Ijumaa, 31 Mei 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”



Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu.

Alhamisi, 30 Mei 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumatano, 29 Mei 2019

Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians



Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians

I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, ni jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo la Mungu. Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu, na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake. Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu, na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

Jumanne, 28 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili.

Jumatatu, 27 Mei 2019

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video)

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video) 

Mungu awahimiza makabila yote, 
mataifa na nyanja zote: 
Sikizeni sauti Yake, muione kazi Yake; 
mzingatie hatima ya wanadamu; 
mfanye Mungu Mtakatifu na Mheshimiwa, 
Mkuu na wa pekee wakuabudiwa, 
ulimwengu wote, na wanadamu, 
waishi chini ya baraka Yake Mungu
kama vizazi vya Ibrahimu, 
walivyoishi na ahadi ya Yehova, 
kama viumbe vya Mungu, Adamu na Hawa, 
walivyoishi bustani Edeni. 

Jumapili, 26 Mei 2019

Ushuhuda wa Injili | Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa


Wenzhong , Beijing
Agosti 11, mwaka wa 2012
Usiku wa Julai 21, mwaka wa 2012, tulikuwa na mafuriko makubwa hapa, ambayo hutokea kwa nadra. Ningependa kumwambia kila mtu aliye na kiu ya Mungu kile nilichokipitia kwa kweli na kukiona wakati huo.
Siku hiyo mume wangu nami tuliutunza uga wa chakula kikavu cha mifugo wa dada yangu. Wakati wa usiku mvua nzito iliendelea kunyesha, na tulienda kulala mapema sana. Saa nne kasorobo usiku ndugu mkwe wangu wa kiume aliita akisema: “Wanaelekea kufungua hodhi! Kila kitu kitafurikiwa!

Jumamosi, 25 Mei 2019

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu



Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake. Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu. Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya. Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake. Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana. Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia. Tunaondolewa vizuizi na ubaguzi wetu, tunaishi ndani ya upendo wa Mungu.