Jumatatu, 29 Aprili 2019

Uchaguzi kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu Juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

Umeme wa Mashariki | Uchaguzi kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu Juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

1. Yohana alianza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni miaka saba kabla ya ubatizo wa Yesu. Kwa watu, kazi aliyoifanya ilionekana kuwa juu zaidi ya kazi ya baadaye ya Yesu, ilhali yeye alikuwa, hata hivyo, nabii tu. Hakufanya kazi au kuzungumza ndani ya hekalu, lakini katika miji na vijiji nje yake. Hii alifanya, bila shaka, miongoni mwa taifa la Wayahudi, hasa wale waliokuwa maskini.

Jumapili, 28 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”

Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”


Mwenyezi Mungu anasema, “Katika furaha na huzuni ya kutengana na kisha kuunganika Kwangu na mwanadamu, hatuwezi kubadilishana mawazo. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena?

Jumamosi, 27 Aprili 2019

maneno ya Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

maneno ya Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu inayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi zaidi hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi zaidi bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa.

Ijumaa, 26 Aprili 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha. Viumbe vyote haviwezi kwenda nje ya sheria hizi na haziwezi kuvunjwa.

Jumatano, 24 Aprili 2019

Matamshi ya Kristo | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Mwenyezi Mungu alisema , Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa.

Jumanne, 23 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarifa na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kudumisha na kupata umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana.