mirefu kiasi hicho. Nina uhakika wote mmekwishawahi kusikia juu ya mimea ya mshubiri. Japan ni midogo sana, miembamba sana, lakini mimea ya mshubiri Marekeni ni mikubwa sana. Hii ni tofauti. Ni aina ile ile ya mmea ikiwa na jina lile lile, lakini katika bara la Marekani ni mkubwa kiasi–kweli kuna tofauti. Tofauti katika vipengele hivi tofautitofauti zinaweza zisionekane au kufahamika kwa watu, lakini Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, alivionyesha kinaganaga na aliandaa mazingira tofauti ya kijiografia, mandhari tofauti, na viumbe hai tofauti kwa ajili ya mbari mbalimbali. Kwa sababu Mungu aliumba aina tofautitofauti za watu, Anajua kile ambacho kila mmoja anahitaji na mitindo yao ya maisha ni nini. Kwa hiyo, kile ambacho Mungu aliumba ni chema sana. Sasa mnapaswa kuwa mmeelewa.
Baada ya kuzungumza juu ya baadhi ya vitu hivi, sasa mna uelewa fulani wa mada kuu ambayo tumeijadili hivi punde? Je, mmeielewa kwa kiasi fulani? Kuna sababu ambayo nimeongea kuhusu mambo haya ndani ya mada pana–sasa mnapaswa kuwa mmeelewa angalau kwa muhtasari. Mnaweza kuniambia mmeelewa kwa kiasi gani. (Binadamu wote wamelelewa kwa sheria tu ambazo ziliamuliwa na Mungu kwa ajili ya vitu vyote. Mungu alipokuwa anaamua sheria hizi, Aliandaa mbari tofautitofauti zikiwa na mazingira tofauti, mitindo tofauti ya maisha, vyakula tofauti, na hali ya hewa na halijoto tofauti. Hii ilikuwa hivyo ili binadamu wote waweze kuishi duniani na kuendelea kuishi. Kutokana na hili naweza kuuona mpango wa usimamizi wa Mungu na mipango yake angalifu na sahihi vilevile hekima na ukamilifu Wake.) (Ili kumlea binadamu, Mungu ameamua sheria hizi kwa ajili yetu na Ameandaa mazingira ya kijiografia na vilevile aina tofauti za vyakula. Na ili tuweze kuendelea kuishi ndani ya aina hii ya mazingira Aliandaa sehemu tofauti za kuishi. Kutokana na hili ninaweza kuona kwamba kazi ya Mungu na mipango ipo sahihi sana, na ninaweza kuona upendo Wake kwa sisi binadamu.) Je, kuna mtu yeyote aliye na cha kuongeza? (Sheria na mawanda yaliyoamuliwa na Mungu hayawezi kubadilishwa kabisa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Yote ipo chini ya kanuni Yake.) Tukiangalia kwa mtazamo wa sheria zilizoamriwa na Mungu kwa ukuaji wa vitu vyote, yote hii si kwa ajili ya mwanadamu, haijalishi ni wa aina gani, anaishi chini ya uangalizi wa Mungu–je, wote hawaishi chini ya malezi Yake? Ikiwa sheria hizi zingeharibiwa au Mungu hakuanzisha aina hizi za sheria kwa ajili ya binadamu, majaliwa yao yangekuwa ni nini? Baada ya binadamu kupoteza mazingira yao ya msingi kwa ajili ya kuendelea kuishi, je, wangekuwa na chanzo chochote cha chakula? Inawezekana kwamba vyanzo vya chakula vingekuwa tatizo. Ikiwa watu wangepoteza vyanzo vyao vya chakula, yaani, hawawezi kupata kitu chochote kwa ajili ya kula, pengine wasingeweza kuvumilia hata kwa mwezi mmoja. Watu kuendelea kuishi lingekuwa ni tatizo. Kwa hiyo kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa ajili ya watu kuendelea kuishi, kwa ajili ya wao kuendelea kuwepo na kuongezeka ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya miongoni mwa vitu vyote vinahusiana kwa karibu na haviwezi kutenganishwa na watu kuendelea kuishi. Hakiwezi kutenganishwa na wao kuendelea kuishi. Ikiwa kuendelea kuishi kwa binadamu kulikuwa tatizo, je, usimamizi wa Mungu ungeweza kuendelea? Je, usimamizi wa Mungu bado ungekuwepo? Kwa hiyo usimamizi wa Mungu unakwenda sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu wote ambao Anawalea, na haijalishi Mungu anaandaa kitu gani kwa ajili ya vitu vyote na kile Anachofanya kwa ajili ya binadamu, hii yote ndiyo lazima Kwake, na ni muhimu sana kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ikiwa sheria zote hizi ambazo Mungu aliziamua kwa ajili ya vitu vyote zingekuwa zimeachwa, ikiwa sheria hizi zingekuwa zimevunjwa au zimeharibiwa, vitu vyote visingeweza kuwepo, mazingira ya binadamu ya kuendelea kuwepo yasingekuwepo, na wala riziki zao za kila siku, na wala wao wenyewe. Kwa sababu hii, Usimamizi wa Mungu wa wokovu wa binadamu wala nao usingekuwepo. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kuona waziwazi.
Kila kitu ambacho tumejadili, kila kitu, kila kipengele kimeungana kikamilifu na kuendelea kuishi kwa kila mtu. Mnaweza kusema, "Unachokizungumzia ni kikubwa sana, hatuwezi kukiona," na pengine kuna watu ambao wangeweza kusema "Unachokizungumzia hakinihusu." Hata hivyo, usisahau kwamba unaishi kama sehemu tu ya vitu vyote; wewe ni mshirika wa vitu vyote ndani ya kanuni ya Mungu. Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki–huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake. Baadhi ya watu wanasema: "Mimi sio mkulima, sipandi mazao kwa ajili ya kuishi. Sitegemei mbingu ili nipate chakula changu, kwa hiyo naweza kusema kwamba siendelei kuishi katika mazingira ambayo aliyaanzisha Mungu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Aina hiyo ya mazingira haijanipatia kitu chochote." Lakini hii si kweli. Na kwa nini sio? Unasema kwamba hupandi mazao kwa ajili ya kuishi, lakini huli nafaka? Huli nyama? Huli mayai? Je, huli mbogamboga na matunda. Kila kitu unachokula, vitu hivi vyote unavyovitaka havitenganishwi na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoanzishwa na Mungu kwa ajili ya binadamu. Na chanzo cha kila kitu ambacho binadamu anahitaji hakiwezi kutenganishwa na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, aina hizo za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Maji unayokunywa, nguo unazovaa, na vitu vyote unavyotumia–ni kitu gani kati ya hivi ambacho hakipatikani kutoka katika vitu hivi vyote? Baadhi ya watu husema: "Kuna baadhi ya vitu ambavyo havipatikani kutoka katika vitu vyote hivi." Kama nini? Nipatie mfano. Baadhi husema: "Unaona, plastiki haitokani na vitu vyote hivi. Ni kitu cha kemikali, kitu kilichotengenezwa na mwanadamu." Lakini hii si sahihi. Kwa nini sio? Plastiki imetengenezwa na mwanadamu, ni kitu cha kemikali, lakini vijenzi asilia vya plastiki vilitoka wapi? (Vilitoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu.) Vijenzi asilia vilipatikana kutoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu. Vitu ambavyo unavifurahia, ambavyo unaona, kila kitu ambacho unatumia, vyote vinapatikana kutoka katika vitu vyote ambavyo vilitengenezwa na Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, haijalishi ni mbari gani, haijalishi ni riziki gani, au ni katika aina gani ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo watu wanaishi, hawawezi kujitenganisha na uangalizi wa Mungu. Kwa hiyo mambo haya tuliyoyajadili leo yanahusiana na mada yetu ya "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote"? Kwa hiyo, vitu tulivyovijadili leo, vinaangukia chini ya mada hii kubwa? Ni kwa sababu tu ya uhusiano huu ndio maana nimesema yote haya. Pengine baadhi ya ambayo nimeyazungumzia leo ni ya kidhahania kidogo na ni vigumu kidogo kuweza kuyajadili. Hata hivyo, Nadhani kwamba sasa mnaelewa vizuri kidogo.
Nyakati chache hizi katika ushirika, kiwango cha mada ambazo tumekuwa nazo katika ushirika ni kipana sana, na mawanda yao ni mapana, kwa hiyo unapaswa uwe na jitihada kiasi fulani ili uweze kuzielewa zote. Hii ni kwa sababu mada hizi ni vitu ambavyo watu hawajawahi kukabiliana navyo katika imani yao kwa Mungu. Baadhi ya watu wanaisikia kama muujiza na baadhi ya watu wanaisikia kama hadithi–mtazamo gani ni sahihi? Unasikia haya yote kutoka katika mtazamo gani? Umepata nini kutokana na haya yote? Hebu mtu aseme. (Nimetambua kipengele cha mamlaka ya Mungu na pia nimeona heshima Yake, na kutokana na hili pia ninaweza kuona upendo Wake kwa binadamu. Kila kitu Anachokifanya kinajumuisha mipangilio na mipango Yake angalifu na sahihi kwa ajili ya binadamu. Anatupenda sana na kutuhifadhi kwa upendo mkubwa sana kiasi kwamba hata Ametupatia chakula chetu kwa umakini.) (Tumeyaona matendo ya Mungu, vilevile kwa mbinu gani Amepangilia vitu vyote na kwamba vitu vyote vina sheria hizi na kupitia maneno haya tunaweza kuelewa zaidi juu ya matendo ya Mungu na mpangilio wake angalifu na sahihi kwa ajili ya kumwokoa binadamu.) Kupitia nyakati hizi katika ushirika, Mmeona mawanda ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote ni nini? (Binadamu wote, kila kitu.) Je, Mungu ni Mungu wa mbari moja? Je, ni Mungu wa aina moja ya watu? Je, ni Mungu wa eneo dogo la binadamu? (Hapana, hayupo hivyo.) Kwa kuwa Hayupo hivyo, katika maarifa ya watu juu ya Mungu, ikiwa angekuwa ni Mungu wa sehemu ndogo tu ya binadamu, au ikiwa unaamini kwamba Mungu ni Mungu wako tu, je, mtazamo huu upo sahihi? Kwa kuwa Mungu anasimamia na kutawala vitu vyote, watu wanapaswa kuona matendo Yake, hekima Yake, na ukuu Wake ambavyo vimefunuliwa katika utawala Wake wa vitu vyote. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kufahamu. Ikiwa unasema kwamba Mungu anasimamia viumbe vyote, na Anatawala binadamu wote, lakini kama huna uelewa wowote au umaizi katika utawala Wake kwa binadamu, je, unaweza kutambua kwamba Anatawala vitu vyote? Unaweza? Unaweza kufikiri moyoni mwako, "Ninaweza, kwa sababu ninaona kwamba maisha yangu haya yote yanatawaliwa na Mungu." Je, kweli Mungu ni mdogo kiasi hicho? Hayupo hivyo! Unaona tu wokovu wa Mungu kwa ajili yako na kazi yake kwako, na kutokana na vitu hivi unauona utawala Wake. Hayo ni mawanda finyu sana, na yana athari katika maarifa yako halisi juu ya Mungu. Pia yanaweka mipaka kwenye maarifa yako halisi juu ya utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Ikiwa unayawekea mipaka maarifa Yake kwenye mawanda ya kile ambacho Mungu anatoa kwa ajili yako na wokovu Wake kwa ajili yako, hutaweza kutambua kwamba anatawala kila kitu, kwamba anatawala vitu vyote, na anatawala binadamu wote. Unaposhindwa kutambua haya yote, je, kweli unaweza kutambua ukweli kwamba Mungu anatawala majaliwa yako? Huwezi. Moyoni mwako hutaweza kutambua kipengele hicho–hutoweza kutambua kiwango hicho. Unaelewa, siyo? (Ndiyo.) Kwa kweli, Ninajua ni kwa kiwango gani mnaweza kuelewa mada hizi, maudhui haya ninayoyazungumzia, sasa kwa nini Naendelea kuizungumzia? Ni kwa sababu mada hizi ni mambo ambayo yanapaswa kueleweka kwa kila mfuasi wa Mungu, kila mtu ambaye anataka kuokolewa na Mungu–anapaswa kuelewa mada hizi. Ingawa kwa kipindi hiki, kwa kipindi hiki ambacho huzielewi, siku moja, ambapo maisha yako na uzoefu wako wa ukweli utafikia kiwango fulani, pale ambapo mabadiliko yako ya tabia yako ya maisha yanafikia kiwango fulani na kimo chako kinaongezeka kwa kiwango fulani, maneno haya–mada hizi ambazo naziwasilisha kwako katika ushirika–baada ya hapo tu zitakimu na kuridhisha utafutaji wako wa maarifa ya Mungu. Kwa hiyo maneno haya yalikuwa ni kwa ajili ya kuweka msingi, kuwaandaa kwa ajili ya uelewa wenu wa baadaye kwamba Mungu anatawala vitu vyote na kwa ajili ya uelewa wenu wa Mungu Mwenyewe.
Vyovyote vile uelewa juu ya Mungu ulivyo mkubwa katika mioyo ya watu, unaamua nafasi kubwa kiasi gani Anachukua katika mioyo yao. Vyovyote vile kiwango cha maarifa ya Mungu kilivyo katika mioyo yao ndivyo kwa kiwango kikubwa hadhi Yake ilivyo katika mioyo yao. Ikiwa Mungu unayemfahamu yupo tupu na ni yule asiye yakini, basi Mungu wa kwenye moyo wako pia yupo tupu na ni yule asiye yakini. Ikiwa Mungu unayemfahamu anaishia ndani ya mipaka ya mawanda yako, basi ni Mungu mdogo kweli–Mungu huyo hajaunganishwa na Mungu wa kweli na wala hahusiani na Yeye. Kwa hiyo, kuyajua matendo halisi ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote–haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya hayatenganishwi na maisha ya kila mtu, na maisha halisi ya kila mtu ya kuutafuta ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba Mungu wako kabisa si Mungu wa kweli. Kabisa si Mungu Mwenyewe wa kweli, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini si Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu ambaye Ninamzungumzia ni yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote. Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaongoza binadamu wote kwa njia ya utawala Wake wa vitu vyote, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Sasa unaelewa yote haya, sio? Lengo Langu ni nini kusema yote haya? Iko hivyo ili usiweze kulichukulia hili kirahisi, ili msiamini kwamba mada hizi Nilizozizungumzia hazina uhusiano na kuingia kwenu binafsi katika maisha, na ili msichukue mada hizi kama tu aina ya maarifa au mafundisho. Ikiwa unasikiliza ukiwa na mtazamo kama huo, hutapata kitu hata kimoja. Utapoteza fursa kubwa hii ya kumjua Mungu. Kwa hiyo, sasa unaelewa?
Lengo Langu la kuzungumza juu ya mambo haya yote ni nini? Lengo langu ni kuwafanya watu wamjue Mungu, kuwafanya watu waelewe matendo halisi ya Mungu. Mara utakapomuelewa Mungu na ukaelewa matendo Yake, ni baada ya hapo tu ndipo utakuwa na fursa au uwezekano wa kumjua Mungu. Kwa mfano, ikiwa unataka kumwelewa mtu, ni jinsi gani unaweza kumwelewa? Je, inaweza kuwa kupitia kuangalia umbo lao la nje? Je, inaweza kuwa kupitia kile wanachokivaa, jinsi wanavyovaa? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia jinsi wanavyotembea? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia mawanda ya maarifa yao? Hakika isingeweza kuwa hivyo. Kwa hiyo unamwelewaje mtu? Unafanya hukumu kupitia mawazo ya mtu, kupitia maneno na tabia zake, kupitia kile anachokionyesha na kile anachokifichua. Hivyo ndivyo unavyomjua mtu, unavyomwelewa mtu. Kwa njia ile ile, ikiwa mnahitaji kumjua Mungu, ikiwa mnataka kuelewa upande Wake wa vitendo, upande Wake wa kweli, mnapaswa kumjua Yeye kupitia matendo Yake na kupitika kila kitu halisi Anachofanya. Hii ndiyo njia bora zaidi na ndiyo njia pekee. Kwa hiyo mnaelewa sasa? Mungu anadhihirisha matendo Yake miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa vitu vyote Anavyovitawala na Anashikilia sheria za vitu vyote. Ni lazima kabisa kwa kumuelewa na kumjua Mungu.

2. Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi

Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote kupitia sheria Zake kwa ajili ya viumbe vyote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao. Hii pia ni mada kubwa sana kwenu. Kuweka uwiano wa uhusiano kati ya vitu vyote—je, hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kufanya? Binadamu wenyewe hawawezi. Watu wanaweza tu kuharibu. Hawawezi kuweka uwiano wa uhusiano kati ya vitu vyote; hawana mamlaka makubwa hayo au nguvu. Ni Mungu Mwenyewe ndiye ana aina ya nguvu kuweza kufanya kitu cha aina hii. Kusudi la Mungu la kufanya kitu cha aina hii—kinamsaidia nini? Ni vilevile, inafanana kwa ukaribu na kuendelea kuishi kwa binadamu. Kila kitu ambacho Mungu anataka kufanya ni cha lazima—hakuna kitu ambacho Anaweza au asiweze kufanya. Ili Yeye alinde kuendelea kuishi kwa binadamu na kuwapatia watu mazingira faafu kwa ajili ya kuendelea kuishi, kuna vitu fulani vya lazima, vitu fulani vya muhimu sana ambavyo ni lazima Afanye kulinda kuendelea kuishi kwao.
Kutokana na maana ya moja kwa moja ya kirai "Mungu anaweka uwiano kwa vitu vyote," ni mada pana sana; kwanza inakupatia dhana ili uweze kujua kwamba kuweka uwiano kwa vitu vyote, kabisa ni utawala Wake kwa vitu vyote. Neno "uwiano" linamaanisha nini? Kwanza, "uwiano" unamaanisha kutoruhusu kitu fulani kuwa nje ya uwiano. Kila mtu anajua kuhusu mizani. Unapotumia mizani kupima kitu fulani, unakiweka katika upande mmoja wa kipimo na kuweka uzito katika upande mwingine. Kiasi cha mwisho cha uzito kinaamua uzito wa kitu hicho—huo ndio unaitwa uwiano. Ili kuweka uwiano, uzito wa pande mbili lazima uwe sawa. Mungu aliumba vitu vingi miongoni mwa vitu vyote—Aliumba vitu ambavyo havibadiliki, vitu ambavyo vinajongea, vitu ambavyo vinaishi, na vitu ambavyo vinapumua, vilevile vile ambavyo havipumui. Aliumba idadi kubwa ya vitu—je, ni rahisi kwa vitu hivi vyote kupata uhusiano wa kutegemeana, wa kusaidiana na kuzuiana, wa kuingiliana? Kwa hakika kuna kanuni fulani ndani ya jambo hili. Ingawa inatatiza sana, sio ngumu kwa Mungu. Hata hivyo, kwa watu, ni vigumu sana kufanya utafiti. Inaonekana kama neno rahisi sana—uwiano Hata hivyo, ikiwa watu walilitafiti, ikiwa watu walihitaji kutengeneza uwiano, basi wanataaluma wale wenye akili sana wote wangekuwa wanalifanyia kazi—wanabiolojia wa kibinadamu, mamajusi, wanafizikia, wakemia na hata wanahistoria. Matokeo ya mwisho ya utafiti huo yangekuwa ni nini? Matokeo yake yasingekuwa chochote. Hii ni kwa sababu uumbaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa ajabu sana na binadamu kamwe hataweza kufungua siri zake. Mungu alipoviumba vitu vyote, Alianzisha kanuni kati yao, Alianzisha njia tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa ajili ya kuzuiana, kukamilishana, kuheshimiana, na riziki. Mbinu hizi mbalimbali zinatatiza sana; si rahisi au za kuelekea upande mmoja. Watu wanapotumia akili zao, maarifa yao, na tukio ambalo wamewahi kuona kuthibitisha au kutafiti kanuni zinazoongoza udhibiti wa Mungu wa vitu vyote, vitu hivi ni vigumu sana kuvigundua. Pia ni vigumu sana kugundua au kupata matokeo yoyote. Inaweza ikasemwa kwamba ni vigumu sana watu kupata matokeo. Ni vigumu sana kudumisha uwiano kwa kutegemea akili na maarifa ya binadamu kuongoza viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu. Kwa kuwa watu hawajui kanuni za kuendelea kuishi kwa viumbe vyote, hawajui jinsi ya kulinda aina hii ya uwiano. Kwa hiyo, ikiwa watu wangeweza kusimamia na kuongoza viumbe vyote vya Mungu, kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kuharibu uwiano. Mara tu utakapoharibiwa, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi yangeweza kuharibiwa, na hiyo inapotokea, ingeweza kufuatiwa na mgogoro kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao. Ingesababisha janga. Binadamu anapoishi katikati ya janga, nini kingeweza kutokea mbele yao? Yangekuwa ni matokeo ambayo ni vigumu kuyakisia, vigumu kuyabashiri. Hii ndiyo aina ya hatari ambayo sasa inaikabili dunia.
Basi ni jinsi gani Mungu anaweka uwiano kwenye uhusiano kati ya vitu vyote? Kwanza, kuna baadhi ya maeneo duniani ambayo yamefunikwa na barafu na theluji kwa mwaka mzima, wakati katika baadhi ya maeneo, misimu yote minne ni kama msimu wa machipuo. Hutoweza kabisa kuona kipande cha barafu au chembe ya theluji. Hakuna msimu wa baridi—siku zote ni kama msimu wa machipuo. Hii ni njia moja—ni kutokana na mtazamo mkubwa wa hali ya hewa. Aina ya pili ni pale watu wanapoona milima ikiwa na uoto uliostawi sana, ambapo aina zote za mimea inafunika ardhi; kuna malundo ya msitu na unapotembea katikati yao huwezi hata kuona jua. Katika milima mingine nyasi hata hazioti—kuna safu na safu za milima yenye ukame, isiyokaliwa. Ukiangalia kwa nje, yote ni milima yenye mchanga uliorundikana. Kundi moja la milima limejaa uoto uliositawi, na kundi jingine halina hata nyasi. Hii ni aina ya pili. Katika aina ya tatu, unaweza kuona tabaka la mbuga lisilokuwa na kikomo, uwanda wa kijani unaopunga. Au unaweza kuona jangwa kadri jicho linavyoweza kuona; huoni kiumbe hai yeyote, wala chanzo chochote cha maji, ni sauti tu ya upepo pamoja na mchanga. Katika aina ya nne, sehemu moja imefunikwa na bahari, ambayo imeundwa na eneo kubwa la maji, wakati katika sehemu nyingine unahangaika sana kutafuta chemchemi ya maji. Katika aina ya tano, katika nchi moja mvua ya manyunyu inanyesha mfululizo na ina ukungu na unyevunyevu, wakati kwenye nchi nyingine siku za jua kali ni za kawaida sana na hutaona hata tone moja la mvua. Katika aina ya sita, aina moja ya sehemu ni nchi tambarare ambapo hewa ni finyu sana na ni vigumu kupumua, na katika aina nyingine ya eneo kuna kinamasi na nyanda za chini, ambayo yanatumika kama makazi ya aina mbalimbali ya ndege wahamao. Hizi ni aina tofautitofauti za tabia ya nchi, au tabia za nchi au mazingira ambayo yanaitikia mazingira tofautitifauti ya kijiografia. Hiyo ni sawa na kusema, Mungu anaweka uwiano kwenye mazingira ya msingi ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi kutoka katika mtazamo wa mazingira makubwa, kutoka katika tabia ya nchi kwenda katika mazingira ya kijiografia, kutoka katika vijenzi tofauti vya udongo kwenye kiwango cha vyanzo vya maji ili kupata uwiano kwenye hewa, halijoto na unyevunyevu wa mazingira ambamo watu wanaendelea kuishi. Kwa tofauti hizi za mazingira tofauti ya kijiografia, watu watakuwa na hewa imara na halijoto na unyevunyevu katika misimu tofautitofauti vitakuwa imara. Hii inawaruhusu watu kuendelea kuishi katika aina hiyo ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi siku zote. Hii ni kuzungumza kutokana na mtazamo wa mazingira makubwa. Kwanza, mazingira makubwa yanapaswa kuwekewa uwiano. Hii inafanyika kupitia kutimia kikamilifu maeneo mbalimbali ya kijiografia na mbinu vilevile muachano kati ya tabia za nchi tofautitofauti kwa ajili ya kuzuiana ili kupata uwiano ambao Mungu anataka na ambao binadamu anahitaji. Hii ni kutokana na mtazamo wa mazingira makubwa.
Ukiangalia kwenye maelezo, kama vile uoto, inawezekanaje kuifanya hiyo ipate uwiano? Yaani, ni jinsi gani uoto unaweza kuruhusiwa kuendelea kuishi ndani ya mazingira yenye uwiano kwa ajili ya kuendelea kuishi? Ni kwa kusimamia urefu wa maisha, viwango vya ukuaji, na viwango vya kuzaliana vya aina mbalimbali za mimea ili kulinda mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Chukulia nyasi dogo kama mfano—wakati wa machipuo linachipua, wakati wa kiangazi linatoa maua, na wakati wa majira ya kupukutika majani linatoa matunda. Tunda linaanguka kwenye ardhi na nyasi hii inakufa. Mwaka ujao, mbegu kutoka kwenye tunda inachipua na kukua kulingana na sheria zile zile. Urefu wa maisha ya nyasi ni mafupi sana—inakuwa hai kuanzia msimu wa machipuo hadi msimu wa kupukitika kisha inakufa. Kila mbegu inaanguka ardhini, inakuza mizizi na kuchipuka, inaweka maua na kuzaa matunda—hatua hii inatokea tu wakati wa machipuo, kiangazi na kupukutika, na aina zote za miti pia zina urefu wao wa maisha na vipindi tofauti kwa ajili ya kuchipua na kuzaa matunda. Baadhi ya miti hufa baada tu ya miaka 30 hadi 50—ina urefu wa maisha ya kuanzia miaka 30 hadi 50, lakini matunda yao huanguka ardhini, ambayo kisha hukuza mizizi na machipuko, maua na kuzaa tunda, na kuishi kwa miaka mingine 30 had 50. Hiki ndicho kiwango cha kujirudia kwake. Mti mzee unakufa na mti mdogo unakua—hii ndio maana siku zote unaona miti inaendelea kukua msituni. Lakini pia ina mzunguko wao mzuri na mchakato ama kuzaliwa na kufa. Baadhi ya miti inaweza kuishi kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu moja, na baadhi inaweza kuishi kwa hata miaka elfu tatu. Yenyewe ni aina hiyo ya mimea. Haijalishi ni aina gani ya mmea au urefu wao wa maisha ni mrefu kiasi gani, nikizungumza kwa ujumla, Mungu anasimamia uwiano wake kulingana na kipindi unachoishi, uwezo wake wa kuzaliana, kasi yake ya kuzaliana vilevile kiasi na kiwango chake cha kuzaliana. Hii inawaruhusu, kuanzia majani hadi miti, kuweza kuendelea kusitawi, kukua ndani ya mazingira ya kiikolojia yenye uwiano. Kwa hiyo unapoangalia msitu duniani, haijalishi kama ni miti au majani, unaendelea kujizalisha na kukua kulingana na sheria zake. Haihitaji msaada wa binadamu; haihitaji kazi yoyote ya ziada kutoka kwa binadamu. Ni kwa sababu tu wana aina hii ya uwiano ndipo wana uwezo wa kudumisha mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ni kwa sababu tu wana mazingira faafu kwa ajili ya kuendelea kuishi ndipo misitu hii, kanda hizi za mbuga zinaweza kuendelea kuishi duniani. Uwepo wao unalea kizazi baada ya kizazi cha watu vilevile kizazi baada ya kizazi cha aina zote za viumbe hai vyenye makazi misituni na kwenye kanda za mbuga—ndege na wanyama, wadudu, na aina zote za vijiumbe.
Mungu pia anadhibiti uwiano wa aina zote za wanyama. Uwiano huu unadhibitiwaje? Ni sawa na kwenye mimea—anasimamia uwiano wao na anaamua idadi yao kulingana na uwezo wao wa kuzaliana, ukubwa na kiwango cha kuzaliana kwao na wajibu wanaoufanya miongoni mwa wanyama. Kwa mfano, simba hula pundamilia, kwa hiyo ikiwa idadi ya simba ingezidi idadi ya pundamilia, hatima ya pundamilia ingekuwaje? Wangepotea kabisa. Na ikiwa kuzaliana kwa pundamilia kungekuwa kwa idadi ndogo kuliko idadi ya simba, hatima yao ingekuwaje? Vilevile wangepotea kabisa. Kwa hiyo, idadi ya pundamilia inapaswa kuwa kubwa kuliko idadi ya simba. Hii ni kwa sababu pundamilia hawaishi tu kwa ajili yao; wanaishi pia kwa ajili ya simba. Unaweza pia kusema kwamba kila pundamilia ni sehemu moja ya pundamilia, lakini pia ni chakula katika kinywa cha simba. Kasi ya simba ya kuzaliana haiwezi kamwe kuiacha ile ya pundamilia, kwa hiyo idadi yao haiwezi kuwa kubwa kuliko idadi ya pundamilia. Ni kwa njia hii tu ndipo chanzo cha chakula cha simba kinaweza kuhakikishwa. Ingawa simba ni maadui wa asili wa pundamilia, watu mara kwa mara huwaona wakiwa wamepumzika kwa kustarehe katika eneo moja. Pundamilia hawatapungua idadi au kupotea kabisa kwa sababu simba wanawawinda na kuwala, na simba hawataongezeka idadi yao kwa sababu ya hadhi yao kama "mfalme." Uwiano huu ni kitu ambacho Mungu alikianzisha zamani sana. Yaani, Mungu alianzisha sheria za uwiano kati ya wanyama wote ili kwamba waweze kupata uwiano, na hiki ni kitu ambacho binadamu anaweza kukiona. Je, simba ni adui pekee wa asili wa pundamilia? Mamba pia hula pundamilia. Umeshawahi kuona mamba akimla pundamilia? Kumshuhudia mamba akimla pundamilia pia ni kitendo cha ukatili. Pundamilia anaonekana kuwa mnyama asiyekuwa na msaada kabisa. Hawana ukali kama wa simba, na wanapomkabili adui huyu wa kutisha, wanaweza kukimbia tu. Hawawezi hata kutoa upinzani. Wakati ambapo hawawezi kumshinda mbio simba, wanaweza kujiruhusu tu waliwe naye. Hii inaweza kuonekana mara kwa mara katika ulimwengu wa wanyama. Mnapata wazo gani mnapoona kitu cha namna hii? Je, unamhurumia pundamilia? Je, unamchukia simba? Pundamilia wanaonekana wazuri sana. Lakini simba, siku zote wanawaangalia kwa tamaa. Na kwa upumbavu, pundamilia hawakimbii mbali sana. Wanawaangalia simba pale wakiwasubiri, kwa kawaida wakiwasubiri chini ya kivuli cha mti. Nani anajua ni wakati gani atawala. Je, wanajua hili mioyoni mwao? Wanajua, lakini hawatalihama eneo hilo. Hili ni jambo la ajabu. Jambo hili la ajabu linajumuisha majaliwa ya Mungu, kanuni Yake. Unamhurumia pundamilia lakini huna uwezo wa kumsaidia, na unahisi kwamba simba ni wa kuchukiwa lakini huwezi ukamwepuka. Pundamilia ni chakula ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya simba, lakini haijalishi ni kwa namna gani simba wanawala, pundamilia hawatamalizwa. Idadi ya watoto ambao simba wanazaa ni ndogo sana, na wanazaliana taratibu sana, kwa hiyo hawawezi kuzidi idadi ya pundamilia. Haijalishi wanawala kiasi gani, idadi yao haitakuwa kubwa kuliko ya pundamilia. Hii ni aina ya uwiano.
Lengo la Mungu ni lipi katika kudumisha aina hii ya uwiano? Hii inahusiana na mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi vilevile kuendelea kuishi kwa binadamu. Ikiwa pundamilia au mawindo mengine ya simba—paa au wanyama wengineo—watazaliana taratibu sana na idadi ya simba ikaongezeka haraka, ni aina gani ya hatari ambayo binadamu wangepata? Kwanza, kuku, bata, bata bukini, na mbwa wanaofugwa na watu wangekuwa mawindo ya simba. Hii ni kwa sababu wanaishi nje, kwa hiyo wangekuwa windo la kwanza la simba. Je, vitu hivyo vinatosha simba kula? Baadhi ya kaya wana nguruwe wawili. Kama simba angekuja kutoka milimani na kuwala, je, angeondoka tu baada ya kumaliza. Angefikiri: "Hakuna kitu cha kula milimani, nitabaki hapa tu. Familia hii ina nguruwe—kutakuwa na binadamu wachache sasa ambao nimewala. Hakuna kitu kwa ajili ya mlo unaofuata—je, haukuandaliwa wote? Watu wamekaa tu ndani—hawawezi kubakia humo milele!" Mara tu watu watakapotoka nje, atawala mara moja tu kwa mataya yake. Watu hawana uwezo wa kuweka upinzani. Je, hili lisingekuwa ni tukio la kutisha? Simba kuwala pundamilia ni tukio la kawaida, lakini ikiwa simba angewala watu, lingekuwa ni janga. Janga hili sio kitu ambacho kilipangwa kabla na Mungu, halipo ndani ya sheria Yake, wala kile ambacho amekileta kwa ajili ya binadamu. Badala yake, ni kile ambacho watu wamejiletea wenyewe. Kwa hiyo kama Mungu aonavyo, uwiano kati ya vitu vyote ni muhimu kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Iwe ni mimea au wanyama hawawezi kupoteza uwiano wao sahihi. Mimea, wanyama, milima, na maziwa yamemwandalia binadamu mazingira ya kawaida ya kiikolojia. Hadi pale tu ambapo watu watakuwa na aina hii ya mazingira ya kiikolojia—yenye uwiano—ndipo kuendelea kuishi kwao kutakuwa salama. Ikiwa uwezo wa kuzalisha wa mtu au majani haukuwa mzuri au kasi yake ya uzalishaji ilikuwa ya taratibu sana, udongo ungefanya nini? Je, udongo ungepoteza unyevunyevu wake? Ikiwa udongo ungepoteza unyevunyevu wake, je, lingekuwa tatizo? Ikiwa udongo ungepoteza uoto wake na unyevunyevu wake, ungemomonyoka haraka sana, na mchanga ungetokea badala yake. Udongo usingekuwa na rutuba tena na ungekuwa mchangamchanga, na udongo unapoharibika, mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi pia yanaharibika. Pamoja na uharibifu huu majanga yangeweza kutokea. Bila aina hii ya uwiano wa kiikolojia, bila aina hii ya mazingira ya kiikolojia, watu wangeendelea kuathirika na majanga kwa sababu ya kukosa uwiano baina ya vitu hivi vyote. Kwa mfano, kukosekana kwa uwiano wa kimazingira kunasababisha kuongezeka idadi ya vyura katika eneo fulani—mazingira yao ya kiikolojia yameharibiwa, wote wanakusanyika pamoja, idadi yao inaongezeka haraka sana na watu hata wanaona vyura wanapita mtaani mijini, na idadi kubwa ya vyura barabarani. Ikiwa idadi kubwa ya vyura ingechukua sehemu kubwa ya mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi, hiyo ingeitwaje? Janga. Kwa nini liitwe janga? Wanyama hawa wadogo ambao wana manufaa kwa binadamu wana faida kwa watu wanapobaki katika eneo ambalo ni faafu kwao; wanadumisha uwiano wa mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Mara tu wanapokuwa janga, wataathiri mpangilio wa maisha ya watu. Vitu vyote na vipengele vyote ambavyo chura wanavileta vinaweza kuathiri ubora wa maisha ya watu. Hata ogani zao za kimwili zinaweza kushambuliwa—hii ni moja ya aina ya majanga.
Aina nyingine ya janga, ambalo ni kitu ambacho binadamu wamepitia mara kwa mara—ni kutokea kwa idadi kubwa ya nzige. Hili si janga? Hili ni janga la kutisha. Haijalishi binadamu wana uwezo kiasi gani—watu wanaweza kutengeneza ndege, mizinga, na mabomu ya atomiki—lakini pale ambapo nzige wanawavamia binadamu, wanakuwa na suluhisho gani? Je, wanaweza kuwashambulia kwa mizinga? Je, wanaweza kuwafyatulia risasi kwa bunduki? Hawawezi. Basi wanaweza kuwanyunyizia dawa ya kuua wadudu ili kuwafukuza? Hiyo si rahisi pia. Sasa, kwa nini nzige hao wadogo waje? Kula nafaka. Popote pale nzige watakapokwenda mazao yanafutiliwa mbali kabisa. Kwa umahususi wanakula mazao na nafaka. Popote pale watakapopita nafaka zozote zile zinakwisha! Chini ya uvamizi wa nzige, kufumba na kufumbua, chakula ambacho wakulima wanakitegemea—nafaka za mwaka mzima—zingeweza kuteketezwa kabisa na nzige. Na ujio wa nzige kwa binadamu ni nini? Sio tu kero—ni janga.
Nzige ni aina ya janga, sasa vipi kuhusu panya? Ikiwa panya wanazaliana haraka sana na hakuna bundi au mwewe wa kuwala, watazaliana kwa kasi, haraka kuliko unavyoweza kufikiri. Na ikiwa kuenea kwa panya hakutadhibitiwa, je, binadamu wanaweza kuishi maisha mazuri? Hawawezi. Sasa ni kitu gani ambacho binadamu watakabiliana nacho? (Tauni.) Tauni tu? Panya watakula kila kitu! Watatafuna hata mbao. Ikiwa kuna panya wawili tu katika nyumba, kila mtu kwenye nyumba yote atachukizwa. Wakati mwingine wanaiba mafuta na kula, wakati mwingine wanakula nafaka na kutafuna nguo—hii ndiyo shida ambayo panya wanawapatia watu. Ni panya wadogo tu, lakini watu hawana namna ya kushughulika nao. Wamefanyiwa hata udhalimu na hao panya. Wakati mwingine wanapanda kwenye uchaga wa vyombo—je, vyombo hivyo bado vinaweza kutumiwa? Vyombo hivyo haviwezi kutumika, kuvisafisha hakutasaidia na hata kama utavisafisha hutajisikia una amani, kwa hiyo utavitupa tu nje. Na vitu ambavyo hawali wanavichanachana na kuwa takataka kabisa. Wanatafuna nguo, viatu, mbao, samani—wanatafuna kila kitu. Hakuna haja ya kuzungumzia kundi lote la panya—panya wawili tu wanatosha kufanya uharibifu. Kama wangekuwa janga, madhara yake hayawezi kufikirika.
Kwa hiyo, ikiwa mchwa wadogo wangekuwa janga, janga hilo lingefananaje? Madhara ambayo wangefanya kwa binadamu yasingeweza kupuuzwa. Mchwa kula mbao kwa kiwango ambacho hadi nyumba inaanguka si jambo geni. Uwezo wao hauwezi kupuuzwa. Kwa hiyo, ikiwa mchwa au mayai ya mchwa yatagunduliwa ndani ya nyumba ya mbao, nchini Marekeni, hili ni tukio kubwa sana. Unapaswa kutafuta kampuni yenye weledi na wafanyakazi wataalamu ambao wana uwezo wa kiweledi wa kuwaua. Ikiwa huwezi kuwaua, nyumba hiyo itakuwa vigumu kuiuza na litakuwa tatizo kubwa. Je, ulisikia kuhusu kundi la siafu ambalo lilimla farasi? Kulikuwa na kundi kubwa la siafu walioparamia mwili mzima wa farasi mkubwa, na kilichoachwa kwenye farasi ilikuwa ni mifupa tu. Je, hiyo inaogopesha au vipi? Na mpanda farasi alipoona hilo, alitorokea wapi? Kulikuwa na ziwa karibu, kwa hiyo alikimbilia ziwani na akaogelea kuelekea upande mwingine. Akapona kwa namna hiyo. Lakini baada ya kuwa ameona hivyo, kwa maisha yake yote hakuweza kusahau jinsi ambavyo hao siafu wadogo bila kutarajia walikuwa na nguvu za namna hiyo. Karibu wamle yeye. Ikiwa hangekuwa na farasi, siafu hakika wangemla yeye kwanza, na kwa sababu kulikuwa na maji katikati yao, siafu hawakuweza kutengeneza daraja kwa wakati kwenda kumla. Ikiwa maji hayangekuwepo pale farasi na mtu wote wangeliwa kwa pamoja. Nguvu za siafu haziwezi kupuuzwa.
Na ikiwa aina tofautitofauti ya ndege wangebadilika kuwa janga ingeweza pia kuwa kitu cha kuogofya. Yaani, haijalishi wao ni aina gani ya wanyama au viumbe hai, mara tu watakapopoteza uwiano wao, watakua, kuzaliana, na kuishi ndani ya mawanda yasiyokuwa ya kawaida, mawanda yasiyofuata kanuni. Hiyo ingeweza kuleta madhara yasiyoweza kufikirika kwa binadamu. Hiyo isingeweza kuathiri kuendelea kuishi na maisha ya watu tu, bali pia ingeleta janga kwa binadamu, hata kufikia hatua ambapo watu watapatwa na maangamizo, watapatwa na hatma ya kufa.
Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha. Viumbe vyote haviwezi kwenda nje ya sheria hizi na haziwezi kuvunjwa. Ni ndani ya aina hii tu ya mazingira ya msingi ndipo binadamu wanaweza kuendelea kuishi kwa usalama na kuongezeka, kizazi baada ya kizazi. Ikiwa kiumbe yeyote anakwenda zaidi ya ukubwa au mawanda yaliyoanzishwa na Mungu, au ikiwa anazidi kiwango cha ukuaji, ujirudiaji, au idadi chini ya utawala Wake, mazingira ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yangepata uharibifu wa viwango vinavyotofautiana. Na wakati uo huo, kuendelea kuishi kwa binadamu kungetishiwa. Ikiwa aina moja ya kiumbe hai ni kubwa sana kwa idadi, itawanyang'anya watu chakula chao, kuharibu vyanzo vya maji ya watu, na kuharibu makazi yao. Kwa njia hiyo, kuzaliana kwa binadamu au hali ya kuendelea kuishi ingeathiriwa mara moja. Kwa mfano, maji ni muhimu sana kwa vitu vyote. Ikiwa kuna wanyama wengi sana—ikiwa idadi ya panya, siafu, nzige, na vyura ni kubwa sana na wanahitaji kunywa maji—kunapokuwa na idadi iliyozidi ya wanyama, kiwango cha maji wanayokunywa pia kitaongezeka. Kadri kiwango cha maji wanachokunywa kinaongezeka, ndani ya mawanda haya yasiyobadilika ya vyanzo vya maji ya kunywa na maeneo ya majimaji, maji ya kunywa ya watu na vyanzo vya maji vitapungua, na watapungukiwa maji. Ikiwa maji ya kunywa ya watu yataharibiwa, kuchafuliwa au kuangamizwa kwa sababu aina zote za wanyama zimeongezeka kwa idadi, chini ya aina hiyo ya mazingira katili kwa ajili ya kuendelea kuishi, kuendelea kuishi kwa binadamu hakika kutakuwa kumetishiwa vikali. Ikiwa kuna aina moja au aina kadhaa za viumbe hai ambavyo vinazidi idadi yao inayofaa, hewa, halijoto, unyevunyevu, na hata vijenzi vya hewa ndani ya eneo la binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi litakuwa na sumu na kuharibiwa kwa viwango vinavyotofautiana. Hali kadhalika, chini ya mazingira haya, kuendelea kuishi kwa binadamu na hatma bado vitakuwa chini ya tishio la aina hiyo ya mazingira. Kwa hiyo, ikiwa watu watapoteza uwiano huu, hewa wanayovuta itaharibiwa, maji wanayokunywa yatachafuliwa, na halijoto ambayo wanahitaji pia itabadilika, itaathiriwa kwa viwango tofautitofauti. Ikiwa hiyo itatokea, mazingira asilia ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yataandamwa na madhara na changamoto kubwa. Chini ya aina hii ya mazingira ambapo mazingira ya msingi ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yameharibiwa, hatma na matarajio ya binadamu yatakuwa ni nini? Ni tatizo kubwa sana!
Kwa sababu Mungu anajua vitu vyote ni nini kwa binadamu, wajibu wa kila aina ya kitu, aina gani ya athari kinacho kwa watu, na faida kubwa kiasi gani kinaleta kwa binadamu—katika moyo wa Mungu kuna mpango kwa ajili ya haya yote na Anasimamia kila kipengele cha vitu vyote alivyoviumba, kwa hiyo kwa binadamu, kila kitu Anachofanya ni muhimu sana—vyote ni lazima. Kwa hiyo ama unaona baadhi ya matukio ya kiikolojia miongoni mwa vitu vyote, au baadhi ya sheria za asili miongoni mwa vitu vyote, hutashuku tena ulazima wa kila kitu ambacho kiliumbwa na Mungu. Hutatumia tena maneno ya kijinga kufanya hukumu zisizokuwa na msingi juu ya mipangilio ya Mungu juu ya vitu vyote na njia zake mbalimbali za kuwakimu binadamu. Pia hutafanya mahitimisho yasiyokuwa na msingi juu ya sheria za Mungu kwa ajili ya vitu vyote ambavyo Aliviumba. Je, hii haiko hivyo?
Je, haya yote tuliyoyazungumza ni nini? Yafikirie. Mungu ana nia Yake katika kila kitu anachofanya. Ingawa binadamu hawawezi kuona nia hiyo, siku zote inahusiana na kuendelea kuishi kwa binadamu. Inahusiana bila kutenganishwa nayo—ni ya lazima. Hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kufanya kitu ambacho hakina manufaa. Kwa kila kitu ambacho Anafanya, mpango Wake upo ndani ya nadharia na kanuni zake, ambazo zinajumuisha hekima Yake. Lengo la mpango na nia hiyo ni kwa ajili ya ulinzi wa binadamu, kumsaidia binadamu kuzuia janga, uvamizi wa kiumbe chochote hai, na aina yoyote ya madhara kwa binadamu yasababishwayo na vitu vyote. Kwa hiyo kutokana na matendo ya Mungu ambayo tumeyaona kutoka katika mada hii ambayo tunaijadili, tungeweza kusema kwamba Mungu anawakimu binadamu kwa njia nyingine? Je, tungeweza kusema kwamba Mungu anawalisha na kuwachunga binadamu kwa njia hii? Hakika ungeweza kusema hilo. Sasa mnapaswa kuelewa, je, kuna uhusiano mkubwa kati ya mada hii na anwani ya ushirika wetu, "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote"? (Ndiyo.) Kuna uhusiano mkubwa, na mada hii ni kipengele kimoja chake. Kabla ya kuzungumza kuhusu mada hizi, watu walikuwa tu na fikra zisizo dhahiri juu ya Mungu, Mungu Mwenyewe na matendo Yake—hawakuwa na uelewa wa kweli juu ya vitu hivi. Hata hivyo, watu wanapoambiwa kuhusu matendo Yake na vitu ambavyo Amefanya, wanaweza kuelewa na kufahamu kanuni za kile ambacho Mungu anafanya na wanaweza kupata uelewa juu yake, sio? (Ndiyo.) Ingawa katika moyo wa Mungu, nadharia Zake, kanuni Zake, na Sheria Zake zinatatiza sana Anapokuwa anafanya kitu chochote, Alipotengeneza vitu vyote, na Anapotawala vitu vyote, ikiwa kitu kimoja kimechukuliwa kushiriki na nyinyi katika ushirika, je, hamtaweza kuelewa mioyoni mwenu kwamba haya ni matendo ya Mungu, na yapo thabiti sana? (Ndiyo.) Basi ni kwa jinsi gani uelewa wenu wa sasa juu ya Mungu ni tofauti na ulivyokuwa kabla? Ni tofauti kwa asili yake. Mlichokielewa kabla kilikuwa tupu, kisicho dhahiri sana, na kila mnachokielewa sasa kinajumuisha kiasi kikubwa cha ushahidi thabiti kushikilia matendo ya Mungu, kulinganisha na kile Mungu anacho na alicho. Kwa hiyo, yote ambayo nimeyasema ni nyenzo nzuri sana kwa ajili ya uelewa wa Mungu.
Hayo ndiyo kwa ajili ya kusanyiko la leo. Kwaheri! Kuwa na jioni njema! (Kwa heri, Mwenyezi Mungu.)
Februari 9, 2014
                                                         
                                                                                                               kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Yaliyopendekezwa :Kuelewa Umeme wa Mashariki


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni