Ijumaa, 26 Aprili 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha. Viumbe vyote haviwezi kwenda nje ya sheria hizi na haziwezi kuvunjwa.

Jumatano, 24 Aprili 2019

Matamshi ya Kristo | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Mwenyezi Mungu alisema , Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa.

Jumanne, 23 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarifa na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kudumisha na kupata umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana.

Jumatatu, 22 Aprili 2019

Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu


Mwenyezi Mungu alisema, Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. 

Jumapili, 21 Aprili 2019

maneno ya Mungu | Sura ya 9

maneno ya MunguSura ya 9

Mwenyezi Mungu alisema, Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu haneni lugha ya mwanadamu, wala mwanadamu hawezi kunena lugha ya Mungu, na kwa Mungu, madai ya mwanadamu Kwake ni rahisi, ilhali matakwa ya Mungu kwa mwanadamu hayafikiki na hayafikiriki kwa mwanadamu. Ukweli, hata hivyo, ni kinyume kabisa: Mungu anataka tu “asilimia 0.1” ya mwanadamu.

Jumamosi, 20 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi kwa furaha katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote.