Jumatano, 1 Mei 2019

Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili”

Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili”

1. Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu.

Jumanne, 30 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Tano

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Tano


Mwenyezi Mungu anasema, “Bwana Yesu alipomleta Lazaro kutoka kwa wafu, Alitumia mstari mmoja: “Lazaro, kuja nje.” Hakusema kitu kingine mbali na hiki—maneno haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha hoja kwamba Mungu anaweza kukamilisha chochote kupitia maongezi, kukiwemo kumfufua mtu aliyekufa. Mungu alipoumba viumbe vyote, Alipouumba ulimwengu, Alifanya hivyo kwa maneno. Alitumia amri, maneno yaliyotamkwa kwa mamlaka, na hivyo tu viumbe vyote viliumbwa. Yalikamilishwa hivyo.

Jumatatu, 29 Aprili 2019

Uchaguzi kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu Juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

Umeme wa Mashariki | Uchaguzi kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu Juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

1. Yohana alianza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni miaka saba kabla ya ubatizo wa Yesu. Kwa watu, kazi aliyoifanya ilionekana kuwa juu zaidi ya kazi ya baadaye ya Yesu, ilhali yeye alikuwa, hata hivyo, nabii tu. Hakufanya kazi au kuzungumza ndani ya hekalu, lakini katika miji na vijiji nje yake. Hii alifanya, bila shaka, miongoni mwa taifa la Wayahudi, hasa wale waliokuwa maskini.

Jumapili, 28 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”

Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”


Mwenyezi Mungu anasema, “Katika furaha na huzuni ya kutengana na kisha kuunganika Kwangu na mwanadamu, hatuwezi kubadilishana mawazo. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena?

Jumamosi, 27 Aprili 2019

maneno ya Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

maneno ya Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu inayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi zaidi hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi zaidi bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa.

Ijumaa, 26 Aprili 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha. Viumbe vyote haviwezi kwenda nje ya sheria hizi na haziwezi kuvunjwa.